Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Soma makala yafuatayo Kisha Ujibu Maswali Zamani sana na hata hivi karibu watu wengi kote duniani walikuwa wakiamini kuwa kuna ardhi na mbingu tu basi. Imani hii...

      

Soma makala yafuatayo Kisha Ujibu Maswali
Zamani sana na hata hivi karibu watu wengi kote duniani walikuwa wakiamini kuwa
kuna ardhi na mbingu tu basi. Imani hii ilijikita katika mantiki inayosema kwamba
ardhi au dunia ipo katikati ya maumbile yote na isitoshe, ni tambarare.

Juu ya ardhi ni mbingu ambayo imejaa vimulimuli vidogovidogo sana viitwavyo nyota.
Baina ya vimulimuli vipo viwili vikubwa viitwavyo mwezi na jua. Hivi viwili japo ni
vikubwa kuliko vingine, bado ni vidogo kuliko ardhi.

Hii ndiyo imani iliyoutawala ulimwengu kwa miaka na miaka, na ikawa imekita mizizi.
Lakini jinsi wanajimu walivyozidi kuelimika, waligundua kwamba ukweli wa mambo
umejitenga kando kabisa na imani hii

Ukweli ni kwamba zima tulionalo la rangi ya samawati nusumviringo juu ya paa zetu za
vichwa ni kubwa sana tena. Na si kubwa tu bali lazidi kupanuka. Katika bwaka hili
lipanukalo kila uchao mna galaksi nyingi ajabu zisizokadirika. Ndani ya kila galaksi
mna nyota mamilioni na mamilioni, malaki na kanui. Imejulikana kuwa nyota hizo japo
huonekana kama vimulimuli vidogo sana usiku usiku ni kubwa ajabu. Kadiria
mwenyewe! Jua letu ni nyota kubwa sana. Ukubwa wake umezidi wa dunia mara
nyingi sana, zaidi ya elfu moja! Basi fikiria juu ya ukubwa wote huo. Imegunduliwa ya
kwamba jua ni nyota ndogo sana ikilinganishwa na zingine zilizo katika galaksi yetu tu,
licha ya galaksi nyinginezo zilizoko katika bwaka.

Na haya sio maajabu peke yake. Wataalam wamevumbua mengi ya kushangaza zaidi.
Mathalan, imekuja kufahamika kuwa jua letu ambalo ni nyota, lina sayari tisa
zinazolizunguka. Baadhi ya sayari hizi ni Arthi yetu. Zaibaki, Zuhura, Mirihi, na mshitara
baina ya tisa jumla. Baadhi ya sayari hizi zina visayari vidogo vinavyozizunguka.
Visayari hivi ndivyo viitwavyo miezi. Ardhi yetu ina mwezi miwili ilhali Mshitara ina
kumi na miwili! Sayari hizi zote na visayari vyao, au vitoto ukipenda, havitoi mwanga.
Nuru ya mwezi na nuru ya hizo sayari zinazolizunguka jua letu inatokana na jua
lenyewe. Kwa hakika ni mmeremeto tu unaotufikia sisi kupitia sayari hizi kutoka kwa
nyota hii yetu iitwayo JUA.

Kama wasemavyo washahili ya Mungu ni mengi. Taswira tuliyo nayo katika maelezo
haya yaonyesha jinsi ambavyo mwanadamu licha ya kuwa na akili nyingi, bado
hajawahi kuigusia siri kamili ya mungu. Lakini kwa ufupi twaweza kusema hivi. Ikiwa
katika bwaka lote kuna galaksi nyingi, bila shaka kwa vile jua ni nyota basi zimo sayari
nyingi ajabu zinazozunguka kila nyota au jua kama zipasavyo kuitwa. Kwa vile katika
mfumo- jua imo sayari moja yenye viumbe vyenye uhai, binadamu wakiwemo, basi
bila shaka katika mifumo- jua mingine katika galaksi yetu zipo sayari zinazofanana na ardhi hii yetu, ambazo sina viumbe vilivyo hai- penginepo watu pia! Wanona maajabu?
Na katika magalaksi mengine je? Mambo pengine ni yayo hayo! Kwa hivyo huenda
ikawa peke yetu katika bwaka hili; labda tuna viumbe wenzetu ambao hatutakutana nao
katika uhai wetu kwa sababu uwezo wetu wa kimaumbile, na vile kisayansi ni hatifu.
Lakini, kwa vile mwenye kupanga maajabu hayo yote, yaani Mwenyezi Mungu ni
huyo mmoja basi huenda sote tukakutana Ahera.
Mungu ni mkubwa

(a) Kulingana na habari hii, taja mambo manne ambayo ni imani potovu
(b) Kwa kusema “ ukweli wa mambo umejitenga kando” Mwandishi anamaanisha
nini?
(c) Taja sifa zozote nne za maumbile ya anga zinazopatikana katika habari hii
(d) Taja vitu viwili vipatikanavyo katika galaksi
(e) Taja sayari mbili ambazo ni kubwa kuliko ardhi
(f) Ni ithibati gani iliyotolewa kuonyesha kuwa nyota sio vijataa vidogo?
(g) Bainisha nuru aina mbili tuzionazo angani
(h) (i) Ni neno gani lenye maana sawa na “anga” ama “upeo” katika habari hii?
(ii) Andika neno moja ambalo lina maana sawa na paa kama lilivyotumiwa
katika taarifa
(i) Mwandishi anaposema kuwa katika magalaksi mengine “mambo pengine ni yayo
hayo” anamaanisha nii?

  

Answers


Kavungya
a) Mambo manne ambayo ni imani potovu
1. Kuna mbingu na ardhi tu basi
2. Dunia ipo katikati ya maumbile yote
3. Dunia ni tambarare
4. Juu ya ardhi ni mbingu iliyojaa vimulimuli vidogo kulik ardhi
5. Baina ya vimulimuli vipo viwili vikubwa vitwavyo mwezi na jua
6. Mwezi na jua ni vidogyo kuliko ardhi
7. Mwezi ni nyota

b) Maana ya ‘Ukweli wa mambo umejitenga kando’ ‘ni kwamba
Si kweli au
Ukweli untofautiana na imani hii au
Ni kinyume na imani hii

c) Sifa zozote nne za maumbile ya anga
1. Ina rangi ya samawati
2. Mi nusu mviringo
3. Ni kubwa sana
4. Inazidi kupanuka
5. Ndani ya galaksi nyingi ajabu kila uchao
6. Ndani ya galaksi mna nyota nyingi ajabu
7. Nyata ni kubwa sana.
8. Mna sayari tisa zinazolizunguka jua

d) Taja vitu viwili vipatikanavyo katika galaksi
Sayari na nyota au
Miezi au sayari na jua au
Mirihi, mshitara, zalibaki n.k. na jua

e) Sayari mbili ambazo ni kubwa kuliko ardhi ni
Mshitara, zohali, utaridi, sumbla,
Zohali ni sawa na sarateni au zaratani

f) Nyota sio vijitaa vidogo kwa sababu
Jua ni nyota kubwa sana au
Jua ni dogo likilinganishwa na nyota zingine au nyota ni kubwa ajabu

g) Nuru mbili zilizo angani ni.
Nuru ya jua au nyota iliyo asilia nuru ya sayari au miezi kutokana na
mmeremeto wa jua

h) i) Neno lenye maana sawa “anga” au “ upeo” ni
Bwaka au
Mbingu
ii) Neno lisilo na maana sawa na paa ni
Tosi

i) Maana ya “mambo pengine ni ya hayo” ni
- Kuwa huenda magalaksi mengine yakawa na viumbe hai…Na
pensinge watu pia au
- Huenda magalaksi mengine yakawa na maajabu haya au
- mambo ni sawa nay a ardhi.
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 07:01


Next: Akifisha kifungu kifuatacho “Baba Wafua, ona Barua iliyotoka kwa mwanao. Hata hati haisomeki” “lo” baba watoto akamaka. Hii barua kweli imetoka kwa mwanangu Wafua. “Waniuliza mimi?” Mama akamjibu...
Previous: Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali Mababu walituachia msemo maarufu kuwa “ Kuzaa sio kazi. Kazi kubwa ni kulea.” Busara iliyomo katika methali hii inatupambazukia peupe pindi...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Akifisha kifungu kifuatacho “Baba Wafua, ona Barua iliyotoka kwa mwanao. Hata hati haisomeki” “lo” baba watoto akamaka. Hii barua kweli imetoka kwa mwanangu Wafua. “Waniuliza mimi?” Mama akamjibu...(Solved)

    Akifisha kifungu kifuatacho
    “Baba Wafua, ona Barua iliyotoka kwa mwanao. Hata hati haisomeki” “lo” baba
    watoto akamaka. Hii barua kweli imetoka kwa mwanangu Wafua. “Waniuliza
    mimi?” Mama akamjibu “Tazama maandishi na anwani basi. Shule ya Msingi ya
    Barungani S.L.P 128 Vuga.”

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Ili kupiga vita propaganda za wakoloni mambo leo katika vyuo vikuu vyetu, inafaa kutumia Kiswahili kufundisha masomo yote. Jambo hili ni...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
    Ili kupiga vita propaganda za wakoloni mambo leo katika vyuo vikuu vyetu, inafaa
    kutumia Kiswahili kufundisha masomo yote. Jambo hili ni la lazima na linawezekana
    kabisa, ingawa lina matatizo yake. Jambo linalotakiwa kufanya ni kuchukua
    wananchi wenye elimu ya juu wakatafsiri fikra za wazalendo katika Kiswahili. Kwa njia
    hiyo, lugha ya wanachuo itakuwa ndiyo lugha ile ile ya umma

    Ni jambo la kuepukwa kuwa na lugha mbili ambazo zinasaidia kuwatenga na umma.
    Wasomi wetu watakuwa wamekaribia umma kwa kutumia lugha iliyozoeleka na umma
    wenyewe. Jambo linalotutinga ni hili: mara nyingi wasomi wengine waliozoea
    kutakadamu lugha ya Kiingereza wanapojaribu kuwaeleza watu wengine jambo la
    kieleimu au kitaalamu, hushindwa kabisa. Wao huchanganya sana maneno ya
    Kiingereza na Kishwahili hata kufikia kiasi ambacho mtu wa kawaida haelewi
    chochote.

    Kwa kuwa wakoloni mamboleo wameelewa kwamba lugha ni kioo cha kuchujia
    utamaduni, miaka ya hivi karibuni wamejifunza kwa dhati kuliko wakati mwingine
    kupigania ufundishaji wa lugha zao, hususa, Kifaransi na Kiingereza. Wakati huo wao
    wanatoa porojo kuwa kugha ya Kiswahili haifai na kwamba ni lugha ya watumwa.
    Kwa mfano, utaona katika maandishi mngi kila wanapoorodhesha lugha kuu za dunia.
    Kiswahili hakionyeshwi katika hizo.

    Badala yake wanakiweka kwenye kiwango sawa na Kiganda, Kikikuyu, Kinyamwezi
    na lugha kadha wa kadha za kikabila. Hiyo ni harakati kubwa ya kudanganya umma
    na kukivua Kiswahili hadhi yake ilhali lugha hii inatumiwa na zaidi ya watu milioni
    mia moja wanaosambaa katika sehemu mbalimbali za ulimwengu. Kwa kutumia hila hii,
    wao wanasadikisha watu wengi ili wachukulie Kiswahili kama lugha nyimgine ya
    kikabila. Ndiposa hawa wakoloni mamboleo wanawashawisha baadhi ya watumiaji wa
    Kiswahili wastawishe lugha za makabila mabalimbali na kuonyesha kwamba
    umaarufu wa lugha hizo ni sawa na Kiswahili. Hayo bila shaka ni mawazo. Ukweli
    ulioko ni kwamba mawazo kama haya yawezi keundeleza ukabila. Hata hivyo sharti
    kueleweka kwamba kusema hivyo si kudhalilisha umuhimu wa kukuza lugha za
    kikabila. Tusemacho ni kuwa ukuzaji wa lugha hizo ungekuwa na kusidi moja kuu
    ambalo ni kustawisha Kiswahili kufika ngazi za kimataifa.

    Swali ambalo ni muhimu kujiuliza ni hili: Wakoloni - mamboleo wanatuonaje
    tunapokazania Kiswahili? Je, wanaona ni faida kwao au kwetu? Jambo muhimu zaidi
    ni kutamba jinsi Kiswahili kinavyotuwezesha kuungana na kuwa kitu kimoja. Ni dhahiri
    kwamba wakoloni mamboleo hawafurahili wanapoona kishahili kikituunganisha.
    Machoni mwao Kiswahili ni ishara mojawapo ya kujikomboa kwetu kutokana na
    minyororo yao. Hivi si kusema kwamba hapupaswi kujifunza kiingereza, Kifaranza au
    Kijerumani, la hasha. Tunachosema ni kwamba tutumie Kiswahili ambacho ni kioo
    cha utamaduni wetu.

    (a) Mwandishi amesema nini kuhusu utengano kati ya umma wa wasomi?
    ( Maneno 30 – 40)
    (b) Eleza pingamizi zilizowekwa na wakoloni- mamboleo ili kudunisha
    Kiswahili (maneno 40 – 50)
    (c) Kulingana na mwandishi ni sababu gani zinazofanya wakoloni mamboleo
    kupinga maendeleo ya Kiswahili?

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma Makala yatuatayo kisha ujibu maswali Ama kweli maisha ya vijana wa kisasa yanatofautiana na kuhitilafiana pakubwa na yale ya wazee wao. Sio katika mavazi, lugha, mienendo,...(Solved)

    Soma Makala yatuatayo kisha ujibu maswali
    Ama kweli maisha ya vijana wa kisasa yanatofautiana na kuhitilafiana pakubwa na yale
    ya wazee wao. Sio katika mavazi, lugha, mienendo, mitazamo, mawazo tu bali pia katika
    kipengele kingine chochote utakachofikiria. Yote haya ni vielezo vya jinsi kizazi cha leo
    kinavyoishi katika ulimwengu ambao ni kivuli tu cha ule wa vizazi vilivyotangulia.
    Baadhi ya watu wameieleza hali hii kuwa maisha sio jiwe. Kwao basi, si ajabu katu
    kuwaona vijana wakizungumza lugha yao ya kipekee au wakivaa nguo zinazobana
    ajabu na kudhirisha bayana maungo yao badala ya kuyasitiri.

    Hata hivyo, watu wengi wameonelea kwamba hali ya maisha ya vijana wa leo maasia
    yanayotokana na utundu na hata ukatili wao. Upande huu umetoa rai kwamba kizazi
    hiki kisingepotoka kama tu kingezingatia na kustahi utamaduni wa wahenga wao
    ambamo wazazi wao ndimo walimokulia. Wanazidi kufafanua kuwa nyendo hizi za
    miaka ya nyuma zilithamini sana amali kama waminifu, heshima kwa wazee ama
    wakuu, bidii, ushirikiano, ukarimu, unyenyekevu, hadhari katika kila jambo, utiifu na pia
    kujitegemea. Yote haya yamesahaulika ama tuseme yamepuuzwa katika utamaduni wa
    kisasa.”

    Swali lilozuka sasa ni je tunapaswa kuwahukumu vijana wa leo kwa kutumia vigezo au
    masharti gani? Tuwapige darubini kwa kutegemea hali ilivyo hivi leo duniani ama
    tuwapime kwa mujibu wa jinsi maisha ya baba na babu zao yalivyokuwa. Jibu la swali
    hili ni gumu na sharti lifafanuliwe kwa makini lisije likaegemea upande wowote.

    Mathalan, ni jambo lisilopingika kuwa maisha ni utaratibu unaothirika na hivyo
    kubadilika daima. Angalia kwa mfano jinsi maendeleo ya elimu, sayansi, mawasiliano
    na hata ufundi yalivyoyageuza maisha siku hizi. Yamkini vijana wa barani Afrika
    wakaona na hata kuzungumza wa wenzao kutoka Uropa, Asia na Marekani bila hata
    kunyanyuka hapa kwao nyumbani. Athari ya filamu, video, vitabu, magazeti, majarida
    n.k haikadiriki. Haya kwa kiasi yamewafanya vijana hata kupevuka kabla ya wakati
    wao. Isitoshe, mambo haya yameweza kuwazuzua na kuwaaminisha kuwa yale
    wanayojifunza ni kweli. Matokeo yamekuwa ni wao kuudunisha utamaduni wao wa
    asili na kuupapia ule wa wageni waliowaathiri. Tusisahau kuwa ujana ni tembo la
    mnazi na rahisi kwao kubadili mawazo.

    Lakini hatuwezi kuwasamehe vijana wanaokosa akili razini kwa kupotoshwa na
    kuchacharika na yote, wanayoyapokea kutokea ugenini na hivyo kuanza kudhalilisha
    utamaduni wa Waafrika. Hata hivyo, badala ya kuwakashifu wanapopotea njia
    amakuwapongeza wanapotenda yale tunayoyategemea tu, ni wajibu mkubwa wa
    wazazi kuwaongoza na kuwasaidia vijana kuwa na uwezo mkubwa na kufanya uteuzi
    mwafaka katika maisha yao.
    Maswali

    (a) Kulingana na mwandishi, kundi linalodai kuwa maisha sio jiwe’ lina maoni
    gani?
    (b) Kulingana na taarifa uliyoisoma ni jinsi gani vijana wa kisasa wangeziepuka
    athari mbaya?
    (c) Kwa mujibu wa taarifa hii, utamaduni wa Kiafrika una manufaa. Yataje
    (d) Mwandishi anaposema mambo haya yameweza kuwazuzua na
    kuwaaminisha vijana kuwa yale wanayojifunza ni kweli anamaanisha nini?
    (e) Mbali na wazazi, ni makundi gani mengine ya watu ambayo yanapaswa
    kutoa mawaidha kwa vijana?
    (f) Kwa maoni yako vijana wanapaswa kufanya uteuzi wa namna gani katika
    mvutano huu wa tamaduni?
    (g) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika makala
    (i) Maasia
    (ii) Razini
    (h) Andika methali moja ambayo inaafiki taarifa hii

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika kwa udogo ;ndege mkubwa alitua dirishani(Solved)

    Andika kwa udogo ;ndege mkubwa alitua dirishani.

    Date posted: June 15, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya kiimbo na onyesha dhima yake(Solved)

    Eleza maana ya kiimbo na onyesha dhima yake.

    Date posted: June 9, 2019.  Answers (1)

  • Taja aina mbili za ala(Solved)

    Taja aina mbili za ala

    Date posted: June 9, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha matumizi ya hali "ni" katika wing I.(Solved)

    Onyesha matumizi ya hali "ni" katika wing I.

    Date posted: May 14, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya upangaji lugha na ufafanue sababu ya shughuli hiyo(Solved)

    Eleza maana ya upangaji lugha na ufafanue sababu ya shughuli hiyo

    Date posted: May 14, 2019.  Answers (1)

  • Eleza dhima mbili ya kiimbo(Solved)

    Dhima ya kiimbo

    Date posted: May 14, 2019.  Answers (1)

  • Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo mpitapo kwake mtampata(Solved)

    Ainisha vishazi katika sentensi ifuatayo mpitapo kwake mtampata.

    Date posted: May 14, 2019.  Answers (1)

  • Mambo yepi yanayoweza kusababisha kufa kwa lugha?(Solved)

    Mambo yepi yanayoweza kusababisha kufa kwa lugha?

    Date posted: May 14, 2019.  Answers (1)

  • Taja na ueleze dhima tano ambazo sajili za lugha hutekeleza(Solved)

    Dhima ambazo sajili za lugha hutekeleza

    Date posted: May 14, 2019.  Answers (1)

  • UFAHAMU Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali Ulimwengu unatakiwa kuzua mbinu za kulitatua tatizo la ufukara ambao ni kikwazo kikuu cha juhudi za maendeleo. Ufukara unayakabili mataifa mengi yanayoendelea...(Solved)

    UFAHAMU
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
    Ulimwengu unatakiwa kuzua mbinu za kulitatua tatizo la ufukara ambao ni
    kikwazo kikuu cha juhudi za maendeleo. Ufukara unayakabili mataifa mengi
    yanayoendelea na kuyatosa kwenye shida nyingi huku mataifa ya magharibi
    yakizidi kupiga hatua kubwa za kimaendeleo. Tofauti iliyopo kati ya mataifa
    yanayoendelea na yaliyoendelea inaendeiea kuongezeka kila siku.
    Miongoni mwa sababu zinazochangia katika ufukara huu ni pamoja na ufisadi,
    uongozi mbaya, turathi za kikoloni na uchumi unaotegemea kilimo ambacho
    hutegemea mvua isiyoweza kutabirika. Vilevile, mataifa yanayoendelea yana idadi
    kubwa ya watu inayoupiku uwezo wa mataifa husika. Pamoja na haya, mataifa
    haya hayana uwezo wa kuwakomboa raia wake kutoka katika lindi la umaskini
    huu unaokithiri. Ukosefu wa elimu na nafasi adimu za kazi huchangia pia katika
    tatizo hili. Ni wazi kuwa ufukara una athari hasi kote ulimwenguni. Aghalabu,
    ufukara huchipuza matendo mabaya. Ni rahisi kuwashawishi wananchi maskini
    kushiriki katika uhalifu iii kujinasua kutoka kwenye lindi la kimaskini. Udhaifu huu
    huweza kuzaa mbegu ya kuatika maovu ya kila aina ukiwemo ugaidi. Mataifa
    yaliyoendelea yanatakiwa kuyaburai madeni yanayoyadai mataifa yanayoendelea
    kama njia moja ya kupambana na ufukara. Mataifa haya maskini hutumia asilimia
    kubwa ya mapato ya kitaifa kuyalipia madeni haya. Hali hii imeyafanya mataifa
    haya kushindwa kujikwamua kutoka kwenye minyororo ya ufukara. Njia nyingine
    ya kuyasaidia mataifa haya ni kukubali kutoa ruzuku za kimaendeleo badala ya
    mikopo kwa nchi husika.
    Mataifa yanayoendelea nayo yanatakiwa kuchukua hatua katika kuwanusuru raia
    wake kutoka kwenye dhiki hii.Ni sharti yaibuke na mikakati kabambe ya
    kupambana na ufukara. Itakuwa na faida kubwa iwapo mataifa haya yataunda
    sera zinazotambua ufukara kama tatizo kuu linalozikabili na kuweka mikakati ya
    kuwaokoa raia wake kutoka kwenye tatizo hili. Pamoja na mikakati hii ni kuzalisha
    nafasi za kazi, kuimarisha miundo msingi,kuendeleza elimu inayolenga kutatua
    matatizo maalumu katika jamii na kupanua viwanda. Kuna pia haja ya viongozi
    kuwa waangalifu ili mfumo wa soko huru ambao unaendelezwa na mataifa
    yaliyoendelea usiishie kuwa chanzo cha kufa kwa viwanda asilia. Maamuzi yote ya
    sera za kiuchumi sharti yauzlngatie uhalisia wa maisha ya raia wa mataifa haya.
    (a) Eleza athari za madeni kwa nchi zinazoendelea.
    (b) Kwa nini umaskini unatawala mataifa yanayoendelea?
    (c) Mwandishi anatoa mapendekezo yapi kwa mataifa yanayoendelea katika
    kutatua tatizo la ufukara?
    (d) Mfumo wa soko huru una mathara gani kwa mataifa yanayoendelea?
    (e) Taja visawe vya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu.
    (i)Turathi za kikoloni
    (ii) Kuatika
    (iii) Kuyaburai

    Date posted: May 7, 2019.  Answers (1)

  • MUHTASARI (alama 15) Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. Taifa huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na wanaojitambua kisiasa kama watu walio na mwelekeo, maono na hatima...(Solved)

    MUHTASARI (alama 15)
    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
    Taifa huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na wanaojitambua kisiasa
    kama watu walio na mwelekeo, maono na hatima sawa. Utaifa hujengwa kwenye
    misingi ya mapenzi kwa nchi, Utambuzi wa cheo, eneo, hadhi, rangi na hata
    makabila wanakotoka raia wa taifa moja si chanzo cha kuwatanganisha. Nchi moja
    huweza kuundwa na watu walio na tofauti chungu nzima zikiwemo tofauti za
    kikabila, kitabaka na kimawazo. Hata hivyo, watu hao huwa na folsafa na imani
    sawa kama taifa inayoashiriwa hasa na wimbo wa taifa. Hata hivyo haya yotc
    hayawezi kuwafikia katika kiwango cha kuunda taifa. Uzalendo ndio mhimili
    mkuu wa utaifa. Uzalendo ni mapenzi aliyo nayo mtu kwa nchi yake. Mapenzi
    haya humwongoza mtu katika mawazo yake, itikadi yake, matendo yake,
    matamanio yake na mkabala wake kuhusu nchi na hatima ya nchi yake.
    Mzalendo hawezi kushiriki katika matendo yanayoweza kuiletea nchi yake
    maangamizo kwa vyovyote vile. Mzalendo huongozwa na mwenge wa wema.
    Mzalendo hawezi kushiriki kwenye shughuli zozote zinazohujumu mshikamano wa
    kitaifa. Yeye hatawaliwi na ubinafsi wa kutaka kufaidi nafsi yake naya jamii
    yake finyu. Matendo yake yote huongozwa na ari ya kuiboresha nchi yake.
    Anayeipenda nchi yake hujiepusha na ulafi wa kujilimbikizia mali. Yuko radhi
    kuhasirika mradi taifa lake linufaike.
    Utaifa ni mche aali unaopaliliwa kwa uzalendo, kuepuka uchu wa nafsi na taasubi
    hasi zikuwepo za kikabila na ubinafsi. Hali hii inapofikiwa, hatima ya taifa na
    mustakabali wa raia wake huwa wenye matumaini makubwa.
    (a) Kwa maneno 40 - 50 dondoa sifa kuu za utaifa.
    (b) Ni nini misingi ya kutathmini mzalendo? (maneno 60 - 70)

    Date posted: May 7, 2019.  Answers (1)

  • Tumia nomino yoyote katika ngeli ya I-I kutunga sentensi.(Solved)

    Tumia nomino yoyote katika ngeli ya I-I kutunga sentensi.

    Date posted: May 7, 2019.  Answers (1)

  • Tunga neno lenye muundo huu wa silabi: Irabu + konsonanti + konsonanti + irabu(Solved)

    Tunga neno lenye muundo huu wa silabi:
    Irabu + konsonanti + konsonanti + irabu

    Date posted: May 7, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi hii upya kwa kufuata maagizo: Wasichana wanaingia darasani kwa haraka (andika kinume chake)(Solved)

    Tunga sentensi hii upya kwa kufuata maagizo: Wasichana wanaingia darasani kwa haraka (andika kinume chake)

    Date posted: May 7, 2019.  Answers (1)

  • Tambua kiambishi awali na tamati kati neno: Alalaye(Solved)

    Tambua kiambishi awali na tamati kati neno: Alalaye

    Date posted: May 7, 2019.  Answers (1)

  • Ainisha vivumishi katika sentensi hii: mzee mwenyewe ni mkongwe na amepewa zawadi kwa kuwa shamba lake lilitoa mazao mengi.(Solved)

    Ainisha vivumishi katika sentensi hii: mzee mwenyewe ni mkongwe na amepewa zawadi kwa kuwa shamba lake lilitoa mazao mengi.

    Date posted: May 7, 2019.  Answers (1)

  • Askari wasipopiga doria wala kushikiana na raia hawatakuwa wametuhakikishia usalama. (yakinisha sentensi hii)(Solved)

    Askari wasipopiga doria wala kushikiana na raia hawatakuwa wametuhakikishia usalama. (yakinisha sentensi hii)

    Date posted: May 7, 2019.  Answers (1)