Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Soma makala yafuatayo kisha ujibu mwsawali Utandaridhi (au globalization kwa lugha ya Kingereza) ni jinsi ya maisha inayoendelea kuutawala ulimwengu wote katika karne hii ya 21. Neno...

      

Soma makala yafuatayo kisha ujibu mwsawali
Utandaridhi (au globalization kwa lugha ya Kingereza) ni jinsi ya maisha inayoendelea
kuutawala ulimwengu wote katika karne hii ya 21. Neno utandaridhi ni neno mseto
ambalo maana yake ni utamaduni uliotanda au kuenea ardhi nzima. Mtu mtandaridhi’
hivyo basi ni mtu aliyebebea kikamilifu katika utamaduni huu mpya kwa jinsi moja au
nyingine.

Matandaridhi hujihusisha sana katika kutandaridhisha aina moja au nyingine ya amara
muhimu za kitandaridhi. Hizo ni kama vile biashara za kumataifa, lugha za kimataifa,
aina za mavazi zilizotokea kupendwa ulimwenguni kote, muziki wa kisiku hizi, hasa vile
pop, reggae, raga, rap, ambao asili yake ya hivi majuzi ni Marekani. Muziki huo
waimbaji wake hutumia, sana sana, lugha ya Kiingereza hususan kile cha Marekani na
kadhalika Watandaridhi wana nyenzo zingine kadha wa kadha za kuendeshea maisha yao
au kujitambulisha. Wao huwasiliana kutoka pembe moja ya duni hadi nyingine
wakitumia vitumeme, yaani vyombo vitumiavyo umeme kufanya kazi vya hali ya juu,
kama vile tarakilishi na simu, hata za mkono. Watu hawa hawakosi runinga sebuleni
mwao, usiseme redio. Hawa husikiliza na kutazama habari za kimataifa kupitia mashirika
matandaridhi ya habari kama vile BBC la uingereza CNN la marekani. Aidha watu hawa
husafiri mara kwa mara kwa ndege na vyombo vingine vya kasi. Hawa hawana mipaka.
Wale wanaohusudu utandaridhi wanaamini kindakindaki kwamba utamaduni huu wa
kilimwengu umeleta mlahaka mwema baina ya watu binafsi, makampuni makubwa
makubwa ya kimataifa na usiano bora baina ya mataifa. Watu hawa husikia wakidai ya
kuwa aina hii ya utamaduni imeupigisha mbele ustaarabu wa wanadamu ulimwenguni
kote. Kwa upande mwingine, wakereketwa wa tamaduni za kimsingi za mataifa na
makabila mbalimbali ulimwenguni wanadai ya kwamba utandaridhi umeleta maangamizi
makubwa ya tamaduni hizo. Kwa ajili hiyo basi, utandaridhi umeleta maangamizi
makubwa ya tamaduni hizo. Kwa ajili hiyo basi, utandaridhi umesemekana kwamba
unasababisha kutovuka kwa utu miongoni mwa wanadamu wote, ambao wamo mbioni
kusaka pesa na kuneemesha ubinafsi. Inadaiwa pia kwamba utandaridhi umesababisha
kutovuka kwa adab kwa vijana wengi ulimwenguni kote ghaya ya utovu. Huku kutovuka
kwa adabu kwa vijana wengi ulimwenguni kote ghaya ya utovu. Huku kutovuka kwa
adabu kwa vijana, hasa wale wa mataif yanayojaribu kuendelea, kumeleta zahama
chungu mbovu, ikiwa ni pamoja na kuenea kwa UKIMWI kwa kasi ya kutisha.

a) i) Bainisha kwa kutoa maelezo kamili kwamba utandaridhi ni neno mseto.
ii) Tohoa maneno mawili kutokana na neon kutandaridhisha kisha ueleze
maana za maneno hayo.
b) i) Nini maana ya ‘hawa hawana mipaka?’
ii) Kwa nini watandaridhi wanpenda kusikiliza na kutazama habari kupitia
BBC na CNN?
c) i) Eleza kikamilifu maoni ya watandaridhi kuhusu utamaduni wao
ii) Je, Utandaridhi unalaumiwa kwa nini katika kifungu hiki?
d) Msemo: “ chungu mbovu” ni msemo wa kimtaani tu. Msemo sawa ni upi
e) Eleza maana ya maneno yafuatayo
i) Amara
ii) Mlahaka
iii) Wakereketwa

  

Answers


Kavungya
(a) (i) Bainisha kwa kutoa maelezo kamili kwamba utamdaridhi ni neno la
mseto ( alama 3)
Neno hili limeundwa kutokana na maneno matatu ambayo ni utamaduni,
tanda na ardhi. (Ni neno maana yake ni utamaduni uliotanda au kuenea
ardhi nzima)
(ii) Tohoa maneno mawili kutokana na neno kutandaridhisha kisha ueleze
maana za maneno hayo.
Kutanda - kuenea, kusambaa, kutapakaa
Ridhisha- Kupendeza, kutoshelewa, kufurahisha

(i) - Nini maana ya “ hawa hawana mipaka?”
- Wana uwezo wa kuwasiliana na wenzao kote ulimwenguni
- Wanasafiri kote ulimwenguni
- Wanaweza kufanya kazi kote ulimwenguni
- Hupata habari kupitia mashirika matandaridhi
(ii) - Kwa sababu ni mashirika matanndaridhi ya habari
- Hutangaza habari za ulimwengu au za kimataifa
- Ni njia ya kujitambulisha kama watandaridhi
- Ni njia/ nyenzo za kuendeshea maisha yao

(c) (i) - Utandaridhi umeleta mlahaka mwema baina ya watu, makampuni
makubwa makubwa ya kimataifa / uwiano bora baina ya mataifa.
- Umepigisha mbele ustaarabu wa wanadamu wote.
(ii) - Umeleta maangamizi makubwa ya tamaduni ya kimsingi
- Maangamizo kwa lugha za tamaduni hizo
- Kutoroka kwa utu miongoni mwa wanadamu wote/ kuwemisha
ubingi
- Umeleta zahama chungu (maangamizi) kuenea kwa ukimwi

(d) Chungu nzima

(e) (i) amara- shughuli/ mambo/ nyenzo. Nguzo/ mbinu
(ii) Mlahaka – uhusiano, ushirikiano, uelewano, uwiano
(iii) Wakereketwa – watetezi/ wahadidhina/ wafusi sugu/ wenye imani kali
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 12:11


Next: Eleza maana ya methali Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni
Previous: Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Ukiwa mtoto unadhani ulimwengu ni kipande kimoja cha keki kilicho kitamu mithili ya asali. Hakuna dhiki, hakuna mateso, hakuna kuhuzunika kwa...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions