Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

ISIMU JAMII Soma kifungu kifuatacho ujibu maswali yanayofuata. Kwa mujibu wa sheria kifungu nambari 3 sehemu ya A ya sheri za nchi, umepatikana na hatia ya kutatiza utulivu...

      

ISIMU JAMII
Soma kifungu kifuatacho ujibu maswali yanayofuata.
Kwa mujibu wa sheria kifungu nambari 3 sehemu ya A ya sheri za nchi, umepatikana na
hatia ya kutatiza utulivu wa raia wapenda amani kwa kuwatusi na kutisha kuwapiga.
Kiongozi wa mashtaka amethibitisha haya wa kuwaleta mashahidi ambao wametoa
ushahidi usiotetereka kuhusu vitendo vyako katika tukio hilo. Korti hii imeonelea una
hatia na imeamuru ufungwe jela kwa muda wa miaka miwili bila faini ili liwe funzo
kwako na kwa wenzako wenye tabia kama zako. Una majuma mawili kukata rufani.

a) Lugha iliyo katika kifungu hiki hutumika katika muktadha upi?
b) Toa ushaidi wa jibu lako
c) Zaidi ya sifa zilizo katika kifungu hiki, eleza sifa zingine sita za matumizi ya
ligha katika muktadha huu.

  

Answers


Kavungya
(a) Mahakama / kotini/ Daawa/ Muktaoha wa sheria

(b) 1. Msamiati teule- jelam rufani, mashraka
2. Washikadau/ wahusika kama kiongozi, namashtaka, mashahidi,
hakimu, (jaji), mhalifu
3. Sentensi ni ndefu kimuundo
4. Kurejelea vyungu vya sheria za nchi
5. Lugha ya hakimu ni ya kuamuru
6. Lugha rasmi imetumika
7. Lugha sanifu imetuka
8. Lugha iliyotumika ni ya mfululizo- hakimu anapotoa hukumu
9. Utaratibu mtendo maalum wa kufuatiwa kesi inapoamuliwa
Kortini
10. Lugha ya kuanunu

(c) 1. Lugha yenye kudadisi
2. Lugha yenye kukopa kutoka lugha nyingine
3. Lugha ya heshima
4. Lugha ya ishara hutumiwa uhalisia/ hutumiwa
5. Lugha hudhihirisha ukweli wa mambo
6. Mawakili huzozana kukatizana
7. Lugha ya kishawishi kwa hakimu
8. Lugha ya maagizo
9. Wanasheria wana lugha yao maalum
10. Mshtakiwa/ mshahidi ana uhuru wa kutumia lugha unayoelewa
11. Lugha limufaji kufasiriwa
12. Hakuna lugha ya ucheshi/ utani.
Kavungya answered the question on June 28, 2019 at 09:56


Next: Eleza matumizi ya “na” katika sentensi: Sofia na Raeli wanaandaliwa chai na mpishi
Previous: UFAHAMU Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Wanasaikolojia wanabainisha kati ya sehemu mbili kuu katika akili ya binadamu: Ung’amuzi na ung’amuzibwete. Ung’amuzi ni sehemu ya ubongo ambayo kimsingi hupanua...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions