i) Mtukufu: Tukua/tukuka/tukuzana/tukuzwa
ii) Chumbia/Chumbiana/Chumbiwa
Kavungya answered the question on June 27, 2019 at 13:29
- Tunga sentensi mbili tofauti ukitumia vitenzi hivi vya silabi moja
(i) Pa
(ii) La(Solved)
Tunga sentensi mbili tofauti ukitumia vitenzi hivi vya silabi moja
(i) Pa
(ii) La
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Andika sentensi zifuatazo upya kwa kufuata maagizo
(i) Alicheza kwa bidii akawafurahisha wengi waliohudhuria tamasha hizo
Anza kwa: Kucheza
(ii) Karamu hiyo ilifanya sana, kila mtu alikula chakula...(Solved)
Andika sentensi zifuatazo upya kwa kufuata maagizo
(i) Alicheza kwa bidii akawafurahisha wengi waliohudhuria tamasha hizo
Anza kwa: Kucheza
(ii) Karamu hiyo ilifanya sana, kila mtu alikula chakula akatosheka
Anza kwa: chakula
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- (i) Taja vihusishi vitatu vinavyorejelea mahali, wakati na kiwango
(ii) Tunga sentensi kuonyesha matumizi ya kila kihusishi(Solved)
(i) Taja vihusishi vitatu vinavyorejelea mahali, wakati na kiwango
(ii) Tunga sentensi kuonyesha matumizi ya kila kihusishi
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Andika kifungu hiki kutoka usemi wa taarifa hadi usemi halisi
Watoto waliambiwa na mama yao watakaporudi nyumbani waoge. Wale,
halafu waanse kusoma moja kwa moja badala ya...(Solved)
Andika kifungu hiki kutoka usemi wa taarifa hadi usemi halisi
Watoto waliambiwa na mama yao watakaporudi nyumbani waoge. Wale,
halafu waanse kusoma moja kwa moja badala ya kuharibu wakati wao
kwa kutazama vipindi vya runinga. Aliwakumbusha kuwa wanaofanya
maonyesho kwenye runinga tayari wamefuzu shuleni na wameajiriwa kazi
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Tambulisha kielezi, kivumishi na mnyambuliko wa kitenzi katika sentensi
ifuatayo:
Msichana mrembo alikuja upesi akimkimbilia dadake(Solved)
Tambulisha kielezi, kivumishi na mnyambuliko wa kitenzi katika sentensi
ifuatayo:
Msichana mrembo alikuja upesi akimkimbilia dadake
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Tunga sentensi kuonyesha matumizi sahihi ya viunganishi hivi
(i) Ingawaje
(ii) Ilhali(Solved)
Tunga sentensi kuonyesha matumizi sahihi ya viunganishi hivi
(i) Ingawaje
(ii) Ilhali
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Tunga sentensi mbilimbili kuonyesha matumizi mawili tofauti ya
I. Ka
II. Ndivyo(Solved)
Tunga sentensi mbilimbili kuonyesha matumizi mawili tofauti ya
I. Ka
II. Ndivyo
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo
(i) Kazi yote ni muhimu
(ii) Kazi yoyote ni muhimu(Solved)
Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo
(i) Kazi yote ni muhimu
(ii) Kazi yoyote ni muhimu
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Eleza namna mbili za matumizi ya alama ifuatayo ya uakifishi (;)
(Solved)
Eleza namna mbili za matumizi ya alama ifuatayo ya uakifishi (;)
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Andika udogo na ukubwa wa jina ngoma.(Solved)
Andika udogo na ukubwa wa jina ngoma.
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- MUHTASARI
Maendeleo ya taifa hutegemea jinsi wananchi wanavyolitolea katika kulibingirisha
gurudumu la uchumi wao. Kila mwanajamii anahitajika kujibidisha katika kazi au
taaluma yake. Mzalendo yeyote yule hupata motisha...(Solved)
MUHTASARI
Maendeleo ya taifa hutegemea jinsi wananchi wanavyolitolea katika kulibingirisha
gurudumu la uchumi wao. Kila mwanajamii anahitajika kujibidisha katika kazi au
taaluma yake. Mzalendo yeyote yule hupata motisha ya kufanya kazi iwapo anaweza
kupata ile kazi aliyokuwa akitamani.
Kumakinika katika taaluma Fulani si jambo jepesi na huchukua muda kutengeneza. Kwa
mfano, ili mhazili apate staha ya uhazili sharti apitie ngazi mbali mbali. Mwanzo kabisa
lazima kumpa fursa ya kujiunga na vyuo mbali mbali vya uhazili. Anapojiunga na vyuo
hivyo ndipo safari inapoandaliwa. Kukamilisha safari hii inahitaji muda wa miaka minemitano.
Anapohitimu kuwa tayari ameimudu shughuli hiyo. Hata hivyo, anatakiwa
afanye mazoezi kila mara ili asisahau yanayohitajika katika taaluma hiyo. Wengi
waliokwishapata ujuzi huo wa wale wenzao ambao katika masomo wana utaakamu kama
wao. Ijapokuwa wote ni wahazili, viwango vyao ni tofauti na mishahara pia hutofautiana.
Tofauti hapa ni daraja zao za vyeo. Baada ya kuhitimu na kupata vyeti vya uhazili ni
rahisi kupata au kutopata kazi zenye ujira wa kuvutia. Anayefanikiwa ana sayari ya
kujikakamua hasa kwa upande wa uzingatifu wa kazi kikamilifu na kutunza hadhi ya
ofisi yake.
Kuna mashirika makubwa yanayojiweza kiuchumi, ambayo rasimali yake ni imara.
Mashirika madogo huwa yana rasilmali yenye kuyumbayumba. Mashirika haya yana
wahazili na wanafunzi ambao hupata mishahara duni. Wanafunzi wote hao hufanya kazi
kwa kutokuwa na uhakika wa kulipwa mwisho wa mwezi. Watu kama hao hawawezi
kutilia maanani kazi zao. Mashirika mengine hayana utaratibu maalum, wa kulipa
mishahara kwa vile hutegemea utu wa mkurugenzi. Badhi ya wakuu hao huwa wabanizi
na huwapunja wafanyi kazi wao. Hili ni swala nyeti ambalo linahitaji litatuliwe kwa kuwa na chama cha kupigania haki za wafanyikazi. Wakati wanapotafuta kazi, Wahazili
wengi huwa ni wahitaji na hukubali chochote wanachopewa.
Wale waliobahatika kupata nafasi ya ajira katika kampuni kubwa za kimaataifa,
mishahara huwa ni ya kutia moyo. Katika dunia hii wahazili wana vibarua vigumu, kwa
sababu lazima wapate tajriba na uzoefu wa taaluma inayoendelea na shirika Fulani.
Mhazili anapotumia msamiati usionda sambamba na shughuli za kiofisi hawasiti kufoka.
Wavumilivu miongoni mwao hula mbivu. Hawa hawafi moyo bali hujitahidi zaidi ili
wasikumbwe na kimbunga cha kufokewa. Kuna wengine ambao humwaga unga.
(a) Bila kupoteza iliyokusudiwa na mwandishi wa taarifa, fupisha aya ya kwanza
na ya pili ( maneno 60 – 70) Alama 2 kwa mtiririko)
(b) Kwa kuzingatia aya mbili za mwisho, eleza mambo muhimu yanayoshughulika na
mwandishi ( maneno 60 – 70) alama 2 kwa mtiririko)
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Wahenga walisema “mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.” Hii ina maana ya kuwa ukiogopa
kutumia ufito kumchapa mtoto wako, ukamdekeza atadeka na hatimaye...(Solved)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Wahenga walisema “mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.” Hii ina maana ya kuwa ukiogopa
kutumia ufito kumchapa mtoto wako, ukamdekeza atadeka na hatimaye ataharibika.
Methali hii ina picha yake ambyo ni, “Ukicha mwana kulia, utalia wewe.”
Hizi ni methali zilizojaa busara kubwa. Mathalini wewe ni mzazi au mtu yeyote mzima
aliyetunikiwa madaraka juu ya watoto. Lakini kila wanapokiuka uadilifu au mmoja wao
anapokosea wewe unambembeleza tu, basi huwa unaizorotesha tabia yake. Mwisho,
mtoto huyo anaweza kuishia kuwa mtundu.
Hata hivyo, ni sharti tujue ya kwamba tuko katika njia panda hapa. Kwa upande mmoja,
zamani ilichukuliwa kwamba watoto na hata wanawake watu wazima hawana akili. Kwa
ajili hiyo, iwapo mwanaume mtu mzima ana jambo la kuwaeleza, njia pekee ya
kuliingiza katika “ akili” yao “ hafifu” ni kuwatwanga ili kulikongomeza jambo hili.
Ukweli ni kwamba akili ya mtoto si hafifu hata. Unaweza kusema ni kama mmea, ambao
usiporutubishwa kimakusudi, ukapaliliwa vyema na kustawishwa stahiki yake, basi
hudhoofu” na mwishowe kufifia.
Kwa upande mwingine, mtazamo wa kisasa ni tofauti kabisa, imethibitishwa ya kwamba
wanawake ni sawa kabisa katika maumbile yao wakilinganishwa na wanaume. Kwa jinsi
hiyo, kweli wapo wanawake amabo hawana mwelekeo timamu kuhusu maisha. Lakini ni
kweli pia kuwa wapo wanaume watu wazima mamilioni ambao hawana akili.
Kadhalika, si kweli kuwa watoto wote, kwa sababu ya umri wao tu, basi hawana akili.
Ama kwa kusema kweli binadamu yeyote kuwaliwa na akili zake timamu isipokuwa wale
ambao kwa bahati mbaya maumbile yamewapa akili pungufu. Hili litokeapo basi
tunalikubali tu. Hatuwezi kumlaumu mtu kama huyo au muumba wake. Kwa hakika huu
ndio msingi wa methali. “Akili ni nywele, kila mtu ana zake.” Vinginevyo, mtazamo wa
kizamani ni taasubi kogwe tu za kiume zilizopitwa na wakati.
Aidha, kwa sababu watu wote huzaliwa na akili timamu, tena hawawi watu wazimu
kabla ya kuwa watoto kwanza, mtu mzima yeyote ana hali gani ya kuwadhulumu
watoto na kujipambaniza na lawama za uongo dhidi ya vijana hao kwa madai kuwa
hawana akili? Na je, ikiwa hawana akili, basi ndipo waonewe? Wanyanyaswe? Hili si
jambo la busara. Kurudi mtoto kwa visa vya maonevu ni kumrudisha nyuma kiumbe huyo.
Kurudi kufaako ni kwa kupeleka mbele, sio kwa kurudisha nyuma. Kurudi kuelekezako
mbele ni kwa uongozi mwafaka, uongozi ambao lengo lake ni kummulikia mtoto kurunzi
ilimradi kumwongoza mtoto.
Mtoto ana haki ya kuhudumiwa kwa njia yoyote ifaayo ili akue na akili yake ikomae
kikamilifu. Inafaa asomeshwe, apewe malezi bora ili naye aje alee wengine kistahiki.
(a) “Mapenzi yasiyo kipimo yanaweza kuwa hatari kwa mtoto.” Eleza kikamilifu
huku ukirejelea habari uliyosoma
(b) Fafanua njia panda inayorejelewa na mtunzi
(c) Mtoto analinganishwa na mmea katika taarifa hi, kwamba “usiporutubishwa
kimakusudi, ukapaliliwa vyema na kustawishwa stahiki yake basi hudhofu.”
Tahtmini kulinganishwa huku, huku ukirejelea taarifa
(d) “Akili ni nywele, kila mtu ana zake.” Eleza maana ya ndani ya methali hii
kulingana na taarifa
(e) Onyesha kwamba unaelewa maana ya:
“Kurudi mtoto kwa visa vya maonevu ni kumrudisha nyuma kiumbe huyo”
(f) Eleza maana ya:
(i) Kulikongomeza
(ii) Kujipambaniza
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Andika methali moja inayotokana na maelezo yafuatayo:
Asiye na uwezo ataendelea kuwa bila uwezo hata akifanya bidii namna
gani.(Solved)
Andika methali moja inayotokana na maelezo yafuatayo:
Asiye na uwezo ataendelea kuwa bila uwezo hata akifanya bidii namna
gani.
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Mdudu mwenye mkia uliopinda nchani ambao una sumu ni?(Solved)
Mdudu mwenye mkia uliopinda nchani ambao una sumu ni?
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Mdudu anayetengeneza utandu huitwa?(Solved)
Mdudu anayetengeneza utandu huitwa?
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Tumia tanakali za sauti zifaazo kukamilisha sentensi hizi;
i) Sauti ya waimbaji haikusikika tena, ilikuwa imedidima…wageni
walipofika katika jukwaa.
ii) Simba ni mnyama hodari sana, akimkamata swara humrarua(Solved)
Tumia tanakali za sauti zifaazo kukamilisha sentensi hizi;
i) Sauti ya waimbaji haikusikika tena, ilikuwa imedidima…wageni
walipofika katika jukwaa.
ii) Simba ni mnyama hodari sana, akimkamata swara humrarua
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Kamilisha tashbihi zifuatazo
i) Baidika kama
ii) Mzima kama(Solved)
Kamilisha tashbihi zifuatazo
i) Baidika kama
ii) Mzima kama
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Eleza tofauti baina ya sentensi hizi;
i) Ningekuwa na pesa ningenunua shamba.
ii) Ningelikuwa na pesa ningalinunua shamba(Solved)
Eleza tofauti baina ya sentensi hizi;
i) Ningekuwa na pesa ningenunua shamba.
ii) Ningelikuwa na pesa ningalinunua shamba
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Eleza maana nne-tofauti za sentensi hii;
Alinunuliwa samaki na mtoto wake(Solved)
Eleza maana nne-tofauti za sentensi hii;
Alinunuliwa samaki na mtoto wake
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)
- Andika kinyume;
Mjomba alichomeka upanga kwenye ala(Solved)
Andika kinyume;
Mjomba alichomeka upanga kwenye ala
Date posted: June 27, 2019. Answers (1)