Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Siku hiyo nilipitia mahali hapo kama nilivyokuwa nikimuona siku hizi zote, mwaka nenda mwaka rudi. Nilisimama huku nikishangaa kwa mara nyingine tena. Nilikuwa...

      

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Siku hiyo nilipitia mahali hapo kama nilivyokuwa nikimuona siku hizi zote,
mwaka nenda mwaka rudi. Nilisimama huku nikishangaa kwa mara nyingine
tena.

Nilikuwa najitayarisha kujiendea na hamsini zangu mtu huyo alipojipinda kwa
mbali sana. Kwa hakika nilidhani macho yangu yananihadaa. Nikafikicha macho
yangu nikitumia nishati yote iliyomo mwilini mwangu ili niyatoe matongo
ambayo nilituhumu kwamba ni akili yangu tu iliyokuwa imeniadaa, nikaamua
kuendelea na safari yangu kwenda kujitafutia riziki.

Hatua ya kwanza na ya pili, moyo haukunipa. Sauti katika kilindi cha moyo
wangu ikanisihi na kunitafadhalisha nitazame nyuma. Kutupa jicho nyuma,
nikamnasa mtu huyo akeguka! Nikashtuka sana! Jambo la kwanza nildhani macho
yangu yameingiwa na kitu kilichoyafanya kuona mambo yasiyokuwepo. Pili,
nilidhani iwapo niliyoyaona yana msingi wowote, basi huenda ama nina wazimu,
au yule mtu ni mzuka, hasa kwa vile ilionekana ni mimi tu nimuonaye.
Nilikikuwa niko katika hali ya kufanya uamuzi kuhusu dhana zangu hizi aina aina
mtu huyo alipojigeuzageuza, kisha akafunua macho! Moyo ulinienda mbio.
Nilitaka kutifua vumbi ili wazimu usinizidie, lakini sikupata nafasi. Mtu yule
alijizoazoa na kuketi kitako. Kisha akatokwa na maneno katika lugha iliyofanana
sana na Kiswahili. Niliyaelewa aliyokuwa akisema.

Ajabu ya maajabu, mtu huyo alidai ya kwamba tangu alipolala kivulini hapo
tangu jana baada ya chakula cha mchana, hakuota ndoto hata moja bali usingizi
wake ulikuwa mithili ya gogo! Sasa nilikuwa na hakika kwamba ikiwa mimi sina
wazimu, basi kiumbe yule aliyevaa ngozi iliyochakaa sana katika mpito wa miaka
hakika ana wazimu. Nilitaka kuhakikisha, hivyo nilimkumbusha kwamba
amelala mahali hapo kwa muda wa miaka mingi sana.

Kusikia hayo alianza kunikagua. Akasema nimevaa kizungu. Akanitajia tofauti
nyingi baina ya vijana aliowazoea na mimi. Mwisho wa yote akauliza kama siku
hiyo si tarehe kumi na nane mwezi wa pili mwaka wa 1897. Nikadhani anafanya
mzaha kwa hivyo nikacheka.
Nilipoona kicheko changu kinamuudhi, nikamwambia siku hiyo ni tarehe kumu
na nane mwezi wa pili mwaka wa 1997. Nilipoona ameshangaa kwa dhati,
nikagundua ukweli.
Alikuwa amelala kwa karne nzima!.

a) Eleza hoja nne muhimu zinazojitokeza katika aya tatu za mwanzo.
(Maneno 75-85)
b) Kwa maneno yako mwenyewe, fupisha aya mbili za mwisho bila
kubadilisha maana. (Tumia maneno 40-50)

  

Answers


Kavungya
(a) Hoja
Alikuwa na mazoea ya kupitia pale pale
Alikuwa amelala pale pale bila kutingishika
Alikuwa katika hali hiyo kwa miaka mingi
Alishangaa tena
Alimwona akijipinda kwa mbali akadhani macho yanamhadaa
Alipohakikisha macho yanamdanganya, akaamua kwenda zake
Lakini kutazama nyuma alishtuka kumwona mtu yule akigeuka, akifunua macho na
kuketi
Alizungumza lugha iliyofanana na Kiswahili
(a) Hoja
Mtu huyu alidai kuwa amelala pale kwa siku moja/ muda mfupi
Kiumbe huyu alikuwa amevaklia ngozi iliyochakaa kwa mpito wa wakati
Alimkumbusha kwamba alikuwa amelala pale kwa miaka mingi
Kiumbe yule alimkagua na akasema (amevaa kizungu) alikuwa tofauti na vijana
aliowazoea
Aligundua kuwa alikuwa amelala pale kwa karne nzima

b) Debe shinda haliachi kutika
Kelele za mwenye nyumba hazimgusi mpangaji
Maji ya moto hayachomi nyumba
Kelele za Chura hazimzuii ng’ombe kunywa maji
Vishindo vya mashua havishtui bahari
Manen makali hayavunji usingizi
Nastahamili maovu maneno hayana kovu
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 09:32


Next: Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Mwanamke wa kisasa anazaliwa na kukulia katika mazingira yaliyobadilika mno. Matazamio yake maishani ni tofauti na yale ya wanawake walioishi mapote...
Previous: Jaza kiambishi kifaacho: Ume__________ ona kalamu nyekundu ziliz_______potea?

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Mwanamke wa kisasa anazaliwa na kukulia katika mazingira yaliyobadilika mno. Matazamio yake maishani ni tofauti na yale ya wanawake walioishi mapote...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
    Mwanamke wa kisasa anazaliwa na kukulia katika mazingira yaliyobadilika mno.
    Matazamio yake maishani ni tofauti na yale ya wanawake walioishi mapote mawili
    yaliyopita; wanawake makamu ya nyanyake na mamaake-kuu.

    Yeye hatarajii kuzaliwa, kukua, kuolewa, kuwa mke wa bwana, kumzalia watoto, na
    daima dawamu kuwa ‘mwendani wa jikoni’ akawapikia watoto na bwanake chakula; na
    akitoka jikoni aelekee shambani kulima, kichakani kuchanja kuni, mtoni kufua nguo na
    kuteka maji ya kutumia nyumbani. Mwanamke wa kisasa huandamana na mwanamume.
    Akanyangapo mume naye papo huutia wayo wake.

    Mwanamke wa kisasa huenda shule na kujifunza yote yafunzwayo huko. Hushindana na
    wanawake kwa wanaume na kuibuka mshindi si mara haba. Huibuka mshindi katika
    masomo ya lugha, historia, jiografia, hesabu, sayansi na mengineyo, sawa na
    mwanamume.

    Mwanamke wa kisasa hutaka kufanya kazi za kibega, akazifanya. Akataka kuwa
    mwalimu, akawa. Akataka kuwa daktari, akafanikiwa. Almuradi, siku hizi mwanamke
    hufanya kazi yoyote ile afanyayo mwanamume. Kuna wanawake marubani wa ndege,
    masonara, waashi, wahandishi, madereva wa magari, mawakili, mahakimu, mawaziri
    wakuu na hata marais wa nchi. Hakuna kazi isiyofanywa na mwanamke siku hizi.

    Mwanamke wa kisasa hateswi akafyata ulimi. Anapohiniwa yeye hupigania haki yake
    kwa dhati na hamasa. Katu hakubali ‘mahali pake’ katika jamii alipotengewa na
    wanaume wenye mawazo ya kihafidhina yaliyopitwa na wakati.

    Siku hizi mwanamke huolewa tu wakati amepata kazi ya kumwezesha kujikimu maishani
    au pale anapokuwa na hakika kwamba biashara yake, iwapo ni mfanyi biashara, imepiga
    hatua ya kutomrudisha ukutani.

    Mwanamke wa kisasa haamuliwi katika jambo lolote, bali hufanya maamuzi yake
    mwenyewe. Kwa upande mwingine, mwanamume wa ‘kisasa’, ambaye bado amefungwa
    pingu na taasubi za kiume, hapendezwi na mwanamke huyu. Huuma kidole akatamani ya
    kale, lakini wapi! Analazimika kumkubali mwanamke huyu kama mshirika sawa
    maishani, na kuishi naye, apende asipende. Shingo upande analazimika kukubali kwamba
    mabadiliko haya sio mithili ya kiwingu kipitacho, bali ni ya aushi.

    a) Msemo ‘mwendani wa vijungu jiko’ unadhihirisha hali gani ya
    mwanamke katika jamii?
    b) Jamii imemfanya mwanamke kuwa hayawani wa mizigo. Fafanua
    c) Eleza maana ya ‘akanyagapo mume papo huutia wayo wake.’
    d) Zungumzia maswala ya ndoa na elimu huku ukilinganisha mwanamke wa
    kiasili na wa kisasa.
    e) Mwanamume wa kisasa anamwonaje mwanamke wa kisasa?
    f) Taja mifano minne ya ‘mawazo ya kihafidhina.
    g) Eleza maana ya:
    (i) Akafyata ulimu……………………………………………
    (ii) Ukatani…………………………………………………….
    (iii) Taasubi za kiume………………………………………….
    (iv) Aushi…………………….………………………………..

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia kirejeshi ( kihusiano) cha ngeli cha mwisho Mwanafunzi anayefanikiwa maishani ni yule anayesoma kwa bidii na pia anayetii wakuu wake(Solved)

    Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia kirejeshi ( kihusiano) cha ngeli cha mwisho
    Mwanafunzi anayefanikiwa maishani ni yule anayesoma kwa bidii na pia
    anayetii wakuu wake

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tumia semi hizi katika sentensi kuonyesha maana: (i) Kuchokoachokoa maneno (ii) Kumeza shubiri(Solved)

    Tumia semi hizi katika sentensi kuonyesha maana:
    (i) Kuchokoachokoa maneno
    (ii) Kumeza shubiri

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunatumia viashiria vya kuthibitisha kwa mfano kitabu kiki hiki. Sasa kamilisha Ni mbwa …………………….. aliyekula chakula cha mtoto(Solved)

    Tunatumia viashiria vya kuthibitisha kwa mfano kitabu kiki hiki. Sasa kamilisha
    Ni mbwa …………………….. aliyekula chakula cha mtoto

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza tofauti mbili muhimu za kimaumbile kati ya wanyama (i) Kifaru (ii) Nyati(Solved)

    Eleza tofauti mbili muhimu za kimaumbile kati ya wanyama
    (i) Kifaru
    (ii) Nyati

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tumia kiulizio – pi – kukamilisha (i) Ni mitume ………………………. Aliowataja? (ii) Ni kiziwi ………………………. . Aliyemwona akipita?(Solved)

    Tumia kiulizio – pi – kukamilisha
    (i) Ni mitume ………………………. Aliowataja?
    (ii) Ni kiziwi ………………………. . Aliyemwona akipita?

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Watu wafuatao wanafanya kazi gani (i) Mhasibu (ii) Mhazili(Solved)

    Watu wafuatao wanafanya kazi gani
    (i) Mhasibu
    (ii) Mhazili

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tumia viunganishi vingine badala ya vile vilivyotumiwa katika sentensi hizi: (i) Anayetafuta hachoki hata akichoka keshapata (ii) Ngonjeeni hadi washiriki wote wafike(Solved)

    Tumia viunganishi vingine badala ya vile vilivyotumiwa katika sentensi hizi:
    (i) Anayetafuta hachoki hata akichoka keshapata
    (ii) Ngonjeeni hadi washiriki wote wafike

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Taja madini mawili ambayo yametukuzwa zaidi, moja kwa thamani yake ya kifedha na nyingine kwa kutengeneza vyuma vigumu kuliko madini mengine(Solved)

    Taja madini mawili ambayo yametukuzwa zaidi, moja kwa thamani yake ya
    kifedha na nyingine kwa kutengeneza vyuma vigumu kuliko madini mengine

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha kielezi, kivumishi, kitenzi na jina katika sentensi: Watu wane walipeperushwa juu kwa juu na upepo mkali(Solved)

    Onyesha kielezi, kivumishi, kitenzi na jina katika sentensi:
    Watu wane walipeperushwa juu kwa juu na upepo mkali

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Akifisha kifungu hiki: Nilopomwendea aliniangalia kisha akaniambia siamini kuwa ni wewe uliyeandika insha hii.(Solved)

    Akifisha kifungu hiki:
    Nilopomwendea aliniangalia kisha akaniambia siamini kuwa ni wewe uliyeandika
    insha hii.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala haya kisha ujibu maswali yanayofuata Lugha ya Kiswahili ni lugha iliyoendelea sana. Leo hii lugha hii inasema na watu wote nchini Tanzania, Rwanda na Burundi,...(Solved)

    Soma makala haya kisha ujibu maswali yanayofuata
    Lugha ya Kiswahili ni lugha iliyoendelea sana. Leo hii lugha hii inasema na watu wote
    nchini Tanzania, Rwanda na Burundi, inasemwa na watu wote nchini Kenya. Nchini
    Uganda, Zaire, Malawi, msumbiji, Zambia, Somalia, Bukini (Madagascar) na Ngazija
    (Comoro), inasemwa na asilimia kubwa za wananchi wa huko. Aidha lugha hii ina
    wasemaji si haba katika kisiwa cha Sokta na nchini Oman.

    Fauka ya maendeleo haya, Kiswahili kinatumika kwa minajili ya matangazo ya habari
    katika idhaa nyingi za mashirika ya habari ulimwenguni. Nchi zenye idhara za Kiswahili
    ni kama vile hizi zetu za Afrika ya Mashariki na kati, Afrika ya kusini, Nigeria, Ghana,
    Uingereza, ( shirika la B.B.C) Marekani ( shirika la V.O.A), Ujerumani ( shirika la
    Radio Deutch Welle, Cologue), Urusi ( Radio Moscow), China, India na kadhalika.

    Maendeleo mengine yanapatikana katika upande wa elimu, Marekani peke yake, kuna
    vyuo zaidi ya mia moja vinavyofundisha Kiswahili kama lugha muhimu ya kigeni. Huko
    Uingereza vyuo kama London, Carmbridge na Oxford vinafundisha lugha hii. Nci
    nyingine ambazo zina vyuo vinavyofunza lugha ya Kiswahili ni kama vile Japan, Korea,
    Ghana, Nigeria na kadhalika

    Kweli Kiswahili kimeendelea jamani. Lakini je, kilianza vipi? Na ilikuwaje kikaweza
    kupiga hatua hizi zote?
    Kiswahili kilianza kuzungumzwa na kabila dogo la watu waliokuwa wakiitwa wangozi.
    Watu hawa walikuwa wakiishi mahali palipoitwa shumgwaya. Shungata ni nchi ya
    zamani iliyokuwa eneo lililoko katika nchi katika nchi mbili jirani ambazo siku hizi ni
    Kenya na Somalia. Kabila hili la wangozi iliishi irani na makabila mengine kama vile
    wajikenda, wapokomo, Wamalakote ( au Waelwana) na Wangazija ( kabla hawajahamia
    visiwa vya Ngazija) Lugha ya wangozi siku hizo, ambayo ndiyo mzazi wa Kiswahili
    cha leo, ilijulikana kwa jina kingozi. Kama ilivyosemwa hapo awali, kingozi kilisemwa
    na watu wachache sana.

    Je lugha hii ilikuwaje mpaka ikapata maendeleo haya makubwa tunayoyashuhudia siku
    hizi? Ama kwa hakika, Kiswahili ni lugha iliyobahatika tu. Inaweza kusemwa kwamba
    lugha hii ilipendelewa na mazingira na historia.

    Jambo la kwanza, wageni waliotoka mashariki ya kati kifukia hizi janibu zetu Afrika ya
    mashariki walikaribishwa vizuri na hawa wangozi. Wakaingilia wageni na wenyeji
    kindakindaki, kidini, kitawala, kibiashara na kitamaduni kwa jumla. Punde si punde
    wangozi, ambao baadaye walijulikana kama waswahili na wageni hawa, wakaelimika
    katika dini (ya kiisilamu), biashara na mambo ya utawala aina mpya. Lugha yao nayo
    ikapanuka pale ilipochukua msamiati ya kigeni hususan wa Kiarabu na Kiajemi na
    kuufanya uwe wake, ili kueleza kwa rahisi zaidi mambo haya mageni katika taaluma za
    dini, biashara, siasa na hata sayansi kama vile unajimu. Wakati huo, lugha ya Wangozi
    sasa ikaitwa Kiswahili wala sio kiangozi. Tatizo hapa ni kuwa kwa vile Kiswahili
    kilichukua msamiati mwingi wa kigeni ili kuelezea taaluma hizi mpya, baadaye kimekujashukiwa kwamba ni lugha ya kigeni ilhali ni lugha ya Kiafrika asilia, na kitovu
    chake ni nchi mpya za kiafrika ziitwazo Kenya na Somalia hii leo.

    (a) Thibitisha kuwa Kiswahili kimekuwa lugha ya kimaitaifa ( maneno 35 – 40)
    (b) Eleza kwa ufupi asili ya Kiswahili hadi kuja kwa wageni ( maneno 20 – 25)
    (c) Ukitumia maneno yako mwenyewe, eleza ujumbe uliomo katika aya ya mwisho

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata Kuna sayansi mpya inayoitwa “cloning” kwa lugha ya Kiingereza. Pengine kwa sasa tuite “kutumbisha.” Sayansi hii tayari imeleta mapinduzi makubkwa...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata
    Kuna sayansi mpya inayoitwa “cloning” kwa lugha ya Kiingereza. Pengine kwa sasa tuite
    “kutumbisha.” Sayansi hii tayari imeleta mapinduzi makubkwa katika uzalishaji mimea
    na uvunani. Imesemekana ya kwamba, ghairi ya wivu na kijicho baina ya jamii
    mbalimbali ulimwenguni, aina hii ya sayanzi ina uwezo na kuangamiza kabisa janga la
    njaa katika sayari hii yetu. Kivipi? Rahisi kabisa. Ni kwamba mbegu moja tu ya aina
    yoyote ya mmea, baada ya kuneemeshwa vyumba vyake vidogo ambavyo ndivyo hasa
    msingi wa uhai vinaweza kunyunyiziwa dawa maalum ili vitawanyike mara hata
    mamilioni na kuwa mimea kamili…. Mamilioni!

    Sayansi hii tarari inatumiwa kukuza viazi na vyakula vingine. Hii ina maana ya kwamba
    mashamba makubwa si muhimu siku hizi, yaani vyakula vingi kabisa vinaweza kukuzwa
    mahali padogo sana. Kwa hivyo hivi karibuni tu, kutakuwa hakuna haja ya kupigania
    mashamba.

    Vyema. Hebu sasa tuangalie zilizokwishapigishwa hii sayansi ya “kutumbisha” na mahali
    binadamu alipofika kimaendeleo kwa sababu ya hatua hizo. Jambo la kwanza sayansi hii
    tayari imeshatumiwa kuzalishia wanyama wengi, wengi sana wadogo wadogo kwa lengo
    la kuendeleza mbele utafiti. Kufikia sasa, wanyama hawa waliotengenezwa na binadamu
    katika maabara yake bado wanahifadhiwa mumo humo walimotengenezwa. Hii ni hatua
    kubwa na binadamu anastakili pongezi kwa jinsi anayotumia akili yake kuvumbua ibura
    hizi zote.

    Hata hivyo imesemwa kwamba kuchamba kwingi ni kuondoa mavi. Binadamu kama
    ijulikanavyo, anajaribu sana jujitakasa kwa kujitenga mbali sana na asili yake ya unyama
    ili aufikie ubinadamu mkamilifu. Hapana ubaya hapo. Lakini tukirudi nyuma tunakuta ya
    kwamba binadamu sasa aneingia tama kubwa sana kuliko wakati wowote ule. Tamaa hii
    imeletwa na ujuzi wake katika sayansi hii ya “kutumbisha.” Sasa binadamu ana jua
    vizuri sana kwamba kwa vile ana ujuzi wa kutengeza panya na hata kondoo katika
    maabara basi hata ujuzi wa kutengeneza binadamu pia anao! Na hapo ndipo tatizo lilipo.
    Swali hi hili: Je, ujuzi huu utatufikisha wapi? Na kikomo chake kitakuwaje?

    Binadamu sasa ujuzi wake unamtia wasiwasi. Wataalam wa sayansi hii wamejiuliza mara
    nyingi nini kitakachotokea ujuzi huu utakapomilikiwa na mwenda wazimu mweledi.”
    Watu kadha wa kadha, miongoni mwao wakiwa wanasiasa wamejiuliza mara
    zisizohesabika swali hili: kama Hitler angekuwa na ujuzi huu, angekuwa na lazima gani
    ya kuwaulia mbali wayahudi milioni sita wasiokuwa na hitia isipokuwa na nywele
    nyeusi na hawakuwa weupe sana kama wazungu? Hitler aliamini ya kwamba “mtu
    mzuri” ni mwenye pua ya upanga (kama mzungu), macho ya buluu nywele rangi ya dhahabu na mwenye kimo cha futi sita au zaidi kidogo. Hivyo lengo lake lilikuwa ni
    kubuni taifa la watu wazuri pekee ambao mwisho watautawala ulimwengu na kuenea
    duniani kote. Katika mpango wake, watu weusi wote wangefaa kuangamizwa tu ili watoe
    nafasi kwa watu aliowaona yeye kuwa bora.

    Sasa baada ya sayansi hili ya “kutumbisha” kuvumbuliwa, wataalam wametishika sana.
    Wamewaza jinsi ambavyo Hitler angeweza kufanya kama angekuwa mjuzi wa taaluma
    hiyo.

    Kitisho hiki kimezidi kuwatwanga wataalam na wasiokuwa wataalam hivi majuzi tu
    ilipogunduliwa maiti ya msichana wa miaka kumi na mine huko milima ya Andes,
    Amerika ya kusini. Msichana huyo alikuwa ametolewa kafara miaka karne tano zilizo
    pita lakini hakuoza kwa sababu ya baridi kali ya barafu milimani.

    Kwa sababu ya dukuduku la uvumbuzi ambalo haliishi dhana za kiajabu ubongo wa
    binadamu, wataalamu wa “kuchezea” maumbile walipomwona msichana huyo maiti,
    upesi upesi wakampima. Walipofanya hivyo wakagundua ya kwamba mayai yake ni
    timamu kabisa wala hayajaharibiwa na mpito wa karne. Papo hapo wengine wakajiwa na
    wazo la kuyatoa mayai hayo na kuyahifadhi kwenye mabara. Tamaa ikazidi zaidi ya
    zaidi. Baadhi ya wataalamu wakajiwa na wazo la “kuyaneemesha” mayai hayo na mbegu
    za uzazui za wanaume. Kwa lengo gani? Kuunda watoto amabo mama yao alikufa
    zamani za kale ili waonekane watakuwa watu wa aina gani!

    Sasa fikiria mwenyewe! Watoto hawa wa maabara wakiwa weledi zaidi ya binadamu
    yeyote yeyote wa kisasa lakini watiifu kama mbwa na paka itakuwaje? Hakuna
    atakayefikiria “kutumbisha” ili tuwe na vijitumwa vyetu vipenzi majumbani mwetu
    vinavyofanana nasi badala ya paka na mbwa wasiovishwa nguo?

    (a) Andika kichwa kifaacho kwa nakala hii
    (b) Kutumia sayansi ya “kutumbisha” kunaweza kumsaidia binadamu kuangamiza
    mabaa gani mawili yanayomkabili sasa?
    (c) Unadhani ni kwa nini wanyama waliozalishwa kwa kutumia sayansi hii bado
    wamo maabarani?
    (d) Fafanua methali “kuchamba kwingi nikuondoka na mavi” kulingana na muktadha
    wa habari hii
    (e) Kuna ubaya gani kutumbisha watu?
    (f) Mwandishi anaonekana kutishwa sana na uwezekano wa sayansi ya kutumbisha
    kuishia mikononi mwa “wendawazimu weledi” kwani kuna hatari gani?
    (g) Eleza kwa ukamilifu matatizo yanayoweza kuukumba ulimwengu iwapo mayai ya
    msichana wa Andes yatatumbishwa

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Bila kunyambua, andika maneno mawili ambayo yanatokana na shina moja na neno: imani(Solved)

    Bila kunyambua, andika maneno mawili ambayo yanatokana na shina
    moja na neno: imani

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi ya neno moja ambayo ina visehemu vifuatavyo vya sarufi - Kiima - Wakati - Kirejeleo - Kiswahili kitendwa - Kitenzi(Solved)

    Tunga sentensi ya neno moja ambayo ina visehemu vifuatavyo vya
    sarufi
    - Kiima
    - Wakati
    - Kirejeleo
    - Kiswahili kitendwa
    - Kitenzi

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Mahali palipohamwa panaitwa?(Solved)

    Mahali palipohamwa panaitwa?

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana mbili mbili zinazotokana na sentensi zifuatazo (i) Mtoto alitimua mbio, kuona nyoka (ii) Juma alifagia chakula (iii) Sisikii vizuri(Solved)

    Eleza maana mbili mbili zinazotokana na sentensi zifuatazo
    (i) Mtoto alitimua mbio, kuona nyoka
    (ii) Juma alifagia chakula
    (iii) Sisikii vizuri

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika methali nyingine ambayo maana yake ni kinyume cha Riziki kama ajali huitambui ijapo(Solved)

    Andika methali nyingine ambayo maana yake ni kinyume cha
    Riziki kama ajali huitambui ijapo

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya misemo ifuatayo kwa kuitungia sentensi moja moja Kuramba kisogo Kuzunguka mbuyu(Solved)

    Eleza maana ya misemo ifuatayo kwa kuitungia sentensi moja moja
    Kuramba kisogo
    Kuzunguka mbuyu

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Bila kubadilisha maana, andika sentensi zifuatazo ukitumia kirejeleo cha ngeli kifaacho (i) Nyumbu alishinda farasi kukimbia (ii) Milango yote yajifunga ovyo, nenda uakafunge (iii) Hamisi amekata nyasi vizuri...(Solved)

    Bila kubadilisha maana, andika sentensi zifuatazo ukitumia kirejeleo cha ngeli
    kifaacho
    (i) Nyumbu alishinda farasi kukimbia
    (ii) Milango yote yajifunga ovyo, nenda uakafunge
    (iii) Hamisi amekata nyasi vizuri
    (iv) Jiwe lile liliangukia matunda

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)