Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Kati ya viumbe wote waishio ulimwenguni, hakuna kiumbe aliyepevuka mawazo kama binadamu. Kiumbe huyu amewapiku wale wengine kwa njia nyingi, hata...

      

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Kati ya viumbe wote waishio ulimwenguni, hakuna kiumbe aliyepevuka mawazo kama
binadamu. Kiumbe huyu amewapiku wale wengine kwa njia nyingi, hata kuweza
kuwatawala na kuwapangia maisha yao. Binadamu amekirimiwa uwezo wa kuyatawala
mazingira na kukabidhiwa hekima ya kuweza kusana ala mbalimbali ili kuyakabili
mazingira hayo. Hekima hii humwezesha kusitiri kizazi chake.

Aidha, ametunukiwa uwezo mkubwa wa kuivinjari sayari hii yetu katika ilhamu yake ya
kutaka kuvumbua ‘siri’ za maumbile, amejasiri hata kuzitalii sayari nyingine nje ya uso
wa ulimwengu huu. Si ajabu kwamba iwapo wanyama wengine wangepewa urazini wa
kuongea kama yeye, wangalimwandikia tumbi la vitabu kusiuf busara yake. Sifa za
ujasiri wake kamwe hazingewatoka vinywani mwao!

Hata hivyo, kuna tofauti nyingine kubwa kati ya binadamu na hayawani, Tofauti hii
inaweza kumvua binadamu sifa zake zote na kuuona ukwasi wa maarifa yake kama
ishare ya maangamizi ya ulimwengu. Hii ni kutokana na hasara anayosababisha katika
mazingira tulivu walivyoumbiwa viumbe wote.

Uzuri wa ulimwengu tunamoishi humpendeza kila kiumbe hata yule anayemchukia
binadamu kama nzi. Wote hufurahia mazingira yao; hewa safi itokayo milimani,
chemichemi, mito na vijito mnamotiririka maji safi, vilele vya milima vilivyokumbatiwa
na theluji daima dahari, yakiwemo mabonde na tambarare zinazohimili uhai wa viumbe
wengi.

Urembo huo wa kiasili hauwezi kukamilika bila vichaka na misitu inayoipamba sayari hii
huku ikileta mvua. Mapambo yote haya huendeshwea na nguvu za maumbile; nguvu
ambazo hazisababishwi na kuwa hatari kwa uhai wake na ule wa viumbe wenzake kwa
sababu anayaharibu maumbile kwa kiasi kikubwa kinachomtisha yeye mwenyewe. Hii ni
kwa sababu gani? Sababu zipo nyingi.

Sababu mojawapo ni uchafuzi wa maji kama rasimali muhimu ya kiasili. Uchafuzi huu
umewaletea viumbe na mimea maafa mengi, yakiwemo maradhi mbalimbali. Kwa kweli
bila maji, uhai utatoweka duniani. Uharibifu mkubwa wa maji machafu yenye sumu hasa
kutoka viwandani na kuingia kwenye mito na bahari, huwadhuru biumbe wengine ambao
makao yao ni majini. Maji huleta madhara si tu kwa mimea bali hat kwa binadamu
kupitia kwa ulaji wa vyakula.

Misituni rasilimali nyngine inayokimu viumbe, lakini binadamu anaiponza. Ukataji wa
miti kiholela hasa kwenye sehemu za chmichemi husababisha uhaba wa mvua. Uhaba
huo nao huleta kiangazi kinachokausha mimea na visima vya maji. Mchapuko wa ujenzi wa viwanda hasa katika nchi zilizostawi wanasayansi wanaohusika na hali za anga
umesababisha taharuki na wasiwasi mwingi. Hii ni kwa sababu umenyosha kuwa ule
utandu unaozuia miale ya jua kupenya moja kwa moja kweye sayari hii na juhatarisha
uhai, sasa unaanza kutoweka taratibu. Hii ni kutokana na hewa chafu itokayo viwandani.
Kwa kadri binadamu anavyozidi kujiimarisha kiviwanda ndivyo ambavyo mabaki
yaviwanda yanavyozidi hatua hii, ni binadamu atakuwa amechangia pakubwa katika
kutowesha uhai wa viumbe wote ulimwenguni.

Mikutano mingi ya kmataifa imefanywa nab ado inaendelea kufanywa kila uchao ili
kutahadharisha umma wa ulimwengu dhidi ya uharibifu wa mazingira na mali asili.
‘Ajenda’ za mikutano hiyo hasa zinalenga nchi zilizostawi kwani hizi ndizo zinazochafua
mazingira kwa kasi zaidi kuliko zile zinazostawi . Mapendekezo mengi yametolewa
katika vikao hivyo ili kusuluhisha tatizo hili lakini ni hatua chache mno zinazochuliwa
kurekebisha mamba.

Inatupasa sisi wenyewe kuchukua jukumu la kusafisha mazingira yetu. Tuwafunze pia
watoto wetu kuhifadhi mazingira yanapochafuliwa au kuharibiwa. Tukumbuke kuwa
Mwana hufuata kisogo cha nina.Mazingira yanpochafuliwa au kuharibiwa, afya zetu
zimo hatarini, na hali hii pia ni tisho kwa viumbe wengine, hata vimatu! Kila mmoja
wetu anawajibika kutunza mazingira anamoishi kwa manufaa yetu sote na kwa vizazi
vijavyo.

a) Kulingana na taarifa hii, kwa nini binadamu anahesabiwa kuwa na uharibifu
mkubwa kushinda wanyama wengine?
b) Onyesha uhusiano uliopo baina ya maendeleo ya binadamu na uharibifu wa
mazingira.
c) Ni kwa nini mwandishi anahofia zaidi athari za miale ya jua?
d) Eleza kwa ufupi hasara zinazoweza kusababishwa na uharibifu wa mazingira.
e) taja hatua mbili ambazo mwanadamu angeweza kuchukua ili kupunguza madhara
ya viwanda.
f) Kulingana na makala haya ni nini maana ya methali “mwana hufuata kisogo cha
nina?”
g) Eleza maana ya
(i) Kusana
(ii) Mchapuko

  

Answers


Kavungya
(a) Kutokana na busara yake/ urazini/ hekima/ uwezo wake/ maarifa yake ya
kuweza kuyatawala mazingira. Binadamu anasababisha hasara/ anahatarisha
maisha ya viumbe vyote/ anaharibu mazingira akisingizia maendeleo
(Akiegemea upande wa maarifa akose kutaja matendo ya uharibifu mpe alama
2) Akiegemea pande zote mbili mpe
(b) Binadamu hujaribu kujiimarisha kimaisha kwa kukata miti kutegemea bidhaa
viwandani na hivyo kusababisha ukosefu wa mvua, kuwepo kwa jangwa,
ukataji wa miti uchafuzi wa maji, uchafuzi wa hewa, maji yakitiririka kwa
mito yanaleta madhara mbalimbali.
(c) Itaangamiza maisha ya viumbe vyote
Miale ya jua yenye smu itatufikia moja kwa moja na kutowesha uhai wa
viumbe vyote.
Miale ya jua itaangamiza/ itatowesha uhai/ kusababisha maafa/ kuhatarisha
uhai.
(Wazo la kutoa uhai lijitokeze)
(d) Kusababisha ukosefu wa mvua/ uhaba wa mvua
Maafa yameimei au viumbe pamoja ya maradhi
Uhai utotoweka duniani
Kuwadhuru viumbe wa majini
Madhara kwa mimea na binadamu kupitia kwa ulaji wa vyakula
Kiangazi/ kukauka kwa mimea na visima vya maji
Uharibifu wa utandu
(e) Sisi wenyewe kuchukua jukumu la kusafisha mazingira yetu
Kuwafunza watoto kuhifadhi mazingira yao ni kuyaweka safi
Kutahadharisha umma wa ulimwengu dhidi ya uharibifu wa mazingira na
mali asili
Kuzuia hewa yenye sumu kutoka viwandani na kuzuia kusambaa kwa gesi
Kusafisha maji yaendayo mitoni
Kujenga viwanda mbali na makao ya wanadamu
(f) Mtoto hufuata maagizo (tabia na mwenendo) wa mamaye/ mtoto hufuata
tabia ya mamaye.
(g) (i) Kusana- kutengeneza/ kuvumba kuanda/ kubuni/ kuzua
(ii) Mchapuko- kuongezeka kwa kasi/ kwa haraka/ kuibuka kwa kasi upesi
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 11:11


Next: Geuza sentensi hizi kutoka msemo wa taarifa hadi msemo halisi i) Mama alisema nichukue nafaka yetu nikauze sokoni ii) Mwalimu aliomba aletewe vitabu vyake kutoka darasani
Previous: Eleza maana mbili tofauti za sentensi hii Wenzake wamelipwa pesa zao, yeye bado amelala

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions