Ala sogezi-ala za kutamka ambazo husonga mfano ulimi na mdomo
Ala tuli-hutulia wakati Wa kutamka mfano ufizi,meno,kaa kaa gumu,kaa kaa laini,pua,koromeo
MBOROGO answered the question on June 9, 2019 at 04:24
- Onyesha matumizi ya hali "ni" katika wing I.(Solved)
Onyesha matumizi ya hali "ni" katika wing I.
Date posted: May 14, 2019. Answers (1)
- Eleza maana ya upangaji lugha na ufafanue sababu ya shughuli hiyo(Solved)
Eleza maana ya upangaji lugha na ufafanue sababu ya shughuli hiyo
Date posted: May 14, 2019. Answers (1)
- Eleza dhima mbili ya kiimbo(Solved)
Dhima ya kiimbo
Date posted: May 14, 2019. Answers (1)
- Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo mpitapo kwake mtampata(Solved)
Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo mpitapo kwake mtampata.
Date posted: May 14, 2019. Answers (1)
- Mambo yepi yanayoweza kusababisha kufa kwa lugha?(Solved)
Mambo yepi yanayoweza kusababisha kufa kwa lugha?
Date posted: May 14, 2019. Answers (1)
- Taja na ueleze dhima tano ambazo sajili za lugha hutekeleza(Solved)
Dhima ambazo sajili za lugha hutekeleza
Date posted: May 14, 2019. Answers (1)
- UFAHAMU
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Ulimwengu unatakiwa kuzua mbinu za kulitatua tatizo la ufukara ambao ni
kikwazo kikuu cha juhudi za maendeleo. Ufukara unayakabili mataifa mengi
yanayoendelea...(Solved)
UFAHAMU
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Ulimwengu unatakiwa kuzua mbinu za kulitatua tatizo la ufukara ambao ni
kikwazo kikuu cha juhudi za maendeleo. Ufukara unayakabili mataifa mengi
yanayoendelea na kuyatosa kwenye shida nyingi huku mataifa ya magharibi
yakizidi kupiga hatua kubwa za kimaendeleo. Tofauti iliyopo kati ya mataifa
yanayoendelea na yaliyoendelea inaendeiea kuongezeka kila siku.
Miongoni mwa sababu zinazochangia katika ufukara huu ni pamoja na ufisadi,
uongozi mbaya, turathi za kikoloni na uchumi unaotegemea kilimo ambacho
hutegemea mvua isiyoweza kutabirika. Vilevile, mataifa yanayoendelea yana idadi
kubwa ya watu inayoupiku uwezo wa mataifa husika. Pamoja na haya, mataifa
haya hayana uwezo wa kuwakomboa raia wake kutoka katika lindi la umaskini
huu unaokithiri. Ukosefu wa elimu na nafasi adimu za kazi huchangia pia katika
tatizo hili. Ni wazi kuwa ufukara una athari hasi kote ulimwenguni. Aghalabu,
ufukara huchipuza matendo mabaya. Ni rahisi kuwashawishi wananchi maskini
kushiriki katika uhalifu iii kujinasua kutoka kwenye lindi la kimaskini. Udhaifu huu
huweza kuzaa mbegu ya kuatika maovu ya kila aina ukiwemo ugaidi. Mataifa
yaliyoendelea yanatakiwa kuyaburai madeni yanayoyadai mataifa yanayoendelea
kama njia moja ya kupambana na ufukara. Mataifa haya maskini hutumia asilimia
kubwa ya mapato ya kitaifa kuyalipia madeni haya. Hali hii imeyafanya mataifa
haya kushindwa kujikwamua kutoka kwenye minyororo ya ufukara. Njia nyingine
ya kuyasaidia mataifa haya ni kukubali kutoa ruzuku za kimaendeleo badala ya
mikopo kwa nchi husika.
Mataifa yanayoendelea nayo yanatakiwa kuchukua hatua katika kuwanusuru raia
wake kutoka kwenye dhiki hii.Ni sharti yaibuke na mikakati kabambe ya
kupambana na ufukara. Itakuwa na faida kubwa iwapo mataifa haya yataunda
sera zinazotambua ufukara kama tatizo kuu linalozikabili na kuweka mikakati ya
kuwaokoa raia wake kutoka kwenye tatizo hili. Pamoja na mikakati hii ni kuzalisha
nafasi za kazi, kuimarisha miundo msingi,kuendeleza elimu inayolenga kutatua
matatizo maalumu katika jamii na kupanua viwanda. Kuna pia haja ya viongozi
kuwa waangalifu ili mfumo wa soko huru ambao unaendelezwa na mataifa
yaliyoendelea usiishie kuwa chanzo cha kufa kwa viwanda asilia. Maamuzi yote ya
sera za kiuchumi sharti yauzlngatie uhalisia wa maisha ya raia wa mataifa haya.
(a) Eleza athari za madeni kwa nchi zinazoendelea.
(b) Kwa nini umaskini unatawala mataifa yanayoendelea?
(c) Mwandishi anatoa mapendekezo yapi kwa mataifa yanayoendelea katika
kutatua tatizo la ufukara?
(d) Mfumo wa soko huru una mathara gani kwa mataifa yanayoendelea?
(e) Taja visawe vya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu.
(i)Turathi za kikoloni
(ii) Kuatika
(iii) Kuyaburai
Date posted: May 7, 2019. Answers (1)
- MUHTASARI (alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Taifa huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na wanaojitambua kisiasa
kama watu walio na mwelekeo, maono na hatima...(Solved)
MUHTASARI (alama 15)
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
Taifa huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na wanaojitambua kisiasa
kama watu walio na mwelekeo, maono na hatima sawa. Utaifa hujengwa kwenye
misingi ya mapenzi kwa nchi, Utambuzi wa cheo, eneo, hadhi, rangi na hata
makabila wanakotoka raia wa taifa moja si chanzo cha kuwatanganisha. Nchi moja
huweza kuundwa na watu walio na tofauti chungu nzima zikiwemo tofauti za
kikabila, kitabaka na kimawazo. Hata hivyo, watu hao huwa na folsafa na imani
sawa kama taifa inayoashiriwa hasa na wimbo wa taifa. Hata hivyo haya yotc
hayawezi kuwafikia katika kiwango cha kuunda taifa. Uzalendo ndio mhimili
mkuu wa utaifa. Uzalendo ni mapenzi aliyo nayo mtu kwa nchi yake. Mapenzi
haya humwongoza mtu katika mawazo yake, itikadi yake, matendo yake,
matamanio yake na mkabala wake kuhusu nchi na hatima ya nchi yake.
Mzalendo hawezi kushiriki katika matendo yanayoweza kuiletea nchi yake
maangamizo kwa vyovyote vile. Mzalendo huongozwa na mwenge wa wema.
Mzalendo hawezi kushiriki kwenye shughuli zozote zinazohujumu mshikamano wa
kitaifa. Yeye hatawaliwi na ubinafsi wa kutaka kufaidi nafsi yake naya jamii
yake finyu. Matendo yake yote huongozwa na ari ya kuiboresha nchi yake.
Anayeipenda nchi yake hujiepusha na ulafi wa kujilimbikizia mali. Yuko radhi
kuhasirika mradi taifa lake linufaike.
Utaifa ni mche aali unaopaliliwa kwa uzalendo, kuepuka uchu wa nafsi na taasubi
hasi zikuwepo za kikabila na ubinafsi. Hali hii inapofikiwa, hatima ya taifa na
mustakabali wa raia wake huwa wenye matumaini makubwa.
(a) Kwa maneno 40 - 50 dondoa sifa kuu za utaifa.
(b) Ni nini misingi ya kutathmini mzalendo? (maneno 60 - 70)
Date posted: May 7, 2019. Answers (1)
- Tumia nomino yoyote katika ngeli ya I-I kutunga sentensi.(Solved)
Tumia nomino yoyote katika ngeli ya I-I kutunga sentensi.
Date posted: May 7, 2019. Answers (1)
- Tunga neno lenye muundo huu wa silabi:
Irabu + konsonanti + konsonanti + irabu(Solved)
Tunga neno lenye muundo huu wa silabi:
Irabu + konsonanti + konsonanti + irabu
Date posted: May 7, 2019. Answers (1)
- Tunga sentensi hii upya kwa kufuata maagizo: Wasichana wanaingia darasani kwa haraka (andika kinume chake)(Solved)
Tunga sentensi hii upya kwa kufuata maagizo: Wasichana wanaingia darasani kwa haraka (andika kinume chake)
Date posted: May 7, 2019. Answers (1)
- Tambua kiambishi awali na tamati kati neno: Alalaye(Solved)
Tambua kiambishi awali na tamati kati neno: Alalaye
Date posted: May 7, 2019. Answers (1)
- Ainisha vivumishi katika sentensi hii: mzee mwenyewe ni mkongwe na amepewa zawadi kwa kuwa shamba lake lilitoa mazao mengi.(Solved)
Ainisha vivumishi katika sentensi hii: mzee mwenyewe ni mkongwe na amepewa zawadi kwa kuwa shamba lake lilitoa mazao mengi.
Date posted: May 7, 2019. Answers (1)
- Askari wasipopiga doria wala kushikiana na raia hawatakuwa wametuhakikishia usalama. (yakinisha sentensi hii)(Solved)
Askari wasipopiga doria wala kushikiana na raia hawatakuwa wametuhakikishia usalama. (yakinisha sentensi hii)
Date posted: May 7, 2019. Answers (1)
- "Shughuli yetu itakamilika kesho", mama alimwambia mwanaye Juma.
(Andika katika usemi wa taarifa).(Solved)
"Shughuli yetu itakamilika kesho", mama alimwambia mwanaye Juma.
(Andika katika usemi wa taarifa).
Date posted: May 7, 2019. Answers (1)
- Dhihirisha matumizi matatu tofauti ya kimaana yatakayotokea ketenzi
"ona" kikinyambuliwa katika kirai hiki "ona ndoto".(Solved)
Dhihirisha matumizi matatu tofauti ya kimaana yatakayotokea ketenzi
"ona" kikinyambuliwa katika kirai hiki "ona ndoto".
Date posted: May 7, 2019. Answers (1)
- Eleza matumizi ya hali za "ka" na "hu" katika sentensi zifuatazo:
(i) Balozi huja hapa kila mara.
(ii) Mpishi alipika, akapakuwa na akagawa chakula.(Solved)
Eleza matumizi ya hali za "ka" na "hu" katika sentensi zifuatazo:
(i) Balozi huja hapa kila mara.
(ii) Mpishi alipika, akapakuwa na akagawa chakula.
Date posted: May 7, 2019. Answers (1)
- Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi: Tuiiitwa na baba.
Mtendaji ni baba(Solved)
Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi: Tuiiitwa na baba.
Mtendaji ni baba
Date posted: May 7, 2019. Answers (1)
- Akifisha: Shangazi alimwambia mwanawe njoo nikupcleke kwenu jioni
mtoto aliuliza kwetu wapi?(Solved)
Akifisha: Shangazi alimwambia mwanawe njoo nikupcleke kwenu jioni
mtoto aliuliza kwetu wapi?
Date posted: May 7, 2019. Answers (1)
- Eleza matumizi mawili ya kiambishi -ji-.(Solved)
Eleza matumizi mawili ya kiambishi -ji-.
Date posted: May 7, 2019. Answers (1)