Soma Makala yatuatayo kisha ujibu maswali Ama kweli maisha ya vijana wa kisasa yanatofautiana na kuhitilafiana pakubwa na yale ya wazee wao. Sio katika mavazi, lugha, mienendo,...

      

Soma Makala yatuatayo kisha ujibu maswali
Ama kweli maisha ya vijana wa kisasa yanatofautiana na kuhitilafiana pakubwa na yale
ya wazee wao. Sio katika mavazi, lugha, mienendo, mitazamo, mawazo tu bali pia katika
kipengele kingine chochote utakachofikiria. Yote haya ni vielezo vya jinsi kizazi cha leo
kinavyoishi katika ulimwengu ambao ni kivuli tu cha ule wa vizazi vilivyotangulia.
Baadhi ya watu wameieleza hali hii kuwa maisha sio jiwe. Kwao basi, si ajabu katu
kuwaona vijana wakizungumza lugha yao ya kipekee au wakivaa nguo zinazobana
ajabu na kudhirisha bayana maungo yao badala ya kuyasitiri.

Hata hivyo, watu wengi wameonelea kwamba hali ya maisha ya vijana wa leo maasia
yanayotokana na utundu na hata ukatili wao. Upande huu umetoa rai kwamba kizazi
hiki kisingepotoka kama tu kingezingatia na kustahi utamaduni wa wahenga wao
ambamo wazazi wao ndimo walimokulia. Wanazidi kufafanua kuwa nyendo hizi za
miaka ya nyuma zilithamini sana amali kama waminifu, heshima kwa wazee ama
wakuu, bidii, ushirikiano, ukarimu, unyenyekevu, hadhari katika kila jambo, utiifu na pia
kujitegemea. Yote haya yamesahaulika ama tuseme yamepuuzwa katika utamaduni wa
kisasa.”

Swali lilozuka sasa ni je tunapaswa kuwahukumu vijana wa leo kwa kutumia vigezo au
masharti gani? Tuwapige darubini kwa kutegemea hali ilivyo hivi leo duniani ama
tuwapime kwa mujibu wa jinsi maisha ya baba na babu zao yalivyokuwa. Jibu la swali
hili ni gumu na sharti lifafanuliwe kwa makini lisije likaegemea upande wowote.

Mathalan, ni jambo lisilopingika kuwa maisha ni utaratibu unaothirika na hivyo
kubadilika daima. Angalia kwa mfano jinsi maendeleo ya elimu, sayansi, mawasiliano
na hata ufundi yalivyoyageuza maisha siku hizi. Yamkini vijana wa barani Afrika
wakaona na hata kuzungumza wa wenzao kutoka Uropa, Asia na Marekani bila hata
kunyanyuka hapa kwao nyumbani. Athari ya filamu, video, vitabu, magazeti, majarida
n.k haikadiriki. Haya kwa kiasi yamewafanya vijana hata kupevuka kabla ya wakati
wao. Isitoshe, mambo haya yameweza kuwazuzua na kuwaaminisha kuwa yale
wanayojifunza ni kweli. Matokeo yamekuwa ni wao kuudunisha utamaduni wao wa
asili na kuupapia ule wa wageni waliowaathiri. Tusisahau kuwa ujana ni tembo la
mnazi na rahisi kwao kubadili mawazo.

Lakini hatuwezi kuwasamehe vijana wanaokosa akili razini kwa kupotoshwa na
kuchacharika na yote, wanayoyapokea kutokea ugenini na hivyo kuanza kudhalilisha
utamaduni wa Waafrika. Hata hivyo, badala ya kuwakashifu wanapopotea njia
amakuwapongeza wanapotenda yale tunayoyategemea tu, ni wajibu mkubwa wa
wazazi kuwaongoza na kuwasaidia vijana kuwa na uwezo mkubwa na kufanya uteuzi
mwafaka katika maisha yao.
Maswali

(a) Kulingana na mwandishi, kundi linalodai kuwa maisha sio jiwe’ lina maoni
gani?
(b) Kulingana na taarifa uliyoisoma ni jinsi gani vijana wa kisasa wangeziepuka
athari mbaya?
(c) Kwa mujibu wa taarifa hii, utamaduni wa Kiafrika una manufaa. Yataje
(d) Mwandishi anaposema mambo haya yameweza kuwazuzua na
kuwaaminisha vijana kuwa yale wanayojifunza ni kweli anamaanisha nini?
(e) Mbali na wazazi, ni makundi gani mengine ya watu ambayo yanapaswa
kutoa mawaidha kwa vijana?
(f) Kwa maoni yako vijana wanapaswa kufanya uteuzi wa namna gani katika
mvutano huu wa tamaduni?
(g) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika makala
(i) Maasia
(ii) Razini
(h) Andika methali moja ambayo inaafiki taarifa hii

  

Answers


Kavungya
A. Lazima maisha yabadilike kwa kutegemea wakati na mwingiliano wa tamaduni.
B Kwa kuzingatia utamaduni wa wahenga wao ambamo wazazi wao ndio
walimokulia.
C Uaminifu, heshima kwa wakuu, bidii ushirikiano, ukarimu, ungenyekevu, hadhari
katika jambo, utiifu na kujitegemea.
D mambo haya yanawapotosha wakaona kuwa yale ya zamani hayana mafao na
kuwa yale maendeleo ya siku hizi kama video, filamu, vitabu elimu nk. Ndiyo
pekee yafaayo kuzingatiwa na kufuatwa.
-alaye juu ya maisha ya zamani
-maisha ya leo (siku hizi)
E. Waalimu, majirani, wanasiasa, wahubiri
F. Wanapaswa kuchagua yale mazuri kutoka kwa utamaduni wa kiafrika na pia
kutoka kwa usasa wayafuate.
G. Maovu, Maasi, tulivu, Makini
H. Usiache mbachao kwa mswala upitao
Mwacha mila ni mtumwa
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 06:32


Next: Read the passage below and answer the questions that follow.
Previous: Read the passage below and then answer the questions that follow:

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions