Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Ulimwengu unapaswa kuzuka na mbinu za Kulitadarukia tatizo la umaskini ambao unakwamiza juhudi za maendeleo. Umaskini unaoyakabili mataifa yanayoendelea. Unayatosa kwenye dhiki...

      

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Ulimwengu unapaswa kuzuka na mbinu za Kulitadarukia tatizo la umaskini ambao
unakwamiza juhudi za maendeleo. Umaskini unaoyakabili mataifa yanayoendelea.
Unayatosa kwenye dhiki kubwa huku mataifa ya kimagharibi yakitpiga hatua kubwa
kimaendeleo. Ufa uliopo baina ya mataifa yanayoendelea na yalo yaliyoendelea kama
vile Marekani, nchi za Ulaya na Ujapani unapanuka kila uchao.

Vyanzo vya umaskinin huu ni anuwai mathalan, ufusadi, uongozi mbaya, turathi za
kikoloni, uchumi kuegemea mvua isiyotabarika, idadi ya watu inayoupik uwezo wa
uchumi wa taifa linalohusika na ukosefu wa nyenzo na amali za kuwakwamua raia
kutoka lindi la umaskini. Ukosefu adimu za ajira huchangia pia katika tatizo hili.

Jamii ya ulimwengu inapaswa kuelewa kuwa umaskini unaoathiri nchi Fulani una athari
pan asana. Uvunigu unaotokana na umaskini unaweza kuweza kuwa mboji ambako
matendo ya kihalifu ili kujinasua kutoka dhiki ile. Hii inaweza kuwa mbegu ya kuatika
maovu kama ugaidi na uhalifu wa kila aina.

Mataifa ya magharibi yanapaswa kuyaburai madeni mataifa yanayoendelea kama njia
mojawapo ya kupambana na umaskini. Asilimia kubwa ya pato la kitaifa katika mataifa
mengi hutumika kuyalipa madeni hayo. Katika hali hii inakuwa muhali kwa mataifa hayo
kujikwamua kutokana na pingu za umaskini. Njia nyingine ni kustahabu kutoa ruzuku za
kimaendeleo badala ya mikopo kwa nchi zinazoendelea.

Kwa upande wake, mataifa yanayoendelea yanapaswa kuibuka na mikakati bora ya
kupambana na umaskini. Ni muhimu pawepo na sera zinazotambua ukweli kuwa
asilimia kubwa ya raia wa mataifa hayo ni maskini. Pana dharural ya kuzalisha nafasi za
ajira, kupanua viwanda hususan vinavyohusiana na zaraa ambayo ni tegemeo kuu la
mataifa mengi, kuendeleza elimu na kuimarisha miundo msingi. Ipo haja pia ya mataifa
haya kuhakikisha kuwa mfumo wa soko huru unaotawala ulimwengu sasa huishii kuwa
chanzo cha kufa kwa viwanda asilia na kuendeleza masikini zaidi. Kwa ufupi, maamuzi
yote ya sera za kiuchumi lazima yazingatie uhalishi wa maisha ya raia wa mataifa hayo.

a) Kwa nini umaskini umetamalaki katika mataifa yanayoendelea?
b) Madeni yana athari gani kwa mataifa yanayoendelea?
c) Ni mapendekezo yapi ambayo mwandishi anatoa kwa mataifa machanga kuhusu
utatuzi wa tatizo la umaskini?
d) Mfumo wa soko huru una mathara gani kwa mataifa machanga?
e) Ukirejea kifungu, eleza maana ya:
i) Kulitadarukia
ii) Kuatika
iii) Kuyaburai madeni

  

Answers


Kavungya

(a) 1. Ufisadi
2. Uongozi mbaya
3. Turathi za kikoloni
4. Uchumi unauegamizwa kwenye kilimo
5. Idadi ya watu inayopiku uwezo wa uchumi
6. Okosefu wa amani kukwamua raia kuto lindi la umaskini
7. Ukosefu wa elimu na nafasi za ajira
8. Madeni za kigeni

(b) Kudidimiza maendeleo
Umaskini – kuzidisha
Husababisha uhalifu

(c) 1. Kuwa na sera bora zinazotambua raia wengi wa mataifa hayo ni
Maskini
2. Kizalilisha nafasi za ajira (kazi)
3. Kupanua viwaada hasa vinavyohisiana na kilimo
4. Kuendeleza elimu
5. Kuimarisha miuondo msingi
6. Kuchunga mfumo wa soko huru kuwa viwanda asiliha kuzidisha
Umaskini

(d) Kuua viwanda asilia
Kuendeleza umaskini

(e) (i) Kulikabili nalo, kulitatua, kulishughulikia, kulitanzua kupambana
Nalo, kulingazia, komesha
(ii) Kuzua, kupanda, kukuza, kuanzisha, kuotesha
(iii) Kuondolea, kusaheha, kuyafeleli
Kavungya answered the question on June 28, 2019 at 06:26


Next: Mbuni huzaa matunda gani?
Previous: MUHTASARI Ajira ya watoto ni tatizo sugu linalokumba ulimwengu wa sasa , hasa katika nchi zinazozoendelea. Jambo la kusikitisha ni kwamba hivi ndivyo ilivyo katika nchi nyingi za...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Mbuni huzaa matunda gani?(Solved)

    Mbuni huzaa matunda gani?

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • Haya ni magonjwa gani? I Matubwitubwi II Tetewanga(Solved)

    Haya ni magonjwa gani?
    I Matubwitubwi
    II Tetewanga

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • Kati ya madini haya taja yale yanayopatikana baharini Zinduna Zebaki Lulu Ambari Yakuti Marumaru(Solved)

    Kati ya madini haya taja yale yanayopatikana baharini
    Zinduna Zebaki
    Lulu Ambari
    Yakuti Marumaru

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • Jaza jedwali Kiume Kike Mjakazi Jogoo Fahali(Solved)

    Jaza jedwali
    Kiume Kike
    Mjakazi
    Jogoo
    Fahali

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya: (i) Sina pa kuuweka uso wangu (ii) Ana mkono wa buli(Solved)

    Eleza maana ya:
    (i) Sina pa kuuweka uso wangu
    (ii) Ana mkono wa buli

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana mbili tofauti za sentensi hii Mamake Juma na Mariamu walitutembelea(Solved)

    Eleza maana mbili tofauti za sentensi hii
    Mamake Juma na Mariamu walitutembelea

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • Geuza vitenzi hivi viwe majina (i) Shukuru (ii) Enda(Solved)

    Geuza vitenzi hivi viwe majina
    (i) Shukuru
    (ii) Enda

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi hii upya kwa kufuata maagizo Nilikuwa nimejitayarisha vizuri kwa hivyo sikuona ugumu wo wote katika safari yangu. Anza: safari(Solved)

    Andika sentensi hii upya kwa kufuata maagizo
    Nilikuwa nimejitayarisha vizuri kwa hivyo sikuona ugumu wo wote
    katika safari yangu.
    Anza: safari

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • Tumia – ndi pamoja na viashiria vya ngeli kujaza mapengo (i) Wewe ___________ ninayekutafuta (ii) Nyinyi ___________ mnaoongoza(Solved)

    Tumia – ndi pamoja na viashiria vya ngeli kujaza mapengo
    (i) Wewe ___________ ninayekutafuta
    (ii) Nyinyi ___________ mnaoongoza

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • Kanusha sentensi hii: Tumechukua nguo chache kuuza(Solved)

    Kanusha sentensi hii:
    Tumechukua nguo chache kuuza

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • Huku ukitoa mifano, fafanua miundo mitatu ya majina katika ngeli ya JI-MA(Solved)

    Huku ukitoa mifano, fafanua miundo mitatu ya majina katika ngeli ya
    JI-MA

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • Eleza matumizi ya na katika sentensi: Halima na Asha wanasaidiana(Solved)

    Eleza matumizi ya na katika sentensi:
    Halima na Asha wanasaidiana

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • Andika kwa wingi Pahala hapa ni pake(Solved)

    Andika kwa wingi
    Pahala hapa ni pake

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • Eleza matumizi ya kwa katika sentensi hii Aliimba kwa sauti tamu(Solved)

    Eleza matumizi ya kwa katika sentensi hii
    Aliimba kwa sauti tamu

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • Kamilisha jedwali Kufanya Kufanyia Kufanywa Kula Kuunga(Solved)

    Kamilisha jedwali
    Kufanya Kufanyia Kufanywa
    Kula
    Kuunga

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha aina ya vivumishi katika sentensi hii Nyumba yangu ni maridadi(Solved)

    Bainisha aina ya vivumishi katika sentensi hii
    Nyumba yangu ni maridadi

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • UFUPISHO Ujambazi wa kimataifa ni tatizo lilolowasumbua walimwengu kwa muda mrefu sana. Serikali nyingi zimetumia mapesi mengi kwa miaka mingi sana zikijitahidi kupambana na janga hii. Hata hivyo,...(Solved)

    UFUPISHO
    Ujambazi wa kimataifa ni tatizo lilolowasumbua walimwengu kwa muda mrefu sana.
    Serikali nyingi zimetumia mapesi mengi kwa miaka mingi sana zikijitahidi kupambana
    na janga hii. Hata hivyo, fanaka haijapatikana wala haielekei kamwe kuwa itapatikana leo
    au karne nyingi baadaye.

    Yumkini tatizo kubwa lililopo ni kuhusu jelezi la dhana ya “ujambazi” tena “wa
    kimataifa”. Hili ni tatizo mojawapo na yapo mengi sana. Tatizo la pili ni kiburi. Kuna
    wale watu binafsi na hasa viongozi wan chi kubwakubwa na serikali zao zilizojiaminisha
    kuwa ujambazi ni balaa kweli, tena belua, lakini huo ni wa huko, wala hauwezi kuwagusa
    licha ya kuwashtua wao.

    Kulingana na maoni watakaburi hao, ujambazi ni wa watu “washenzi” wasiostaarabika,
    wapatikanao katika nchi zisizoendelea bado. Ujambazi pekee wanaouona unafaa
    kukabiliwa ni dhidi ya mbubujiko wa madawa ya kulevya uliosababishwa na
    vinyangarika kutoka nchi hizo maaluni za “ ulimwengu wa tatu”. Kulingana na
    wastaarabu wan chi zilizoendelea, vinyangarika hivi ndivyo hasa adui mkubwa wa
    ustaarabu ulimwenguni na ni sharti vifagiliwe mbali bila huruma. Baada ya
    kusagwasagwa, ulimwengu mstaarabu utazidi kutononoka na ahadi ya mbingu hapa
    ardhini itakamilika.

    Imani ya watu ya kuwa ujambazi wa kimataifa. Hata iwapo upo, hauwezi kuwashtua
    wala kuwatingisha wao ilikuwa kamili na timamu. Ilikuwa kamili na timamu hadi
    hapo mwezi Septemba tarehe 11 mwaka wa 2001, ndege tatu za abiria zilipoelekezwa
    katika majumba mawili ya fahari, yenye urefu wa zaidi ya ghorofa mia moja na
    kuyatwangilia mbali. Mshtuko na kimako! Kimako kwa kuwa, kabla ya siku hiyo,
    wanarekani kudhai kwamba ingewezekana taifa lolote au mtu yeyote kuthubutu
    kuishambulia nchi yao, taifa wasifa lililojihami barabara dhidi ya aina yeyote ile ya
    uchokozi kutoka pembe lolote la dunia.

    Hakuna ulimwengu mzima, aliyeamini kuwa marekani ingeeza kushambuliwa. Kwa ajili
    hiyo, mshtuko uliitingisha ardhi yote na huzuni ilitanda kote, kama kwamba sayari nzima
    imeshambuliwa, wala sio marekani pekee.

    Mintarafu hiyo, marekani ilipolipiza kisasi kwa kuwaunguza waliokuwemo na
    wasiokuwemo kwa mabomu hatari huko Afghanistan, idadi kubwa ya watu duniani
    ilishangilia na kusherehekea. Kwa nahati mbaya, tafsiri ya shambulizi la minara- pacha
    ya Newyork na lile la Pentagon, uti wa uwezo wa kivita wa Marekani, ilizorota. Kuna
    wengi waliodhani huo ni mwanzo wa vita vya Waislamu dhidi ya Wakristo na kwa
    muda, Waislamu wote wakashukiwa kimakosa kuwa ni majambazi wa kimataifa.

    (a) Bila bubadilisha maana, fupisha aya tatu za kwanza ( maneno 65 – 75)
    Matayarisho
    Nakala safi (alama 10, 2 za utiririko)
    (b) Ukizingira aya, tatu za mwisho, fafanua fikira za watu wa mambo yote
    yaliyotokea
    Baada ya Septemba tarehe 11, 2001 (maneno 65 – 75) (alama 10, 2 za
    utiririko)
    Matayarisho
    Nakala safi

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Nairobi , mji mkuu wa Kenya, ni jiji la maajabu na mastaajabu chungu nzima. Nadhari ya mtu anayewahi kuingia jiji hili...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
    Nairobi , mji mkuu wa Kenya, ni jiji la maajabu na mastaajabu chungu nzima. Nadhari
    ya mtu anayewahi kuingia jiji hili kwa mara ya kwanza huvutiwa na huo msheheneko wa
    majumba ya fahari, marefu ajabu, kiasi cha minazi mitano- sita iliyounganishwa
    kuelekea juu mbinguni.

    Jumba linalowavutia watu wengi ni lile la makongamano ya kimataifa liitwalo kwa
    kiingereza Kenyatta International Conference Centre. Jumba hili, hadi miaka michache
    ilipopita, ndilo lililokuwa refu zaidi mjini. Jumba lenyewe lina ghorofa ishirini na tisa
    hivi, Usipohesabu hilo pambo kama kofia kileleni mwake, linalojulikana kama
    mwavuli. Hata hivyo, miaka michache iliyopita jingo hili lilipitwa kwa urefu na mnara
    wa Nyakati ( Times Tower) Mnara huo hasa ni jumba linaloafiki lakabu yake ya
    kikwaruza mawingu. Jumba hili lina ghorofa zisizopungua thelathini na mbili.

    Mbali na majumba haya mawili, kuna majumba mengine zaidi ya ishirini katikati ya jiji
    ambayo, japo mengine ni mafupi kiasi, maumbo ya kustaajabisha kweli kweli. Hebu
    zingatia mwenyewe jumba liitwalo “mdomo wa kengele” au bell - bottom” ambalo ni
    vioo vitupu, toka chini hadi juu. Fauka ya haya, umbo lake ni la kipekee ulimwenguni
    kote. Jumba hili lina kama miguu, kisha kiuno mithili ya kinu hivi japo si mviringo.
    Linapaa juu, mbali sana, likichukua umbo pana kuliko lilivyo chini. Umbo la fua pana
    kama kengele.

    Halafu rudia barabara. Hizi hazina hesabu katikati ya jiji ni pona, tena safi sana. Magari
    yanayotumia barabara hizi ni kochokocho, ya kila aina na yanashindania nafasi.

    Ajabu kubwa ya Nairobi hata hivyo ni idadi ya watu. Hakuna hasa anayejua idadi kamili
    ya watu wa Nairobi, lakini sio kupiga chuku ninaposema kwamba, hasa nyakati za
    kuelekea kazini asubuhi, kwenda kula chakula cha mchana, kuelekea nyumbani baada
    ya kazi na kuvuka barabara wakati wa msongamano, watu hukanyagana. Mtu anayesema
    kwamba watu wa Nairobi ni wengi kama chungu, au kama mchanga wa ufuo wa bahari,
    hatii chumvi

    Watu wa Nairobi, kwa tabia na mavazi, si kama watu wa kwingineko nchini Kenya.
    Watu hawa kuvalia nadhifu sana. Wanawake ni warembo ajabu na hutengeneza nywele
    zao mithili ya hurulaini peponi. Wengi huvaa suruali ndefu! Kucha zao na midomo yao
    hupata rangi maridadi sana. Huzungumza Kiswahili na kiingereza takriban wakati wote.
    Wanawake wengi ajabu huendesha magari yao wenyewe, jambo ambalo litakushangaza
    mara tu uingiapo jijini, hasa kama ulilelewa ukidhani maskani mwafaka ya wanawake ni
    jikoni peke yake, yaani kuzingatia ile falsafa kuwa “ kuoa ni kupata jiko”. Wanaume
    nao huvaa suti safi, maridadi na shingoni wamefunga tai stahiki yao. Wanaume hao huendesha magari ya kuyaegesha karibu na afisi zao. Huingia afisini mwao kwa maringo
    na madaha, huku funguo za magari yao zikining’inia vidoleni. Hawa nao husema
    Kiswahili na kiingereza kupitia puani, utadhani ni waingereza hasa.

    Kwa upande mwingine, watoto ni nadhifu kweli hasa watoto wa shule. Hawa huvalia sare
    zilizofuliwa na kunyoshwa vizuri kwa pasi. Wake kwa waume, shingoni huvalia tai.
    Watoto wa shule Nairobi huongea Kiswahili, kiingereza na Sheng, ambayo ni “lahja” yao
    waliyoibuni.
    “Lugha” hii ni mchanganyiko wa Kiswahili. Kiingereza na msamiati mchache wa lugha
    nyingine za wakenya zisemwazo jijini Nairobi na vitongoji vyake.

    Kwa jumla, watu wote wa Nairobi hutembea kasi sana. Hawana hata wakati wa kutembea
    pole pole na kuangazaanga huku na huko. Iwapo wewe ni mgeni jijini, ukizubaa
    utapigwa kumbo na waendelee na hamsini zao kama vile hapakutokea jambo. Hili
    linapojiri, usidhani limefanywa maksudi. La, hasha ni vile tu kwamba Wanairobi hawana
    muda wa kupoteza.

    (a) Kwa nini majumba ya jiji la Nairobi yana majina au lakabu za kiingereza?
    (b) (i) Baadhi ya maajabu ya Nairobi ni barabara safi, msongamano wa magari
    na majumba marefu. Ongezea maajabu mengine manne
    (ii) Watu wa Nairobi wanajipenda kweli kweli. Fafanua
    (c) (i) Je, unadhani watu wa Nairobi kweli hukanyagana? Eleza ni kwa nini
    msimulizi ametoa maelezo hayo
    (ii) Unafikiri ni kwa nini hasa wanawake wa Nairobi wanaonekana nadhifu?
    (d) Kwa nini neno “lahja” limewekwa alama za mtajo?
    (e) Eleza maana ya maneno na tamathali za usemi zifuatazo:
    (i) Nadhari
    (ii) Linaloafiki
    (iii) Kikwaruza mawingu
    (iv) Waendelee na hamsini zao

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • Unda vitenzi kutokana na majina haya: (i) Mtukufu (ii) Mchumba(Solved)

    Unda vitenzi kutokana na majina haya:
    (i) Mtukufu
    (ii) Mchumba

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi mbili tofauti ukitumia vitenzi hivi vya silabi moja (i) Pa (ii) La(Solved)

    Tunga sentensi mbili tofauti ukitumia vitenzi hivi vya silabi moja
    (i) Pa
    (ii) La

    Date posted: June 27, 2019.  Answers (1)