Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Tambulisha viwakilishi katika sentensi zifuatazo, halafu uzigeuze sentensi hizo kwa wingi. (i) Nilisoma kitabu chake (ii) Umekuwa mwadilifu kupindukia (iii) Alishinda nishani ya dhahabu

      

Tambulisha viwakilishi katika sentensi zifuatazo, halafu uzigeuze sentensi
hizo kwa wingi.
(i) Nilisoma kitabu chake
(ii) Umekuwa mwadilifu kupindukia
(iii) Alishinda nishani ya dhahabu

  

Answers


Kavungya
(i) Nilisoma kitabu chake
Tulisoma vitabu vyao
(ii) Umekuwa mwadilifu kupindukia
Mmekuwa waadilifu kupindukia
(iii) Alishinda nishani ya dhahabu
Walishinda nishani za dhahabu
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 11:42


Next: Eleza matumizi matatu ya KI na utunge sentensi moja kwa kila mojawapo.
Previous: Akifisha sentensi hii: Watu wengi wamezoea kusema ajali bwana basi yakaishia hapo lakini kufanya hivyo ni sawa.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Eleza matumizi matatu ya KI na utunge sentensi moja kwa kila mojawapo.(Solved)

    Eleza matumizi matatu ya KI na utunge sentensi moja kwa kila mojawapo.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Samaki anayejirusha kutoka majini huitwa?(Solved)

    Samaki anayejirusha kutoka majini huitwa?

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Anayefundisha mwari mambo ya nyumbani huitwa?(Solved)

    Anayefundisha mwari mambo ya nyumbani huitwa?

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika kinyume cha i) Shari ii) Oa(Solved)

    Andika kinyume cha
    i) Shari
    ii) Oa

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Kwa kila jozi ya maneno uliyopewa tunga sentensi mbili kutofautisha maana: (i) Ini- Hini (ii) Tairi- Tahiri(Solved)

    Kwa kila jozi ya maneno uliyopewa tunga sentensi mbili kutofautisha
    maana:
    (i) Ini-
    Hini

    (ii) Tairi-
    Tahiri

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika visawe ( maneno yenye maana sawa) vya maneno haya: (i) Sarafu (ii) Keleji. (iii) Daktari.(Solved)

    Andika visawe ( maneno yenye maana sawa) vya maneno haya:
    (i) Sarafu
    (ii) Keleji.
    (iii) Daktari.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza katika sentensi maana ya misemo ifuatayo (i) Uso wa chuma (ii) Kuramba kisogo(Solved)

    Eleza katika sentensi maana ya misemo ifuatayo
    (i) Uso wa chuma
    (ii) Kuramba kisogo

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana mbili tofauti za sentensi hii Wenzake wamelipwa pesa zao, yeye bado amelala(Solved)

    Eleza maana mbili tofauti za sentensi hii
    Wenzake wamelipwa pesa zao, yeye bado amelala

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Kati ya viumbe wote waishio ulimwenguni, hakuna kiumbe aliyepevuka mawazo kama binadamu. Kiumbe huyu amewapiku wale wengine kwa njia nyingi, hata...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
    Kati ya viumbe wote waishio ulimwenguni, hakuna kiumbe aliyepevuka mawazo kama
    binadamu. Kiumbe huyu amewapiku wale wengine kwa njia nyingi, hata kuweza
    kuwatawala na kuwapangia maisha yao. Binadamu amekirimiwa uwezo wa kuyatawala
    mazingira na kukabidhiwa hekima ya kuweza kusana ala mbalimbali ili kuyakabili
    mazingira hayo. Hekima hii humwezesha kusitiri kizazi chake.

    Aidha, ametunukiwa uwezo mkubwa wa kuivinjari sayari hii yetu katika ilhamu yake ya
    kutaka kuvumbua ‘siri’ za maumbile, amejasiri hata kuzitalii sayari nyingine nje ya uso
    wa ulimwengu huu. Si ajabu kwamba iwapo wanyama wengine wangepewa urazini wa
    kuongea kama yeye, wangalimwandikia tumbi la vitabu kusiuf busara yake. Sifa za
    ujasiri wake kamwe hazingewatoka vinywani mwao!

    Hata hivyo, kuna tofauti nyingine kubwa kati ya binadamu na hayawani, Tofauti hii
    inaweza kumvua binadamu sifa zake zote na kuuona ukwasi wa maarifa yake kama
    ishare ya maangamizi ya ulimwengu. Hii ni kutokana na hasara anayosababisha katika
    mazingira tulivu walivyoumbiwa viumbe wote.

    Uzuri wa ulimwengu tunamoishi humpendeza kila kiumbe hata yule anayemchukia
    binadamu kama nzi. Wote hufurahia mazingira yao; hewa safi itokayo milimani,
    chemichemi, mito na vijito mnamotiririka maji safi, vilele vya milima vilivyokumbatiwa
    na theluji daima dahari, yakiwemo mabonde na tambarare zinazohimili uhai wa viumbe
    wengi.

    Urembo huo wa kiasili hauwezi kukamilika bila vichaka na misitu inayoipamba sayari hii
    huku ikileta mvua. Mapambo yote haya huendeshwea na nguvu za maumbile; nguvu
    ambazo hazisababishwi na kuwa hatari kwa uhai wake na ule wa viumbe wenzake kwa
    sababu anayaharibu maumbile kwa kiasi kikubwa kinachomtisha yeye mwenyewe. Hii ni
    kwa sababu gani? Sababu zipo nyingi.

    Sababu mojawapo ni uchafuzi wa maji kama rasimali muhimu ya kiasili. Uchafuzi huu
    umewaletea viumbe na mimea maafa mengi, yakiwemo maradhi mbalimbali. Kwa kweli
    bila maji, uhai utatoweka duniani. Uharibifu mkubwa wa maji machafu yenye sumu hasa
    kutoka viwandani na kuingia kwenye mito na bahari, huwadhuru biumbe wengine ambao
    makao yao ni majini. Maji huleta madhara si tu kwa mimea bali hat kwa binadamu
    kupitia kwa ulaji wa vyakula.

    Misituni rasilimali nyngine inayokimu viumbe, lakini binadamu anaiponza. Ukataji wa
    miti kiholela hasa kwenye sehemu za chmichemi husababisha uhaba wa mvua. Uhaba
    huo nao huleta kiangazi kinachokausha mimea na visima vya maji. Mchapuko wa ujenzi wa viwanda hasa katika nchi zilizostawi wanasayansi wanaohusika na hali za anga
    umesababisha taharuki na wasiwasi mwingi. Hii ni kwa sababu umenyosha kuwa ule
    utandu unaozuia miale ya jua kupenya moja kwa moja kweye sayari hii na juhatarisha
    uhai, sasa unaanza kutoweka taratibu. Hii ni kutokana na hewa chafu itokayo viwandani.
    Kwa kadri binadamu anavyozidi kujiimarisha kiviwanda ndivyo ambavyo mabaki
    yaviwanda yanavyozidi hatua hii, ni binadamu atakuwa amechangia pakubwa katika
    kutowesha uhai wa viumbe wote ulimwenguni.

    Mikutano mingi ya kmataifa imefanywa nab ado inaendelea kufanywa kila uchao ili
    kutahadharisha umma wa ulimwengu dhidi ya uharibifu wa mazingira na mali asili.
    ‘Ajenda’ za mikutano hiyo hasa zinalenga nchi zilizostawi kwani hizi ndizo zinazochafua
    mazingira kwa kasi zaidi kuliko zile zinazostawi . Mapendekezo mengi yametolewa
    katika vikao hivyo ili kusuluhisha tatizo hili lakini ni hatua chache mno zinazochuliwa
    kurekebisha mamba.

    Inatupasa sisi wenyewe kuchukua jukumu la kusafisha mazingira yetu. Tuwafunze pia
    watoto wetu kuhifadhi mazingira yanapochafuliwa au kuharibiwa. Tukumbuke kuwa
    Mwana hufuata kisogo cha nina.Mazingira yanpochafuliwa au kuharibiwa, afya zetu
    zimo hatarini, na hali hii pia ni tisho kwa viumbe wengine, hata vimatu! Kila mmoja
    wetu anawajibika kutunza mazingira anamoishi kwa manufaa yetu sote na kwa vizazi
    vijavyo.

    a) Kulingana na taarifa hii, kwa nini binadamu anahesabiwa kuwa na uharibifu
    mkubwa kushinda wanyama wengine?
    b) Onyesha uhusiano uliopo baina ya maendeleo ya binadamu na uharibifu wa
    mazingira.
    c) Ni kwa nini mwandishi anahofia zaidi athari za miale ya jua?
    d) Eleza kwa ufupi hasara zinazoweza kusababishwa na uharibifu wa mazingira.
    e) taja hatua mbili ambazo mwanadamu angeweza kuchukua ili kupunguza madhara
    ya viwanda.
    f) Kulingana na makala haya ni nini maana ya methali “mwana hufuata kisogo cha
    nina?”
    g) Eleza maana ya
    (i) Kusana
    (ii) Mchapuko

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Geuza sentensi hizi kutoka msemo wa taarifa hadi msemo halisi i) Mama alisema nichukue nafaka yetu nikauze sokoni ii) Mwalimu aliomba aletewe vitabu vyake kutoka darasani(Solved)

    Geuza sentensi hizi kutoka msemo wa taarifa hadi msemo halisi
    i) Mama alisema nichukue nafaka yetu nikauze sokoni
    ii) Mwalimu aliomba aletewe vitabu vyake kutoka darasani

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi za mseto kutokana na mbili fupi ulizopewa a) Mwanafunzi amesoma kwa bidii. Mwanafunzi anataka kupita mtihani b) Leo nimerudi nyumbani. Sipendelei kuishi hapa(Solved)

    Andika sentensi za mseto kutokana na mbili fupi ulizopewa
    a) Mwanafunzi amesoma kwa bidii. Mwanafunzi anataka
    kupita mtihani
    b) Leo nimerudi nyumbani. Sipendelei kuishi hapa

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Kwa kurejea ngeli za mahali, andika sentensi tatu ukionyesha matumizi ya kila moja(Solved)

    Kwa kurejea ngeli za mahali, andika sentensi tatu ukionyesha matumizi ya kila moja

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi zifuatazo katika hali ya kutendewa i) Yule Ngo’mbe alizaa ndama mkubwa jana ii) Mavu hawa wamemsumbua Nyatogo kwa mda mrefu.(Solved)

    Andika sentensi zifuatazo katika hali ya kutendewa
    i) Yule Ngo’mbe alizaa ndama mkubwa jana
    ii) Mavu hawa wamemsumbua Nyatogo kwa mda mrefu.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunaweza kusema katika chumba au i) …………………………………………………..ama ii) ……………………………………………………..(Solved)

    Tunaweza kusema katika chumba au
    i) …………………………………………………..ama
    ii) ……………………………………………………..

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Sahihisha sentensi zifuatazo bila kugeuza maana i) Kikombe chenye kimevunjika ni kipya ii) Nimepeana kitabu kwa mwalimu mkuu(Solved)

    Sahihisha sentensi zifuatazo bila kugeuza maana
    i) Kikombe chenye kimevunjika ni kipya
    ii) Nimepeana kitabu kwa mwalimu mkuu

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi sahihi ukidhihirisha wingi wa majina yafuatayo: i) Ukanda i) Uzee(Solved)

    Tunga sentensi sahihi ukidhihirisha wingi wa majina yafuatayo:
    i) Ukanda
    i) Uzee

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika ukubwa wa Mwizi aliiba kikapu na ngo’mbe(Solved)

    Andika ukubwa wa
    Mwizi aliiba kikapu na ngo’mbe

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika umoja wa sentensi hizi: (i) Kwato za wanyama hutufaidi (ii) Mnataka vyeti vya kuwasaidia?(Solved)

    Andika umoja wa sentensi hizi:
    (i) Kwato za wanyama hutufaidi
    (ii) Mnataka vyeti vya kuwasaidia?

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Kwa kutumia kirejeshi kifaacho, rekebisha sentensi ifuatayo kwa njia mbili tofauti. Yule ndiye mkwasi ambaye aliyenusurika.(Solved)

    Kwa kutumia kirejeshi kifaacho, rekebisha sentensi ifuatayo kwa njia
    mbili tofauti.
    Yule ndiye mkwasi ambaye aliyenusurika.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • UFUPISHO Yusufu Bin Hassan, Mfalme wa mwisho wa halali wa Mombasa, alijitayarisha kuihama himaya yake. Alikuwa amewashinda Wareno, mahasimu wake, vibaya, lakini alijua watarudi na watamwadhibu vikali. Hivyo...(Solved)

    UFUPISHO
    Yusufu Bin Hassan, Mfalme wa mwisho wa halali wa Mombasa, alijitayarisha kuihama
    himaya yake. Alikuwa amewashinda Wareno, mahasimu wake, vibaya, lakini alijua
    watarudi na watamwadhibu vikali. Hivyo basi, badala ya kusubiri waje wazitie baruti
    nyumba na kuzilipua, badala ya kungojea waje wawachinje raia wake kama kuku, badala
    ya kungonja ashuhudie minazi yote kisiwani na miti mingine ya manufaa kukatwa katwa
    na makatili hao, badala ya kujitayarisha yeye mwenyewe mji, faua ya kuikatakata miti
    yote ili Waareno wakija wasikute chochote cha kuvutia macho na watokomee kabisa.
    Alijua asipotekeleza uamuzi huo mkali, basi Wareno watakujja na hasira zote na
    kuadhibu waliomo na wasiokuwemo, kama walivyofanya Faza.

    Unyama uliofanyika huko alikuwa ameusikia ukisimuliwa mara zisizohesabika. Katika
    masimulizi hayo, alikuwa amesikia ya kwamba Falme hiyo ya Faza ilipoasi utawala wa
    Kireno, askari wa Kireno, chini ya uongozi wa Martin Affenso de Mello, walifanya
    unyama hapo mjini Faza ambao ulikuwa haujawahi kutokea, hata katika mawazo.
    Inavyosemekana ni kwamba Wareno waliamua kuangamiza chochote chenye uhai, hata
    wanyama na miti na wakautimiza muradi wao. Ajabu ni kwamba, hata kasisi
    aliyeheshimika sana wa Kireno enzi hizo, Baba Joao dos Santos, aliunga mkono tukio hili
    akisema ya kwamba wafaza walistahili kuadhibiwa. Hakuna mtu hata mmoja upande wa
    Wareno aliyekilaani kitendo hiki cha kutisha.

    Hii ndiyo sababu Mfalme Yusuf na raia wake walipowazima wareno hapo Mombasa,
    aliwaamuru watu wajitolee kuwashabulia kwenye vituo vyao vyote kaitika mwabao
    mzima wa mashariki ya Afrika. Baada ya kuamua hivyo, alienda Uarabun kutafuta silaha
    ili atekeleze azimio lake.

    Alipopata zana za kutosha, ikiwa ni pamoja na silha na meli, alianza kupambana na
    wareno kuo huko Arabuni, mahali pitwapo Shihr. Halafu alielekea mwambao wa pwani
    ya AFrika aliwasumbua sana maadui zake, Mwisho alikita makao yake Bukini ambako
    aliendelea kuwashambulia Wareno kokote walikokuwa.

    a) Eleza sababu zilizomfanya Mfalme Hassan kuuangamiza mji wake, na halafu
    kuuhama (maneno 30-40)
    b) Ukitumia Maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana, fupisha kuanzia aya
    ya pili hadi mwisho wa kifungu (maneo 75-80)

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)