Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Kamilisha jedwali ukifuatia mfano uliopewa Wimbo Mwimbaji Uimbaji Jengo ……………. ………. Pendo ……………. ……….

      

Kamilisha jedwali ukifuatia mfano uliopewa
Wimbo Mwimbaji Uimbaji
Jengo ……………. ……….
Pendo ……………. ……….

  

Answers


Kavungya
Jengo – mjengaji/ mjenzi- Ujengaji/ ujenzi
Pendo - Mpendaji/ mpenzi – upendo/ upendaji
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 10:01


Next: Eleza tofauti iliyopo katika jozi hii ya sentensi. Alimpatia soda ya chupa Alimpatia soda kwa chupa.
Previous: Kamilisha jedwali ukifuatia mfano uliopewa Wimbo Mwimbaji Uimbaji Jengo ……………. ………. Pendo ……………. ……….

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Eleza tofauti iliyopo katika jozi hii ya sentensi. Alimpatia soda ya chupa Alimpatia soda kwa chupa.(Solved)

    Eleza tofauti iliyopo katika jozi hii ya sentensi.
    Alimpatia soda ya chupa
    Alimpatia soda kwa chupa.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Raha ni kitu gani? Je, ni kitu kizuri au kibaya? Mbona kila mutu hipigania na kama ionekanavyo, kila aionjaye hatimaye humwunguza?...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
    Raha ni kitu gani? Je, ni kitu kizuri au kibaya? Mbona kila mutu hipigania na
    kama ionekanavyo, kila aionjaye hatimaye humwunguza? Au pengine wako
    wengine wasiooungua? Hebu basi tuzingatie wale wasemekanao huitafuta sana
    raha na, penginepo wakafanikiwa kuipate.

    Chukua mfano wa msichana na mvulana wapendanao. Hawa wawili
    wanapopendana, lengo lao huwa ni kuoana na wakishaoana, waishi raha
    mustarehe milele na milele. Hata hivyo, jambo la kwanza ni kwamba, hata kabla
    hawajaoana, wanadhikika na kudhikishana kwa kutaka sana kuaminiana si mara
    haba wakati wakiwa wapenzi mar. Mara kadha wa kadha husameheanana
    kuendelea na mapenzi. Baadaye wakiwa na bahati, huona.

    Mara tu wanapooana hugundua kuwa huko kuishi raha mustarehe ilikuwa ni
    ndoto tu ya ujana iliyotengana kabisa na uhalisia. Uhalisia unapowabinikia huwa
    ni kuendelea na huko kudhikishana,kutoridhishana, kutiliana shaka, kuombona
    mamaha na kuendelea tu.

    Ama tumwangalie mwanasiasa. Huyu anapigania usiku na mchana ili awe
    mjumbe. Mwisho anachanguliwa, lakini afikapo bunge, anakuta hakuna
    anayemtambua kama bwana mkubwa. Inambainikia kwamba ubawana- Mkubwa
    hautegemei kuchaguliwa tu, bali unategemea mambo mengine pia, kama vile pesa
    nyingi, magari makibwa, sauti katika jamii na wadhamini wanotambulikana. Raha
    kwa mwanasiasa huyu inakuwa mithili ya mazigzi tu, “maji” uyaonayo kwa mbali
    wakati una kiu kali sana, kumbe si maji bali ni mmemetuko wa jua tu.

    Mwingine wa kupigiwa mfano ni msomi. Huyu huanza bidii yake akiwa mdogo
    sana. Lengo lake huwa ni atambuliwe kote kwa uhohadri wake katika uwanja wa
    elimu. Basi mtu huyu husoma mpaka akaifikia daraja ya juu kabisa ya usomaji.
    Akapata shahada tatu: ya ukapera, ya uzamili nay a uzamifu. Akajiona yu upeoni
    mwa ulimwengu. Akatafuta kazi akapata. Kisha akagundua kwamba watu
    hawakijali sana kisomo chake. Wakamwona ni kama mwehu tu. Fauka ya hayo
    wakamlumu kwa kupoteza muda wake mwingi kupekuapekua vitabu.
    Wakamfananisha na mtu mvivu.

    Mwisho tuangalie mfano wa mwanamuziki . Huyu anahaghaika na wazo la
    kwamba sauti yake ikiwaonga watu, atapendwa sana na wengi na kuwazuzua
    wengi kama mbalamwezi au kuwaongoza kama nyota. Mtu huyu anapofikia kilele
    cha malengo yake hata husahau kama ni binadamu wa kawaida, akawa anaishi
    katika muktadha wa watu kuzirai kwa sababu ya akili kujawa pomoni na upungaji
    wake. Watu hutamani hata kumgusa tu. Hata hivyo, mtu huyu huishis kujisikia
    mkiwa pale wakati unapowadia wa kupumzika. Je, raha yote huwa imekimbilia
    wapi?

    a) “Mapenzi ni kuvumiliana.” Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jinsi
    msemo huu ulivyo muhtasari mwafaka way a pili nay a tatu ya habari hii.
    (Maneno 30-35)
    b) Kwa muhtasari, raha ni “asali chungu. “Fafanua dai hili huku ukirejelea
    mwanasiasa, msomi na mwanamuziki (maneno 45-55)

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali Nchi nyingi za ulimwengu unaoendelea, au ule uliokuwa ukiitwa ulimwengu wa ta zimegawika sehemu mbili mbili. Sehemu hizi zinazidi kutoshabihiana kila...(Solved)

    Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali
    Nchi nyingi za ulimwengu unaoendelea, au ule uliokuwa ukiitwa ulimwengu wa ta
    zimegawika sehemu mbili mbili. Sehemu hizi zinazidi kutoshabihiana kila uchao
    zinatengana kiasi cha kukaribia kupigwa mfano wa masafa ya ardhi na mbingu. Seher
    zenyewe ni mijini na mashabani. Sehemu hizi, hasa ukizitia katika mizani ya hali na jia
    za watu za maisha, zimetofautiana mno. Kiasi cha tofauti hizi ni kikubwa hadi
    kuonekana kama kwamba hazina uhusiano kamwe, mithili ya nchi mbili tofauti.

    Hebu sasa tuzingatie yale yana yozifanya sehemu hizi kukosa kufanana. Hapa
    tutawajibika kuzizingatia tofauti zilizo bayana baina ya watu wa shamba na wa mijini,
    hasa kufungamana na jinsi wanavyoyaendesha maisha yao.

    Jambo lililo wazi ni kwamba watu wa mashambani hawajapiga hatua ya maana kuhusu
    jinsi wanavyuotakikana kuishi katika karne ya ishirini. Watu hawa bado wanaishi kama
    walivyoishi mababu zao. Hawahisi halahala ya jambo lolote. Mategemeo yao ni shamba;
    usubiriwe msimu mzuri wa mvua, watu walime, Mungu akineemeshe kilimo, wavune
    mavuno mema, Chakula kikiwa tayari, wale, walale, siku nyingine warudie mkondo uo
    huo wa kuendesha maisha yao.

    Watu hawa maisha yao yamepangika mikondo mitatu tu: kuzaliwa, kuoa au kuolewa, na
    kufa. Zaidi ya mikondo hii, maisha ya viumbe hawa hayana mabadiliko makubwa.
    Mabadiliko haypendelewi sana huko mashambani. Huko, wanaume ni mabwana,
    wanawake ni mfano wa vijakazi na watoto hawana tofauti kubea na watwana. Mwanume
    akikohoa, mkewe akimbilie kulikokoholewa, na watoto watetemeke. Wanawake wa
    shamba na watoto hawana haki hata ya kunena, wala hawajui haki ni nini.

    Kwa upande mwingine, mijini kuna viwanda, kuna majumba, kuna magari na kuna
    vyombo vingi sana vya maendeleo ya kisiku izi. Watu wa mijini ni watu wa ulimwengu
    kote, wala si watu wa mji mmoja tu. Watu wa mji wowote ulimwenguni huweza
    kuwasiliana na wenzao wa miji mingine kokote kule ulimwenguni kwa njia ya runinga.
    Pia, kwa watu wa mjini, kuona kiumbe kidogo kabisa kisichoweza kuonekana kwa
    macho si ibura hata. Kiumbe cha namna hiyo huonekana kupitia mangala. Na kwa wale
    walioondokea kuwa wanajimu wa kisasa, kuziona sayari na thurea zilizoko mbali sana
    nasi kupitia ningala ni jabo la kawaida sana.

    Watu wa mjini huwa na mabadiliko mengi sana katika maisha yao, wala sio mikondo
    aina tatu tu. Kwa mfano, wanawake wa mijini hawakubali tena kuonewa na wanaume.
    Wanajua vyema sana maslahi yao na wameiweka menke yao mbele; yaani mahali pao
    katika jamii, wakiwa wao ni wanawake. Kupigania haki sawa na wanaume bila kulegeza
    kamba. Huku kupambana kimaisha kama wapambanavyo wanaume na kufanikiwa kufanya kazi za kusikika kam vile uwakili, udaktari, uhandisi, urubani na nyinginezo
    zilizokuwa zikifanywa na wanaume tu. Wanawake wengine hata ni maprofesa! Kweli
    watu wa mijini wameendelea.

    a) Toa maelezo kuhusu tofauti zinazosemekana ni bayana baina ya maisha ya watu
    wa shamba nay ale ya watu wa mijini.
    b) Rejelea “Mungu” katika aya ya tatu na neon “viumbe” katika aya ya nne.
    Bainisha uhusiano uliopo baina ya manen haya mawili, hasa ukizingatia jinsi
    yavyotumiwa katika habari. Je matumizi haya yankupa hisia gani?
    c) Unadhani mwandishi ana maana gani anaposema ya kwamba huko mashambani
    “wanawake ni mfano wa vijakazi, na watoto hawana tofauti kubwa na watwana?”
    d) Orodhesha vifaa vyovyote vitano vilivyotajwa katika taarifa hii, kisha ueleze
    umuhimu wa kila kimoja wapo.
    e) “Watu wa mijini ni watu wa ulimwengu kote” Hapa mwandishi anamaanisha
    nini?
    f) (i) Ni nini maana ya neon menke?
    (ii) Mwandishi anamaliza taarifa yake kwa kusema “Kweli watu wa mijini
    wameendelea.” Kwa muhtasari, ni tabia gani za wanamiji zilizomfanya
    kukiri hivyo.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Kiambishi- U-hutambulisha majina yote ya ngeli ya U (umoja). Hata hivyo baadhi majina hay huchukua viambishi tofauti tofauti katika wingi. Orodhesha majina ma kama hayo, kisha uonyeshe...(Solved)

    Kiambishi- U-hutambulisha majina yote ya ngeli ya U (umoja). Hata
    hivyo baadhi majina hay huchukua viambishi tofauti tofauti katika wingi.
    Orodhesha majina ma kama hayo, kisha uonyeshe viambilshi hivyo tofauti
    vya ngeli (Katika umoja na Wingi)

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana mbili za sentensi: Jua nisemalo ni muhimu kwetu.(Solved)

    Eleza maana mbili za sentensi:
    Jua nisemalo ni muhimu kwetu.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Akifisha: Sijaona kitabu kizuri kama hiki utaniazima siku ngapi bashiri alimuliza sijaona.(Solved)

    Akifisha:
    Sijaona kitabu kizuri kama hiki utaniazima siku ngapi bashiri alimuliza
    sijaona.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Ondoa- amba-bila kubadilisha maana. (i) Kuimba ambako kulisifika siku nyingi sasa kunatia shaka (ii) Mibuni ambayo hupandwa wakati wa mvua hustawi(Solved)

    Ondoa- amba-bila kubadilisha maana.
    (i) Kuimba ambako kulisifika siku nyingi sasa kunatia shaka
    (ii) Mibuni ambayo hupandwa wakati wa mvua hustawi

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Nyambua vitenzi vifuatavyo ili kupata majina (nomino) mawili mawili tofauti: (i) Kumbuka ii)Cheka(Solved)

    Nyambua vitenzi vifuatavyo ili kupata majina (nomino) mawili mawili
    tofauti:
    (i) Kumbuka
    ii)Cheka

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika kwa umoja Tumewaondoleeni matatizo yenu, yafaa mtushukuru.(Solved)

    Andika kwa umoja
    Tumewaondoleeni matatizo yenu, yafaa mtushukuru.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Jaza kiambishi kifaacho: Ume__________ ona kalamu nyekundu ziliz_______potea?(Solved)

    Jaza kiambishi kifaacho:
    Ume__________ ona kalamu nyekundu ziliz_______potea?

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Siku hiyo nilipitia mahali hapo kama nilivyokuwa nikimuona siku hizi zote, mwaka nenda mwaka rudi. Nilisimama huku nikishangaa kwa mara nyingine tena. Nilikuwa...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
    Siku hiyo nilipitia mahali hapo kama nilivyokuwa nikimuona siku hizi zote,
    mwaka nenda mwaka rudi. Nilisimama huku nikishangaa kwa mara nyingine
    tena.

    Nilikuwa najitayarisha kujiendea na hamsini zangu mtu huyo alipojipinda kwa
    mbali sana. Kwa hakika nilidhani macho yangu yananihadaa. Nikafikicha macho
    yangu nikitumia nishati yote iliyomo mwilini mwangu ili niyatoe matongo
    ambayo nilituhumu kwamba ni akili yangu tu iliyokuwa imeniadaa, nikaamua
    kuendelea na safari yangu kwenda kujitafutia riziki.

    Hatua ya kwanza na ya pili, moyo haukunipa. Sauti katika kilindi cha moyo
    wangu ikanisihi na kunitafadhalisha nitazame nyuma. Kutupa jicho nyuma,
    nikamnasa mtu huyo akeguka! Nikashtuka sana! Jambo la kwanza nildhani macho
    yangu yameingiwa na kitu kilichoyafanya kuona mambo yasiyokuwepo. Pili,
    nilidhani iwapo niliyoyaona yana msingi wowote, basi huenda ama nina wazimu,
    au yule mtu ni mzuka, hasa kwa vile ilionekana ni mimi tu nimuonaye.
    Nilikikuwa niko katika hali ya kufanya uamuzi kuhusu dhana zangu hizi aina aina
    mtu huyo alipojigeuzageuza, kisha akafunua macho! Moyo ulinienda mbio.
    Nilitaka kutifua vumbi ili wazimu usinizidie, lakini sikupata nafasi. Mtu yule
    alijizoazoa na kuketi kitako. Kisha akatokwa na maneno katika lugha iliyofanana
    sana na Kiswahili. Niliyaelewa aliyokuwa akisema.

    Ajabu ya maajabu, mtu huyo alidai ya kwamba tangu alipolala kivulini hapo
    tangu jana baada ya chakula cha mchana, hakuota ndoto hata moja bali usingizi
    wake ulikuwa mithili ya gogo! Sasa nilikuwa na hakika kwamba ikiwa mimi sina
    wazimu, basi kiumbe yule aliyevaa ngozi iliyochakaa sana katika mpito wa miaka
    hakika ana wazimu. Nilitaka kuhakikisha, hivyo nilimkumbusha kwamba
    amelala mahali hapo kwa muda wa miaka mingi sana.

    Kusikia hayo alianza kunikagua. Akasema nimevaa kizungu. Akanitajia tofauti
    nyingi baina ya vijana aliowazoea na mimi. Mwisho wa yote akauliza kama siku
    hiyo si tarehe kumi na nane mwezi wa pili mwaka wa 1897. Nikadhani anafanya
    mzaha kwa hivyo nikacheka.
    Nilipoona kicheko changu kinamuudhi, nikamwambia siku hiyo ni tarehe kumu
    na nane mwezi wa pili mwaka wa 1997. Nilipoona ameshangaa kwa dhati,
    nikagundua ukweli.
    Alikuwa amelala kwa karne nzima!.

    a) Eleza hoja nne muhimu zinazojitokeza katika aya tatu za mwanzo.
    (Maneno 75-85)
    b) Kwa maneno yako mwenyewe, fupisha aya mbili za mwisho bila
    kubadilisha maana. (Tumia maneno 40-50)

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Mwanamke wa kisasa anazaliwa na kukulia katika mazingira yaliyobadilika mno. Matazamio yake maishani ni tofauti na yale ya wanawake walioishi mapote...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
    Mwanamke wa kisasa anazaliwa na kukulia katika mazingira yaliyobadilika mno.
    Matazamio yake maishani ni tofauti na yale ya wanawake walioishi mapote mawili
    yaliyopita; wanawake makamu ya nyanyake na mamaake-kuu.

    Yeye hatarajii kuzaliwa, kukua, kuolewa, kuwa mke wa bwana, kumzalia watoto, na
    daima dawamu kuwa ‘mwendani wa jikoni’ akawapikia watoto na bwanake chakula; na
    akitoka jikoni aelekee shambani kulima, kichakani kuchanja kuni, mtoni kufua nguo na
    kuteka maji ya kutumia nyumbani. Mwanamke wa kisasa huandamana na mwanamume.
    Akanyangapo mume naye papo huutia wayo wake.

    Mwanamke wa kisasa huenda shule na kujifunza yote yafunzwayo huko. Hushindana na
    wanawake kwa wanaume na kuibuka mshindi si mara haba. Huibuka mshindi katika
    masomo ya lugha, historia, jiografia, hesabu, sayansi na mengineyo, sawa na
    mwanamume.

    Mwanamke wa kisasa hutaka kufanya kazi za kibega, akazifanya. Akataka kuwa
    mwalimu, akawa. Akataka kuwa daktari, akafanikiwa. Almuradi, siku hizi mwanamke
    hufanya kazi yoyote ile afanyayo mwanamume. Kuna wanawake marubani wa ndege,
    masonara, waashi, wahandishi, madereva wa magari, mawakili, mahakimu, mawaziri
    wakuu na hata marais wa nchi. Hakuna kazi isiyofanywa na mwanamke siku hizi.

    Mwanamke wa kisasa hateswi akafyata ulimi. Anapohiniwa yeye hupigania haki yake
    kwa dhati na hamasa. Katu hakubali ‘mahali pake’ katika jamii alipotengewa na
    wanaume wenye mawazo ya kihafidhina yaliyopitwa na wakati.

    Siku hizi mwanamke huolewa tu wakati amepata kazi ya kumwezesha kujikimu maishani
    au pale anapokuwa na hakika kwamba biashara yake, iwapo ni mfanyi biashara, imepiga
    hatua ya kutomrudisha ukutani.

    Mwanamke wa kisasa haamuliwi katika jambo lolote, bali hufanya maamuzi yake
    mwenyewe. Kwa upande mwingine, mwanamume wa ‘kisasa’, ambaye bado amefungwa
    pingu na taasubi za kiume, hapendezwi na mwanamke huyu. Huuma kidole akatamani ya
    kale, lakini wapi! Analazimika kumkubali mwanamke huyu kama mshirika sawa
    maishani, na kuishi naye, apende asipende. Shingo upande analazimika kukubali kwamba
    mabadiliko haya sio mithili ya kiwingu kipitacho, bali ni ya aushi.

    a) Msemo ‘mwendani wa vijungu jiko’ unadhihirisha hali gani ya
    mwanamke katika jamii?
    b) Jamii imemfanya mwanamke kuwa hayawani wa mizigo. Fafanua
    c) Eleza maana ya ‘akanyagapo mume papo huutia wayo wake.’
    d) Zungumzia maswala ya ndoa na elimu huku ukilinganisha mwanamke wa
    kiasili na wa kisasa.
    e) Mwanamume wa kisasa anamwonaje mwanamke wa kisasa?
    f) Taja mifano minne ya ‘mawazo ya kihafidhina.
    g) Eleza maana ya:
    (i) Akafyata ulimu……………………………………………
    (ii) Ukatani…………………………………………………….
    (iii) Taasubi za kiume………………………………………….
    (iv) Aushi…………………….………………………………..

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia kirejeshi ( kihusiano) cha ngeli cha mwisho Mwanafunzi anayefanikiwa maishani ni yule anayesoma kwa bidii na pia anayetii wakuu wake(Solved)

    Andika upya sentensi ifuatayo ukitumia kirejeshi ( kihusiano) cha ngeli cha mwisho
    Mwanafunzi anayefanikiwa maishani ni yule anayesoma kwa bidii na pia
    anayetii wakuu wake

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tumia semi hizi katika sentensi kuonyesha maana: (i) Kuchokoachokoa maneno (ii) Kumeza shubiri(Solved)

    Tumia semi hizi katika sentensi kuonyesha maana:
    (i) Kuchokoachokoa maneno
    (ii) Kumeza shubiri

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunatumia viashiria vya kuthibitisha kwa mfano kitabu kiki hiki. Sasa kamilisha Ni mbwa …………………….. aliyekula chakula cha mtoto(Solved)

    Tunatumia viashiria vya kuthibitisha kwa mfano kitabu kiki hiki. Sasa kamilisha
    Ni mbwa …………………….. aliyekula chakula cha mtoto

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza tofauti mbili muhimu za kimaumbile kati ya wanyama (i) Kifaru (ii) Nyati(Solved)

    Eleza tofauti mbili muhimu za kimaumbile kati ya wanyama
    (i) Kifaru
    (ii) Nyati

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tumia kiulizio – pi – kukamilisha (i) Ni mitume ………………………. Aliowataja? (ii) Ni kiziwi ………………………. . Aliyemwona akipita?(Solved)

    Tumia kiulizio – pi – kukamilisha
    (i) Ni mitume ………………………. Aliowataja?
    (ii) Ni kiziwi ………………………. . Aliyemwona akipita?

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Watu wafuatao wanafanya kazi gani (i) Mhasibu (ii) Mhazili(Solved)

    Watu wafuatao wanafanya kazi gani
    (i) Mhasibu
    (ii) Mhazili

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tumia viunganishi vingine badala ya vile vilivyotumiwa katika sentensi hizi: (i) Anayetafuta hachoki hata akichoka keshapata (ii) Ngonjeeni hadi washiriki wote wafike(Solved)

    Tumia viunganishi vingine badala ya vile vilivyotumiwa katika sentensi hizi:
    (i) Anayetafuta hachoki hata akichoka keshapata
    (ii) Ngonjeeni hadi washiriki wote wafike

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Taja madini mawili ambayo yametukuzwa zaidi, moja kwa thamani yake ya kifedha na nyingine kwa kutengeneza vyuma vigumu kuliko madini mengine(Solved)

    Taja madini mawili ambayo yametukuzwa zaidi, moja kwa thamani yake ya
    kifedha na nyingine kwa kutengeneza vyuma vigumu kuliko madini mengine

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)