a) Kutumbisha
Sayansi ya kutumbisha
Sayansi mpya
Sayansi ya kutumbisha na matokeo yake
Sayansi ya kutumbisha
Sayansi ya ‘Clong’
Tamaa ya kutumbisha
Ajabu katika uzalishaji
Uzalishaji mpya
Tama ya kutumbisha
b) Njaa
-Upungufu wa ardhi
-Kupigania mashamba
c) Wangali wanafanyiwa utafiti
Hawajui ni madhara gani yanayoweza kuletwe nao/kivao
Hawana uhakika kama wanaweza kuishi nje ya maabara
Sheria haiwaruhusu wanasayansi kuwatoa nje “Yoyote
d) Jinsi binadamu anavyoendelea kufanya utafiti ili ajiondolee unyama ndivyo
anavyojijuta katka maafa au utafiti ukikithiri utaleta maafa.
‘Akijieleza sawasawa
Aliyeshughulikia upande mmoja
e) - Aliyetumbishwa aweza kuwa mweledi zaidi ya binadamu wa kawaida na
kuwatatiza
- Aliyetumbishwa aweza kuwa na uwezo mdogo wa kiakili na hivyo kuwa
mzigo kwa wale wa kawaida
- Ni kuharibu msingi wa jamii
- Aliyetumbishwa si binadamu halisi
- NI kuharibu taasisi za maisha-Utamaduni, itikadi, ndoa, lugha na
kadhalika
- Kutakuwa na maumbile sawa ya watu au kutatokea ukosefu wa maumbile
tofauti.
f) Matumizi mabaya ya ujuzi ule
Mweledi atatumbisha watu wasio wa kawaida
Mweledi aweza kuangamiza ulimwengu huu na kuutawala ulimwengu mpya wote
Kitakuwa na msongamano wa watu duniani
Ukosefu wa huduma muhimu za jamii
g) Watoto hao wanaweza kuwa weledi aidi
Wanaweza kuwa na uwezo mdogo kiakili
Wenti wao watakuwa mayatima
Watarithi kasoro za mwili au magonjwa yasiyo na tiba au yanayo ambukiza na
Kuangamiza binadamu wa kawaida.
Kuwepo kwa uhuru wa kutumbisha mayai ya wafu’
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 08:08
- Bila kunyambua, andika maneno mawili ambayo yanatokana na shina
moja na neno: imani(Solved)
Bila kunyambua, andika maneno mawili ambayo yanatokana na shina
moja na neno: imani
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Tunga sentensi ya neno moja ambayo ina visehemu vifuatavyo vya
sarufi
- Kiima
- Wakati
- Kirejeleo
- Kiswahili kitendwa
- Kitenzi(Solved)
Tunga sentensi ya neno moja ambayo ina visehemu vifuatavyo vya
sarufi
- Kiima
- Wakati
- Kirejeleo
- Kiswahili kitendwa
- Kitenzi
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Mahali palipohamwa panaitwa?(Solved)
Mahali palipohamwa panaitwa?
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Eleza maana mbili mbili zinazotokana na sentensi zifuatazo
(i) Mtoto alitimua mbio, kuona nyoka
(ii) Juma alifagia chakula
(iii) Sisikii vizuri(Solved)
Eleza maana mbili mbili zinazotokana na sentensi zifuatazo
(i) Mtoto alitimua mbio, kuona nyoka
(ii) Juma alifagia chakula
(iii) Sisikii vizuri
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Andika methali nyingine ambayo maana yake ni kinyume cha
Riziki kama ajali huitambui ijapo(Solved)
Andika methali nyingine ambayo maana yake ni kinyume cha
Riziki kama ajali huitambui ijapo
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Eleza maana ya misemo ifuatayo kwa kuitungia sentensi moja moja
Kuramba kisogo
Kuzunguka mbuyu(Solved)
Eleza maana ya misemo ifuatayo kwa kuitungia sentensi moja moja
Kuramba kisogo
Kuzunguka mbuyu
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Bila kubadilisha maana, andika sentensi zifuatazo ukitumia kirejeleo cha ngeli
kifaacho
(i) Nyumbu alishinda farasi kukimbia
(ii) Milango yote yajifunga ovyo, nenda uakafunge
(iii) Hamisi amekata nyasi vizuri...(Solved)
Bila kubadilisha maana, andika sentensi zifuatazo ukitumia kirejeleo cha ngeli
kifaacho
(i) Nyumbu alishinda farasi kukimbia
(ii) Milango yote yajifunga ovyo, nenda uakafunge
(iii) Hamisi amekata nyasi vizuri
(iv) Jiwe lile liliangukia matunda
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Sahihisha bila kubadilisha maana:
(i) Usikuje hapa kwetu kwani sitakuwamo
(ii) Basi la shule imeharibika moshi nyingi inatokea dirishani na maji
inatiririka ovyo(Solved)
Sahihisha bila kubadilisha maana:
(i) Usikuje hapa kwetu kwani sitakuwamo
(ii) Basi la shule imeharibika moshi nyingi inatokea dirishani na maji
inatiririka ovyo
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Andika katika kauli ya kutendesha
(i) Nataka upike chakula hiki vizuri
(ii) Toa ushuru wa forodhani(Solved)
Andika katika kauli ya kutendesha
(i) Nataka upike chakula hiki vizuri
(ii) Toa ushuru wa forodhani
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Badilisha katika udogo kasha uukanushe udogo huo
(i) Guu lake limepona baada ya kuumwa na jibwa la jijini
(ii) Nyumba yenyewe ilijengwa bondeni karibu na mto(Solved)
Badilisha katika udogo kasha uukanushe udogo huo
(i) Guu lake limepona baada ya kuumwa na jibwa la jijini
(ii) Nyumba yenyewe ilijengwa bondeni karibu na mto
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Andika katika msemo wa taarifa
Mzazi: Kesho nataka ufike nyumbani mapema, unasikia?
Mtoto: Nitajaribu, lakini mwalimu alisema tutafanya mtihani jioni(Solved)
Andika katika msemo wa taarifa
Mzazi: Kesho nataka ufike nyumbani mapema, unasikia?
Mtoto: Nitajaribu, lakini mwalimu alisema tutafanya mtihani jioni
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali
Vijana wengi wake kwa waume, walikuwa ndio tu wakamilishe shughuli ya
kusajiliwa chuoni. Walikuwa bado nadhari zao zimetekwa na ugeni, hawajapata
starehe...(Solved)
Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali
Vijana wengi wake kwa waume, walikuwa ndio tu wakamilishe shughuli ya
kusajiliwa chuoni. Walikuwa bado nadhari zao zimetekwa na ugeni, hawajapata
starehe akilini mwao wala kujisikia wamekaribia kama kwao nyumbani. Kwa hakika
mazingira yale mapya yalikuwa yanawapa kiwewe kidogo au tuseme hata woga kiasi.
Kusema kweli, kwa wakati ule walikuwa hawajui ni maisha ya namna gani
yanayowasubiri mahali pale. Hawakuweza kukadiria kwa uyakinifu wowowtw iwapo
makaazi yao pale ya miaka mine mizama kuanzia wakati ule, yangekuwa ya utulivu
na raha au pengine yangeondokea kuwa ya roho juu juu na matatizo chungu mzima.
Wamsubiri mkuu wa Chuo aingie wamsikize atakalosema, kisha ndipo waweze
kubashiri vyema mkondo wa maisha yao utakavyokuwa. Lakini jinsi walivyosubiri
Mkuu wa chuo aingie ukumbini ndivyo wayo wayo lao lilivyozidi kuwacheza shere.
Waliwaza: Ugeni jamani kweli ni taabu. Mawazo mengi yaliwapitia bongoni mwao.
Wakawa kinywa ukumbi mzima, kama kwamba wamekuja mazishini badala ya kuja
kusoma. Waliwaza na kuwazua. Waliona au pengine walidhani kuwa hapa kila kitu
ni tofauti.
Wanafunzi hawa waliona tofauti nyingi kati ya mambo pale chuoni na yale
waliyokuwa wameyazoea. Kwa mfano, mwalimu mkuu hapa hakuitwa ‘ headmaster’
kama kule katika shule za msingi na vile shule za upili aliitwa ‘ vice – chancellor’
Nyumba za kulala hazikuitwa ‘dormitory’ au ‘mabweni’, kama walivyozoea, bali
ziliitwa ‘ halls’ kwa sababu sio kumbi za aina yoyote ile, bali ni nyumba hasa, zenye
vyumba vya kulala, kama walivyozoea kita walipokiwa shule zao za upili huko, bali
hapa wenyewe wenyeji waliita kwa majina mengine kabisa! Mara University, mara
zutafindaki, mara Ndaki kwa ufupi, mara Jamahiri ya na kadhalika na kadhalika!
Waliwaza: kweli mahali hapa wenyewe wenyeji waliita kwa majina mengine kabisa!
Mara kumzubaisha mtu hadi kufikia kiwango cha kuonekana kama zuzu! Hata hivyo
hawakuvunjika moyo, bali walipiga moyo konde wakanena kimoyomoyo: Potelea
mbali! Ukiyavulia nguo, yaoge! Walikuwa wamo katika hali ya kurandaranda katika
ulimwengu wa mawazo pale katika ulimwengu wao mpya, ulimwengu mwingine
kabisa usioafanana hata chembe na ule waliouzoea, mkuu wa chuo alipoingia.
Kuingia mkuu wa chuo wote walisimama kwa pamoja na kwa mijiko, wamekauka
kama askari katika gwaride. Kuona hivyo, mkuu wa chuo akwaashiria wakae tu, bila
kujisumbua. Kicheko kikawatoka bila kukosa adabu na heshima, kasha wakakaa kwa
makini ndio mwanzo wakajisikia wamepoa.
Kuona kuwa sasa wametulia na wamestarehe. Mkuu wa chuo akaanza kwa
kuwaamkua kisha akawajulisha kwa wakuu wote wa vitivo mbali mbali na idara
mbali mbali waliokuwa wamekaa pale jukwani alipo yeye upande huu na huu.
Kufikia hapo, alaka ikawa imeungwa baina ya wenyeji na wageni wao. Kila mtu
akaona mambo yamesibu tena; huo bila shaka ni mwanzo mwema, na kama
ilivyosemwa na wenye busara, siku njema huonekana asubuhi. Hii, Kwa wote ndiyo
asubuhi tu, bali ni asubuhi njema, si haba.
(a) Ukirejelea aya ya kwanza na ya pili, eleza wasiwasi wanafunzi waliokuwa nao
wakati wakisubiri (maneno 45- 55)
(b) Ni mambo gani mageni wanafunzi hawakuyazoea yanayoelezwa katika kifungu
(maneno 25 – 30)
(c) Bila kubadilisha maana, fupisha aya tatu za mwisho kwa kutumia maneno yako
mwenyewe. Tumia maneno 40 -45
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- UFAHAMU
Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali
Binadamu kwa wakati huu amemaka kwa sababu amechafua mazingira yake pasipo
tahadhari. Mathalani insiya amejaza gesi za sumu zitokazo viwandani na...(Solved)
UFAHAMU
Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali
Binadamu kwa wakati huu amemaka kwa sababu amechafua mazingira yake pasipo
tahadhari. Mathalani insiya amejaza gesi za sumu zitokazo viwandani na hata kuchafua
mito kutokana na maji machafu kutoka viwanda hivyo. Takataka zinazotupwa ovyo
ovyo zinarundikana kila mahali. Isitoshe miti inakatwa vivyo hivyo bila simile. Matokeo
ya haya yote ni kwa mfano tunapata mvua ya asidi ambayo huhasiri mimea. Aidha nao
ukanda wa ozoni unaotukinga dhidi ya miali hatari kutoka kwa jua umeharibiwa tayari na
hivyo kuongeza joto duniani. Sehemu nyingi zimeanza kugeuka na kuwa jangwa huku
sehemu zingine zikifurika kwa maji ya mito na mvua. Maji haya yameanza kumeza
visiwa vingi vilivyo baharini. Kutokana na madhara haya, binadamu sasa anatapatapa ili
kutafuta makao kwingine kwenye salama. Ndiposa siku hizi nadhari za binadamu
zimeelekezwa katika mawanda mengine nje kabisa ya kisayari hiki kidogo kiitwacho
dunia.
Kwa miaka mingi sasa binadamu amekuwa akitafakari uwekano wa kuishi katika sayari
nyingine. Hii ndiyo sababu mwaka wa 1969 waamerika walimkanyagisha binadamu wa
kwanza kabisa mwezini. Lengo lilikuwa ni kutalii na kuchunguza uwekano wa binadamu
kuishi huko ili wale watakaoweza wahamie huko, hata mimea. Mwezini ni vumbi tupu
lisiloota chochote. Kipatikanacho kwa wingi sana ni madini tu ambayo hayawezi kufaidi
binadamu kwa lolote.
Sayari nyingine alizozitalii binadamu ni Zuhura, Mirihi, Mushtara na tuseme karibu zote
zinazolizunguka jua. Kilichogunduliwa ni kuwa upo uwezekano wa sayari kama Zuhura
na pengine Mirihi kuwa na mvua, lakini nyingi mno isiyoweza kuruhusus mimea kukua.
Sit u, zuhuria inasemekna kuwa joto sana wakati wa mchana ilhali Mirihi ni baridi sana
siku zote; baridi kiasi cha kuuwa binadamu na wanyama hawawezi kuishi huko.
Mushtara yasemekana kuwa joto ajabu, ambapo hizo sayari nyingine zina joto sana au
zina baridi sana. Habari hii imemfunga binadamu katika jela ya kijisayari chake kiki
hiki kiitwacho dunia anachokichafua uchao.
Je, binadamu amekata tama? Hata kidogo! Ndio mwanzo anajaribu sana kuzikata pingu
alizofunzwa na maumbile. Vipi? Amejaribu kuchunguza uwezekano wa kuihama ardhi
na kuishi baharini, kwa sababu bahari inazidi ardhi mara tatu kwa ukubwa. Na ni vipi
binadamu anadhani anaweza kuishi baharini mahali ambapo hakuumbwa aishi humo
kama samaki?
Jawabu ni kuwa angefanya hivyo kwa kutumia maarifa yake.
Binadamu anaamini kabisa kuwa ana uwezo wa kujenga miji mikubwa mikubwa humo
humo baharini… mikubwa zaidi yah ii tuliyo nayo ardhini. Anaamini ya kuwa anaweza kuitawala bahari kiasi alichitawala ardhi, na hivyo basi kufanya bahari impe
makao na kumlisha bila ya kuyabadilisha maumbile yake. Na iwapo hili halitawezekana
basi, ikiwajibika, abadilishe maumbile yake kwa kujiunda mashavu kwa mfano, ili avute
pumzi ndani ya maji
Njia ya pili ya kuepukana na pingu za maumbile ni kuishi angani. Hii ina maana ya
kujenga miji iliyoelea angani, kama madungu vile. Na kwa vile anga haina kikomo,
binadamu atakuwa amejipatia visayari vyake visivyo idadi ingani!
Njia ya tatu ni kubadilisha umbo lake ili asihasirike na joto wala baridi. Binadamu wa
kisasa anaamini kuwa inawezekana kumuunda upya mtu katika maabara badala ya katika
mamba.
Mtu huyu wa maabra, aitwaye ‘cyborg’ kwa lugha ya Kiingereza, anaweza kuwa na
chuma ndani badala ya mifupa, na mwili wa kawaida wa udongo na maji nje.
Kiunde huyu atakuwa hadhuriki ovyo ovyo kama binadamu wa sasa aliyeumbwa kwa
chumvi, maji na protini. Au bora zaidi, binadamu mpya wa maabarani aundwe kwa
zebaki. Binadamu huyu wa zebaki hafi wala hakatikikatiki. Na iwapo atakatika vipande
vipande, basi kama zebaki hivyo vitaundika tena upya na kumrudishia umbo la awali
kamili.
Njia nyingine ya kuepukana na uangamizi ni kutumia viunde vyake vya electroniki kama
vile tarakilishi yaani kompyuta, na mitambo mingine kama iyo. Binadamu anaamini
kwamba uwezo wa vyombo hivi utakapokamilishwa, basi vitamsaidia kwa lolote lile.
(a) Inasemekana kwamba binadamu anakichafua hiki kisayari chake kila uchao.
Kwa kutumia mifano mitatu, eleza vile binadamu amechafua mazingira yake.
(b) Kwa nini ongezeko la joto limeleta jangwa duniani wa wakati huo huo likaleta
mafuriko?
(c) Eleza sababu mbili zinazomfanya binadamu kuhangaika na kutafuta makao
kwingine
(d) Ni mambo gani yanayomfunga binadamu katika ardhi. Taja mawili
(e) Unadhani ni kwa nini madini mengi yaliyoko mwezini hayaletwi duniani.
Taja na ufafanue sababu mbili
(f) Kulingana na aya mbili za mwisho, eleza jambo ambalo binadamu anajaribu
kukwepa
(g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu
(i) Mashavu
(ii) Madungu
(iii) Asihasirike
(iv) Kiunde
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Mtu akicheza mchezo mahali Fulani tunaweza kusema alichezea hapo
Ukifuata mfano huu, tumia vitenzi vilivyoko katika mabao kukamilisha
(i) Ali hapo (la)
(ii) Ali hapo (fa)
(iii) Ali hapo...(Solved)
Mtu akicheza mchezo mahali Fulani tunaweza kusema alichezea hapo
Ukifuata mfano huu, tumia vitenzi vilivyoko katika mabao kukamilisha
(i) Ali hapo (la)
(ii) Ali hapo (fa)
(iii) Ali hapo (oa)
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Eleza matumizi ya ‘Po’ katika sentensi hii
Nilipofika nilimwona pale alipokuwa amesimama(Solved)
Eleza matumizi ya ‘Po’ katika sentensi hii
Nilipofika nilimwona pale alipokuwa amesimama
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Andika katika msemo wa taarifa
“Nitakuwa nikija hapa kila siku kukuona”, Kamau alimwambia shangazi
yake(Solved)
Andika katika msemo wa taarifa
“Nitakuwa nikija hapa kila siku kukuona”, Kamau alimwambia shangazi
yake
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Andika katika msemo halisi
Mvulana alimwambia baba yake kuwa alitaka kwenda sokoni(Solved)
Andika katika msemo halisi
Mvulana alimwambia baba yake kuwa alitaka kwenda sokoni
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Kutokana na vitenzi tunaweza kuunda majina na pia kutokana na majina
tunaweza kuunda vitenzi. Mfano
Jina ...(Solved)
Kutokana na vitenzi tunaweza kuunda majina na pia kutokana na majina
tunaweza kuunda vitenzi. Mfano
Jina Kitendo
Mwuzaji Uza
Mauzo Uza
Wimbo Imba
Sasa kamilisha:
Jina Kitenzi
(i) Mnanda
(ii) Kikomo
(iii) Ruhusa
(iv) ashiki
(v) husudu
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Tunasema: Mtoto huyu mzuri anapendeza
Ukitumia majina yafuatayo kamilisha sentensi ukifuata mfano ulio hapo juu
(i) Ngome
(ii) Mitume
(iii) Heshima
(iv) Ng’ombe
(v) Vilema(Solved)
Tunasema: Mtoto huyu mzuri anapendeza
Ukitumia majina yafuatayo kamilisha sentensi ukifuata mfano ulio hapo juu
(i) Ngome
(ii) Mitume
(iii) Heshima
(iv) Ng’ombe
(v) Vilema
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Eleza kazi ifanywayo na
(i) Mhariri
(ii) Jasusi(Solved)
Eleza kazi ifanywayo na
(i) Mhariri
(ii) Jasusi
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)