Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Ukiwa mtoto unadhani ulimwengu ni kipande kimoja cha keki kilicho kitamu mithili ya asali. Hakuna dhiki, hakuna mateso, hakuna kuhuzunika kwa...

      

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Ukiwa mtoto unadhani ulimwengu ni kipande kimoja cha keki kilicho kitamu mithili ya
asali. Hakuna dhiki, hakuna mateso, hakuna kuhuzunika kwa aina yoyote. Neno huzuni
linasikika masikioni kama neno lisiloelekea kwenye uhalisia wowote. Kwa watoto dunia
imejaa raha, starehe na vicheko visivyoisha. Maisha ni ahadi njema, yenye matokeo ya
kufurahisha na kustarehesha tu, sio KUDHIKISHA NA KUHUZUNISHA.

Huyu tunayemzumgumzia hapa ni mtoto mdogo ambaye hajajua kubainisha
kitendekacho mkono wake wa kushoto na kile kinachofanyika hasa katika mkono wake
wa kulia. Hata hivyo, jinsi mtoto anavyoendelea kukua na kufahamikiwa na mambo,
vigambo na kadhia zinazoendelea katika mazingira yake, anabainikiwa na mengi
machungu ambayo huleta huzuni, sio raha.

Hebu tuanze na nyumbani kwao mtoto. Aghalabu, watoto wote hupendwa kwao
nyumbani, iwapo wazazi wao ni watu wangwana na wana nafasi ya kulea watoto wao
bila taabu. Hata hivyo watoto huchapwa pale wanapokuwa watundu, jambo ambalo
huwahuzunisha sana, japo ni wajibu wa wazazi sababu, kama isemwavyo, mcha mwana
kulia hulia yeye. Pili, inajulikana wazi kwamba watoto wengi siku hizi huenda shule,
huko shule, wao hupendelea sana kucheza kuliko kusoma. Ili wasome kama
inavyotakikana, ni sharti waelekezwe barabara katika njia hiyo na walimu wao. Katika
kuelekezwa huku, walimu wanaweza kulazimika kuwaadhibu, hasa wale watoto ambao
huzembea na kutofanya kazi zao wanazopewa kufanya nyumbani kama kawaida ya
mfumo wa shule ilivyo. Watoto ambao huzembea na kutofanya kazi zao wanazopewa
kufanya nyumbani kama kawaida ya mfumo wa shule ilivyo. Watoto wa aina hii
wanapotiwa adabu raha hujitenga na huzuni huwatawala.

Huzuni, hivyo basi, inaonekana ya kuwa ni uso wa pili katika maisha ya mwanadamu,
uso wa kwanza ukiwa raha. Na kwa hakika wanaohuzunika si watoto peke yao. Kila mtu
duniani ni sharti, katika wakati mmoja au mwingine, azongwe na huzuni. Inajulikana
wazi kwamba wanadamu wote hawapendi huzuni asilani na hakika kabisa, kila binadamu huchukia huzuni na kustahabu raha. Hata hivyo, raha humjia binadamu kwa nadra sana,
ilhali huzuni humvamia wakati wowote, hata akiwa humo katikati ya kustarehe. Si tu,
inajulikana dhahiri shahiri kwamba hakuna mtu asiyewahi kuonja huzuni, japo wapo
watu wengi kweli kweli wasiowahi kuonja raha maishani mwao.

Zingatia mtoto anaezaliwa, halafu wazazi wake wanaaga dunia, pengine katika ajali,
kabla mtoto mwenyewe hajaweza kujikimu. Mtoto huyu anaishi kutegemea jamaa za
wazazi wake. Watu hawa wasipokuwa na nafasi wao wenyewe kimaisha pamoja na
ukarimu unaohitajika basi mtoto anateseka na kuhuzunika sana katika maisha yake yote.
Ama zingatia mtoto anayetupwa na mamake kijana, aliyempata bila kupanga. Hata mtoto
huyu akiokotwa na kulelewa na wahisani, maisha yake yatakuwa ya taabu, dhiki na
huzuni. Au zingatia mtoto anayelelewa na mama wa kambo anayeondokea kuwa
mwovu. Mtoto huyu atakayoijua ni huzuni tu. Ama zingatia mtoto ambaye babake ni
mlevi na unalojua ni kurudi nyumbani kufurahia kupiga watoto wote na mama yao ndipo
apate usingizi mnono. Mtoto mwenye baba wa aina hiyo atakayoijua ni huzuni tu, sir aha
asilani.

a) Ukitumia maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana, fupisha aya
nne za mwanzo (Maneno -100)
b) Ukizingatia aya ya mwisho, eleza hali mbalimbali zinazowatia watoto
huzuni. (Maneno 40-45)

  

Answers


Kavungya
(a) (i) Mtoto hudhani/ hufikiri ulimwenguni umejaa raha na hauna
huzuni/ hudhani ulimwengu ni kipande kitamu cha keki/ hakuna
mates/ maisha ni ahadi njema bila huzuni.
(ii) Mtoto huyu ni yule ambaye hajajua kubainisha mambo
(iii) Anavyoendelea kukua akafahamishwa/ anabainisha na mengi
yaletayo huzuni
(iv) Ingawa watoto hupendwa kwao, wanapokuwa watundu
huadhibiwa nao huhuzunika
(v) Shuleni wanapozembea kazi wanaadhibiwa na pili huwahuzunisha
(vi) Hivyo basi huzuni ni ya pili katika maisha ya binadamu, sio ya
kwanza ukiwa raha.
(vii) Kila mtu duniani huzongwa na huzuni/ huhuzinika
(viii) Raha humjia mwanadamu kwa nadra ilhali huzuni humvamia
wakati wowote.
(ix) Wapo watu wengi wasiowahi kuonja raha maishani mwao
(alama 10) ( kila jambo limalizikie katika huzuni)

(b) - Mtoto anapofiwa na wazazi/ wazazi kuaga dunia
- Mtoto anayetupwa na mamake kijana
- Anayelelewa na mama wa kambo mwovu
- Mtoto ambaye babake ni mlevi
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 12:14


Next: Soma makala yafuatayo kisha ujibu mwsawali Utandaridhi (au globalization kwa lugha ya Kingereza) ni jinsi ya maisha inayoendelea kuutawala ulimwengu wote katika karne hii ya 21. Neno...
Previous: Tumia viashiria vya kutilia mkazo katika sentensi zifuatazo i) Kibogoyo………. Ndiye anayehitaji meno ya dhahabu. ii) Vyakula……………mvipikavyo nyinyi, nasi twavipika

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions