UFAHAMU Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali Binadamu kwa wakati huu amemaka kwa sababu amechafua mazingira yake pasipo tahadhari. Mathalani insiya amejaza gesi za sumu zitokazo viwandani na...

      

UFAHAMU
Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali
Binadamu kwa wakati huu amemaka kwa sababu amechafua mazingira yake pasipo
tahadhari. Mathalani insiya amejaza gesi za sumu zitokazo viwandani na hata kuchafua
mito kutokana na maji machafu kutoka viwanda hivyo. Takataka zinazotupwa ovyo
ovyo zinarundikana kila mahali. Isitoshe miti inakatwa vivyo hivyo bila simile. Matokeo
ya haya yote ni kwa mfano tunapata mvua ya asidi ambayo huhasiri mimea. Aidha nao
ukanda wa ozoni unaotukinga dhidi ya miali hatari kutoka kwa jua umeharibiwa tayari na
hivyo kuongeza joto duniani. Sehemu nyingi zimeanza kugeuka na kuwa jangwa huku
sehemu zingine zikifurika kwa maji ya mito na mvua. Maji haya yameanza kumeza
visiwa vingi vilivyo baharini. Kutokana na madhara haya, binadamu sasa anatapatapa ili
kutafuta makao kwingine kwenye salama. Ndiposa siku hizi nadhari za binadamu
zimeelekezwa katika mawanda mengine nje kabisa ya kisayari hiki kidogo kiitwacho
dunia.

Kwa miaka mingi sasa binadamu amekuwa akitafakari uwekano wa kuishi katika sayari
nyingine. Hii ndiyo sababu mwaka wa 1969 waamerika walimkanyagisha binadamu wa
kwanza kabisa mwezini. Lengo lilikuwa ni kutalii na kuchunguza uwekano wa binadamu
kuishi huko ili wale watakaoweza wahamie huko, hata mimea. Mwezini ni vumbi tupu
lisiloota chochote. Kipatikanacho kwa wingi sana ni madini tu ambayo hayawezi kufaidi
binadamu kwa lolote.

Sayari nyingine alizozitalii binadamu ni Zuhura, Mirihi, Mushtara na tuseme karibu zote
zinazolizunguka jua. Kilichogunduliwa ni kuwa upo uwezekano wa sayari kama Zuhura
na pengine Mirihi kuwa na mvua, lakini nyingi mno isiyoweza kuruhusus mimea kukua.
Sit u, zuhuria inasemekna kuwa joto sana wakati wa mchana ilhali Mirihi ni baridi sana
siku zote; baridi kiasi cha kuuwa binadamu na wanyama hawawezi kuishi huko.
Mushtara yasemekana kuwa joto ajabu, ambapo hizo sayari nyingine zina joto sana au
zina baridi sana. Habari hii imemfunga binadamu katika jela ya kijisayari chake kiki
hiki kiitwacho dunia anachokichafua uchao.

Je, binadamu amekata tama? Hata kidogo! Ndio mwanzo anajaribu sana kuzikata pingu
alizofunzwa na maumbile. Vipi? Amejaribu kuchunguza uwezekano wa kuihama ardhi
na kuishi baharini, kwa sababu bahari inazidi ardhi mara tatu kwa ukubwa. Na ni vipi
binadamu anadhani anaweza kuishi baharini mahali ambapo hakuumbwa aishi humo
kama samaki?
Jawabu ni kuwa angefanya hivyo kwa kutumia maarifa yake.

Binadamu anaamini kabisa kuwa ana uwezo wa kujenga miji mikubwa mikubwa humo
humo baharini… mikubwa zaidi yah ii tuliyo nayo ardhini. Anaamini ya kuwa anaweza kuitawala bahari kiasi alichitawala ardhi, na hivyo basi kufanya bahari impe
makao na kumlisha bila ya kuyabadilisha maumbile yake. Na iwapo hili halitawezekana
basi, ikiwajibika, abadilishe maumbile yake kwa kujiunda mashavu kwa mfano, ili avute
pumzi ndani ya maji

Njia ya pili ya kuepukana na pingu za maumbile ni kuishi angani. Hii ina maana ya
kujenga miji iliyoelea angani, kama madungu vile. Na kwa vile anga haina kikomo,
binadamu atakuwa amejipatia visayari vyake visivyo idadi ingani!

Njia ya tatu ni kubadilisha umbo lake ili asihasirike na joto wala baridi. Binadamu wa
kisasa anaamini kuwa inawezekana kumuunda upya mtu katika maabara badala ya katika
mamba.
Mtu huyu wa maabra, aitwaye ‘cyborg’ kwa lugha ya Kiingereza, anaweza kuwa na
chuma ndani badala ya mifupa, na mwili wa kawaida wa udongo na maji nje.

Kiunde huyu atakuwa hadhuriki ovyo ovyo kama binadamu wa sasa aliyeumbwa kwa
chumvi, maji na protini. Au bora zaidi, binadamu mpya wa maabarani aundwe kwa
zebaki. Binadamu huyu wa zebaki hafi wala hakatikikatiki. Na iwapo atakatika vipande
vipande, basi kama zebaki hivyo vitaundika tena upya na kumrudishia umbo la awali
kamili.

Njia nyingine ya kuepukana na uangamizi ni kutumia viunde vyake vya electroniki kama
vile tarakilishi yaani kompyuta, na mitambo mingine kama iyo. Binadamu anaamini
kwamba uwezo wa vyombo hivi utakapokamilishwa, basi vitamsaidia kwa lolote lile.

(a) Inasemekana kwamba binadamu anakichafua hiki kisayari chake kila uchao.
Kwa kutumia mifano mitatu, eleza vile binadamu amechafua mazingira yake.
(b) Kwa nini ongezeko la joto limeleta jangwa duniani wa wakati huo huo likaleta
mafuriko?
(c) Eleza sababu mbili zinazomfanya binadamu kuhangaika na kutafuta makao
kwingine
(d) Ni mambo gani yanayomfunga binadamu katika ardhi. Taja mawili
(e) Unadhani ni kwa nini madini mengi yaliyoko mwezini hayaletwi duniani.
Taja na ufafanue sababu mbili
(f) Kulingana na aya mbili za mwisho, eleza jambo ambalo binadamu anajaribu
kukwepa
(g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu
(i) Mashavu
(ii) Madungu
(iii) Asihasirike
(iv) Kiunde

  

Answers


Kavungya
a) Gesi hatari kutoka viwandani
Moshi kutoka viwandani
Utupaji ovyo ovyowa takataka
b) - Miji ikishakatwa mizizi iliyshikilia udongo haiku tena hivyo
kukinyesha maji yanateremka ovyoovyo.
- Maji ya bahari yakipata joto inapanuka na kufukika yenyewe
- Maji yakipata joto mvuke unakuwa mwingi na mawingi mazito ya
yanaleta mvua nyingin ya ghafla.
- Miti ikikatwa joto linaleta majagwa.
c) Ongezeko la watu duniani
Amechafua mazingira yake
d) Kugundua kuwa mwezini hakuna hewa ama mvua
kuwa sayari nyingine mf. Mirihi zina mvua lakini ni nyingi zaidi
Kuwa sayari nyingine zina jota zaidi na nyingine zina baridi zaidi
e. Hakuna hewa huko ambayo wachimbaji wangevuta wakichimba
Ni ghali kama kupekeka watu na mitambo ya kuchimbia madini hayo
f. Mauti kwa kujaribu kuunda kiunde cha zebaki na pia kutumia viumbe vya
elektroniki au kompyuta
g Mashavu – viungo vy samaki vya kuvutia hewa
Madungu Makao yanayolea angani/viota vya ndege
Asihasirike - Asidhurike/asipate madhara
Kiunde - Kitu kilichoundwa na binadamu
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 07:39


Next: Mtu akicheza mchezo mahali Fulani tunaweza kusema alichezea hapo Ukifuata mfano huu, tumia vitenzi vilivyoko katika mabao kukamilisha (i) Ali hapo (la) (ii) Ali hapo (fa) (iii) Ali hapo...
Previous: Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali Vijana wengi wake kwa waume, walikuwa ndio tu wakamilishe shughuli ya kusajiliwa chuoni. Walikuwa bado nadhari zao zimetekwa na ugeni, hawajapata starehe...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Mtu akicheza mchezo mahali Fulani tunaweza kusema alichezea hapo Ukifuata mfano huu, tumia vitenzi vilivyoko katika mabao kukamilisha (i) Ali hapo (la) (ii) Ali hapo (fa) (iii) Ali hapo...(Solved)

    Mtu akicheza mchezo mahali Fulani tunaweza kusema alichezea hapo
    Ukifuata mfano huu, tumia vitenzi vilivyoko katika mabao kukamilisha
    (i) Ali hapo (la)
    (ii) Ali hapo (fa)
    (iii) Ali hapo (oa)

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza matumizi ya ‘Po’ katika sentensi hii Nilipofika nilimwona pale alipokuwa amesimama(Solved)

    Eleza matumizi ya ‘Po’ katika sentensi hii
    Nilipofika nilimwona pale alipokuwa amesimama

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika katika msemo wa taarifa “Nitakuwa nikija hapa kila siku kukuona”, Kamau alimwambia shangazi yake(Solved)

    Andika katika msemo wa taarifa
    “Nitakuwa nikija hapa kila siku kukuona”, Kamau alimwambia shangazi
    yake

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika katika msemo halisi Mvulana alimwambia baba yake kuwa alitaka kwenda sokoni(Solved)

    Andika katika msemo halisi
    Mvulana alimwambia baba yake kuwa alitaka kwenda sokoni

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Kutokana na vitenzi tunaweza kuunda majina na pia kutokana na majina tunaweza kuunda vitenzi. Mfano Jina ...(Solved)

    Kutokana na vitenzi tunaweza kuunda majina na pia kutokana na majina
    tunaweza kuunda vitenzi. Mfano
    Jina Kitendo
    Mwuzaji Uza
    Mauzo Uza
    Wimbo Imba

    Sasa kamilisha:
    Jina Kitenzi
    (i) Mnanda
    (ii) Kikomo
    (iii) Ruhusa
    (iv) ashiki
    (v) husudu

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunasema: Mtoto huyu mzuri anapendeza Ukitumia majina yafuatayo kamilisha sentensi ukifuata mfano ulio hapo juu (i) Ngome (ii) Mitume (iii) Heshima (iv) Ng’ombe (v) Vilema(Solved)

    Tunasema: Mtoto huyu mzuri anapendeza
    Ukitumia majina yafuatayo kamilisha sentensi ukifuata mfano ulio hapo juu
    (i) Ngome
    (ii) Mitume
    (iii) Heshima
    (iv) Ng’ombe
    (v) Vilema

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza kazi ifanywayo na (i) Mhariri (ii) Jasusi(Solved)

    Eleza kazi ifanywayo na
    (i) Mhariri
    (ii) Jasusi

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Akifisha kifungu kifuatacho Bwana mwenyekiti wetu wa leo wazazi wote na hata wanafunzi leo ni siku muhimu je mngependa niwafahamishe msaada tuliopokea kutoka kwa wizara ya elimu(Solved)

    Akifisha kifungu kifuatacho
    Bwana mwenyekiti wetu wa leo wazazi wote na hata wanafunzi leo ni siku
    muhimu je mngependa niwafahamishe msaada tuliopokea kutoka kwa wizara ya
    elimu

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Fafanua maana za misemo ifuatayo kwa kuitungia sentensi (i) Kula uyundo (ii) Kula uhondo(Solved)

    Fafanua maana za misemo ifuatayo kwa kuitungia sentensi
    (i) Kula uyundo
    (ii) Kula uhondo

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi zifuatazo ukitumia kinyume cha neno lililoandikwa kwa herufi za Mlazo (i) Usijaribu kupaaza sauti unapoimba (ii) Huyu ni mtu mwenye busara (iii) Binadamu hawezi kumuumbua mwenzake(Solved)

    Andika sentensi zifuatazo ukitumia kinyume cha neno lililoandikwa kwa herufi za
    Mlazo
    (i) Usijaribu kupaaza sauti unapoimba
    (ii) Huyu ni mtu mwenye busara
    (iii) Binadamu hawezi kumuumbua mwenzake

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya sentensi hizi (i) Mikono yao imeshikana (ii) Mikono yao imeshikamana(Solved)

    Eleza maana ya sentensi hizi
    (i) Mikono yao imeshikana
    (ii) Mikono yao imeshikamana

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Sahihisha makosa yaliyomo katika sentensi mbili zifuatazo (i) Bei za vitu zimepanda juu sana siku hizi (ii) Weka mizigo kwa gari(Solved)

    Sahihisha makosa yaliyomo katika sentensi mbili zifuatazo
    (i) Bei za vitu zimepanda juu sana siku hizi
    (ii) Weka mizigo kwa gari

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali Mababu walituachia msemo maarufu kuwa “ Kuzaa sio kazi. Kazi kubwa ni kulea.” Busara iliyomo katika methali hii inatupambazukia peupe pindi...(Solved)

    Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali
    Mababu walituachia msemo maarufu kuwa “ Kuzaa sio kazi. Kazi kubwa ni kulea.”
    Busara iliyomo katika methali hii inatupambazukia peupe pindi tukianza kuchunguza
    maisha ya vijana wa siku hizi katika jamii zote, hasa zile za Afrika. Kwa upande
    mmoja, maisha ya vijana hawa yanaonyesha cheche ya matumaini kwa maisha ya siku
    za usoni kwa sifa zao za mori na kupenda kujaribu na kushika mambo upesi kama
    sumaku. Lakini kwa upande wa pili, tunashuhudia upotevu wa kimawazo na hulka
    ambayo ndiyo kipingamizi cha kuendelea kwao kama raia wa kutegemewa.

    Kuwanyeshea vijana lawama na kashifa za kila aina hakufai wala hakufui dafu katika
    juhudi za kuwaongoza na kuwalea. Kwa hili hatuna budi kusadiki, “mtoto umleavyo
    ndivyo akuavyo.” Basi hivyo badala ya kuwashambulia vijana wenyewe. Tutafanya
    hivyo kwa imani kuwa “mwiba uchomeako ndiko utokeako.” Kiini cha matatizo ya
    vijana wa leo ni namna ya mwongozo na vielezo wanavyopokea kutoka kwa wazazi,
    waalimu, viongozi wa kijamii wakiwemo pia wale wa medhehebu tofauti na hasa kutokana na vyombo tofauti vya habari: vitabu majarida, filamu, magazeti na
    kadhalika.

    Jamii ina haki gani kuwashtumu vijana iwapo mzazi, tangu utotoni mwao
    amewahubiria maji na huku mwenyewe anakunywa mvinyo? Kama fasihi na
    maandishi mengine wanayoyabugia vijana yamejazwa amali, picha, jazanda na taswira
    zinazohimidi ugeni na kutweza Uafrika, tutashangazwa na nini pale vijana
    watakapoanza kupania zile zile amali za ugenini? Iwapo jamii na mazingira
    wanamokulia vijana yanatukuza kitu kuliko utu. Hatupaswi kupepesa macho na
    kukonyeza tunapowaona vijana wakihalifu sheria zote kwa tamaa ya kujinufaisha binafsi.

    Ni hoja isiyopingika kuwa kulea sio tu kulisha na kuvisha au kumpeleka mtoto
    shuleni sharti itambulike wazi wazi kuwa sehemu kubwa ya elimu na mwongozo
    unaoathiri mienendo ya jijana na watoto haitokani na yale waambiwayo bali hasa yote
    wanaoyashuhudia kwa macho na hisia zao.

    (a) Katika aya ya kwanza, maisha ya vijana wa kisasa yameelezwaje?
    (b) Kwa nini vijana hawapaswi kulaumiwa kulingana na mwandishi
    Maneno 30 – 35
    (c) Eleza sifa za malezi bora
    (Maneno 20 – 25)

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo Kisha Ujibu Maswali Zamani sana na hata hivi karibu watu wengi kote duniani walikuwa wakiamini kuwa kuna ardhi na mbingu tu basi. Imani hii...(Solved)

    Soma makala yafuatayo Kisha Ujibu Maswali
    Zamani sana na hata hivi karibu watu wengi kote duniani walikuwa wakiamini kuwa
    kuna ardhi na mbingu tu basi. Imani hii ilijikita katika mantiki inayosema kwamba
    ardhi au dunia ipo katikati ya maumbile yote na isitoshe, ni tambarare.

    Juu ya ardhi ni mbingu ambayo imejaa vimulimuli vidogovidogo sana viitwavyo nyota.
    Baina ya vimulimuli vipo viwili vikubwa viitwavyo mwezi na jua. Hivi viwili japo ni
    vikubwa kuliko vingine, bado ni vidogo kuliko ardhi.

    Hii ndiyo imani iliyoutawala ulimwengu kwa miaka na miaka, na ikawa imekita mizizi.
    Lakini jinsi wanajimu walivyozidi kuelimika, waligundua kwamba ukweli wa mambo
    umejitenga kando kabisa na imani hii

    Ukweli ni kwamba zima tulionalo la rangi ya samawati nusumviringo juu ya paa zetu za
    vichwa ni kubwa sana tena. Na si kubwa tu bali lazidi kupanuka. Katika bwaka hili
    lipanukalo kila uchao mna galaksi nyingi ajabu zisizokadirika. Ndani ya kila galaksi
    mna nyota mamilioni na mamilioni, malaki na kanui. Imejulikana kuwa nyota hizo japo
    huonekana kama vimulimuli vidogo sana usiku usiku ni kubwa ajabu. Kadiria
    mwenyewe! Jua letu ni nyota kubwa sana. Ukubwa wake umezidi wa dunia mara
    nyingi sana, zaidi ya elfu moja! Basi fikiria juu ya ukubwa wote huo. Imegunduliwa ya
    kwamba jua ni nyota ndogo sana ikilinganishwa na zingine zilizo katika galaksi yetu tu,
    licha ya galaksi nyinginezo zilizoko katika bwaka.

    Na haya sio maajabu peke yake. Wataalam wamevumbua mengi ya kushangaza zaidi.
    Mathalan, imekuja kufahamika kuwa jua letu ambalo ni nyota, lina sayari tisa
    zinazolizunguka. Baadhi ya sayari hizi ni Arthi yetu. Zaibaki, Zuhura, Mirihi, na mshitara
    baina ya tisa jumla. Baadhi ya sayari hizi zina visayari vidogo vinavyozizunguka.
    Visayari hivi ndivyo viitwavyo miezi. Ardhi yetu ina mwezi miwili ilhali Mshitara ina
    kumi na miwili! Sayari hizi zote na visayari vyao, au vitoto ukipenda, havitoi mwanga.
    Nuru ya mwezi na nuru ya hizo sayari zinazolizunguka jua letu inatokana na jua
    lenyewe. Kwa hakika ni mmeremeto tu unaotufikia sisi kupitia sayari hizi kutoka kwa
    nyota hii yetu iitwayo JUA.

    Kama wasemavyo washahili ya Mungu ni mengi. Taswira tuliyo nayo katika maelezo
    haya yaonyesha jinsi ambavyo mwanadamu licha ya kuwa na akili nyingi, bado
    hajawahi kuigusia siri kamili ya mungu. Lakini kwa ufupi twaweza kusema hivi. Ikiwa
    katika bwaka lote kuna galaksi nyingi, bila shaka kwa vile jua ni nyota basi zimo sayari
    nyingi ajabu zinazozunguka kila nyota au jua kama zipasavyo kuitwa. Kwa vile katika
    mfumo- jua imo sayari moja yenye viumbe vyenye uhai, binadamu wakiwemo, basi
    bila shaka katika mifumo- jua mingine katika galaksi yetu zipo sayari zinazofanana na ardhi hii yetu, ambazo sina viumbe vilivyo hai- penginepo watu pia! Wanona maajabu?
    Na katika magalaksi mengine je? Mambo pengine ni yayo hayo! Kwa hivyo huenda
    ikawa peke yetu katika bwaka hili; labda tuna viumbe wenzetu ambao hatutakutana nao
    katika uhai wetu kwa sababu uwezo wetu wa kimaumbile, na vile kisayansi ni hatifu.
    Lakini, kwa vile mwenye kupanga maajabu hayo yote, yaani Mwenyezi Mungu ni
    huyo mmoja basi huenda sote tukakutana Ahera.
    Mungu ni mkubwa

    (a) Kulingana na habari hii, taja mambo manne ambayo ni imani potovu
    (b) Kwa kusema “ ukweli wa mambo umejitenga kando” Mwandishi anamaanisha
    nini?
    (c) Taja sifa zozote nne za maumbile ya anga zinazopatikana katika habari hii
    (d) Taja vitu viwili vipatikanavyo katika galaksi
    (e) Taja sayari mbili ambazo ni kubwa kuliko ardhi
    (f) Ni ithibati gani iliyotolewa kuonyesha kuwa nyota sio vijataa vidogo?
    (g) Bainisha nuru aina mbili tuzionazo angani
    (h) (i) Ni neno gani lenye maana sawa na “anga” ama “upeo” katika habari hii?
    (ii) Andika neno moja ambalo lina maana sawa na paa kama lilivyotumiwa
    katika taarifa
    (i) Mwandishi anaposema kuwa katika magalaksi mengine “mambo pengine ni yayo
    hayo” anamaanisha nii?

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Akifisha kifungu kifuatacho “Baba Wafua, ona Barua iliyotoka kwa mwanao. Hata hati haisomeki” “lo” baba watoto akamaka. Hii barua kweli imetoka kwa mwanangu Wafua. “Waniuliza mimi?” Mama akamjibu...(Solved)

    Akifisha kifungu kifuatacho
    “Baba Wafua, ona Barua iliyotoka kwa mwanao. Hata hati haisomeki” “lo” baba
    watoto akamaka. Hii barua kweli imetoka kwa mwanangu Wafua. “Waniuliza
    mimi?” Mama akamjibu “Tazama maandishi na anwani basi. Shule ya Msingi ya
    Barungani S.L.P 128 Vuga.”

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Ili kupiga vita propaganda za wakoloni mambo leo katika vyuo vikuu vyetu, inafaa kutumia Kiswahili kufundisha masomo yote. Jambo hili ni...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
    Ili kupiga vita propaganda za wakoloni mambo leo katika vyuo vikuu vyetu, inafaa
    kutumia Kiswahili kufundisha masomo yote. Jambo hili ni la lazima na linawezekana
    kabisa, ingawa lina matatizo yake. Jambo linalotakiwa kufanya ni kuchukua
    wananchi wenye elimu ya juu wakatafsiri fikra za wazalendo katika Kiswahili. Kwa njia
    hiyo, lugha ya wanachuo itakuwa ndiyo lugha ile ile ya umma

    Ni jambo la kuepukwa kuwa na lugha mbili ambazo zinasaidia kuwatenga na umma.
    Wasomi wetu watakuwa wamekaribia umma kwa kutumia lugha iliyozoeleka na umma
    wenyewe. Jambo linalotutinga ni hili: mara nyingi wasomi wengine waliozoea
    kutakadamu lugha ya Kiingereza wanapojaribu kuwaeleza watu wengine jambo la
    kieleimu au kitaalamu, hushindwa kabisa. Wao huchanganya sana maneno ya
    Kiingereza na Kishwahili hata kufikia kiasi ambacho mtu wa kawaida haelewi
    chochote.

    Kwa kuwa wakoloni mamboleo wameelewa kwamba lugha ni kioo cha kuchujia
    utamaduni, miaka ya hivi karibuni wamejifunza kwa dhati kuliko wakati mwingine
    kupigania ufundishaji wa lugha zao, hususa, Kifaransi na Kiingereza. Wakati huo wao
    wanatoa porojo kuwa kugha ya Kiswahili haifai na kwamba ni lugha ya watumwa.
    Kwa mfano, utaona katika maandishi mngi kila wanapoorodhesha lugha kuu za dunia.
    Kiswahili hakionyeshwi katika hizo.

    Badala yake wanakiweka kwenye kiwango sawa na Kiganda, Kikikuyu, Kinyamwezi
    na lugha kadha wa kadha za kikabila. Hiyo ni harakati kubwa ya kudanganya umma
    na kukivua Kiswahili hadhi yake ilhali lugha hii inatumiwa na zaidi ya watu milioni
    mia moja wanaosambaa katika sehemu mbalimbali za ulimwengu. Kwa kutumia hila hii,
    wao wanasadikisha watu wengi ili wachukulie Kiswahili kama lugha nyimgine ya
    kikabila. Ndiposa hawa wakoloni mamboleo wanawashawisha baadhi ya watumiaji wa
    Kiswahili wastawishe lugha za makabila mabalimbali na kuonyesha kwamba
    umaarufu wa lugha hizo ni sawa na Kiswahili. Hayo bila shaka ni mawazo. Ukweli
    ulioko ni kwamba mawazo kama haya yawezi keundeleza ukabila. Hata hivyo sharti
    kueleweka kwamba kusema hivyo si kudhalilisha umuhimu wa kukuza lugha za
    kikabila. Tusemacho ni kuwa ukuzaji wa lugha hizo ungekuwa na kusidi moja kuu
    ambalo ni kustawisha Kiswahili kufika ngazi za kimataifa.

    Swali ambalo ni muhimu kujiuliza ni hili: Wakoloni - mamboleo wanatuonaje
    tunapokazania Kiswahili? Je, wanaona ni faida kwao au kwetu? Jambo muhimu zaidi
    ni kutamba jinsi Kiswahili kinavyotuwezesha kuungana na kuwa kitu kimoja. Ni dhahiri
    kwamba wakoloni mamboleo hawafurahili wanapoona kishahili kikituunganisha.
    Machoni mwao Kiswahili ni ishara mojawapo ya kujikomboa kwetu kutokana na
    minyororo yao. Hivi si kusema kwamba hapupaswi kujifunza kiingereza, Kifaranza au
    Kijerumani, la hasha. Tunachosema ni kwamba tutumie Kiswahili ambacho ni kioo
    cha utamaduni wetu.

    (a) Mwandishi amesema nini kuhusu utengano kati ya umma wa wasomi?
    ( Maneno 30 – 40)
    (b) Eleza pingamizi zilizowekwa na wakoloni- mamboleo ili kudunisha
    Kiswahili (maneno 40 – 50)
    (c) Kulingana na mwandishi ni sababu gani zinazofanya wakoloni mamboleo
    kupinga maendeleo ya Kiswahili?

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma Makala yatuatayo kisha ujibu maswali Ama kweli maisha ya vijana wa kisasa yanatofautiana na kuhitilafiana pakubwa na yale ya wazee wao. Sio katika mavazi, lugha, mienendo,...(Solved)

    Soma Makala yatuatayo kisha ujibu maswali
    Ama kweli maisha ya vijana wa kisasa yanatofautiana na kuhitilafiana pakubwa na yale
    ya wazee wao. Sio katika mavazi, lugha, mienendo, mitazamo, mawazo tu bali pia katika
    kipengele kingine chochote utakachofikiria. Yote haya ni vielezo vya jinsi kizazi cha leo
    kinavyoishi katika ulimwengu ambao ni kivuli tu cha ule wa vizazi vilivyotangulia.
    Baadhi ya watu wameieleza hali hii kuwa maisha sio jiwe. Kwao basi, si ajabu katu
    kuwaona vijana wakizungumza lugha yao ya kipekee au wakivaa nguo zinazobana
    ajabu na kudhirisha bayana maungo yao badala ya kuyasitiri.

    Hata hivyo, watu wengi wameonelea kwamba hali ya maisha ya vijana wa leo maasia
    yanayotokana na utundu na hata ukatili wao. Upande huu umetoa rai kwamba kizazi
    hiki kisingepotoka kama tu kingezingatia na kustahi utamaduni wa wahenga wao
    ambamo wazazi wao ndimo walimokulia. Wanazidi kufafanua kuwa nyendo hizi za
    miaka ya nyuma zilithamini sana amali kama waminifu, heshima kwa wazee ama
    wakuu, bidii, ushirikiano, ukarimu, unyenyekevu, hadhari katika kila jambo, utiifu na pia
    kujitegemea. Yote haya yamesahaulika ama tuseme yamepuuzwa katika utamaduni wa
    kisasa.”

    Swali lilozuka sasa ni je tunapaswa kuwahukumu vijana wa leo kwa kutumia vigezo au
    masharti gani? Tuwapige darubini kwa kutegemea hali ilivyo hivi leo duniani ama
    tuwapime kwa mujibu wa jinsi maisha ya baba na babu zao yalivyokuwa. Jibu la swali
    hili ni gumu na sharti lifafanuliwe kwa makini lisije likaegemea upande wowote.

    Mathalan, ni jambo lisilopingika kuwa maisha ni utaratibu unaothirika na hivyo
    kubadilika daima. Angalia kwa mfano jinsi maendeleo ya elimu, sayansi, mawasiliano
    na hata ufundi yalivyoyageuza maisha siku hizi. Yamkini vijana wa barani Afrika
    wakaona na hata kuzungumza wa wenzao kutoka Uropa, Asia na Marekani bila hata
    kunyanyuka hapa kwao nyumbani. Athari ya filamu, video, vitabu, magazeti, majarida
    n.k haikadiriki. Haya kwa kiasi yamewafanya vijana hata kupevuka kabla ya wakati
    wao. Isitoshe, mambo haya yameweza kuwazuzua na kuwaaminisha kuwa yale
    wanayojifunza ni kweli. Matokeo yamekuwa ni wao kuudunisha utamaduni wao wa
    asili na kuupapia ule wa wageni waliowaathiri. Tusisahau kuwa ujana ni tembo la
    mnazi na rahisi kwao kubadili mawazo.

    Lakini hatuwezi kuwasamehe vijana wanaokosa akili razini kwa kupotoshwa na
    kuchacharika na yote, wanayoyapokea kutokea ugenini na hivyo kuanza kudhalilisha
    utamaduni wa Waafrika. Hata hivyo, badala ya kuwakashifu wanapopotea njia
    amakuwapongeza wanapotenda yale tunayoyategemea tu, ni wajibu mkubwa wa
    wazazi kuwaongoza na kuwasaidia vijana kuwa na uwezo mkubwa na kufanya uteuzi
    mwafaka katika maisha yao.
    Maswali

    (a) Kulingana na mwandishi, kundi linalodai kuwa maisha sio jiwe’ lina maoni
    gani?
    (b) Kulingana na taarifa uliyoisoma ni jinsi gani vijana wa kisasa wangeziepuka
    athari mbaya?
    (c) Kwa mujibu wa taarifa hii, utamaduni wa Kiafrika una manufaa. Yataje
    (d) Mwandishi anaposema mambo haya yameweza kuwazuzua na
    kuwaaminisha vijana kuwa yale wanayojifunza ni kweli anamaanisha nini?
    (e) Mbali na wazazi, ni makundi gani mengine ya watu ambayo yanapaswa
    kutoa mawaidha kwa vijana?
    (f) Kwa maoni yako vijana wanapaswa kufanya uteuzi wa namna gani katika
    mvutano huu wa tamaduni?
    (g) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika makala
    (i) Maasia
    (ii) Razini
    (h) Andika methali moja ambayo inaafiki taarifa hii

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika kwa udogo ;ndege mkubwa alitua dirishani(Solved)

    Andika kwa udogo ;ndege mkubwa alitua dirishani.

    Date posted: June 15, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya kiimbo na onyesha dhima yake(Solved)

    Eleza maana ya kiimbo na onyesha dhima yake.

    Date posted: June 9, 2019.  Answers (1)

  • Taja aina mbili za ala(Solved)

    Taja aina mbili za ala

    Date posted: June 9, 2019.  Answers (1)