Eleza katika sentensi maana ya misemo ifuatayo (i) Uso wa chuma (ii) Kuramba kisogo

      

Eleza katika sentensi maana ya misemo ifuatayo
(i) Uso wa chuma
(ii) Kuramba kisogo

  

Answers


Kavungya
(i) Uso wa chuma
Sentensi ionyeshe uso usionyeshe hisia zozote
(ii) Kuramba kisogo
Sentensi yaonyesha kusengenya kwa kutumia ishara
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 11:20


Next: Eleza maana mbili tofauti za sentensi hii Wenzake wamelipwa pesa zao, yeye bado amelala
Previous: Andika visawe ( maneno yenye maana sawa) vya maneno haya: (i) Sarafu (ii) Keleji. (iii) Daktari.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Eleza maana mbili tofauti za sentensi hii Wenzake wamelipwa pesa zao, yeye bado amelala(Solved)

    Eleza maana mbili tofauti za sentensi hii
    Wenzake wamelipwa pesa zao, yeye bado amelala

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Kati ya viumbe wote waishio ulimwenguni, hakuna kiumbe aliyepevuka mawazo kama binadamu. Kiumbe huyu amewapiku wale wengine kwa njia nyingi, hata...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
    Kati ya viumbe wote waishio ulimwenguni, hakuna kiumbe aliyepevuka mawazo kama
    binadamu. Kiumbe huyu amewapiku wale wengine kwa njia nyingi, hata kuweza
    kuwatawala na kuwapangia maisha yao. Binadamu amekirimiwa uwezo wa kuyatawala
    mazingira na kukabidhiwa hekima ya kuweza kusana ala mbalimbali ili kuyakabili
    mazingira hayo. Hekima hii humwezesha kusitiri kizazi chake.

    Aidha, ametunukiwa uwezo mkubwa wa kuivinjari sayari hii yetu katika ilhamu yake ya
    kutaka kuvumbua ‘siri’ za maumbile, amejasiri hata kuzitalii sayari nyingine nje ya uso
    wa ulimwengu huu. Si ajabu kwamba iwapo wanyama wengine wangepewa urazini wa
    kuongea kama yeye, wangalimwandikia tumbi la vitabu kusiuf busara yake. Sifa za
    ujasiri wake kamwe hazingewatoka vinywani mwao!

    Hata hivyo, kuna tofauti nyingine kubwa kati ya binadamu na hayawani, Tofauti hii
    inaweza kumvua binadamu sifa zake zote na kuuona ukwasi wa maarifa yake kama
    ishare ya maangamizi ya ulimwengu. Hii ni kutokana na hasara anayosababisha katika
    mazingira tulivu walivyoumbiwa viumbe wote.

    Uzuri wa ulimwengu tunamoishi humpendeza kila kiumbe hata yule anayemchukia
    binadamu kama nzi. Wote hufurahia mazingira yao; hewa safi itokayo milimani,
    chemichemi, mito na vijito mnamotiririka maji safi, vilele vya milima vilivyokumbatiwa
    na theluji daima dahari, yakiwemo mabonde na tambarare zinazohimili uhai wa viumbe
    wengi.

    Urembo huo wa kiasili hauwezi kukamilika bila vichaka na misitu inayoipamba sayari hii
    huku ikileta mvua. Mapambo yote haya huendeshwea na nguvu za maumbile; nguvu
    ambazo hazisababishwi na kuwa hatari kwa uhai wake na ule wa viumbe wenzake kwa
    sababu anayaharibu maumbile kwa kiasi kikubwa kinachomtisha yeye mwenyewe. Hii ni
    kwa sababu gani? Sababu zipo nyingi.

    Sababu mojawapo ni uchafuzi wa maji kama rasimali muhimu ya kiasili. Uchafuzi huu
    umewaletea viumbe na mimea maafa mengi, yakiwemo maradhi mbalimbali. Kwa kweli
    bila maji, uhai utatoweka duniani. Uharibifu mkubwa wa maji machafu yenye sumu hasa
    kutoka viwandani na kuingia kwenye mito na bahari, huwadhuru biumbe wengine ambao
    makao yao ni majini. Maji huleta madhara si tu kwa mimea bali hat kwa binadamu
    kupitia kwa ulaji wa vyakula.

    Misituni rasilimali nyngine inayokimu viumbe, lakini binadamu anaiponza. Ukataji wa
    miti kiholela hasa kwenye sehemu za chmichemi husababisha uhaba wa mvua. Uhaba
    huo nao huleta kiangazi kinachokausha mimea na visima vya maji. Mchapuko wa ujenzi wa viwanda hasa katika nchi zilizostawi wanasayansi wanaohusika na hali za anga
    umesababisha taharuki na wasiwasi mwingi. Hii ni kwa sababu umenyosha kuwa ule
    utandu unaozuia miale ya jua kupenya moja kwa moja kweye sayari hii na juhatarisha
    uhai, sasa unaanza kutoweka taratibu. Hii ni kutokana na hewa chafu itokayo viwandani.
    Kwa kadri binadamu anavyozidi kujiimarisha kiviwanda ndivyo ambavyo mabaki
    yaviwanda yanavyozidi hatua hii, ni binadamu atakuwa amechangia pakubwa katika
    kutowesha uhai wa viumbe wote ulimwenguni.

    Mikutano mingi ya kmataifa imefanywa nab ado inaendelea kufanywa kila uchao ili
    kutahadharisha umma wa ulimwengu dhidi ya uharibifu wa mazingira na mali asili.
    ‘Ajenda’ za mikutano hiyo hasa zinalenga nchi zilizostawi kwani hizi ndizo zinazochafua
    mazingira kwa kasi zaidi kuliko zile zinazostawi . Mapendekezo mengi yametolewa
    katika vikao hivyo ili kusuluhisha tatizo hili lakini ni hatua chache mno zinazochuliwa
    kurekebisha mamba.

    Inatupasa sisi wenyewe kuchukua jukumu la kusafisha mazingira yetu. Tuwafunze pia
    watoto wetu kuhifadhi mazingira yanapochafuliwa au kuharibiwa. Tukumbuke kuwa
    Mwana hufuata kisogo cha nina.Mazingira yanpochafuliwa au kuharibiwa, afya zetu
    zimo hatarini, na hali hii pia ni tisho kwa viumbe wengine, hata vimatu! Kila mmoja
    wetu anawajibika kutunza mazingira anamoishi kwa manufaa yetu sote na kwa vizazi
    vijavyo.

    a) Kulingana na taarifa hii, kwa nini binadamu anahesabiwa kuwa na uharibifu
    mkubwa kushinda wanyama wengine?
    b) Onyesha uhusiano uliopo baina ya maendeleo ya binadamu na uharibifu wa
    mazingira.
    c) Ni kwa nini mwandishi anahofia zaidi athari za miale ya jua?
    d) Eleza kwa ufupi hasara zinazoweza kusababishwa na uharibifu wa mazingira.
    e) taja hatua mbili ambazo mwanadamu angeweza kuchukua ili kupunguza madhara
    ya viwanda.
    f) Kulingana na makala haya ni nini maana ya methali “mwana hufuata kisogo cha
    nina?”
    g) Eleza maana ya
    (i) Kusana
    (ii) Mchapuko

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Geuza sentensi hizi kutoka msemo wa taarifa hadi msemo halisi i) Mama alisema nichukue nafaka yetu nikauze sokoni ii) Mwalimu aliomba aletewe vitabu vyake kutoka darasani(Solved)

    Geuza sentensi hizi kutoka msemo wa taarifa hadi msemo halisi
    i) Mama alisema nichukue nafaka yetu nikauze sokoni
    ii) Mwalimu aliomba aletewe vitabu vyake kutoka darasani

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi za mseto kutokana na mbili fupi ulizopewa a) Mwanafunzi amesoma kwa bidii. Mwanafunzi anataka kupita mtihani b) Leo nimerudi nyumbani. Sipendelei kuishi hapa(Solved)

    Andika sentensi za mseto kutokana na mbili fupi ulizopewa
    a) Mwanafunzi amesoma kwa bidii. Mwanafunzi anataka
    kupita mtihani
    b) Leo nimerudi nyumbani. Sipendelei kuishi hapa

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Kwa kurejea ngeli za mahali, andika sentensi tatu ukionyesha matumizi ya kila moja(Solved)

    Kwa kurejea ngeli za mahali, andika sentensi tatu ukionyesha matumizi ya kila moja

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi zifuatazo katika hali ya kutendewa i) Yule Ngo’mbe alizaa ndama mkubwa jana ii) Mavu hawa wamemsumbua Nyatogo kwa mda mrefu.(Solved)

    Andika sentensi zifuatazo katika hali ya kutendewa
    i) Yule Ngo’mbe alizaa ndama mkubwa jana
    ii) Mavu hawa wamemsumbua Nyatogo kwa mda mrefu.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunaweza kusema katika chumba au i) …………………………………………………..ama ii) ……………………………………………………..(Solved)

    Tunaweza kusema katika chumba au
    i) …………………………………………………..ama
    ii) ……………………………………………………..

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Sahihisha sentensi zifuatazo bila kugeuza maana i) Kikombe chenye kimevunjika ni kipya ii) Nimepeana kitabu kwa mwalimu mkuu(Solved)

    Sahihisha sentensi zifuatazo bila kugeuza maana
    i) Kikombe chenye kimevunjika ni kipya
    ii) Nimepeana kitabu kwa mwalimu mkuu

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi sahihi ukidhihirisha wingi wa majina yafuatayo: i) Ukanda i) Uzee(Solved)

    Tunga sentensi sahihi ukidhihirisha wingi wa majina yafuatayo:
    i) Ukanda
    i) Uzee

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika ukubwa wa Mwizi aliiba kikapu na ngo’mbe(Solved)

    Andika ukubwa wa
    Mwizi aliiba kikapu na ngo’mbe

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika umoja wa sentensi hizi: (i) Kwato za wanyama hutufaidi (ii) Mnataka vyeti vya kuwasaidia?(Solved)

    Andika umoja wa sentensi hizi:
    (i) Kwato za wanyama hutufaidi
    (ii) Mnataka vyeti vya kuwasaidia?

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Kwa kutumia kirejeshi kifaacho, rekebisha sentensi ifuatayo kwa njia mbili tofauti. Yule ndiye mkwasi ambaye aliyenusurika.(Solved)

    Kwa kutumia kirejeshi kifaacho, rekebisha sentensi ifuatayo kwa njia
    mbili tofauti.
    Yule ndiye mkwasi ambaye aliyenusurika.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • UFUPISHO Yusufu Bin Hassan, Mfalme wa mwisho wa halali wa Mombasa, alijitayarisha kuihama himaya yake. Alikuwa amewashinda Wareno, mahasimu wake, vibaya, lakini alijua watarudi na watamwadhibu vikali. Hivyo...(Solved)

    UFUPISHO
    Yusufu Bin Hassan, Mfalme wa mwisho wa halali wa Mombasa, alijitayarisha kuihama
    himaya yake. Alikuwa amewashinda Wareno, mahasimu wake, vibaya, lakini alijua
    watarudi na watamwadhibu vikali. Hivyo basi, badala ya kusubiri waje wazitie baruti
    nyumba na kuzilipua, badala ya kungojea waje wawachinje raia wake kama kuku, badala
    ya kungonja ashuhudie minazi yote kisiwani na miti mingine ya manufaa kukatwa katwa
    na makatili hao, badala ya kujitayarisha yeye mwenyewe mji, faua ya kuikatakata miti
    yote ili Waareno wakija wasikute chochote cha kuvutia macho na watokomee kabisa.
    Alijua asipotekeleza uamuzi huo mkali, basi Wareno watakujja na hasira zote na
    kuadhibu waliomo na wasiokuwemo, kama walivyofanya Faza.

    Unyama uliofanyika huko alikuwa ameusikia ukisimuliwa mara zisizohesabika. Katika
    masimulizi hayo, alikuwa amesikia ya kwamba Falme hiyo ya Faza ilipoasi utawala wa
    Kireno, askari wa Kireno, chini ya uongozi wa Martin Affenso de Mello, walifanya
    unyama hapo mjini Faza ambao ulikuwa haujawahi kutokea, hata katika mawazo.
    Inavyosemekana ni kwamba Wareno waliamua kuangamiza chochote chenye uhai, hata
    wanyama na miti na wakautimiza muradi wao. Ajabu ni kwamba, hata kasisi
    aliyeheshimika sana wa Kireno enzi hizo, Baba Joao dos Santos, aliunga mkono tukio hili
    akisema ya kwamba wafaza walistahili kuadhibiwa. Hakuna mtu hata mmoja upande wa
    Wareno aliyekilaani kitendo hiki cha kutisha.

    Hii ndiyo sababu Mfalme Yusuf na raia wake walipowazima wareno hapo Mombasa,
    aliwaamuru watu wajitolee kuwashabulia kwenye vituo vyao vyote kaitika mwabao
    mzima wa mashariki ya Afrika. Baada ya kuamua hivyo, alienda Uarabun kutafuta silaha
    ili atekeleze azimio lake.

    Alipopata zana za kutosha, ikiwa ni pamoja na silha na meli, alianza kupambana na
    wareno kuo huko Arabuni, mahali pitwapo Shihr. Halafu alielekea mwambao wa pwani
    ya AFrika aliwasumbua sana maadui zake, Mwisho alikita makao yake Bukini ambako
    aliendelea kuwashambulia Wareno kokote walikokuwa.

    a) Eleza sababu zilizomfanya Mfalme Hassan kuuangamiza mji wake, na halafu
    kuuhama (maneno 30-40)
    b) Ukitumia Maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana, fupisha kuanzia aya
    ya pili hadi mwisho wa kifungu (maneo 75-80)

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala afuatayo kisha ujibu maswali yanafuata. Katika falme ya Pate ya enzi za kale, kulikuwa n binti Sultani aliyeitwa Mwanakishwira. Alipopata umri wa miaka kumi na...(Solved)

    Soma makala afuatayo kisha ujibu maswali yanafuata.
    Katika falme ya Pate ya enzi za kale, kulikuwa n binti Sultani aliyeitwa Mwanakishwira.
    Alipopata umri wa miaka kumi na mine tu, Mwanakishwira alikuwa tayari ni mrefu na
    mkubwa, na alionekana kuwa msichana mzima mwenye umri wa miaka kumi na minane.
    Alikuwa nadhifu na mzuri sana wa sura, kiasi cha kubandikwa lakabu ya malaika.
    Lipendeza sana macho fauka ya kuwa alikuwa na akili nyingi mno. Katika umri huo,
    alikuwa amemaliza masomo yake yote katika madrassa iliyokuwa hapo, na aliweza
    kuikariri. Kurhani yote bila kigezigezi. Babake, Mfalme, aliuma videole akilia ngoa kuwa
    motto mwenye akili hiyo ni mke wala sio mume. Aliwaza ya kuwa kama angekuwa
    mvulana, angempeleleka zutafindaki ya Al-Azhar huko Misri kuendelea na masomo ya
    juu katika chuo hicho kisifika.

    Wakati mfalme akiuma vidole kuhusu junsia ya motto wake, wanaume wengi hapo mjini
    walikuwa wakimeza mate. Mtu aliyememezewa mate alikuwa ni yeye huyo
    Mwanakishwira. Walimmezea mate kwa sababu kila mmoja wao alitaka kumwoa awe
    mkewe. Kumwoa Mwanakishwira kulikuwa na manufaa ya kupata mke mwenye uzuri
    wa shani, kama nyota, na aidha kuwa Mfalme baada ya mwenye kukikalia kuaga dunia,
    sababu yeye hakuwa na mrithi mwingine.

    Basi ikawa ni kila mtu kujipendekeza kwa mfalme…Kila mtu bila kujali nasaba.
    Walijipendekeza wakwasi na mwakata pia. Mwisho Mfalme, Kwa vile alikuwa
    anasumbuliwa sana, na wakati huohuo aliogopa kuwa asipomwoza mapema binti yake
    huenda akaharibika, akaamua kuruhusu wachumba wamchumbie.

    Uamuzi huu ulimshtua sana Mwanakishwira, Mshutuko aliopata ulimtia ugonjwa na
    kumdoofisha kabisa. Akadhoofu hadi Mfalme akaingiwa na hofu ya kuwa motto wake
    atakufa. Akaamua kumwuliza kinachomdhoofisha. Mwanakishwira. Mwanakishwira
    akasema kimdhoofishacho ni mwezi. Akipata mwezi, na nafuu pia ataipata.

    Kusikia hivyo, Mfalme akatokwa na kijasho chembachemba. Akafikiria kwamba labda
    motto wake amemalizwa kabisa na uwele, na sasa yaweweseka tu, wala hana akili razini
    ya kutambua na kupanga mambo.

    Hata hivyo hakuvunkika moyo kabisa. Akaamua kupata tafsiri ya kitendawili hicho
    kutoka kwa waheshimiwa wake hapo mjini. Ambao wote walitaka mumwoa
    Mwanakishwira.

    Kwanza akamwendea Waziri Mkuu akamwulia tafsiri ya mwezi autakao binti yake.
    Waziri akasema mwezi utakikanao ni wa dhahabu. Alipoambiwa hivyo motto akzidi
    kudhoofu. Mfalme akakasirika sana. Akawaendea wakwasi wengine kama vile Kadhi, Mnajimu na Kadhalika. Hawa wote wakamzidisha ugonjwa binti Mfalme kwa sababu
    jawabu walizotoa ni kuwa mgonjwa alihitaji mwezi wa almasi, fedha na hata hatua!

    Mwisho kabisa, Mfalme akamwendea Mvulana aliyeckuwa mchungaji. Huyu
    akamwaidhi Mfalme kwamba aulize mgonjwa aseme mwenyewe aina ya mwezi
    aitakayo. Jawabu hili halikumfurahisha Mfalme, japo alienda kamwuliza binti yake,
    kama alivyoambiwa. Alipoulizwa Mwanakishwira akasema mwezi autakao ni kishaufu
    kilicho na umbo la mwezi mchanga kilichotengenezwa na chuma. Mfalme alishangaa
    sana, Hata hivyo akamfulia kisaufu alichokitaka mgonjwa. Alipokivaa, Mwanakishwira
    akapata nafuu mara moja na akaendelea na nafuu hiyo hadi akapona kabisa.

    Kuona hivyo, Mfalme akawateremsha vyeo wakwasi wote humo mjini, na kuteua
    wengine mahali pao. Kwa upande mwingine, mchungaji akaozwa binti Mfalme na
    kupewa madaraka ya Waziri Mkuu. Hatimaye, Mfalme alipoaga dunia, mchungaji akawa
    Mfalme na Mwanakishwira akawa Malkia.

    a) Zungumzia swala la meuke (yaani mahali pa mwanamke au mwanamume katika
    jamii) katika falme ya pate ya enzi hiyo.
    b) i) Kwa nini Mfale iliwauliza wakwsi kwanza tafsiri ya kitendawili
    ii) Kwa nini mfalme alishangazwa na jawabu la binti yake?
    c) “Akili ni nywele, kila mtu ana zake” Dhihirisha jinsi methali hii inavyobainika
    katika hadithi hii
    d) Ni nini maoni yako kuhusu mwanamume aliyemwoa Mwanakishwira na kwa nini
    alikubali kuolewa na huyo?
    e) Eleza maana ya maneno na tamathali za semi zifuatazo
    i) Fauka ya kuwa
    ii) Akilia ngoa
    iii) Uzuri wa shani
    iv) Akamwaidhi

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya: i) Juhudi zake hizo si chochote bali ni kutapatapa kwa mfamaji ii) Leo kapasua yote, hata mtama kamwagia kuku.(Solved)

    Eleza maana ya:
    i) Juhudi zake hizo si chochote bali ni kutapatapa kwa mfamaji
    ii) Leo kapasua yote, hata mtama kamwagia kuku.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Kamilisha: i) Bumba la …………………….. ii) Genge la……………………..(Solved)

    Kamilisha:
    i) Bumba la ……………………..
    ii) Genge la……………………..

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi tatu zikionyesha maana tatu za neno chungu.(Solved)

    Tunga sentensi tatu zikionyesha maana tatu za neno chungu.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Taja methali inayoafikiana na maelezo haya: i) Wengine wanapoozana na kugombana, kunao wanaofurahia kabisa hali hiyo. ii) Afadhali kuhudhuria huo mkutano hata kama umechelewa(Solved)

    Taja methali inayoafikiana na maelezo haya:
    i) Wengine wanapoozana na kugombana, kunao
    wanaofurahia kabisa hali hiyo.
    ii) Afadhali kuhudhuria huo mkutano hata kama umechelewa

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunawaitaje watu hawa? (i) Mtu anayebeba mizigo kwa ujira (ii) Mtu anayeshughulikia elemu ya nyota(Solved)

    Tunawaitaje watu hawa?
    (i) Mtu anayebeba mizigo kwa ujira
    (ii) Mtu anayeshughulikia elemu ya nyota

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Sahihisha sentensi hizi: (i) Bahasha ilionunuliwa jana ni kubwa na mzuri (ii) Mananasi hizi zinauzwa ghali kwa sababu zimeiva vizuri sana(Solved)

    Sahihisha sentensi hizi:
    (i) Bahasha ilionunuliwa jana ni kubwa na mzuri
    (ii) Mananasi hizi zinauzwa ghali kwa sababu zimeiva vizuri sana

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)