Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
a) Maendelo ya taifa hutegemea bidii/kujitolea kwa wananchi kazini (ii)
mazalendo hupata motisha apatapo aliyatamani (iii) Taaluma yoyote
huchukua muda kutengenea kumakinika katika taluma Fulani. Huchukua
muda kutengenea (iv) Mnazili lazima ahitimu darasani/mhazini ahitimu
katika masomo rasmi ya darasa (v) anatakiwa afanye mazoezi kila mara ili
asisahau (vii) wengi huona kuwa hawatapata kazi nzuri/ ya msharara
mzuri. Wengi hulinganisha wenzao wenye viwango tofauti au mishara
tofauti/ ni rahisi kupata kazi zenye ujira wa kuvutia (viii) anayefanikiwa ni
lazima/ni sharti yapaswa ajikakamue kazini.
b) mashariki makubwa yanajiweza kiuchumi kuliko madogo. (2) Mashirika
madogo hulipa mishahara duni isiyotegemewa (3) wafanyikazi hawawezi
kutilia maanani kazi yao (4) Baadhi ya wakurigemzo jwabanizi na
kuwapunja wafani kazi wao au/ ulipaji wa mishahara hutegemea utu wa
mkurugenzi au/Masharika mengine hayana ustaratibu maalum ya kulipa
mishahara (5) kuna haja ya kuwa na chama cha kupigania haki za wafanyi
kazi. (6) Waliazili vingine ni wahitaji na hukubali chochote wanachopewa
(7) wanao ajiriwa katika kampuni za kimaataifa mashirika makubwa
hulipwa mishahara mikubwa (8) Wahazili lazima wapate tajuiba/ uzoefu
na wawe wavumililivu (9) wakurugenzi wasio na subira huwafokea na /au
hufutwa au kuwafuta kazi/wahazili wasio makinika hufokewa na au
hufutwa kazi
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 13:06
- Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Wahenga walisema “mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.” Hii ina maana ya kuwa ukiogopa
kutumia ufito kumchapa mtoto wako, ukamdekeza atadeka na hatimaye...(Solved)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Wahenga walisema “mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.” Hii ina maana ya kuwa ukiogopa
kutumia ufito kumchapa mtoto wako, ukamdekeza atadeka na hatimaye ataharibika.
Methali hii ina picha yake ambyo ni, “Ukicha mwana kulia, utalia wewe.”
Hizi ni methali zilizojaa busara kubwa. Mathalini wewe ni mzazi au mtu yeyote mzima
aliyetunikiwa madaraka juu ya watoto. Lakini kila wanapokiuka uadilifu au mmoja wao
anapokosea wewe unambembeleza tu, basi huwa unaizorotesha tabia yake. Mwisho,
mtoto huyo anaweza kuishia kuwa mtundu.
Hata hivyo, ni sharti tujue ya kwamba tuko katika njia panda hapa. Kwa upande mmoja,
zamani ilichukuliwa kwamba watoto na hata wanawake watu wazima hawana akili. Kwa
ajili hiyo, iwapo mwanaume mtu mzima ana jambo la kuwaeleza, njia pekee ya
kuliingiza katika “ akili” yao “ hafifu” ni kuwatwanga ili kulikongomeza jambo hili.
Ukweli ni kwamba akili ya mtoto si hafifu hata. Unaweza kusema ni kama mmea, ambao
usiporutubishwa kimakusudi, ukapaliliwa vyema na kustawishwa stahiki yake, basi
hudhoofu” na mwishowe kufifia.
Kwa upande mwingine, mtazamo wa kisasa ni tofauti kabisa, imethibitishwa ya kwamba
wanawake ni sawa kabisa katika maumbile yao wakilinganishwa na wanaume. Kwa jinsi
hiyo, kweli wapo wanawake amabo hawana mwelekeo timamu kuhusu maisha. Lakini ni
kweli pia kuwa wapo wanaume watu wazima mamilioni ambao hawana akili.
Kadhalika, si kweli kuwa watoto wote, kwa sababu ya umri wao tu, basi hawana akili.
Ama kwa kusema kweli binadamu yeyote kuwaliwa na akili zake timamu isipokuwa wale
ambao kwa bahati mbaya maumbile yamewapa akili pungufu. Hili litokeapo basi
tunalikubali tu. Hatuwezi kumlaumu mtu kama huyo au muumba wake. Kwa hakika huu
ndio msingi wa methali. “Akili ni nywele, kila mtu ana zake.” Vinginevyo, mtazamo wa
kizamani ni taasubi kogwe tu za kiume zilizopitwa na wakati.
Aidha, kwa sababu watu wote huzaliwa na akili timamu, tena hawawi watu wazimu
kabla ya kuwa watoto kwanza, mtu mzima yeyote ana hali gani ya kuwadhulumu
watoto na kujipambaniza na lawama za uongo dhidi ya vijana hao kwa madai kuwa
hawana akili? Na je, ikiwa hawana akili, basi ndipo waonewe? Wanyanyaswe? Hili si
jambo la busara. Kurudi mtoto kwa visa vya maonevu ni kumrudisha nyuma kiumbe huyo.
Kurudi kufaako ni kwa kupeleka mbele, sio kwa kurudisha nyuma. Kurudi kuelekezako
mbele ni kwa uongozi mwafaka, uongozi ambao lengo lake ni kummulikia mtoto kurunzi
ilimradi kumwongoza mtoto.
Mtoto ana haki ya kuhudumiwa kwa njia yoyote ifaayo ili akue na akili yake ikomae
kikamilifu. Inafaa asomeshwe, apewe malezi bora ili naye aje alee wengine kistahiki.
(a) “Mapenzi yasiyo kipimo yanaweza kuwa hatari kwa mtoto.” Eleza kikamilifu
huku ukirejelea habari uliyosoma
(b) Fafanua njia panda inayorejelewa na mtunzi
(c) Mtoto analinganishwa na mmea katika taarifa hi, kwamba “usiporutubishwa
kimakusudi, ukapaliliwa vyema na kustawishwa stahiki yake basi hudhofu.”
Tahtmini kulinganishwa huku, huku ukirejelea taarifa
(d) “Akili ni nywele, kila mtu ana zake.” Eleza maana ya ndani ya methali hii
kulingana na taarifa
(e) Onyesha kwamba unaelewa maana ya:
“Kurudi mtoto kwa visa vya maonevu ni kumrudisha nyuma kiumbe huyo”
(f) Eleza maana ya:
(i) Kulikongomeza
(ii) Kujipambaniza
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Andika methali moja inayotokana na maelezo yafuatayo:
Asiye na uwezo ataendelea kuwa bila uwezo hata akifanya bidii namna
gani.(Solved)
Andika methali moja inayotokana na maelezo yafuatayo:
Asiye na uwezo ataendelea kuwa bila uwezo hata akifanya bidii namna
gani.
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Mdudu mwenye mkia uliopinda nchani ambao una sumu ni?(Solved)
Mdudu mwenye mkia uliopinda nchani ambao una sumu ni?
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Mdudu anayetengeneza utandu huitwa?(Solved)
Mdudu anayetengeneza utandu huitwa?
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Tumia tanakali za sauti zifaazo kukamilisha sentensi hizi;
i) Sauti ya waimbaji haikusikika tena, ilikuwa imedidima…wageni
walipofika katika jukwaa.
ii) Simba ni mnyama hodari sana, akimkamata swara humrarua(Solved)
Tumia tanakali za sauti zifaazo kukamilisha sentensi hizi;
i) Sauti ya waimbaji haikusikika tena, ilikuwa imedidima…wageni
walipofika katika jukwaa.
ii) Simba ni mnyama hodari sana, akimkamata swara humrarua
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Kamilisha tashbihi zifuatazo
i) Baidika kama
ii) Mzima kama(Solved)
Kamilisha tashbihi zifuatazo
i) Baidika kama
ii) Mzima kama
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Eleza tofauti baina ya sentensi hizi;
i) Ningekuwa na pesa ningenunua shamba.
ii) Ningelikuwa na pesa ningalinunua shamba(Solved)
Eleza tofauti baina ya sentensi hizi;
i) Ningekuwa na pesa ningenunua shamba.
ii) Ningelikuwa na pesa ningalinunua shamba
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Eleza maana nne-tofauti za sentensi hii;
Alinunuliwa samaki na mtoto wake(Solved)
Eleza maana nne-tofauti za sentensi hii;
Alinunuliwa samaki na mtoto wake
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Andika kinyume;
Mjomba alichomeka upanga kwenye ala(Solved)
Andika kinyume;
Mjomba alichomeka upanga kwenye ala
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Kanusha
Ungemwuliza vizuri angekujibu bila wasiwasi(Solved)
Kanusha
Ungemwuliza vizuri angekujibu bila wasiwasi
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Andika vitensi vinavyotokana na majina haya;
i) Mfuasi
ii) Kifaa
iii) Mharibifu(Solved)
Andika vitensi vinavyotokana na majina haya;
i) Mfuasi
ii) Kifaa
iii) Mharibifu
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Piga mstari vivumishi katika sentensi hizi
i) Sina nguo yoyote niwezayo kuvaa
ii) Mtoto mwenyewe ataileta kalamu(Solved)
Piga mstari vivumishi katika sentensi hizi
i) Sina nguo yoyote niwezayo kuvaa
ii) Mtoto mwenyewe ataileta kalamu
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Andika kwa msemo halisi sentensi. Tajiri alishangaa kuwa niliweza kuubeba mzigo huo peke yangu.(Solved)
Andika kwa msemo halisi sentensi. Tajiri alishangaa kuwa niliweza kuubeba mzigo huo peke yangu.
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Ziandike upya sentensi zifuatazo kwa kufuata maagizo uliyopewa.
i) Nimemleta paka ili aue panya wote wanaotusumbua hapa kwetu
nyumbani. (Anza: Panya…)
ii) Mbwa ambaye aliripotiwa kuwa ameibwa amepatikana...(Solved)
Ziandike upya sentensi zifuatazo kwa kufuata maagizo uliyopewa.
i) Nimemleta paka ili aue panya wote wanaotusumbua hapa kwetu
nyumbani. (Anza: Panya…)
ii) Mbwa ambaye aliripotiwa kuwa ameibwa amepatikana katika
bwawa la maji (Anza: katika bwawa…..)
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Unganisha sentensi zifuatazo kwa kutumia viunganishi vifaavyo.
i) Chakula hiki hakina mchuzi. Hakina chumve
ii) Romeo aliamka. Alitazama saa yake
Akala kiamsha kinywa mbio mbio(Solved)
Unganisha sentensi zifuatazo kwa kutumia viunganishi vifaavyo.
i) Chakula hiki hakina mchuzi. Hakina chumve
ii) Romeo aliamka. Alitazama saa yake
Akala kiamsha kinywa mbio mbio
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Geuza sentensi zifuatazo ziwe katika hali ya umoja
i) Huku kuimba kwenu kuzuri kutawapendez wageni
ii) Hii miche ni mizuri sana, itatufaa(Solved)
Geuza sentensi zifuatazo ziwe katika hali ya umoja
i) Huku kuimba kwenu kuzuri kutawapendez wageni
ii) Hii miche ni mizuri sana, itatufaa
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Tumia viashiria vya kutilia mkazo katika sentensi zifuatazo
i) Kibogoyo………. Ndiye anayehitaji meno ya dhahabu.
ii) Vyakula……………mvipikavyo nyinyi, nasi twavipika(Solved)
Tumia viashiria vya kutilia mkazo katika sentensi zifuatazo
i) Kibogoyo………. Ndiye anayehitaji meno ya dhahabu.
ii) Vyakula……………mvipikavyo nyinyi, nasi twavipika
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Ukiwa mtoto unadhani ulimwengu ni kipande kimoja cha keki kilicho kitamu mithili ya
asali. Hakuna dhiki, hakuna mateso, hakuna kuhuzunika kwa...(Solved)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Ukiwa mtoto unadhani ulimwengu ni kipande kimoja cha keki kilicho kitamu mithili ya
asali. Hakuna dhiki, hakuna mateso, hakuna kuhuzunika kwa aina yoyote. Neno huzuni
linasikika masikioni kama neno lisiloelekea kwenye uhalisia wowote. Kwa watoto dunia
imejaa raha, starehe na vicheko visivyoisha. Maisha ni ahadi njema, yenye matokeo ya
kufurahisha na kustarehesha tu, sio KUDHIKISHA NA KUHUZUNISHA.
Huyu tunayemzumgumzia hapa ni mtoto mdogo ambaye hajajua kubainisha
kitendekacho mkono wake wa kushoto na kile kinachofanyika hasa katika mkono wake
wa kulia. Hata hivyo, jinsi mtoto anavyoendelea kukua na kufahamikiwa na mambo,
vigambo na kadhia zinazoendelea katika mazingira yake, anabainikiwa na mengi
machungu ambayo huleta huzuni, sio raha.
Hebu tuanze na nyumbani kwao mtoto. Aghalabu, watoto wote hupendwa kwao
nyumbani, iwapo wazazi wao ni watu wangwana na wana nafasi ya kulea watoto wao
bila taabu. Hata hivyo watoto huchapwa pale wanapokuwa watundu, jambo ambalo
huwahuzunisha sana, japo ni wajibu wa wazazi sababu, kama isemwavyo, mcha mwana
kulia hulia yeye. Pili, inajulikana wazi kwamba watoto wengi siku hizi huenda shule,
huko shule, wao hupendelea sana kucheza kuliko kusoma. Ili wasome kama
inavyotakikana, ni sharti waelekezwe barabara katika njia hiyo na walimu wao. Katika
kuelekezwa huku, walimu wanaweza kulazimika kuwaadhibu, hasa wale watoto ambao
huzembea na kutofanya kazi zao wanazopewa kufanya nyumbani kama kawaida ya
mfumo wa shule ilivyo. Watoto ambao huzembea na kutofanya kazi zao wanazopewa
kufanya nyumbani kama kawaida ya mfumo wa shule ilivyo. Watoto wa aina hii
wanapotiwa adabu raha hujitenga na huzuni huwatawala.
Huzuni, hivyo basi, inaonekana ya kuwa ni uso wa pili katika maisha ya mwanadamu,
uso wa kwanza ukiwa raha. Na kwa hakika wanaohuzunika si watoto peke yao. Kila mtu
duniani ni sharti, katika wakati mmoja au mwingine, azongwe na huzuni. Inajulikana
wazi kwamba wanadamu wote hawapendi huzuni asilani na hakika kabisa, kila binadamu huchukia huzuni na kustahabu raha. Hata hivyo, raha humjia binadamu kwa nadra sana,
ilhali huzuni humvamia wakati wowote, hata akiwa humo katikati ya kustarehe. Si tu,
inajulikana dhahiri shahiri kwamba hakuna mtu asiyewahi kuonja huzuni, japo wapo
watu wengi kweli kweli wasiowahi kuonja raha maishani mwao.
Zingatia mtoto anaezaliwa, halafu wazazi wake wanaaga dunia, pengine katika ajali,
kabla mtoto mwenyewe hajaweza kujikimu. Mtoto huyu anaishi kutegemea jamaa za
wazazi wake. Watu hawa wasipokuwa na nafasi wao wenyewe kimaisha pamoja na
ukarimu unaohitajika basi mtoto anateseka na kuhuzunika sana katika maisha yake yote.
Ama zingatia mtoto anayetupwa na mamake kijana, aliyempata bila kupanga. Hata mtoto
huyu akiokotwa na kulelewa na wahisani, maisha yake yatakuwa ya taabu, dhiki na
huzuni. Au zingatia mtoto anayelelewa na mama wa kambo anayeondokea kuwa
mwovu. Mtoto huyu atakayoijua ni huzuni tu. Ama zingatia mtoto ambaye babake ni
mlevi na unalojua ni kurudi nyumbani kufurahia kupiga watoto wote na mama yao ndipo
apate usingizi mnono. Mtoto mwenye baba wa aina hiyo atakayoijua ni huzuni tu, sir aha
asilani.
a) Ukitumia maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana, fupisha aya
nne za mwanzo (Maneno -100)
b) Ukizingatia aya ya mwisho, eleza hali mbalimbali zinazowatia watoto
huzuni. (Maneno 40-45)
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Soma makala yafuatayo kisha ujibu mwsawali
Utandaridhi (au globalization kwa lugha ya Kingereza) ni jinsi ya maisha inayoendelea
kuutawala ulimwengu wote katika karne hii ya 21. Neno...(Solved)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu mwsawali
Utandaridhi (au globalization kwa lugha ya Kingereza) ni jinsi ya maisha inayoendelea
kuutawala ulimwengu wote katika karne hii ya 21. Neno utandaridhi ni neno mseto
ambalo maana yake ni utamaduni uliotanda au kuenea ardhi nzima. Mtu mtandaridhi’
hivyo basi ni mtu aliyebebea kikamilifu katika utamaduni huu mpya kwa jinsi moja au
nyingine.
Matandaridhi hujihusisha sana katika kutandaridhisha aina moja au nyingine ya amara
muhimu za kitandaridhi. Hizo ni kama vile biashara za kumataifa, lugha za kimataifa,
aina za mavazi zilizotokea kupendwa ulimwenguni kote, muziki wa kisiku hizi, hasa vile
pop, reggae, raga, rap, ambao asili yake ya hivi majuzi ni Marekani. Muziki huo
waimbaji wake hutumia, sana sana, lugha ya Kiingereza hususan kile cha Marekani na
kadhalika Watandaridhi wana nyenzo zingine kadha wa kadha za kuendeshea maisha yao
au kujitambulisha. Wao huwasiliana kutoka pembe moja ya duni hadi nyingine
wakitumia vitumeme, yaani vyombo vitumiavyo umeme kufanya kazi vya hali ya juu,
kama vile tarakilishi na simu, hata za mkono. Watu hawa hawakosi runinga sebuleni
mwao, usiseme redio. Hawa husikiliza na kutazama habari za kimataifa kupitia mashirika
matandaridhi ya habari kama vile BBC la uingereza CNN la marekani. Aidha watu hawa
husafiri mara kwa mara kwa ndege na vyombo vingine vya kasi. Hawa hawana mipaka.
Wale wanaohusudu utandaridhi wanaamini kindakindaki kwamba utamaduni huu wa
kilimwengu umeleta mlahaka mwema baina ya watu binafsi, makampuni makubwa
makubwa ya kimataifa na usiano bora baina ya mataifa. Watu hawa husikia wakidai ya
kuwa aina hii ya utamaduni imeupigisha mbele ustaarabu wa wanadamu ulimwenguni
kote. Kwa upande mwingine, wakereketwa wa tamaduni za kimsingi za mataifa na
makabila mbalimbali ulimwenguni wanadai ya kwamba utandaridhi umeleta maangamizi
makubwa ya tamaduni hizo. Kwa ajili hiyo basi, utandaridhi umeleta maangamizi
makubwa ya tamaduni hizo. Kwa ajili hiyo basi, utandaridhi umesemekana kwamba
unasababisha kutovuka kwa utu miongoni mwa wanadamu wote, ambao wamo mbioni
kusaka pesa na kuneemesha ubinafsi. Inadaiwa pia kwamba utandaridhi umesababisha
kutovuka kwa adab kwa vijana wengi ulimwenguni kote ghaya ya utovu. Huku kutovuka
kwa adabu kwa vijana wengi ulimwenguni kote ghaya ya utovu. Huku kutovuka kwa
adabu kwa vijana, hasa wale wa mataif yanayojaribu kuendelea, kumeleta zahama
chungu mbovu, ikiwa ni pamoja na kuenea kwa UKIMWI kwa kasi ya kutisha.
a) i) Bainisha kwa kutoa maelezo kamili kwamba utandaridhi ni neno mseto.
ii) Tohoa maneno mawili kutokana na neon kutandaridhisha kisha ueleze
maana za maneno hayo.
b) i) Nini maana ya ‘hawa hawana mipaka?’
ii) Kwa nini watandaridhi wanpenda kusikiliza na kutazama habari kupitia
BBC na CNN?
c) i) Eleza kikamilifu maoni ya watandaridhi kuhusu utamaduni wao
ii) Je, Utandaridhi unalaumiwa kwa nini katika kifungu hiki?
d) Msemo: “ chungu mbovu” ni msemo wa kimtaani tu. Msemo sawa ni upi
e) Eleza maana ya maneno yafuatayo
i) Amara
ii) Mlahaka
iii) Wakereketwa
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Eleza maana ya methali
Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni(Solved)
Eleza maana ya methali
Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)