Chai, chumvi, sukari. Mvua, barafu, huzuni, teknolojia
Kavungya answered the question on June 28, 2019 at 09:02
- MUHTASARI
Ajira ya watoto ni tatizo sugu linalokumba ulimwengu wa sasa , hasa katika nchi
zinazozoendelea. Jambo la kusikitisha ni kwamba hivi ndivyo ilivyo katika nchi nyingi
za...(Solved)
MUHTASARI
Ajira ya watoto ni tatizo sugu linalokumba ulimwengu wa sasa , hasa katika nchi
zinazozoendelea. Jambo la kusikitisha ni kwamba hivi ndivyo ilivyo katika nchi nyingi
za ulimwengu huu. Kuna idadi kubwa ya watoto wanaoajiriwa katika nyanja mbalimbali
za jamii. Zipo sababu nyingi zinazowasukuma watoto kutafuta ajira barani Afrika kwa
mfano, familia nyingi huishi maisha ya ufukara hivi kwamba hushindwa kuyatimiza
mahitaji muhimu hususan kwa watoto. Kapanda kwa gharama ya maisha kunazidisha
viwango vya umaskini. Ukosefu wa lishe pia huwafanya watotto kutoroka nyumbani
kutfuta ajira. Janga la UKIMWI limesababisha kuwepo kwa idadi kubwa ya mayatima
wanaoshia kutafuta ajira ili kuyakimu maisha. UKIMWI umezifanya nyingi pia
kuwaondoa watoto shule ili waweze kuajriwa kwa lengo la kuanzisha pato la familia
hizo. Watoto wengine hutoroka makwao kwa sababu ya maonevu. Maonevu haya ni
kama vile kupigwa, kutukanawa kila wakati, kunyanyaswa kijinsia na kadhalika. Huko
nje hutaabishwa kimwili na kiakili. Hufanyishwa kazi za sulubu zenye malipo duni au
wasilipwe kabisa. Hili huwasononeshe na kuathiri afya yao.
Uundaji wa Umoja wa Afrika hivi majuzi ni hatua muhimu ya kushughulikia matatizo ya
Afrika kama vile ajura ya watoto, kuzorota kwa miundo msingi, magonjwa, njaa,
umaskini, ufisadi na ukabila. Katika kushughulikia haki za watoto, nchi za Afrika hazina
budi kuzingatia masharti yalivyowekwa na Umuja wa Mataifa kuhusu haki za watoto.
Nchi nyingi za Afrika ziliidhinisha mkataba wa marsharti hayo ikiwemo inchi ya Kenya.
Nchi hizi basi lazima zishughulikie haki za watoto kupitia sheria za nchi. Watoto ni
rasilimali muhimu na ndio tumaini la kuwepo kwa kizazi cha binadamu.
a) Eleza mambo yote muhimu anaazungumzia mwandishi katika aya ya kwanza
(maneno 45-50) (alama 7, 1 ya utiririko)
Matayarisho
Jibu
b) Bila kubadilisha maana aliyokusudia mwandishi, fupisha aya mbili za mwisho
(maneno 50-55) (alama 8, 1 ya utiririko)
Matayarisho
Jibu
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Ulimwengu unapaswa kuzuka na mbinu za Kulitadarukia tatizo la umaskini ambao
unakwamiza juhudi za maendeleo. Umaskini unaoyakabili mataifa yanayoendelea.
Unayatosa kwenye dhiki...(Solved)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Ulimwengu unapaswa kuzuka na mbinu za Kulitadarukia tatizo la umaskini ambao
unakwamiza juhudi za maendeleo. Umaskini unaoyakabili mataifa yanayoendelea.
Unayatosa kwenye dhiki kubwa huku mataifa ya kimagharibi yakitpiga hatua kubwa
kimaendeleo. Ufa uliopo baina ya mataifa yanayoendelea na yalo yaliyoendelea kama
vile Marekani, nchi za Ulaya na Ujapani unapanuka kila uchao.
Vyanzo vya umaskinin huu ni anuwai mathalan, ufusadi, uongozi mbaya, turathi za
kikoloni, uchumi kuegemea mvua isiyotabarika, idadi ya watu inayoupik uwezo wa
uchumi wa taifa linalohusika na ukosefu wa nyenzo na amali za kuwakwamua raia
kutoka lindi la umaskini. Ukosefu adimu za ajira huchangia pia katika tatizo hili.
Jamii ya ulimwengu inapaswa kuelewa kuwa umaskini unaoathiri nchi Fulani una athari
pan asana. Uvunigu unaotokana na umaskini unaweza kuweza kuwa mboji ambako
matendo ya kihalifu ili kujinasua kutoka dhiki ile. Hii inaweza kuwa mbegu ya kuatika
maovu kama ugaidi na uhalifu wa kila aina.
Mataifa ya magharibi yanapaswa kuyaburai madeni mataifa yanayoendelea kama njia
mojawapo ya kupambana na umaskini. Asilimia kubwa ya pato la kitaifa katika mataifa
mengi hutumika kuyalipa madeni hayo. Katika hali hii inakuwa muhali kwa mataifa hayo
kujikwamua kutokana na pingu za umaskini. Njia nyingine ni kustahabu kutoa ruzuku za
kimaendeleo badala ya mikopo kwa nchi zinazoendelea.
Kwa upande wake, mataifa yanayoendelea yanapaswa kuibuka na mikakati bora ya
kupambana na umaskini. Ni muhimu pawepo na sera zinazotambua ukweli kuwa
asilimia kubwa ya raia wa mataifa hayo ni maskini. Pana dharural ya kuzalisha nafasi za
ajira, kupanua viwanda hususan vinavyohusiana na zaraa ambayo ni tegemeo kuu la
mataifa mengi, kuendeleza elimu na kuimarisha miundo msingi. Ipo haja pia ya mataifa
haya kuhakikisha kuwa mfumo wa soko huru unaotawala ulimwengu sasa huishii kuwa
chanzo cha kufa kwa viwanda asilia na kuendeleza masikini zaidi. Kwa ufupi, maamuzi
yote ya sera za kiuchumi lazima yazingatie uhalishi wa maisha ya raia wa mataifa hayo.
a) Kwa nini umaskini umetamalaki katika mataifa yanayoendelea?
b) Madeni yana athari gani kwa mataifa yanayoendelea?
c) Ni mapendekezo yapi ambayo mwandishi anatoa kwa mataifa machanga kuhusu
utatuzi wa tatizo la umaskini?
d) Mfumo wa soko huru una mathara gani kwa mataifa machanga?
e) Ukirejea kifungu, eleza maana ya:
i) Kulitadarukia
ii) Kuatika
iii) Kuyaburai madeni
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- Mbuni huzaa matunda gani?(Solved)
Mbuni huzaa matunda gani?
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- Haya ni magonjwa gani?
I Matubwitubwi
II Tetewanga(Solved)
Haya ni magonjwa gani?
I Matubwitubwi
II Tetewanga
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- Kati ya madini haya taja yale yanayopatikana baharini
Zinduna Zebaki
Lulu Ambari
Yakuti Marumaru(Solved)
Kati ya madini haya taja yale yanayopatikana baharini
Zinduna Zebaki
Lulu Ambari
Yakuti Marumaru
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- Jaza jedwali
Kiume Kike
Mjakazi
Jogoo
Fahali(Solved)
Jaza jedwali
Kiume Kike
Mjakazi
Jogoo
Fahali
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- Eleza maana ya:
(i) Sina pa kuuweka uso wangu
(ii) Ana mkono wa buli(Solved)
Eleza maana ya:
(i) Sina pa kuuweka uso wangu
(ii) Ana mkono wa buli
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- Eleza maana mbili tofauti za sentensi hii
Mamake Juma na Mariamu walitutembelea(Solved)
Eleza maana mbili tofauti za sentensi hii
Mamake Juma na Mariamu walitutembelea
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- Geuza vitenzi hivi viwe majina
(i) Shukuru
(ii) Enda(Solved)
Geuza vitenzi hivi viwe majina
(i) Shukuru
(ii) Enda
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- Andika sentensi hii upya kwa kufuata maagizo
Nilikuwa nimejitayarisha vizuri kwa hivyo sikuona ugumu wo wote
katika safari yangu.
Anza: safari(Solved)
Andika sentensi hii upya kwa kufuata maagizo
Nilikuwa nimejitayarisha vizuri kwa hivyo sikuona ugumu wo wote
katika safari yangu.
Anza: safari
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- Tumia – ndi pamoja na viashiria vya ngeli kujaza mapengo
(i) Wewe ___________ ninayekutafuta
(ii) Nyinyi ___________ mnaoongoza(Solved)
Tumia – ndi pamoja na viashiria vya ngeli kujaza mapengo
(i) Wewe ___________ ninayekutafuta
(ii) Nyinyi ___________ mnaoongoza
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- Kanusha sentensi hii:
Tumechukua nguo chache kuuza(Solved)
Kanusha sentensi hii:
Tumechukua nguo chache kuuza
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- Huku ukitoa mifano, fafanua miundo mitatu ya majina katika ngeli ya
JI-MA(Solved)
Huku ukitoa mifano, fafanua miundo mitatu ya majina katika ngeli ya
JI-MA
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- Eleza matumizi ya na katika sentensi:
Halima na Asha wanasaidiana(Solved)
Eleza matumizi ya na katika sentensi:
Halima na Asha wanasaidiana
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- Andika kwa wingi
Pahala hapa ni pake(Solved)
Andika kwa wingi
Pahala hapa ni pake
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- Eleza matumizi ya kwa katika sentensi hii
Aliimba kwa sauti tamu(Solved)
Eleza matumizi ya kwa katika sentensi hii
Aliimba kwa sauti tamu
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- Kamilisha jedwali
Kufanya Kufanyia Kufanywa
Kula
Kuunga(Solved)
Kamilisha jedwali
Kufanya Kufanyia Kufanywa
Kula
Kuunga
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- Bainisha aina ya vivumishi katika sentensi hii
Nyumba yangu ni maridadi(Solved)
Bainisha aina ya vivumishi katika sentensi hii
Nyumba yangu ni maridadi
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- UFUPISHO
Ujambazi wa kimataifa ni tatizo lilolowasumbua walimwengu kwa muda mrefu sana.
Serikali nyingi zimetumia mapesi mengi kwa miaka mingi sana zikijitahidi kupambana
na janga hii. Hata hivyo,...(Solved)
UFUPISHO
Ujambazi wa kimataifa ni tatizo lilolowasumbua walimwengu kwa muda mrefu sana.
Serikali nyingi zimetumia mapesi mengi kwa miaka mingi sana zikijitahidi kupambana
na janga hii. Hata hivyo, fanaka haijapatikana wala haielekei kamwe kuwa itapatikana leo
au karne nyingi baadaye.
Yumkini tatizo kubwa lililopo ni kuhusu jelezi la dhana ya “ujambazi” tena “wa
kimataifa”. Hili ni tatizo mojawapo na yapo mengi sana. Tatizo la pili ni kiburi. Kuna
wale watu binafsi na hasa viongozi wan chi kubwakubwa na serikali zao zilizojiaminisha
kuwa ujambazi ni balaa kweli, tena belua, lakini huo ni wa huko, wala hauwezi kuwagusa
licha ya kuwashtua wao.
Kulingana na maoni watakaburi hao, ujambazi ni wa watu “washenzi” wasiostaarabika,
wapatikanao katika nchi zisizoendelea bado. Ujambazi pekee wanaouona unafaa
kukabiliwa ni dhidi ya mbubujiko wa madawa ya kulevya uliosababishwa na
vinyangarika kutoka nchi hizo maaluni za “ ulimwengu wa tatu”. Kulingana na
wastaarabu wan chi zilizoendelea, vinyangarika hivi ndivyo hasa adui mkubwa wa
ustaarabu ulimwenguni na ni sharti vifagiliwe mbali bila huruma. Baada ya
kusagwasagwa, ulimwengu mstaarabu utazidi kutononoka na ahadi ya mbingu hapa
ardhini itakamilika.
Imani ya watu ya kuwa ujambazi wa kimataifa. Hata iwapo upo, hauwezi kuwashtua
wala kuwatingisha wao ilikuwa kamili na timamu. Ilikuwa kamili na timamu hadi
hapo mwezi Septemba tarehe 11 mwaka wa 2001, ndege tatu za abiria zilipoelekezwa
katika majumba mawili ya fahari, yenye urefu wa zaidi ya ghorofa mia moja na
kuyatwangilia mbali. Mshtuko na kimako! Kimako kwa kuwa, kabla ya siku hiyo,
wanarekani kudhai kwamba ingewezekana taifa lolote au mtu yeyote kuthubutu
kuishambulia nchi yao, taifa wasifa lililojihami barabara dhidi ya aina yeyote ile ya
uchokozi kutoka pembe lolote la dunia.
Hakuna ulimwengu mzima, aliyeamini kuwa marekani ingeeza kushambuliwa. Kwa ajili
hiyo, mshtuko uliitingisha ardhi yote na huzuni ilitanda kote, kama kwamba sayari nzima
imeshambuliwa, wala sio marekani pekee.
Mintarafu hiyo, marekani ilipolipiza kisasi kwa kuwaunguza waliokuwemo na
wasiokuwemo kwa mabomu hatari huko Afghanistan, idadi kubwa ya watu duniani
ilishangilia na kusherehekea. Kwa nahati mbaya, tafsiri ya shambulizi la minara- pacha
ya Newyork na lile la Pentagon, uti wa uwezo wa kivita wa Marekani, ilizorota. Kuna
wengi waliodhani huo ni mwanzo wa vita vya Waislamu dhidi ya Wakristo na kwa
muda, Waislamu wote wakashukiwa kimakosa kuwa ni majambazi wa kimataifa.
(a) Bila bubadilisha maana, fupisha aya tatu za kwanza ( maneno 65 – 75)
Matayarisho
Nakala safi (alama 10, 2 za utiririko)
(b) Ukizingira aya, tatu za mwisho, fafanua fikira za watu wa mambo yote
yaliyotokea
Baada ya Septemba tarehe 11, 2001 (maneno 65 – 75) (alama 10, 2 za
utiririko)
Matayarisho
Nakala safi
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Nairobi , mji mkuu wa Kenya, ni jiji la maajabu na mastaajabu chungu nzima. Nadhari
ya mtu anayewahi kuingia jiji hili...(Solved)
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali
Nairobi , mji mkuu wa Kenya, ni jiji la maajabu na mastaajabu chungu nzima. Nadhari
ya mtu anayewahi kuingia jiji hili kwa mara ya kwanza huvutiwa na huo msheheneko wa
majumba ya fahari, marefu ajabu, kiasi cha minazi mitano- sita iliyounganishwa
kuelekea juu mbinguni.
Jumba linalowavutia watu wengi ni lile la makongamano ya kimataifa liitwalo kwa
kiingereza Kenyatta International Conference Centre. Jumba hili, hadi miaka michache
ilipopita, ndilo lililokuwa refu zaidi mjini. Jumba lenyewe lina ghorofa ishirini na tisa
hivi, Usipohesabu hilo pambo kama kofia kileleni mwake, linalojulikana kama
mwavuli. Hata hivyo, miaka michache iliyopita jingo hili lilipitwa kwa urefu na mnara
wa Nyakati ( Times Tower) Mnara huo hasa ni jumba linaloafiki lakabu yake ya
kikwaruza mawingu. Jumba hili lina ghorofa zisizopungua thelathini na mbili.
Mbali na majumba haya mawili, kuna majumba mengine zaidi ya ishirini katikati ya jiji
ambayo, japo mengine ni mafupi kiasi, maumbo ya kustaajabisha kweli kweli. Hebu
zingatia mwenyewe jumba liitwalo “mdomo wa kengele” au bell - bottom” ambalo ni
vioo vitupu, toka chini hadi juu. Fauka ya haya, umbo lake ni la kipekee ulimwenguni
kote. Jumba hili lina kama miguu, kisha kiuno mithili ya kinu hivi japo si mviringo.
Linapaa juu, mbali sana, likichukua umbo pana kuliko lilivyo chini. Umbo la fua pana
kama kengele.
Halafu rudia barabara. Hizi hazina hesabu katikati ya jiji ni pona, tena safi sana. Magari
yanayotumia barabara hizi ni kochokocho, ya kila aina na yanashindania nafasi.
Ajabu kubwa ya Nairobi hata hivyo ni idadi ya watu. Hakuna hasa anayejua idadi kamili
ya watu wa Nairobi, lakini sio kupiga chuku ninaposema kwamba, hasa nyakati za
kuelekea kazini asubuhi, kwenda kula chakula cha mchana, kuelekea nyumbani baada
ya kazi na kuvuka barabara wakati wa msongamano, watu hukanyagana. Mtu anayesema
kwamba watu wa Nairobi ni wengi kama chungu, au kama mchanga wa ufuo wa bahari,
hatii chumvi
Watu wa Nairobi, kwa tabia na mavazi, si kama watu wa kwingineko nchini Kenya.
Watu hawa kuvalia nadhifu sana. Wanawake ni warembo ajabu na hutengeneza nywele
zao mithili ya hurulaini peponi. Wengi huvaa suruali ndefu! Kucha zao na midomo yao
hupata rangi maridadi sana. Huzungumza Kiswahili na kiingereza takriban wakati wote.
Wanawake wengi ajabu huendesha magari yao wenyewe, jambo ambalo litakushangaza
mara tu uingiapo jijini, hasa kama ulilelewa ukidhani maskani mwafaka ya wanawake ni
jikoni peke yake, yaani kuzingatia ile falsafa kuwa “ kuoa ni kupata jiko”. Wanaume
nao huvaa suti safi, maridadi na shingoni wamefunga tai stahiki yao. Wanaume hao huendesha magari ya kuyaegesha karibu na afisi zao. Huingia afisini mwao kwa maringo
na madaha, huku funguo za magari yao zikining’inia vidoleni. Hawa nao husema
Kiswahili na kiingereza kupitia puani, utadhani ni waingereza hasa.
Kwa upande mwingine, watoto ni nadhifu kweli hasa watoto wa shule. Hawa huvalia sare
zilizofuliwa na kunyoshwa vizuri kwa pasi. Wake kwa waume, shingoni huvalia tai.
Watoto wa shule Nairobi huongea Kiswahili, kiingereza na Sheng, ambayo ni “lahja” yao
waliyoibuni.
“Lugha” hii ni mchanganyiko wa Kiswahili. Kiingereza na msamiati mchache wa lugha
nyingine za wakenya zisemwazo jijini Nairobi na vitongoji vyake.
Kwa jumla, watu wote wa Nairobi hutembea kasi sana. Hawana hata wakati wa kutembea
pole pole na kuangazaanga huku na huko. Iwapo wewe ni mgeni jijini, ukizubaa
utapigwa kumbo na waendelee na hamsini zao kama vile hapakutokea jambo. Hili
linapojiri, usidhani limefanywa maksudi. La, hasha ni vile tu kwamba Wanairobi hawana
muda wa kupoteza.
(a) Kwa nini majumba ya jiji la Nairobi yana majina au lakabu za kiingereza?
(b) (i) Baadhi ya maajabu ya Nairobi ni barabara safi, msongamano wa magari
na majumba marefu. Ongezea maajabu mengine manne
(ii) Watu wa Nairobi wanajipenda kweli kweli. Fafanua
(c) (i) Je, unadhani watu wa Nairobi kweli hukanyagana? Eleza ni kwa nini
msimulizi ametoa maelezo hayo
(ii) Unafikiri ni kwa nini hasa wanawake wa Nairobi wanaonekana nadhifu?
(d) Kwa nini neno “lahja” limewekwa alama za mtajo?
(e) Eleza maana ya maneno na tamathali za usemi zifuatazo:
(i) Nadhari
(ii) Linaloafiki
(iii) Kikwaruza mawingu
(iv) Waendelee na hamsini zao
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)