Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Nairobi , mji mkuu wa Kenya, ni jiji la maajabu na mastaajabu chungu nzima. Nadhari ya mtu anayewahi kuingia jiji hili...

      

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Nairobi , mji mkuu wa Kenya, ni jiji la maajabu na mastaajabu chungu nzima. Nadhari
ya mtu anayewahi kuingia jiji hili kwa mara ya kwanza huvutiwa na huo msheheneko wa
majumba ya fahari, marefu ajabu, kiasi cha minazi mitano- sita iliyounganishwa
kuelekea juu mbinguni.

Jumba linalowavutia watu wengi ni lile la makongamano ya kimataifa liitwalo kwa
kiingereza Kenyatta International Conference Centre. Jumba hili, hadi miaka michache
ilipopita, ndilo lililokuwa refu zaidi mjini. Jumba lenyewe lina ghorofa ishirini na tisa
hivi, Usipohesabu hilo pambo kama kofia kileleni mwake, linalojulikana kama
mwavuli. Hata hivyo, miaka michache iliyopita jingo hili lilipitwa kwa urefu na mnara
wa Nyakati ( Times Tower) Mnara huo hasa ni jumba linaloafiki lakabu yake ya
kikwaruza mawingu. Jumba hili lina ghorofa zisizopungua thelathini na mbili.

Mbali na majumba haya mawili, kuna majumba mengine zaidi ya ishirini katikati ya jiji
ambayo, japo mengine ni mafupi kiasi, maumbo ya kustaajabisha kweli kweli. Hebu
zingatia mwenyewe jumba liitwalo “mdomo wa kengele” au bell - bottom” ambalo ni
vioo vitupu, toka chini hadi juu. Fauka ya haya, umbo lake ni la kipekee ulimwenguni
kote. Jumba hili lina kama miguu, kisha kiuno mithili ya kinu hivi japo si mviringo.
Linapaa juu, mbali sana, likichukua umbo pana kuliko lilivyo chini. Umbo la fua pana
kama kengele.

Halafu rudia barabara. Hizi hazina hesabu katikati ya jiji ni pona, tena safi sana. Magari
yanayotumia barabara hizi ni kochokocho, ya kila aina na yanashindania nafasi.

Ajabu kubwa ya Nairobi hata hivyo ni idadi ya watu. Hakuna hasa anayejua idadi kamili
ya watu wa Nairobi, lakini sio kupiga chuku ninaposema kwamba, hasa nyakati za
kuelekea kazini asubuhi, kwenda kula chakula cha mchana, kuelekea nyumbani baada
ya kazi na kuvuka barabara wakati wa msongamano, watu hukanyagana. Mtu anayesema
kwamba watu wa Nairobi ni wengi kama chungu, au kama mchanga wa ufuo wa bahari,
hatii chumvi

Watu wa Nairobi, kwa tabia na mavazi, si kama watu wa kwingineko nchini Kenya.
Watu hawa kuvalia nadhifu sana. Wanawake ni warembo ajabu na hutengeneza nywele
zao mithili ya hurulaini peponi. Wengi huvaa suruali ndefu! Kucha zao na midomo yao
hupata rangi maridadi sana. Huzungumza Kiswahili na kiingereza takriban wakati wote.
Wanawake wengi ajabu huendesha magari yao wenyewe, jambo ambalo litakushangaza
mara tu uingiapo jijini, hasa kama ulilelewa ukidhani maskani mwafaka ya wanawake ni
jikoni peke yake, yaani kuzingatia ile falsafa kuwa “ kuoa ni kupata jiko”. Wanaume
nao huvaa suti safi, maridadi na shingoni wamefunga tai stahiki yao. Wanaume hao huendesha magari ya kuyaegesha karibu na afisi zao. Huingia afisini mwao kwa maringo
na madaha, huku funguo za magari yao zikining’inia vidoleni. Hawa nao husema
Kiswahili na kiingereza kupitia puani, utadhani ni waingereza hasa.

Kwa upande mwingine, watoto ni nadhifu kweli hasa watoto wa shule. Hawa huvalia sare
zilizofuliwa na kunyoshwa vizuri kwa pasi. Wake kwa waume, shingoni huvalia tai.
Watoto wa shule Nairobi huongea Kiswahili, kiingereza na Sheng, ambayo ni “lahja” yao
waliyoibuni.
“Lugha” hii ni mchanganyiko wa Kiswahili. Kiingereza na msamiati mchache wa lugha
nyingine za wakenya zisemwazo jijini Nairobi na vitongoji vyake.

Kwa jumla, watu wote wa Nairobi hutembea kasi sana. Hawana hata wakati wa kutembea
pole pole na kuangazaanga huku na huko. Iwapo wewe ni mgeni jijini, ukizubaa
utapigwa kumbo na waendelee na hamsini zao kama vile hapakutokea jambo. Hili
linapojiri, usidhani limefanywa maksudi. La, hasha ni vile tu kwamba Wanairobi hawana
muda wa kupoteza.

(a) Kwa nini majumba ya jiji la Nairobi yana majina au lakabu za kiingereza?
(b) (i) Baadhi ya maajabu ya Nairobi ni barabara safi, msongamano wa magari
na majumba marefu. Ongezea maajabu mengine manne
(ii) Watu wa Nairobi wanajipenda kweli kweli. Fafanua
(c) (i) Je, unadhani watu wa Nairobi kweli hukanyagana? Eleza ni kwa nini
msimulizi ametoa maelezo hayo
(ii) Unafikiri ni kwa nini hasa wanawake wa Nairobi wanaonekana nadhifu?
(d) Kwa nini neno “lahja” limewekwa alama za mtajo?
(e) Eleza maana ya maneno na tamathali za usemi zifuatazo:
(i) Nadhari
(ii) Linaloafiki
(iii) Kikwaruza mawingu
(iv) Waendelee na hamsini zao

  

Answers


Kavungya
a) - Kiingereza ni lugha ya kimataif
- Kiingereza ni lugha rasmi nchini
- Kiingereza ni mojawapo ya lugha zitumiwazo Nairobi
- Ni athari ya waingereza walioitawala nchi hii

b) i) - Idadi ya watu ni kubwa/watu ni wengi
- Watu huvalia nadhifu/wanawake ni warembo/wanawake
huvaa suraali ndefu /wanawake hutengeza nywele
zao/wanawake hupaka rangi kucha zao na midomo yao
Watu huzungumza Kiswahili na Kiingereza karibu kila
wakati. Wanawake wengi hendesha magari yao wenyewe
- Majumba mengine yana maumbo ya kipekee
- Barabara ni nyingi na pana
- Kuna magari mengi ya kila aina
- Wanaume husema Kiswahili na Kiingereza kupitia puani
- Wanaume hutembea kwa maringo wakining’iniza funguo
za magari mikononi
- Watoto wa shule husema Kiswahili, Kiingereza na sheng’
- Watu wa Nairobi hutembea Kwa kasi sana bila simile
ii) - Watu huvalia nadhaifu
- Huzungumza Kiswahili na Kiingereza karibu kila wakati
- Wanawake wengi huendesha magari yao
- Wanaume husema Kiswahili na Kiingerexa kupitia puani
- Watu hutembea kwa kasi sana bila simile
- Watoto huzungumza Kiswahili, Kiingereza na sheng’

c) i) - Ndio kwa sababu watu wa Nairobi ni wengi sana
- La. Anapiga chukukuonyesha wingi wa watu wa Nairobi
ii) Ili wapendeze
- Kazi wafanyazo haziwachafui
- Wanajiweza kifedha
- Ili waafiki heshima zao.

d) - Limetumika nje ya muktadha/sheng si lahaja

e) i) Fikira/fikra/mawazo/mtazamo
ii) Linalofaa/linalolingana na/linalopatana
na/linaloakisi/linalostahiki/linlosadifu
iii) Jumba refu
iv) Waendelee na shughuli/kazi/plikapilka/harakati zao
Kavungya answered the question on June 28, 2019 at 05:34


Next: Unda vitenzi kutokana na majina haya: (i) Mtukufu (ii) Mchumba
Previous: UFUPISHO Ujambazi wa kimataifa ni tatizo lilolowasumbua walimwengu kwa muda mrefu sana. Serikali nyingi zimetumia mapesi mengi kwa miaka mingi sana zikijitahidi kupambana na janga hii. Hata hivyo,...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions


  • Unda vitenzi kutokana na majina haya: (i) Mtukufu (ii) Mchumba(Solved)

    Unda vitenzi kutokana na majina haya:
    (i) Mtukufu
    (ii) Mchumba

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi mbili tofauti ukitumia vitenzi hivi vya silabi moja (i) Pa (ii) La(Solved)

    Tunga sentensi mbili tofauti ukitumia vitenzi hivi vya silabi moja
    (i) Pa
    (ii) La

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi zifuatazo upya kwa kufuata maagizo (i) Alicheza kwa bidii akawafurahisha wengi waliohudhuria tamasha hizo Anza kwa: Kucheza (ii) Karamu hiyo ilifanya sana, kila mtu alikula chakula...(Solved)

    Andika sentensi zifuatazo upya kwa kufuata maagizo
    (i) Alicheza kwa bidii akawafurahisha wengi waliohudhuria tamasha hizo
    Anza kwa: Kucheza
    (ii) Karamu hiyo ilifanya sana, kila mtu alikula chakula akatosheka
    Anza kwa: chakula

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • (i) Taja vihusishi vitatu vinavyorejelea mahali, wakati na kiwango (ii) Tunga sentensi kuonyesha matumizi ya kila kihusishi(Solved)

    (i) Taja vihusishi vitatu vinavyorejelea mahali, wakati na kiwango
    (ii) Tunga sentensi kuonyesha matumizi ya kila kihusishi

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika kifungu hiki kutoka usemi wa taarifa hadi usemi halisi Watoto waliambiwa na mama yao watakaporudi nyumbani waoge. Wale, halafu waanse kusoma moja kwa moja badala ya...(Solved)

    Andika kifungu hiki kutoka usemi wa taarifa hadi usemi halisi
    Watoto waliambiwa na mama yao watakaporudi nyumbani waoge. Wale,
    halafu waanse kusoma moja kwa moja badala ya kuharibu wakati wao
    kwa kutazama vipindi vya runinga. Aliwakumbusha kuwa wanaofanya
    maonyesho kwenye runinga tayari wamefuzu shuleni na wameajiriwa kazi

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tambulisha kielezi, kivumishi na mnyambuliko wa kitenzi katika sentensi ifuatayo: Msichana mrembo alikuja upesi akimkimbilia dadake(Solved)

    Tambulisha kielezi, kivumishi na mnyambuliko wa kitenzi katika sentensi
    ifuatayo:
    Msichana mrembo alikuja upesi akimkimbilia dadake

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi kuonyesha matumizi sahihi ya viunganishi hivi (i) Ingawaje (ii) Ilhali(Solved)

    Tunga sentensi kuonyesha matumizi sahihi ya viunganishi hivi
    (i) Ingawaje
    (ii) Ilhali

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi mbilimbili kuonyesha matumizi mawili tofauti ya I. Ka II. Ndivyo(Solved)

    Tunga sentensi mbilimbili kuonyesha matumizi mawili tofauti ya
    I. Ka
    II. Ndivyo

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo (i) Kazi yote ni muhimu (ii) Kazi yoyote ni muhimu(Solved)

    Tofautisha maana ya sentensi zifuatazo
    (i) Kazi yote ni muhimu
    (ii) Kazi yoyote ni muhimu

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza namna mbili za matumizi ya alama ifuatayo ya uakifishi (;) (Solved)

    Eleza namna mbili za matumizi ya alama ifuatayo ya uakifishi (;)

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika udogo na ukubwa wa jina ngoma.(Solved)

    Andika udogo na ukubwa wa jina ngoma.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • MUHTASARI Maendeleo ya taifa hutegemea jinsi wananchi wanavyolitolea katika kulibingirisha gurudumu la uchumi wao. Kila mwanajamii anahitajika kujibidisha katika kazi au taaluma yake. Mzalendo yeyote yule hupata motisha...(Solved)

    MUHTASARI
    Maendeleo ya taifa hutegemea jinsi wananchi wanavyolitolea katika kulibingirisha
    gurudumu la uchumi wao. Kila mwanajamii anahitajika kujibidisha katika kazi au
    taaluma yake. Mzalendo yeyote yule hupata motisha ya kufanya kazi iwapo anaweza
    kupata ile kazi aliyokuwa akitamani.

    Kumakinika katika taaluma Fulani si jambo jepesi na huchukua muda kutengeneza. Kwa
    mfano, ili mhazili apate staha ya uhazili sharti apitie ngazi mbali mbali. Mwanzo kabisa
    lazima kumpa fursa ya kujiunga na vyuo mbali mbali vya uhazili. Anapojiunga na vyuo
    hivyo ndipo safari inapoandaliwa. Kukamilisha safari hii inahitaji muda wa miaka minemitano.
    Anapohitimu kuwa tayari ameimudu shughuli hiyo. Hata hivyo, anatakiwa
    afanye mazoezi kila mara ili asisahau yanayohitajika katika taaluma hiyo. Wengi
    waliokwishapata ujuzi huo wa wale wenzao ambao katika masomo wana utaakamu kama
    wao. Ijapokuwa wote ni wahazili, viwango vyao ni tofauti na mishahara pia hutofautiana.
    Tofauti hapa ni daraja zao za vyeo. Baada ya kuhitimu na kupata vyeti vya uhazili ni
    rahisi kupata au kutopata kazi zenye ujira wa kuvutia. Anayefanikiwa ana sayari ya
    kujikakamua hasa kwa upande wa uzingatifu wa kazi kikamilifu na kutunza hadhi ya
    ofisi yake.

    Kuna mashirika makubwa yanayojiweza kiuchumi, ambayo rasimali yake ni imara.
    Mashirika madogo huwa yana rasilmali yenye kuyumbayumba. Mashirika haya yana
    wahazili na wanafunzi ambao hupata mishahara duni. Wanafunzi wote hao hufanya kazi
    kwa kutokuwa na uhakika wa kulipwa mwisho wa mwezi. Watu kama hao hawawezi
    kutilia maanani kazi zao. Mashirika mengine hayana utaratibu maalum, wa kulipa
    mishahara kwa vile hutegemea utu wa mkurugenzi. Badhi ya wakuu hao huwa wabanizi
    na huwapunja wafanyi kazi wao. Hili ni swala nyeti ambalo linahitaji litatuliwe kwa kuwa na chama cha kupigania haki za wafanyikazi. Wakati wanapotafuta kazi, Wahazili
    wengi huwa ni wahitaji na hukubali chochote wanachopewa.

    Wale waliobahatika kupata nafasi ya ajira katika kampuni kubwa za kimaataifa,
    mishahara huwa ni ya kutia moyo. Katika dunia hii wahazili wana vibarua vigumu, kwa
    sababu lazima wapate tajriba na uzoefu wa taaluma inayoendelea na shirika Fulani.
    Mhazili anapotumia msamiati usionda sambamba na shughuli za kiofisi hawasiti kufoka.
    Wavumilivu miongoni mwao hula mbivu. Hawa hawafi moyo bali hujitahidi zaidi ili
    wasikumbwe na kimbunga cha kufokewa. Kuna wengine ambao humwaga unga.

    (a) Bila kupoteza iliyokusudiwa na mwandishi wa taarifa, fupisha aya ya kwanza
    na ya pili ( maneno 60 – 70) Alama 2 kwa mtiririko)
    (b) Kwa kuzingatia aya mbili za mwisho, eleza mambo muhimu yanayoshughulika na
    mwandishi ( maneno 60 – 70) alama 2 kwa mtiririko)

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Wahenga walisema “mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.” Hii ina maana ya kuwa ukiogopa kutumia ufito kumchapa mtoto wako, ukamdekeza atadeka na hatimaye...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
    Wahenga walisema “mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.” Hii ina maana ya kuwa ukiogopa
    kutumia ufito kumchapa mtoto wako, ukamdekeza atadeka na hatimaye ataharibika.
    Methali hii ina picha yake ambyo ni, “Ukicha mwana kulia, utalia wewe.”

    Hizi ni methali zilizojaa busara kubwa. Mathalini wewe ni mzazi au mtu yeyote mzima
    aliyetunikiwa madaraka juu ya watoto. Lakini kila wanapokiuka uadilifu au mmoja wao
    anapokosea wewe unambembeleza tu, basi huwa unaizorotesha tabia yake. Mwisho,
    mtoto huyo anaweza kuishia kuwa mtundu.

    Hata hivyo, ni sharti tujue ya kwamba tuko katika njia panda hapa. Kwa upande mmoja,
    zamani ilichukuliwa kwamba watoto na hata wanawake watu wazima hawana akili. Kwa
    ajili hiyo, iwapo mwanaume mtu mzima ana jambo la kuwaeleza, njia pekee ya
    kuliingiza katika “ akili” yao “ hafifu” ni kuwatwanga ili kulikongomeza jambo hili.
    Ukweli ni kwamba akili ya mtoto si hafifu hata. Unaweza kusema ni kama mmea, ambao
    usiporutubishwa kimakusudi, ukapaliliwa vyema na kustawishwa stahiki yake, basi
    hudhoofu” na mwishowe kufifia.

    Kwa upande mwingine, mtazamo wa kisasa ni tofauti kabisa, imethibitishwa ya kwamba
    wanawake ni sawa kabisa katika maumbile yao wakilinganishwa na wanaume. Kwa jinsi
    hiyo, kweli wapo wanawake amabo hawana mwelekeo timamu kuhusu maisha. Lakini ni
    kweli pia kuwa wapo wanaume watu wazima mamilioni ambao hawana akili.
    Kadhalika, si kweli kuwa watoto wote, kwa sababu ya umri wao tu, basi hawana akili.
    Ama kwa kusema kweli binadamu yeyote kuwaliwa na akili zake timamu isipokuwa wale
    ambao kwa bahati mbaya maumbile yamewapa akili pungufu. Hili litokeapo basi
    tunalikubali tu. Hatuwezi kumlaumu mtu kama huyo au muumba wake. Kwa hakika huu
    ndio msingi wa methali. “Akili ni nywele, kila mtu ana zake.” Vinginevyo, mtazamo wa
    kizamani ni taasubi kogwe tu za kiume zilizopitwa na wakati.

    Aidha, kwa sababu watu wote huzaliwa na akili timamu, tena hawawi watu wazimu
    kabla ya kuwa watoto kwanza, mtu mzima yeyote ana hali gani ya kuwadhulumu
    watoto na kujipambaniza na lawama za uongo dhidi ya vijana hao kwa madai kuwa
    hawana akili? Na je, ikiwa hawana akili, basi ndipo waonewe? Wanyanyaswe? Hili si
    jambo la busara. Kurudi mtoto kwa visa vya maonevu ni kumrudisha nyuma kiumbe huyo.
    Kurudi kufaako ni kwa kupeleka mbele, sio kwa kurudisha nyuma. Kurudi kuelekezako
    mbele ni kwa uongozi mwafaka, uongozi ambao lengo lake ni kummulikia mtoto kurunzi
    ilimradi kumwongoza mtoto.

    Mtoto ana haki ya kuhudumiwa kwa njia yoyote ifaayo ili akue na akili yake ikomae
    kikamilifu. Inafaa asomeshwe, apewe malezi bora ili naye aje alee wengine kistahiki.

    (a) “Mapenzi yasiyo kipimo yanaweza kuwa hatari kwa mtoto.” Eleza kikamilifu
    huku ukirejelea habari uliyosoma
    (b) Fafanua njia panda inayorejelewa na mtunzi
    (c) Mtoto analinganishwa na mmea katika taarifa hi, kwamba “usiporutubishwa
    kimakusudi, ukapaliliwa vyema na kustawishwa stahiki yake basi hudhofu.”
    Tahtmini kulinganishwa huku, huku ukirejelea taarifa
    (d) “Akili ni nywele, kila mtu ana zake.” Eleza maana ya ndani ya methali hii
    kulingana na taarifa
    (e) Onyesha kwamba unaelewa maana ya:
    “Kurudi mtoto kwa visa vya maonevu ni kumrudisha nyuma kiumbe huyo”
    (f) Eleza maana ya:
    (i) Kulikongomeza
    (ii) Kujipambaniza

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Andika methali moja inayotokana na maelezo yafuatayo: Asiye na uwezo ataendelea kuwa bila uwezo hata akifanya bidii namna gani.(Solved)

    Andika methali moja inayotokana na maelezo yafuatayo:
    Asiye na uwezo ataendelea kuwa bila uwezo hata akifanya bidii namna
    gani.

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Mdudu mwenye mkia uliopinda nchani ambao una sumu ni?(Solved)

    Mdudu mwenye mkia uliopinda nchani ambao una sumu ni?

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Mdudu anayetengeneza utandu huitwa?(Solved)

    Mdudu anayetengeneza utandu huitwa?

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tumia tanakali za sauti zifaazo kukamilisha sentensi hizi; i) Sauti ya waimbaji haikusikika tena, ilikuwa imedidima…wageni walipofika katika jukwaa. ii) Simba ni mnyama hodari sana, akimkamata swara humrarua(Solved)

    Tumia tanakali za sauti zifaazo kukamilisha sentensi hizi;
    i) Sauti ya waimbaji haikusikika tena, ilikuwa imedidima…wageni
    walipofika katika jukwaa.
    ii) Simba ni mnyama hodari sana, akimkamata swara humrarua

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Kamilisha tashbihi zifuatazo i) Baidika kama ii) Mzima kama(Solved)

    Kamilisha tashbihi zifuatazo
    i) Baidika kama
    ii) Mzima kama

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza tofauti baina ya sentensi hizi; i) Ningekuwa na pesa ningenunua shamba. ii) Ningelikuwa na pesa ningalinunua shamba(Solved)

    Eleza tofauti baina ya sentensi hizi;
    i) Ningekuwa na pesa ningenunua shamba.
    ii) Ningelikuwa na pesa ningalinunua shamba

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana nne-tofauti za sentensi hii; Alinunuliwa samaki na mtoto wake(Solved)

    Eleza maana nne-tofauti za sentensi hii;
    Alinunuliwa samaki na mtoto wake

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)