UFUPISHO Yusufu Bin Hassan, Mfalme wa mwisho wa halali wa Mombasa, alijitayarisha kuihama himaya yake. Alikuwa amewashinda Wareno, mahasimu wake, vibaya, lakini alijua watarudi na watamwadhibu vikali. Hivyo...

      

UFUPISHO
Yusufu Bin Hassan, Mfalme wa mwisho wa halali wa Mombasa, alijitayarisha kuihama
himaya yake. Alikuwa amewashinda Wareno, mahasimu wake, vibaya, lakini alijua
watarudi na watamwadhibu vikali. Hivyo basi, badala ya kusubiri waje wazitie baruti
nyumba na kuzilipua, badala ya kungojea waje wawachinje raia wake kama kuku, badala
ya kungonja ashuhudie minazi yote kisiwani na miti mingine ya manufaa kukatwa katwa
na makatili hao, badala ya kujitayarisha yeye mwenyewe mji, faua ya kuikatakata miti
yote ili Waareno wakija wasikute chochote cha kuvutia macho na watokomee kabisa.
Alijua asipotekeleza uamuzi huo mkali, basi Wareno watakujja na hasira zote na
kuadhibu waliomo na wasiokuwemo, kama walivyofanya Faza.

Unyama uliofanyika huko alikuwa ameusikia ukisimuliwa mara zisizohesabika. Katika
masimulizi hayo, alikuwa amesikia ya kwamba Falme hiyo ya Faza ilipoasi utawala wa
Kireno, askari wa Kireno, chini ya uongozi wa Martin Affenso de Mello, walifanya
unyama hapo mjini Faza ambao ulikuwa haujawahi kutokea, hata katika mawazo.
Inavyosemekana ni kwamba Wareno waliamua kuangamiza chochote chenye uhai, hata
wanyama na miti na wakautimiza muradi wao. Ajabu ni kwamba, hata kasisi
aliyeheshimika sana wa Kireno enzi hizo, Baba Joao dos Santos, aliunga mkono tukio hili
akisema ya kwamba wafaza walistahili kuadhibiwa. Hakuna mtu hata mmoja upande wa
Wareno aliyekilaani kitendo hiki cha kutisha.

Hii ndiyo sababu Mfalme Yusuf na raia wake walipowazima wareno hapo Mombasa,
aliwaamuru watu wajitolee kuwashabulia kwenye vituo vyao vyote kaitika mwabao
mzima wa mashariki ya Afrika. Baada ya kuamua hivyo, alienda Uarabun kutafuta silaha
ili atekeleze azimio lake.

Alipopata zana za kutosha, ikiwa ni pamoja na silha na meli, alianza kupambana na
wareno kuo huko Arabuni, mahali pitwapo Shihr. Halafu alielekea mwambao wa pwani
ya AFrika aliwasumbua sana maadui zake, Mwisho alikita makao yake Bukini ambako
aliendelea kuwashambulia Wareno kokote walikokuwa.

a) Eleza sababu zilizomfanya Mfalme Hassan kuuangamiza mji wake, na halafu
kuuhama (maneno 30-40)
b) Ukitumia Maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana, fupisha kuanzia aya
ya pili hadi mwisho wa kifungu (maneo 75-80)

  

Answers


Kavungya
(a) (i) Alikuwa amewashinda wareno mahasimu wake na kwa hivyo wangendi
kumwadhibu vikali
(ii) Ili Wareno wakija wakija wasikute chochote cha kuwavutia macho na
watukomee kabisa
(iii) Hakutaka yaliyowapata wafaza yampate yeye na watu wake.

(b) (i) Faza alipoasi utawala wa Kireno aliangamizwa kinyama/ faza ilipoasi
utawala wa Kireno Wareno waliangamiza chochote chenye uhai
(ii) Kila mreno hata kasisi aliunga mkono tokeo hili/ hakuna mreno hata
mmoja aliyekilaani kitendo hiki.
(iii) Mfalme Yusuf baada ya kuwashinda Wareno aliwaamuru watu wake
wahame aungamize mji ili wareno warudipo wasipate chochote cha
kuwavutia.
(iv) Aliamua kuwashambulia Wareno katika vyao vyote katika mwambao
mzima wa mashariki ya Afrika.
(v) Alienda Uarabuni kutafuta silaha
(vi) Alianza kuwashambulia Wareno kuko huko uarabuni kisha akaendelea
kuwashambulia katika mwambao wa Afrika mashariki na kokote
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 10:35


Next: Soma makala afuatayo kisha ujibu maswali yanafuata. Katika falme ya Pate ya enzi za kale, kulikuwa n binti Sultani aliyeitwa Mwanakishwira. Alipopata umri wa miaka kumi na...
Previous: Kwa kutumia kirejeshi kifaacho, rekebisha sentensi ifuatayo kwa njia mbili tofauti. Yule ndiye mkwasi ambaye aliyenusurika.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Soma makala afuatayo kisha ujibu maswali yanafuata. Katika falme ya Pate ya enzi za kale, kulikuwa n binti Sultani aliyeitwa Mwanakishwira. Alipopata umri wa miaka kumi na...(Solved)

    Soma makala afuatayo kisha ujibu maswali yanafuata.
    Katika falme ya Pate ya enzi za kale, kulikuwa n binti Sultani aliyeitwa Mwanakishwira.
    Alipopata umri wa miaka kumi na mine tu, Mwanakishwira alikuwa tayari ni mrefu na
    mkubwa, na alionekana kuwa msichana mzima mwenye umri wa miaka kumi na minane.
    Alikuwa nadhifu na mzuri sana wa sura, kiasi cha kubandikwa lakabu ya malaika.
    Lipendeza sana macho fauka ya kuwa alikuwa na akili nyingi mno. Katika umri huo,
    alikuwa amemaliza masomo yake yote katika madrassa iliyokuwa hapo, na aliweza
    kuikariri. Kurhani yote bila kigezigezi. Babake, Mfalme, aliuma videole akilia ngoa kuwa
    motto mwenye akili hiyo ni mke wala sio mume. Aliwaza ya kuwa kama angekuwa
    mvulana, angempeleleka zutafindaki ya Al-Azhar huko Misri kuendelea na masomo ya
    juu katika chuo hicho kisifika.

    Wakati mfalme akiuma vidole kuhusu junsia ya motto wake, wanaume wengi hapo mjini
    walikuwa wakimeza mate. Mtu aliyememezewa mate alikuwa ni yeye huyo
    Mwanakishwira. Walimmezea mate kwa sababu kila mmoja wao alitaka kumwoa awe
    mkewe. Kumwoa Mwanakishwira kulikuwa na manufaa ya kupata mke mwenye uzuri
    wa shani, kama nyota, na aidha kuwa Mfalme baada ya mwenye kukikalia kuaga dunia,
    sababu yeye hakuwa na mrithi mwingine.

    Basi ikawa ni kila mtu kujipendekeza kwa mfalme…Kila mtu bila kujali nasaba.
    Walijipendekeza wakwasi na mwakata pia. Mwisho Mfalme, Kwa vile alikuwa
    anasumbuliwa sana, na wakati huohuo aliogopa kuwa asipomwoza mapema binti yake
    huenda akaharibika, akaamua kuruhusu wachumba wamchumbie.

    Uamuzi huu ulimshtua sana Mwanakishwira, Mshutuko aliopata ulimtia ugonjwa na
    kumdoofisha kabisa. Akadhoofu hadi Mfalme akaingiwa na hofu ya kuwa motto wake
    atakufa. Akaamua kumwuliza kinachomdhoofisha. Mwanakishwira. Mwanakishwira
    akasema kimdhoofishacho ni mwezi. Akipata mwezi, na nafuu pia ataipata.

    Kusikia hivyo, Mfalme akatokwa na kijasho chembachemba. Akafikiria kwamba labda
    motto wake amemalizwa kabisa na uwele, na sasa yaweweseka tu, wala hana akili razini
    ya kutambua na kupanga mambo.

    Hata hivyo hakuvunkika moyo kabisa. Akaamua kupata tafsiri ya kitendawili hicho
    kutoka kwa waheshimiwa wake hapo mjini. Ambao wote walitaka mumwoa
    Mwanakishwira.

    Kwanza akamwendea Waziri Mkuu akamwulia tafsiri ya mwezi autakao binti yake.
    Waziri akasema mwezi utakikanao ni wa dhahabu. Alipoambiwa hivyo motto akzidi
    kudhoofu. Mfalme akakasirika sana. Akawaendea wakwasi wengine kama vile Kadhi, Mnajimu na Kadhalika. Hawa wote wakamzidisha ugonjwa binti Mfalme kwa sababu
    jawabu walizotoa ni kuwa mgonjwa alihitaji mwezi wa almasi, fedha na hata hatua!

    Mwisho kabisa, Mfalme akamwendea Mvulana aliyeckuwa mchungaji. Huyu
    akamwaidhi Mfalme kwamba aulize mgonjwa aseme mwenyewe aina ya mwezi
    aitakayo. Jawabu hili halikumfurahisha Mfalme, japo alienda kamwuliza binti yake,
    kama alivyoambiwa. Alipoulizwa Mwanakishwira akasema mwezi autakao ni kishaufu
    kilicho na umbo la mwezi mchanga kilichotengenezwa na chuma. Mfalme alishangaa
    sana, Hata hivyo akamfulia kisaufu alichokitaka mgonjwa. Alipokivaa, Mwanakishwira
    akapata nafuu mara moja na akaendelea na nafuu hiyo hadi akapona kabisa.

    Kuona hivyo, Mfalme akawateremsha vyeo wakwasi wote humo mjini, na kuteua
    wengine mahali pao. Kwa upande mwingine, mchungaji akaozwa binti Mfalme na
    kupewa madaraka ya Waziri Mkuu. Hatimaye, Mfalme alipoaga dunia, mchungaji akawa
    Mfalme na Mwanakishwira akawa Malkia.

    a) Zungumzia swala la meuke (yaani mahali pa mwanamke au mwanamume katika
    jamii) katika falme ya pate ya enzi hiyo.
    b) i) Kwa nini Mfale iliwauliza wakwsi kwanza tafsiri ya kitendawili
    ii) Kwa nini mfalme alishangazwa na jawabu la binti yake?
    c) “Akili ni nywele, kila mtu ana zake” Dhihirisha jinsi methali hii inavyobainika
    katika hadithi hii
    d) Ni nini maoni yako kuhusu mwanamume aliyemwoa Mwanakishwira na kwa nini
    alikubali kuolewa na huyo?
    e) Eleza maana ya maneno na tamathali za semi zifuatazo
    i) Fauka ya kuwa
    ii) Akilia ngoa
    iii) Uzuri wa shani
    iv) Akamwaidhi

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya: i) Juhudi zake hizo si chochote bali ni kutapatapa kwa mfamaji ii) Leo kapasua yote, hata mtama kamwagia kuku.(Solved)

    Eleza maana ya:
    i) Juhudi zake hizo si chochote bali ni kutapatapa kwa mfamaji
    ii) Leo kapasua yote, hata mtama kamwagia kuku.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Kamilisha: i) Bumba la …………………….. ii) Genge la……………………..(Solved)

    Kamilisha:
    i) Bumba la ……………………..
    ii) Genge la……………………..

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi tatu zikionyesha maana tatu za neno chungu.(Solved)

    Tunga sentensi tatu zikionyesha maana tatu za neno chungu.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Taja methali inayoafikiana na maelezo haya: i) Wengine wanapoozana na kugombana, kunao wanaofurahia kabisa hali hiyo. ii) Afadhali kuhudhuria huo mkutano hata kama umechelewa(Solved)

    Taja methali inayoafikiana na maelezo haya:
    i) Wengine wanapoozana na kugombana, kunao
    wanaofurahia kabisa hali hiyo.
    ii) Afadhali kuhudhuria huo mkutano hata kama umechelewa

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunawaitaje watu hawa? (i) Mtu anayebeba mizigo kwa ujira (ii) Mtu anayeshughulikia elemu ya nyota(Solved)

    Tunawaitaje watu hawa?
    (i) Mtu anayebeba mizigo kwa ujira
    (ii) Mtu anayeshughulikia elemu ya nyota

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Sahihisha sentensi hizi: (i) Bahasha ilionunuliwa jana ni kubwa na mzuri (ii) Mananasi hizi zinauzwa ghali kwa sababu zimeiva vizuri sana(Solved)

    Sahihisha sentensi hizi:
    (i) Bahasha ilionunuliwa jana ni kubwa na mzuri
    (ii) Mananasi hizi zinauzwa ghali kwa sababu zimeiva vizuri sana

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika upya sentensi zifuatazo ukitumia neno amba (i) Kijiti kilichovunjika kilimwumiza Amina guu kenyaplex (ii) Barua zitakazoandikwa na baba kesho zitatumwa mwaka ujao.(Solved)

    Andika upya sentensi zifuatazo ukitumia neno amba
    (i) Kijiti kilichovunjika kilimwumiza Amina guu kenyaplex
    (ii) Barua zitakazoandikwa na baba kesho zitatumwa mwaka
    ujao.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika kwa wingi: (i) Uta wake ni mrefu na mkubwa sana (ii) Merikebu itayokayofika kesho itango’a nanga kesho kutwa.(Solved)

    Andika kwa wingi:
    (i) Uta wake ni mrefu na mkubwa sana
    (ii) Merikebu itayokayofika kesho itango’a nanga kesho kutwa.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Taja na ubainishe aina za viwakilishi katika sentensi zifuatazo (i) Ile minazi yangu niliyopalilia inakua vizuri (ii) Mimi ninataka kumwona mwanariadha aliyepata nishani ya dhahabu(Solved)

    Taja na ubainishe aina za viwakilishi katika sentensi zifuatazo
    (i) Ile minazi yangu niliyopalilia inakua vizuri
    (ii) Mimi ninataka kumwona mwanariadha aliyepata nishani ya
    dhahabu

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi ukionyesha matumizi ya vitenzi vya silabi moja katika jinsi ya kutendesha ukitumia silabi hizi (i) -la (ii) nywa (iii) fa(Solved)

    Tunga sentensi ukionyesha matumizi ya vitenzi vya silabi moja
    katika jinsi ya kutendesha ukitumia silabi hizi
    (i) -la
    (ii) nywa
    (iii) fa

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi moja moja ukitumia alama zifuatazo za uakifishaji (i) Ritifaa (ii) Parandesi (iii) Dukuduku (iv) Mshangao.(Solved)

    Tunga sentensi moja moja ukitumia alama zifuatazo za uakifishaji
    (i) Ritifaa
    (ii) Parandesi
    (iii) Dukuduku
    (iv) Mshangao.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika kwa msemo halisi Yohana alisema kwamba njiani kulikuwa kumenyesha sana ndio sababu tulichekelewa(Solved)

    Andika kwa msemo halisi
    Yohana alisema kwamba njiani kulikuwa kumenyesha sana ndio sababu tulichekelewa

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Taja vielezi vinavyopatikana katika sentensi hizi; kisha ueleze ni vielezi vya aina gani (i) Aliamka alfajiri (ii) Mtu huyu ni hodari sana(Solved)

    Taja vielezi vinavyopatikana katika sentensi hizi; kisha ueleze ni vielezi vya aina gani
    (i) Aliamka alfajiri
    (ii) Mtu huyu ni hodari sana

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Kamilisha jedwali ukifuatia mfano uliopewa Wimbo Mwimbaji Uimbaji Jengo ……………. ………. Pendo ……………. ……….(Solved)

    Kamilisha jedwali ukifuatia mfano uliopewa
    Wimbo Mwimbaji Uimbaji
    Jengo ……………. ……….
    Pendo ……………. ……….

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Kamilisha jedwali ukifuatia mfano uliopewa Wimbo Mwimbaji Uimbaji Jengo ……………. ………. Pendo ……………. ……….(Solved)

    Kamilisha jedwali ukifuatia mfano uliopewa
    Wimbo Mwimbaji Uimbaji
    Jengo ……………. ……….
    Pendo ……………. ……….

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza tofauti iliyopo katika jozi hii ya sentensi. Alimpatia soda ya chupa Alimpatia soda kwa chupa.(Solved)

    Eleza tofauti iliyopo katika jozi hii ya sentensi.
    Alimpatia soda ya chupa
    Alimpatia soda kwa chupa.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Raha ni kitu gani? Je, ni kitu kizuri au kibaya? Mbona kila mutu hipigania na kama ionekanavyo, kila aionjaye hatimaye humwunguza?...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
    Raha ni kitu gani? Je, ni kitu kizuri au kibaya? Mbona kila mutu hipigania na
    kama ionekanavyo, kila aionjaye hatimaye humwunguza? Au pengine wako
    wengine wasiooungua? Hebu basi tuzingatie wale wasemekanao huitafuta sana
    raha na, penginepo wakafanikiwa kuipate.

    Chukua mfano wa msichana na mvulana wapendanao. Hawa wawili
    wanapopendana, lengo lao huwa ni kuoana na wakishaoana, waishi raha
    mustarehe milele na milele. Hata hivyo, jambo la kwanza ni kwamba, hata kabla
    hawajaoana, wanadhikika na kudhikishana kwa kutaka sana kuaminiana si mara
    haba wakati wakiwa wapenzi mar. Mara kadha wa kadha husameheanana
    kuendelea na mapenzi. Baadaye wakiwa na bahati, huona.

    Mara tu wanapooana hugundua kuwa huko kuishi raha mustarehe ilikuwa ni
    ndoto tu ya ujana iliyotengana kabisa na uhalisia. Uhalisia unapowabinikia huwa
    ni kuendelea na huko kudhikishana,kutoridhishana, kutiliana shaka, kuombona
    mamaha na kuendelea tu.

    Ama tumwangalie mwanasiasa. Huyu anapigania usiku na mchana ili awe
    mjumbe. Mwisho anachanguliwa, lakini afikapo bunge, anakuta hakuna
    anayemtambua kama bwana mkubwa. Inambainikia kwamba ubawana- Mkubwa
    hautegemei kuchaguliwa tu, bali unategemea mambo mengine pia, kama vile pesa
    nyingi, magari makibwa, sauti katika jamii na wadhamini wanotambulikana. Raha
    kwa mwanasiasa huyu inakuwa mithili ya mazigzi tu, “maji” uyaonayo kwa mbali
    wakati una kiu kali sana, kumbe si maji bali ni mmemetuko wa jua tu.

    Mwingine wa kupigiwa mfano ni msomi. Huyu huanza bidii yake akiwa mdogo
    sana. Lengo lake huwa ni atambuliwe kote kwa uhohadri wake katika uwanja wa
    elimu. Basi mtu huyu husoma mpaka akaifikia daraja ya juu kabisa ya usomaji.
    Akapata shahada tatu: ya ukapera, ya uzamili nay a uzamifu. Akajiona yu upeoni
    mwa ulimwengu. Akatafuta kazi akapata. Kisha akagundua kwamba watu
    hawakijali sana kisomo chake. Wakamwona ni kama mwehu tu. Fauka ya hayo
    wakamlumu kwa kupoteza muda wake mwingi kupekuapekua vitabu.
    Wakamfananisha na mtu mvivu.

    Mwisho tuangalie mfano wa mwanamuziki . Huyu anahaghaika na wazo la
    kwamba sauti yake ikiwaonga watu, atapendwa sana na wengi na kuwazuzua
    wengi kama mbalamwezi au kuwaongoza kama nyota. Mtu huyu anapofikia kilele
    cha malengo yake hata husahau kama ni binadamu wa kawaida, akawa anaishi
    katika muktadha wa watu kuzirai kwa sababu ya akili kujawa pomoni na upungaji
    wake. Watu hutamani hata kumgusa tu. Hata hivyo, mtu huyu huishis kujisikia
    mkiwa pale wakati unapowadia wa kupumzika. Je, raha yote huwa imekimbilia
    wapi?

    a) “Mapenzi ni kuvumiliana.” Kwa maneno yako mwenyewe, eleza jinsi
    msemo huu ulivyo muhtasari mwafaka way a pili nay a tatu ya habari hii.
    (Maneno 30-35)
    b) Kwa muhtasari, raha ni “asali chungu. “Fafanua dai hili huku ukirejelea
    mwanasiasa, msomi na mwanamuziki (maneno 45-55)

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali Nchi nyingi za ulimwengu unaoendelea, au ule uliokuwa ukiitwa ulimwengu wa ta zimegawika sehemu mbili mbili. Sehemu hizi zinazidi kutoshabihiana kila...(Solved)

    Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali
    Nchi nyingi za ulimwengu unaoendelea, au ule uliokuwa ukiitwa ulimwengu wa ta
    zimegawika sehemu mbili mbili. Sehemu hizi zinazidi kutoshabihiana kila uchao
    zinatengana kiasi cha kukaribia kupigwa mfano wa masafa ya ardhi na mbingu. Seher
    zenyewe ni mijini na mashabani. Sehemu hizi, hasa ukizitia katika mizani ya hali na jia
    za watu za maisha, zimetofautiana mno. Kiasi cha tofauti hizi ni kikubwa hadi
    kuonekana kama kwamba hazina uhusiano kamwe, mithili ya nchi mbili tofauti.

    Hebu sasa tuzingatie yale yana yozifanya sehemu hizi kukosa kufanana. Hapa
    tutawajibika kuzizingatia tofauti zilizo bayana baina ya watu wa shamba na wa mijini,
    hasa kufungamana na jinsi wanavyoyaendesha maisha yao.

    Jambo lililo wazi ni kwamba watu wa mashambani hawajapiga hatua ya maana kuhusu
    jinsi wanavyuotakikana kuishi katika karne ya ishirini. Watu hawa bado wanaishi kama
    walivyoishi mababu zao. Hawahisi halahala ya jambo lolote. Mategemeo yao ni shamba;
    usubiriwe msimu mzuri wa mvua, watu walime, Mungu akineemeshe kilimo, wavune
    mavuno mema, Chakula kikiwa tayari, wale, walale, siku nyingine warudie mkondo uo
    huo wa kuendesha maisha yao.

    Watu hawa maisha yao yamepangika mikondo mitatu tu: kuzaliwa, kuoa au kuolewa, na
    kufa. Zaidi ya mikondo hii, maisha ya viumbe hawa hayana mabadiliko makubwa.
    Mabadiliko haypendelewi sana huko mashambani. Huko, wanaume ni mabwana,
    wanawake ni mfano wa vijakazi na watoto hawana tofauti kubea na watwana. Mwanume
    akikohoa, mkewe akimbilie kulikokoholewa, na watoto watetemeke. Wanawake wa
    shamba na watoto hawana haki hata ya kunena, wala hawajui haki ni nini.

    Kwa upande mwingine, mijini kuna viwanda, kuna majumba, kuna magari na kuna
    vyombo vingi sana vya maendeleo ya kisiku izi. Watu wa mijini ni watu wa ulimwengu
    kote, wala si watu wa mji mmoja tu. Watu wa mji wowote ulimwenguni huweza
    kuwasiliana na wenzao wa miji mingine kokote kule ulimwenguni kwa njia ya runinga.
    Pia, kwa watu wa mjini, kuona kiumbe kidogo kabisa kisichoweza kuonekana kwa
    macho si ibura hata. Kiumbe cha namna hiyo huonekana kupitia mangala. Na kwa wale
    walioondokea kuwa wanajimu wa kisasa, kuziona sayari na thurea zilizoko mbali sana
    nasi kupitia ningala ni jabo la kawaida sana.

    Watu wa mjini huwa na mabadiliko mengi sana katika maisha yao, wala sio mikondo
    aina tatu tu. Kwa mfano, wanawake wa mijini hawakubali tena kuonewa na wanaume.
    Wanajua vyema sana maslahi yao na wameiweka menke yao mbele; yaani mahali pao
    katika jamii, wakiwa wao ni wanawake. Kupigania haki sawa na wanaume bila kulegeza
    kamba. Huku kupambana kimaisha kama wapambanavyo wanaume na kufanikiwa kufanya kazi za kusikika kam vile uwakili, udaktari, uhandisi, urubani na nyinginezo
    zilizokuwa zikifanywa na wanaume tu. Wanawake wengine hata ni maprofesa! Kweli
    watu wa mijini wameendelea.

    a) Toa maelezo kuhusu tofauti zinazosemekana ni bayana baina ya maisha ya watu
    wa shamba nay ale ya watu wa mijini.
    b) Rejelea “Mungu” katika aya ya tatu na neon “viumbe” katika aya ya nne.
    Bainisha uhusiano uliopo baina ya manen haya mawili, hasa ukizingatia jinsi
    yavyotumiwa katika habari. Je matumizi haya yankupa hisia gani?
    c) Unadhani mwandishi ana maana gani anaposema ya kwamba huko mashambani
    “wanawake ni mfano wa vijakazi, na watoto hawana tofauti kubwa na watwana?”
    d) Orodhesha vifaa vyovyote vitano vilivyotajwa katika taarifa hii, kisha ueleze
    umuhimu wa kila kimoja wapo.
    e) “Watu wa mijini ni watu wa ulimwengu kote” Hapa mwandishi anamaanisha
    nini?
    f) (i) Ni nini maana ya neon menke?
    (ii) Mwandishi anamaliza taarifa yake kwa kusema “Kweli watu wa mijini
    wameendelea.” Kwa muhtasari, ni tabia gani za wanamiji zilizomfanya
    kukiri hivyo.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Kiambishi- U-hutambulisha majina yote ya ngeli ya U (umoja). Hata hivyo baadhi majina hay huchukua viambishi tofauti tofauti katika wingi. Orodhesha majina ma kama hayo, kisha uonyeshe...(Solved)

    Kiambishi- U-hutambulisha majina yote ya ngeli ya U (umoja). Hata
    hivyo baadhi majina hay huchukua viambishi tofauti tofauti katika wingi.
    Orodhesha majina ma kama hayo, kisha uonyeshe viambilshi hivyo tofauti
    vya ngeli (Katika umoja na Wingi)

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)