Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Wahenga walisema “mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.” Hii ina maana ya kuwa ukiogopa kutumia ufito kumchapa mtoto wako, ukamdekeza atadeka na hatimaye...

      

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Wahenga walisema “mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.” Hii ina maana ya kuwa ukiogopa
kutumia ufito kumchapa mtoto wako, ukamdekeza atadeka na hatimaye ataharibika.
Methali hii ina picha yake ambyo ni, “Ukicha mwana kulia, utalia wewe.”

Hizi ni methali zilizojaa busara kubwa. Mathalini wewe ni mzazi au mtu yeyote mzima
aliyetunikiwa madaraka juu ya watoto. Lakini kila wanapokiuka uadilifu au mmoja wao
anapokosea wewe unambembeleza tu, basi huwa unaizorotesha tabia yake. Mwisho,
mtoto huyo anaweza kuishia kuwa mtundu.

Hata hivyo, ni sharti tujue ya kwamba tuko katika njia panda hapa. Kwa upande mmoja,
zamani ilichukuliwa kwamba watoto na hata wanawake watu wazima hawana akili. Kwa
ajili hiyo, iwapo mwanaume mtu mzima ana jambo la kuwaeleza, njia pekee ya
kuliingiza katika “ akili” yao “ hafifu” ni kuwatwanga ili kulikongomeza jambo hili.
Ukweli ni kwamba akili ya mtoto si hafifu hata. Unaweza kusema ni kama mmea, ambao
usiporutubishwa kimakusudi, ukapaliliwa vyema na kustawishwa stahiki yake, basi
hudhoofu” na mwishowe kufifia.

Kwa upande mwingine, mtazamo wa kisasa ni tofauti kabisa, imethibitishwa ya kwamba
wanawake ni sawa kabisa katika maumbile yao wakilinganishwa na wanaume. Kwa jinsi
hiyo, kweli wapo wanawake amabo hawana mwelekeo timamu kuhusu maisha. Lakini ni
kweli pia kuwa wapo wanaume watu wazima mamilioni ambao hawana akili.
Kadhalika, si kweli kuwa watoto wote, kwa sababu ya umri wao tu, basi hawana akili.
Ama kwa kusema kweli binadamu yeyote kuwaliwa na akili zake timamu isipokuwa wale
ambao kwa bahati mbaya maumbile yamewapa akili pungufu. Hili litokeapo basi
tunalikubali tu. Hatuwezi kumlaumu mtu kama huyo au muumba wake. Kwa hakika huu
ndio msingi wa methali. “Akili ni nywele, kila mtu ana zake.” Vinginevyo, mtazamo wa
kizamani ni taasubi kogwe tu za kiume zilizopitwa na wakati.

Aidha, kwa sababu watu wote huzaliwa na akili timamu, tena hawawi watu wazimu
kabla ya kuwa watoto kwanza, mtu mzima yeyote ana hali gani ya kuwadhulumu
watoto na kujipambaniza na lawama za uongo dhidi ya vijana hao kwa madai kuwa
hawana akili? Na je, ikiwa hawana akili, basi ndipo waonewe? Wanyanyaswe? Hili si
jambo la busara. Kurudi mtoto kwa visa vya maonevu ni kumrudisha nyuma kiumbe huyo.
Kurudi kufaako ni kwa kupeleka mbele, sio kwa kurudisha nyuma. Kurudi kuelekezako
mbele ni kwa uongozi mwafaka, uongozi ambao lengo lake ni kummulikia mtoto kurunzi
ilimradi kumwongoza mtoto.

Mtoto ana haki ya kuhudumiwa kwa njia yoyote ifaayo ili akue na akili yake ikomae
kikamilifu. Inafaa asomeshwe, apewe malezi bora ili naye aje alee wengine kistahiki.

(a) “Mapenzi yasiyo kipimo yanaweza kuwa hatari kwa mtoto.” Eleza kikamilifu
huku ukirejelea habari uliyosoma
(b) Fafanua njia panda inayorejelewa na mtunzi
(c) Mtoto analinganishwa na mmea katika taarifa hi, kwamba “usiporutubishwa
kimakusudi, ukapaliliwa vyema na kustawishwa stahiki yake basi hudhofu.”
Tahtmini kulinganishwa huku, huku ukirejelea taarifa
(d) “Akili ni nywele, kila mtu ana zake.” Eleza maana ya ndani ya methali hii
kulingana na taarifa
(e) Onyesha kwamba unaelewa maana ya:
“Kurudi mtoto kwa visa vya maonevu ni kumrudisha nyuma kiumbe huyo”
(f) Eleza maana ya:
(i) Kulikongomeza
(ii) Kujipambaniza

  

Answers


Kavungya
a) Kutomchapa/kubembeleza/kumdekeza motto anapokosea/anakiuka uadilifu
unamharibu/unamzorotesha tabia zake/Unamfanya mtundu
Akitumia Methali
Sehemu mbili maki 3. akishughulika nusu ya jumla ya
b) Mtazamo wa zamani ambapo ulichukuliwa kuwa watoto na hata wanawake
hawana akili lakini ukweli ni kwamba watu wana akili sawa/wote wan akili
sawa/wote wanafanana/wanaume na wanawake. Ni utata unaoletwa na misimamo
miwili tofauti usasa na ukale. Lazima agusie usasa na ukale
c) Kama ambavyo mmea hudhoofa usipotuuzwa ndivyo ambavyo motto huzorota
kitabia asipopewa malezi mazuri atazorota kitabia. Upande moja ni
Mtoto asipopewa malezi mazuri atazorota kitambia Akisema ni kweli
au ni sawa/ ni hivyo ni
d) Wanaume kuwadharau watoto na wanawake kwamba wana akili pungufu ni
makosa
Akinusisha wanawake, watoto na taarifa
Si lazima ataje wanaume.
Binadamu yoyote huzaliwa na akili zake; hivyo basi si haki kudharualiana kwa
misingi ya kiakili
Binadamu yoyote huzaliwa na akili zake
f) i) Kushindilia/ kulifanya lieleweke
kulishukumiza/kulilazimisha
ii) Kujiaminisha /kujidai/kujiepusha
Kujifanya/kujigangaza/ kukwepa/ kujiberegeza/ kujibambanya/ kujitia/
kujipambaniza.
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 13:03


Next: Andika methali moja inayotokana na maelezo yafuatayo: Asiye na uwezo ataendelea kuwa bila uwezo hata akifanya bidii namna gani.
Previous: MUHTASARI Maendeleo ya taifa hutegemea jinsi wananchi wanavyolitolea katika kulibingirisha gurudumu la uchumi wao. Kila mwanajamii anahitajika kujibidisha katika kazi au taaluma yake. Mzalendo yeyote yule hupata motisha...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Andika methali moja inayotokana na maelezo yafuatayo: Asiye na uwezo ataendelea kuwa bila uwezo hata akifanya bidii namna gani.(Solved)

    Andika methali moja inayotokana na maelezo yafuatayo:
    Asiye na uwezo ataendelea kuwa bila uwezo hata akifanya bidii namna
    gani.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Mdudu mwenye mkia uliopinda nchani ambao una sumu ni?(Solved)

    Mdudu mwenye mkia uliopinda nchani ambao una sumu ni?

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Mdudu anayetengeneza utandu huitwa?(Solved)

    Mdudu anayetengeneza utandu huitwa?

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tumia tanakali za sauti zifaazo kukamilisha sentensi hizi; i) Sauti ya waimbaji haikusikika tena, ilikuwa imedidima…wageni walipofika katika jukwaa. ii) Simba ni mnyama hodari sana, akimkamata swara humrarua(Solved)

    Tumia tanakali za sauti zifaazo kukamilisha sentensi hizi;
    i) Sauti ya waimbaji haikusikika tena, ilikuwa imedidima…wageni
    walipofika katika jukwaa.
    ii) Simba ni mnyama hodari sana, akimkamata swara humrarua

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Kamilisha tashbihi zifuatazo i) Baidika kama ii) Mzima kama(Solved)

    Kamilisha tashbihi zifuatazo
    i) Baidika kama
    ii) Mzima kama

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza tofauti baina ya sentensi hizi; i) Ningekuwa na pesa ningenunua shamba. ii) Ningelikuwa na pesa ningalinunua shamba(Solved)

    Eleza tofauti baina ya sentensi hizi;
    i) Ningekuwa na pesa ningenunua shamba.
    ii) Ningelikuwa na pesa ningalinunua shamba

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana nne-tofauti za sentensi hii; Alinunuliwa samaki na mtoto wake(Solved)

    Eleza maana nne-tofauti za sentensi hii;
    Alinunuliwa samaki na mtoto wake

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika kinyume; Mjomba alichomeka upanga kwenye ala(Solved)

    Andika kinyume;
    Mjomba alichomeka upanga kwenye ala

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Kanusha Ungemwuliza vizuri angekujibu bila wasiwasi(Solved)

    Kanusha
    Ungemwuliza vizuri angekujibu bila wasiwasi

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika vitensi vinavyotokana na majina haya; i) Mfuasi ii) Kifaa iii) Mharibifu(Solved)

    Andika vitensi vinavyotokana na majina haya;
    i) Mfuasi
    ii) Kifaa
    iii) Mharibifu

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Piga mstari vivumishi katika sentensi hizi i) Sina nguo yoyote niwezayo kuvaa ii) Mtoto mwenyewe ataileta kalamu(Solved)

    Piga mstari vivumishi katika sentensi hizi
    i) Sina nguo yoyote niwezayo kuvaa
    ii) Mtoto mwenyewe ataileta kalamu

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika kwa msemo halisi sentensi. Tajiri alishangaa kuwa niliweza kuubeba mzigo huo peke yangu.(Solved)

    Andika kwa msemo halisi sentensi. Tajiri alishangaa kuwa niliweza kuubeba mzigo huo peke yangu.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Ziandike upya sentensi zifuatazo kwa kufuata maagizo uliyopewa. i) Nimemleta paka ili aue panya wote wanaotusumbua hapa kwetu nyumbani. (Anza: Panya…) ii) Mbwa ambaye aliripotiwa kuwa ameibwa amepatikana...(Solved)

    Ziandike upya sentensi zifuatazo kwa kufuata maagizo uliyopewa.
    i) Nimemleta paka ili aue panya wote wanaotusumbua hapa kwetu
    nyumbani. (Anza: Panya…)
    ii) Mbwa ambaye aliripotiwa kuwa ameibwa amepatikana katika
    bwawa la maji (Anza: katika bwawa…..)

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Unganisha sentensi zifuatazo kwa kutumia viunganishi vifaavyo. i) Chakula hiki hakina mchuzi. Hakina chumve ii) Romeo aliamka. Alitazama saa yake Akala kiamsha kinywa mbio mbio(Solved)

    Unganisha sentensi zifuatazo kwa kutumia viunganishi vifaavyo.
    i) Chakula hiki hakina mchuzi. Hakina chumve
    ii) Romeo aliamka. Alitazama saa yake
    Akala kiamsha kinywa mbio mbio

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Geuza sentensi zifuatazo ziwe katika hali ya umoja i) Huku kuimba kwenu kuzuri kutawapendez wageni ii) Hii miche ni mizuri sana, itatufaa(Solved)

    Geuza sentensi zifuatazo ziwe katika hali ya umoja
    i) Huku kuimba kwenu kuzuri kutawapendez wageni
    ii) Hii miche ni mizuri sana, itatufaa

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tumia viashiria vya kutilia mkazo katika sentensi zifuatazo i) Kibogoyo………. Ndiye anayehitaji meno ya dhahabu. ii) Vyakula……………mvipikavyo nyinyi, nasi twavipika(Solved)

    Tumia viashiria vya kutilia mkazo katika sentensi zifuatazo
    i) Kibogoyo………. Ndiye anayehitaji meno ya dhahabu.
    ii) Vyakula……………mvipikavyo nyinyi, nasi twavipika

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Ukiwa mtoto unadhani ulimwengu ni kipande kimoja cha keki kilicho kitamu mithili ya asali. Hakuna dhiki, hakuna mateso, hakuna kuhuzunika kwa...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
    Ukiwa mtoto unadhani ulimwengu ni kipande kimoja cha keki kilicho kitamu mithili ya
    asali. Hakuna dhiki, hakuna mateso, hakuna kuhuzunika kwa aina yoyote. Neno huzuni
    linasikika masikioni kama neno lisiloelekea kwenye uhalisia wowote. Kwa watoto dunia
    imejaa raha, starehe na vicheko visivyoisha. Maisha ni ahadi njema, yenye matokeo ya
    kufurahisha na kustarehesha tu, sio KUDHIKISHA NA KUHUZUNISHA.

    Huyu tunayemzumgumzia hapa ni mtoto mdogo ambaye hajajua kubainisha
    kitendekacho mkono wake wa kushoto na kile kinachofanyika hasa katika mkono wake
    wa kulia. Hata hivyo, jinsi mtoto anavyoendelea kukua na kufahamikiwa na mambo,
    vigambo na kadhia zinazoendelea katika mazingira yake, anabainikiwa na mengi
    machungu ambayo huleta huzuni, sio raha.

    Hebu tuanze na nyumbani kwao mtoto. Aghalabu, watoto wote hupendwa kwao
    nyumbani, iwapo wazazi wao ni watu wangwana na wana nafasi ya kulea watoto wao
    bila taabu. Hata hivyo watoto huchapwa pale wanapokuwa watundu, jambo ambalo
    huwahuzunisha sana, japo ni wajibu wa wazazi sababu, kama isemwavyo, mcha mwana
    kulia hulia yeye. Pili, inajulikana wazi kwamba watoto wengi siku hizi huenda shule,
    huko shule, wao hupendelea sana kucheza kuliko kusoma. Ili wasome kama
    inavyotakikana, ni sharti waelekezwe barabara katika njia hiyo na walimu wao. Katika
    kuelekezwa huku, walimu wanaweza kulazimika kuwaadhibu, hasa wale watoto ambao
    huzembea na kutofanya kazi zao wanazopewa kufanya nyumbani kama kawaida ya
    mfumo wa shule ilivyo. Watoto ambao huzembea na kutofanya kazi zao wanazopewa
    kufanya nyumbani kama kawaida ya mfumo wa shule ilivyo. Watoto wa aina hii
    wanapotiwa adabu raha hujitenga na huzuni huwatawala.

    Huzuni, hivyo basi, inaonekana ya kuwa ni uso wa pili katika maisha ya mwanadamu,
    uso wa kwanza ukiwa raha. Na kwa hakika wanaohuzunika si watoto peke yao. Kila mtu
    duniani ni sharti, katika wakati mmoja au mwingine, azongwe na huzuni. Inajulikana
    wazi kwamba wanadamu wote hawapendi huzuni asilani na hakika kabisa, kila binadamu huchukia huzuni na kustahabu raha. Hata hivyo, raha humjia binadamu kwa nadra sana,
    ilhali huzuni humvamia wakati wowote, hata akiwa humo katikati ya kustarehe. Si tu,
    inajulikana dhahiri shahiri kwamba hakuna mtu asiyewahi kuonja huzuni, japo wapo
    watu wengi kweli kweli wasiowahi kuonja raha maishani mwao.

    Zingatia mtoto anaezaliwa, halafu wazazi wake wanaaga dunia, pengine katika ajali,
    kabla mtoto mwenyewe hajaweza kujikimu. Mtoto huyu anaishi kutegemea jamaa za
    wazazi wake. Watu hawa wasipokuwa na nafasi wao wenyewe kimaisha pamoja na
    ukarimu unaohitajika basi mtoto anateseka na kuhuzunika sana katika maisha yake yote.
    Ama zingatia mtoto anayetupwa na mamake kijana, aliyempata bila kupanga. Hata mtoto
    huyu akiokotwa na kulelewa na wahisani, maisha yake yatakuwa ya taabu, dhiki na
    huzuni. Au zingatia mtoto anayelelewa na mama wa kambo anayeondokea kuwa
    mwovu. Mtoto huyu atakayoijua ni huzuni tu. Ama zingatia mtoto ambaye babake ni
    mlevi na unalojua ni kurudi nyumbani kufurahia kupiga watoto wote na mama yao ndipo
    apate usingizi mnono. Mtoto mwenye baba wa aina hiyo atakayoijua ni huzuni tu, sir aha
    asilani.

    a) Ukitumia maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana, fupisha aya
    nne za mwanzo (Maneno -100)
    b) Ukizingatia aya ya mwisho, eleza hali mbalimbali zinazowatia watoto
    huzuni. (Maneno 40-45)

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu mwsawali Utandaridhi (au globalization kwa lugha ya Kingereza) ni jinsi ya maisha inayoendelea kuutawala ulimwengu wote katika karne hii ya 21. Neno...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu mwsawali
    Utandaridhi (au globalization kwa lugha ya Kingereza) ni jinsi ya maisha inayoendelea
    kuutawala ulimwengu wote katika karne hii ya 21. Neno utandaridhi ni neno mseto
    ambalo maana yake ni utamaduni uliotanda au kuenea ardhi nzima. Mtu mtandaridhi’
    hivyo basi ni mtu aliyebebea kikamilifu katika utamaduni huu mpya kwa jinsi moja au
    nyingine.

    Matandaridhi hujihusisha sana katika kutandaridhisha aina moja au nyingine ya amara
    muhimu za kitandaridhi. Hizo ni kama vile biashara za kumataifa, lugha za kimataifa,
    aina za mavazi zilizotokea kupendwa ulimwenguni kote, muziki wa kisiku hizi, hasa vile
    pop, reggae, raga, rap, ambao asili yake ya hivi majuzi ni Marekani. Muziki huo
    waimbaji wake hutumia, sana sana, lugha ya Kiingereza hususan kile cha Marekani na
    kadhalika Watandaridhi wana nyenzo zingine kadha wa kadha za kuendeshea maisha yao
    au kujitambulisha. Wao huwasiliana kutoka pembe moja ya duni hadi nyingine
    wakitumia vitumeme, yaani vyombo vitumiavyo umeme kufanya kazi vya hali ya juu,
    kama vile tarakilishi na simu, hata za mkono. Watu hawa hawakosi runinga sebuleni
    mwao, usiseme redio. Hawa husikiliza na kutazama habari za kimataifa kupitia mashirika
    matandaridhi ya habari kama vile BBC la uingereza CNN la marekani. Aidha watu hawa
    husafiri mara kwa mara kwa ndege na vyombo vingine vya kasi. Hawa hawana mipaka.
    Wale wanaohusudu utandaridhi wanaamini kindakindaki kwamba utamaduni huu wa
    kilimwengu umeleta mlahaka mwema baina ya watu binafsi, makampuni makubwa
    makubwa ya kimataifa na usiano bora baina ya mataifa. Watu hawa husikia wakidai ya
    kuwa aina hii ya utamaduni imeupigisha mbele ustaarabu wa wanadamu ulimwenguni
    kote. Kwa upande mwingine, wakereketwa wa tamaduni za kimsingi za mataifa na
    makabila mbalimbali ulimwenguni wanadai ya kwamba utandaridhi umeleta maangamizi
    makubwa ya tamaduni hizo. Kwa ajili hiyo basi, utandaridhi umeleta maangamizi
    makubwa ya tamaduni hizo. Kwa ajili hiyo basi, utandaridhi umesemekana kwamba
    unasababisha kutovuka kwa utu miongoni mwa wanadamu wote, ambao wamo mbioni
    kusaka pesa na kuneemesha ubinafsi. Inadaiwa pia kwamba utandaridhi umesababisha
    kutovuka kwa adab kwa vijana wengi ulimwenguni kote ghaya ya utovu. Huku kutovuka
    kwa adabu kwa vijana wengi ulimwenguni kote ghaya ya utovu. Huku kutovuka kwa
    adabu kwa vijana, hasa wale wa mataif yanayojaribu kuendelea, kumeleta zahama
    chungu mbovu, ikiwa ni pamoja na kuenea kwa UKIMWI kwa kasi ya kutisha.

    a) i) Bainisha kwa kutoa maelezo kamili kwamba utandaridhi ni neno mseto.
    ii) Tohoa maneno mawili kutokana na neon kutandaridhisha kisha ueleze
    maana za maneno hayo.
    b) i) Nini maana ya ‘hawa hawana mipaka?’
    ii) Kwa nini watandaridhi wanpenda kusikiliza na kutazama habari kupitia
    BBC na CNN?
    c) i) Eleza kikamilifu maoni ya watandaridhi kuhusu utamaduni wao
    ii) Je, Utandaridhi unalaumiwa kwa nini katika kifungu hiki?
    d) Msemo: “ chungu mbovu” ni msemo wa kimtaani tu. Msemo sawa ni upi
    e) Eleza maana ya maneno yafuatayo
    i) Amara
    ii) Mlahaka
    iii) Wakereketwa

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya methali Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni(Solved)

    Eleza maana ya methali
    Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana mbili tofauti za Rudi(Solved)

    Eleza maana mbili tofauti za Rudi

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)