Soma makala afuatayo kisha ujibu maswali yanafuata. Katika falme ya Pate ya enzi za kale, kulikuwa n binti Sultani aliyeitwa Mwanakishwira. Alipopata umri wa miaka kumi na...

      

Soma makala afuatayo kisha ujibu maswali yanafuata.
Katika falme ya Pate ya enzi za kale, kulikuwa n binti Sultani aliyeitwa Mwanakishwira.
Alipopata umri wa miaka kumi na mine tu, Mwanakishwira alikuwa tayari ni mrefu na
mkubwa, na alionekana kuwa msichana mzima mwenye umri wa miaka kumi na minane.
Alikuwa nadhifu na mzuri sana wa sura, kiasi cha kubandikwa lakabu ya malaika.
Lipendeza sana macho fauka ya kuwa alikuwa na akili nyingi mno. Katika umri huo,
alikuwa amemaliza masomo yake yote katika madrassa iliyokuwa hapo, na aliweza
kuikariri. Kurhani yote bila kigezigezi. Babake, Mfalme, aliuma videole akilia ngoa kuwa
motto mwenye akili hiyo ni mke wala sio mume. Aliwaza ya kuwa kama angekuwa
mvulana, angempeleleka zutafindaki ya Al-Azhar huko Misri kuendelea na masomo ya
juu katika chuo hicho kisifika.

Wakati mfalme akiuma vidole kuhusu junsia ya motto wake, wanaume wengi hapo mjini
walikuwa wakimeza mate. Mtu aliyememezewa mate alikuwa ni yeye huyo
Mwanakishwira. Walimmezea mate kwa sababu kila mmoja wao alitaka kumwoa awe
mkewe. Kumwoa Mwanakishwira kulikuwa na manufaa ya kupata mke mwenye uzuri
wa shani, kama nyota, na aidha kuwa Mfalme baada ya mwenye kukikalia kuaga dunia,
sababu yeye hakuwa na mrithi mwingine.

Basi ikawa ni kila mtu kujipendekeza kwa mfalme…Kila mtu bila kujali nasaba.
Walijipendekeza wakwasi na mwakata pia. Mwisho Mfalme, Kwa vile alikuwa
anasumbuliwa sana, na wakati huohuo aliogopa kuwa asipomwoza mapema binti yake
huenda akaharibika, akaamua kuruhusu wachumba wamchumbie.

Uamuzi huu ulimshtua sana Mwanakishwira, Mshutuko aliopata ulimtia ugonjwa na
kumdoofisha kabisa. Akadhoofu hadi Mfalme akaingiwa na hofu ya kuwa motto wake
atakufa. Akaamua kumwuliza kinachomdhoofisha. Mwanakishwira. Mwanakishwira
akasema kimdhoofishacho ni mwezi. Akipata mwezi, na nafuu pia ataipata.

Kusikia hivyo, Mfalme akatokwa na kijasho chembachemba. Akafikiria kwamba labda
motto wake amemalizwa kabisa na uwele, na sasa yaweweseka tu, wala hana akili razini
ya kutambua na kupanga mambo.

Hata hivyo hakuvunkika moyo kabisa. Akaamua kupata tafsiri ya kitendawili hicho
kutoka kwa waheshimiwa wake hapo mjini. Ambao wote walitaka mumwoa
Mwanakishwira.

Kwanza akamwendea Waziri Mkuu akamwulia tafsiri ya mwezi autakao binti yake.
Waziri akasema mwezi utakikanao ni wa dhahabu. Alipoambiwa hivyo motto akzidi
kudhoofu. Mfalme akakasirika sana. Akawaendea wakwasi wengine kama vile Kadhi, Mnajimu na Kadhalika. Hawa wote wakamzidisha ugonjwa binti Mfalme kwa sababu
jawabu walizotoa ni kuwa mgonjwa alihitaji mwezi wa almasi, fedha na hata hatua!

Mwisho kabisa, Mfalme akamwendea Mvulana aliyeckuwa mchungaji. Huyu
akamwaidhi Mfalme kwamba aulize mgonjwa aseme mwenyewe aina ya mwezi
aitakayo. Jawabu hili halikumfurahisha Mfalme, japo alienda kamwuliza binti yake,
kama alivyoambiwa. Alipoulizwa Mwanakishwira akasema mwezi autakao ni kishaufu
kilicho na umbo la mwezi mchanga kilichotengenezwa na chuma. Mfalme alishangaa
sana, Hata hivyo akamfulia kisaufu alichokitaka mgonjwa. Alipokivaa, Mwanakishwira
akapata nafuu mara moja na akaendelea na nafuu hiyo hadi akapona kabisa.

Kuona hivyo, Mfalme akawateremsha vyeo wakwasi wote humo mjini, na kuteua
wengine mahali pao. Kwa upande mwingine, mchungaji akaozwa binti Mfalme na
kupewa madaraka ya Waziri Mkuu. Hatimaye, Mfalme alipoaga dunia, mchungaji akawa
Mfalme na Mwanakishwira akawa Malkia.

a) Zungumzia swala la meuke (yaani mahali pa mwanamke au mwanamume katika
jamii) katika falme ya pate ya enzi hiyo.
b) i) Kwa nini Mfale iliwauliza wakwsi kwanza tafsiri ya kitendawili
ii) Kwa nini mfalme alishangazwa na jawabu la binti yake?
c) “Akili ni nywele, kila mtu ana zake” Dhihirisha jinsi methali hii inavyobainika
katika hadithi hii
d) Ni nini maoni yako kuhusu mwanamume aliyemwoa Mwanakishwira na kwa nini
alikubali kuolewa na huyo?
e) Eleza maana ya maneno na tamathali za semi zifuatazo
i) Fauka ya kuwa
ii) Akilia ngoa
iii) Uzuri wa shani
iv) Akamwaidhi

  

Answers


Kavungya
(a) (i) Mwanaume
Alikuwa na uwezo wa kuamua
Alistahili elimu ya juu
Ni mrithi
Ni kiongozi
Ni mwenye akili bora
Alidhaminiwa kuliko bora
Alidhaminiwa kuliko mwanamke
Ni mshauri
(ii) Mwanamke
Hatoi kupata elimu ya juu
Hastahili kurithi mali/ ufalme
Si kiongozi
Wa kuolewa
Ni chombo cha kutamanika
Ana akili dhaifu/ ana akili duni

(b) (i) Kwa nini mfalme aliwauliza wakwasi kwanza tafsiri ya kitendawili
Waliaminika au walidhaminiwa kuwa wenye ujuzi na maarifa
Waliheshimiwa/ Nasaba bora/ Ukoo mzuri
Walikuwa washauri wakuu wa mfalme
Alitarajia mmoja wao amuoe bintiye hoja yeyote iliyokamilika
(ii) Kwa nini Mfalme alishangaza na jawabu la binti yake
Mfalme alitarajia thamani ya tiba iwe kubwa
Kishaufu ni kitu duni

(c) “Akili ni nywele, kila mtu ana zake.” Dhihirisha jinsi methali hii
inavyobainika katika hadithi hii
1. Mwanakishwira alikuwa na akili bora kuliko mfalme/ wakwasi
2. Mchungaji alikuwa na akili nyingi kuliko mfalme
3. Mwanakishwira na mchungaji walikuwa na akili nyingi kuliko wakuasi na
Mfalme
Lazima pande zote mbili zilinganishwe wenye maarifa na wasio maarifa kila
upande.

(d) Ni nini maoni yako kuhusu mwanaume aliyemwona mwanakishwira na
kwa nini alikubali kuolewa na huyo.
1. Mwanaume hana taasubi ya kiume
2. Mchungaji ana akili sawa na Mwanakishwira
3. Mchungaji ndiye alitoa tiba ya ugonjwa wake
4. Mmoja alifumba fumbo (mwanakishwira) na mwingine akafumbua (mchungaji)
Hoja yoyoye moja

(e) (i) Licha ya kuwa/ bali na/ zaidi ya kuwa/ juu ya hayo/ vile vile/ pia/
isitoshe/aidha/ kuongeza
(ii) Akilalamika/ alifura/ alihuzunika/ akisononeka/ akiwa na uchungu aliopita
kiazi
(iii) Uzuri usio fifani/ wa ajabu/ mwingi sana
(iv) Akamshauri/ akampa mawaidha/ akamwasihi/ akamwangazia/
akamwambia/ akamwarifu
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 10:32


Next: Eleza maana ya: i) Juhudi zake hizo si chochote bali ni kutapatapa kwa mfamaji ii) Leo kapasua yote, hata mtama kamwagia kuku.
Previous: UFUPISHO Yusufu Bin Hassan, Mfalme wa mwisho wa halali wa Mombasa, alijitayarisha kuihama himaya yake. Alikuwa amewashinda Wareno, mahasimu wake, vibaya, lakini alijua watarudi na watamwadhibu vikali. Hivyo...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions