Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Unganisha sentensi zifuatazo kwa kutumia viunganishi vifaavyo. i) Chakula hiki hakina mchuzi. Hakina chumve ii) Romeo aliamka. Alitazama saa yake Akala kiamsha kinywa mbio mbio

      

Unganisha sentensi zifuatazo kwa kutumia viunganishi vifaavyo.
i) Chakula hiki hakina mchuzi. Hakina chumve
ii) Romeo aliamka. Alitazama saa yake
Akala kiamsha kinywa mbio mbio

  

Answers


Kavungya
i) Chakula hiki hakina mchuzi wala chumvi
ii) Romeo aliamka, akatazama saa yake kisha/halfu akala kiamsha
kinywa
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 12:20


Next: Geuza sentensi zifuatazo ziwe katika hali ya umoja i) Huku kuimba kwenu kuzuri kutawapendez wageni ii) Hii miche ni mizuri sana, itatufaa
Previous: Ziandike upya sentensi zifuatazo kwa kufuata maagizo uliyopewa. i) Nimemleta paka ili aue panya wote wanaotusumbua hapa kwetu nyumbani. (Anza: Panya…) ii) Mbwa ambaye aliripotiwa kuwa ameibwa amepatikana...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Geuza sentensi zifuatazo ziwe katika hali ya umoja i) Huku kuimba kwenu kuzuri kutawapendez wageni ii) Hii miche ni mizuri sana, itatufaa(Solved)

    Geuza sentensi zifuatazo ziwe katika hali ya umoja
    i) Huku kuimba kwenu kuzuri kutawapendez wageni
    ii) Hii miche ni mizuri sana, itatufaa

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tumia viashiria vya kutilia mkazo katika sentensi zifuatazo i) Kibogoyo………. Ndiye anayehitaji meno ya dhahabu. ii) Vyakula……………mvipikavyo nyinyi, nasi twavipika(Solved)

    Tumia viashiria vya kutilia mkazo katika sentensi zifuatazo
    i) Kibogoyo………. Ndiye anayehitaji meno ya dhahabu.
    ii) Vyakula……………mvipikavyo nyinyi, nasi twavipika

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Ukiwa mtoto unadhani ulimwengu ni kipande kimoja cha keki kilicho kitamu mithili ya asali. Hakuna dhiki, hakuna mateso, hakuna kuhuzunika kwa...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
    Ukiwa mtoto unadhani ulimwengu ni kipande kimoja cha keki kilicho kitamu mithili ya
    asali. Hakuna dhiki, hakuna mateso, hakuna kuhuzunika kwa aina yoyote. Neno huzuni
    linasikika masikioni kama neno lisiloelekea kwenye uhalisia wowote. Kwa watoto dunia
    imejaa raha, starehe na vicheko visivyoisha. Maisha ni ahadi njema, yenye matokeo ya
    kufurahisha na kustarehesha tu, sio KUDHIKISHA NA KUHUZUNISHA.

    Huyu tunayemzumgumzia hapa ni mtoto mdogo ambaye hajajua kubainisha
    kitendekacho mkono wake wa kushoto na kile kinachofanyika hasa katika mkono wake
    wa kulia. Hata hivyo, jinsi mtoto anavyoendelea kukua na kufahamikiwa na mambo,
    vigambo na kadhia zinazoendelea katika mazingira yake, anabainikiwa na mengi
    machungu ambayo huleta huzuni, sio raha.

    Hebu tuanze na nyumbani kwao mtoto. Aghalabu, watoto wote hupendwa kwao
    nyumbani, iwapo wazazi wao ni watu wangwana na wana nafasi ya kulea watoto wao
    bila taabu. Hata hivyo watoto huchapwa pale wanapokuwa watundu, jambo ambalo
    huwahuzunisha sana, japo ni wajibu wa wazazi sababu, kama isemwavyo, mcha mwana
    kulia hulia yeye. Pili, inajulikana wazi kwamba watoto wengi siku hizi huenda shule,
    huko shule, wao hupendelea sana kucheza kuliko kusoma. Ili wasome kama
    inavyotakikana, ni sharti waelekezwe barabara katika njia hiyo na walimu wao. Katika
    kuelekezwa huku, walimu wanaweza kulazimika kuwaadhibu, hasa wale watoto ambao
    huzembea na kutofanya kazi zao wanazopewa kufanya nyumbani kama kawaida ya
    mfumo wa shule ilivyo. Watoto ambao huzembea na kutofanya kazi zao wanazopewa
    kufanya nyumbani kama kawaida ya mfumo wa shule ilivyo. Watoto wa aina hii
    wanapotiwa adabu raha hujitenga na huzuni huwatawala.

    Huzuni, hivyo basi, inaonekana ya kuwa ni uso wa pili katika maisha ya mwanadamu,
    uso wa kwanza ukiwa raha. Na kwa hakika wanaohuzunika si watoto peke yao. Kila mtu
    duniani ni sharti, katika wakati mmoja au mwingine, azongwe na huzuni. Inajulikana
    wazi kwamba wanadamu wote hawapendi huzuni asilani na hakika kabisa, kila binadamu huchukia huzuni na kustahabu raha. Hata hivyo, raha humjia binadamu kwa nadra sana,
    ilhali huzuni humvamia wakati wowote, hata akiwa humo katikati ya kustarehe. Si tu,
    inajulikana dhahiri shahiri kwamba hakuna mtu asiyewahi kuonja huzuni, japo wapo
    watu wengi kweli kweli wasiowahi kuonja raha maishani mwao.

    Zingatia mtoto anaezaliwa, halafu wazazi wake wanaaga dunia, pengine katika ajali,
    kabla mtoto mwenyewe hajaweza kujikimu. Mtoto huyu anaishi kutegemea jamaa za
    wazazi wake. Watu hawa wasipokuwa na nafasi wao wenyewe kimaisha pamoja na
    ukarimu unaohitajika basi mtoto anateseka na kuhuzunika sana katika maisha yake yote.
    Ama zingatia mtoto anayetupwa na mamake kijana, aliyempata bila kupanga. Hata mtoto
    huyu akiokotwa na kulelewa na wahisani, maisha yake yatakuwa ya taabu, dhiki na
    huzuni. Au zingatia mtoto anayelelewa na mama wa kambo anayeondokea kuwa
    mwovu. Mtoto huyu atakayoijua ni huzuni tu. Ama zingatia mtoto ambaye babake ni
    mlevi na unalojua ni kurudi nyumbani kufurahia kupiga watoto wote na mama yao ndipo
    apate usingizi mnono. Mtoto mwenye baba wa aina hiyo atakayoijua ni huzuni tu, sir aha
    asilani.

    a) Ukitumia maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana, fupisha aya
    nne za mwanzo (Maneno -100)
    b) Ukizingatia aya ya mwisho, eleza hali mbalimbali zinazowatia watoto
    huzuni. (Maneno 40-45)

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu mwsawali Utandaridhi (au globalization kwa lugha ya Kingereza) ni jinsi ya maisha inayoendelea kuutawala ulimwengu wote katika karne hii ya 21. Neno...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu mwsawali
    Utandaridhi (au globalization kwa lugha ya Kingereza) ni jinsi ya maisha inayoendelea
    kuutawala ulimwengu wote katika karne hii ya 21. Neno utandaridhi ni neno mseto
    ambalo maana yake ni utamaduni uliotanda au kuenea ardhi nzima. Mtu mtandaridhi’
    hivyo basi ni mtu aliyebebea kikamilifu katika utamaduni huu mpya kwa jinsi moja au
    nyingine.

    Matandaridhi hujihusisha sana katika kutandaridhisha aina moja au nyingine ya amara
    muhimu za kitandaridhi. Hizo ni kama vile biashara za kumataifa, lugha za kimataifa,
    aina za mavazi zilizotokea kupendwa ulimwenguni kote, muziki wa kisiku hizi, hasa vile
    pop, reggae, raga, rap, ambao asili yake ya hivi majuzi ni Marekani. Muziki huo
    waimbaji wake hutumia, sana sana, lugha ya Kiingereza hususan kile cha Marekani na
    kadhalika Watandaridhi wana nyenzo zingine kadha wa kadha za kuendeshea maisha yao
    au kujitambulisha. Wao huwasiliana kutoka pembe moja ya duni hadi nyingine
    wakitumia vitumeme, yaani vyombo vitumiavyo umeme kufanya kazi vya hali ya juu,
    kama vile tarakilishi na simu, hata za mkono. Watu hawa hawakosi runinga sebuleni
    mwao, usiseme redio. Hawa husikiliza na kutazama habari za kimataifa kupitia mashirika
    matandaridhi ya habari kama vile BBC la uingereza CNN la marekani. Aidha watu hawa
    husafiri mara kwa mara kwa ndege na vyombo vingine vya kasi. Hawa hawana mipaka.
    Wale wanaohusudu utandaridhi wanaamini kindakindaki kwamba utamaduni huu wa
    kilimwengu umeleta mlahaka mwema baina ya watu binafsi, makampuni makubwa
    makubwa ya kimataifa na usiano bora baina ya mataifa. Watu hawa husikia wakidai ya
    kuwa aina hii ya utamaduni imeupigisha mbele ustaarabu wa wanadamu ulimwenguni
    kote. Kwa upande mwingine, wakereketwa wa tamaduni za kimsingi za mataifa na
    makabila mbalimbali ulimwenguni wanadai ya kwamba utandaridhi umeleta maangamizi
    makubwa ya tamaduni hizo. Kwa ajili hiyo basi, utandaridhi umeleta maangamizi
    makubwa ya tamaduni hizo. Kwa ajili hiyo basi, utandaridhi umesemekana kwamba
    unasababisha kutovuka kwa utu miongoni mwa wanadamu wote, ambao wamo mbioni
    kusaka pesa na kuneemesha ubinafsi. Inadaiwa pia kwamba utandaridhi umesababisha
    kutovuka kwa adab kwa vijana wengi ulimwenguni kote ghaya ya utovu. Huku kutovuka
    kwa adabu kwa vijana wengi ulimwenguni kote ghaya ya utovu. Huku kutovuka kwa
    adabu kwa vijana, hasa wale wa mataif yanayojaribu kuendelea, kumeleta zahama
    chungu mbovu, ikiwa ni pamoja na kuenea kwa UKIMWI kwa kasi ya kutisha.

    a) i) Bainisha kwa kutoa maelezo kamili kwamba utandaridhi ni neno mseto.
    ii) Tohoa maneno mawili kutokana na neon kutandaridhisha kisha ueleze
    maana za maneno hayo.
    b) i) Nini maana ya ‘hawa hawana mipaka?’
    ii) Kwa nini watandaridhi wanpenda kusikiliza na kutazama habari kupitia
    BBC na CNN?
    c) i) Eleza kikamilifu maoni ya watandaridhi kuhusu utamaduni wao
    ii) Je, Utandaridhi unalaumiwa kwa nini katika kifungu hiki?
    d) Msemo: “ chungu mbovu” ni msemo wa kimtaani tu. Msemo sawa ni upi
    e) Eleza maana ya maneno yafuatayo
    i) Amara
    ii) Mlahaka
    iii) Wakereketwa

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya methali Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni(Solved)

    Eleza maana ya methali
    Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana mbili tofauti za Rudi(Solved)

    Eleza maana mbili tofauti za Rudi

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tumia misemo ifuatayo katika sentensi; i) Enda nguu ii) Chemsha roho(Solved)

    Tumia misemo ifuatayo katika sentensi;
    i) Enda nguu
    ii) Chemsha roho

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunga Sentensi zitakazobainisha maana ya jozi za maneno zifuatazo: i) Mbari Mbali ii) Kaakaa Gaagaa(Solved)

    Tunga Sentensi zitakazobainisha maana ya jozi za maneno
    zifuatazo:
    i) Mbari
    Mbali
    ii) Kaakaa
    Gaagaa

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi ukionyesha matumizi ya i) –enye ii)-enyewe(Solved)

    Tunga sentensi ukionyesha matumizi ya
    i) –enye
    ii)-enyewe

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Ukizingatia nenolililo katika mabano, andika sentensi hizi atika hali ya kutendeka. i) Daraja hili (vuka) tu wakati wa kiangazi. ii) Kitabu hicho (soma) ijapokuwa sura zingine sura...(Solved)

    Ukizingatia nenolililo katika mabano, andika sentensi hizi atika hali ya
    kutendeka. (alama 2)
    i) Daraja hili (vuka) tu wakati wa kiangazi.
    ii) Kitabu hicho (soma) ijapokuwa sura zingine sura zingine hazimo.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Yapange majina yafuatayo katika ngeli zake i) Neno ii) Kiongozi iii) Mate (Solved)

    Yapange majina yafuatayo katika ngeli zake
    i) Neno
    ii) Kiongozi
    iii) Mate

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi hizi upya ukitumia o-ote. i) Chakula kikibaki hutupiliwa mbali ii) Kila nyumba unayoingia unapata watoto wawili(Solved)

    Andika sentensi hizi upya ukitumia o-ote.
    i) Chakula kikibaki hutupiliwa mbali
    ii) Kila nyumba unayoingia unapata watoto wawili

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Sahihisha sentensi zifuatazo i) Kile kitabu kilipasuka ni changu ii) Matofali haya yanatumiwa kwa ujenzi wa nyumba(Solved)

    Sahihisha sentensi zifuatazo
    i) Kile kitabu kilipasuka ni changu
    ii) Matofali haya yanatumiwa kwa ujenzi wa nyumba

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi hizi kwa umoja i) Mafuta haya yanachuruzika sana ii) Miinuko ile ndiyo mwanzo wa milima ya Chungu.(Solved)

    Andika sentensi hizi kwa umoja
    i) Mafuta haya yanachuruzika sana
    ii) Miinuko ile ndiyo mwanzo wa milima ya Chungu.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Akifisha sentensi hii: Watu wengi wamezoea kusema ajali bwana basi yakaishia hapo lakini kufanya hivyo ni sawa.(Solved)

    Akifisha sentensi hii:
    Watu wengi wamezoea kusema ajali bwana basi yakaishia hapo lakini
    kufanya hivyo ni sawa.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tambulisha viwakilishi katika sentensi zifuatazo, halafu uzigeuze sentensi hizo kwa wingi. (i) Nilisoma kitabu chake (ii) Umekuwa mwadilifu kupindukia (iii) Alishinda nishani ya dhahabu(Solved)

    Tambulisha viwakilishi katika sentensi zifuatazo, halafu uzigeuze sentensi
    hizo kwa wingi.
    (i) Nilisoma kitabu chake
    (ii) Umekuwa mwadilifu kupindukia
    (iii) Alishinda nishani ya dhahabu

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza matumizi matatu ya KI na utunge sentensi moja kwa kila mojawapo.(Solved)

    Eleza matumizi matatu ya KI na utunge sentensi moja kwa kila mojawapo.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Samaki anayejirusha kutoka majini huitwa?(Solved)

    Samaki anayejirusha kutoka majini huitwa?

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Anayefundisha mwari mambo ya nyumbani huitwa?(Solved)

    Anayefundisha mwari mambo ya nyumbani huitwa?

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika kinyume cha i) Shari ii) Oa(Solved)

    Andika kinyume cha
    i) Shari
    ii) Oa

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)