UFAHAMU Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Wanasaikolojia wanabainisha kati ya sehemu mbili kuu katika akili ya binadamu: Ung’amuzi na ung’amuzibwete. Ung’amuzi ni sehemu ya ubongo ambayo kimsingi hupanua...

      

UFAHAMU
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Wanasaikolojia wanabainisha kati ya sehemu mbili kuu katika akili ya binadamu:
Ung’amuzi na ung’amuzibwete. Ung’amuzi ni sehemu ya ubongo ambayo kimsingi
hupanua na kudadavua yanayotendeka hususan mchana. Ung’amuzibwete ni
kibinimethali chake; hufanya kazi wakati binadamu anapolemazwa na usingizi. Baadhi
ya mambo anayoshuhudia binadamu mchana yanaingia kwenye ung’amuzibwete wake na
kutokeza katika ndoto zake usiku.

Kwa mujibu wa mawazo ya Sigmund freud, mwanasaikolojia wa jadi anayechukuliwa
nawengi kama mwasisi wa taaluma ya saikolojia, mambo yanayopatikana katika
unga’amuzibwete mambo yana sifa hasi. Freud alidahili kuwa binadamu huyaficha na
kuyabania kwenye ung’amuzibwete mambo ambayo hawezi juyasema kadamnasi.
Alieleza kuwa matamanio yasiyokubalika, makatazo ya jamii, fikra na kauli
zilizoharamishwa na miko ya kijamii hubanwa katika ung’amuzibwete. Shehena hiyo
ndiyo inayochipuza kwa njia ya ishara za ndoto, mitelezo ya kauli, yaani maneno au kauli
zinazotukoka bila wenye kukusudia, ishara na lugha ya kitamathali katika uandishi wa
kibunifu na kadhalika.

Ung’amuzibwete un uwezo mkubwa wa kuathiri matendo ya binadamu. Huu ndio
msingi unaowafanya wanasaikolojia wengi, akiwepo freud, kusema kuwa tajiriba ya
motto inaweza kufichwa kwenye sehemu hiyo na hatimaye kuishia kutokeza katika utu
uzima wake. Kwa kuwa tunapoingiliana na binadamu wenzetu kila siku
tunayang’amuzibwete unapotawala binadamu wenzetu watashindwa kutuelewa. Hii
ndiyo hali anayokuwa nayo mwendawazimu. Ung’amuzibwete wake hutawala. Sisi
tunaotawaliwa na ung’amuzi tunashindwa kumwelewa; naye bila shaka anashindwa
kutuelewa.

Carl Gustav Jung, aliyewahi kuwa mwanafunzi wa Freud, aliupinga mwelekeo wa Freud
wa kuungalia ung’amuzibwete kama jaa la mawazo mabaya, matamanio, nia, fikira tuli
na dhana ambazo ni hasi. Jung alizuka na dhana mbili muhimu: Ung’amuzibwete wa
kibinafsi na un’gabuzibwete jumuishi. Alisema mambo, fikra na uzoefu wowote mbaya
unaomuhusu mtu binafsi . Dhana ya ung’a muzibwete jumuishi aliitumia kuelezea
sehemu ya akili ya binadamu ambayo inamfanya ayatende matendo Fulani kama
binadamu wenzake licha ya tofauti zao kiwakati na kijiografia. Kwa mfano, binadamu
wengi wana sherehe za kuzaliwa motto, kuoza, ibada au mviga unaohusiana na kifo licha
ya tofauti zao. Jung alisema kuwa kinachochochea hali hii ni urithi Fulani wa kila
mwanadamu. Urithi huo unapatikana katika ung’amuzibwete jumuishi.

Upo mwafikiano kati ya wataalamu hawa wawili kuwa ung’auzibwete una uwezo wa
kuathiri ung’amuzi matendo ya binadamu ya king’amuzi. Wanasaikolojia wanashikilia kuwa binadamu hawezi kukamilika bila kuzihusisha sehemu zote mbile kwa sababu
zinaathiriana.

a) Kwan in ung’amuzibwete unaelezwa kama kinyme cha ung’amuzi?
b) Eleza mtazamo wa Freud kuhusu ung’amuzibwete.
c) Kwa mujibu wa Freud yaliyomo kwenye ung’amuzibwete hudhihirika vipi?
d) Eleza tofauti ya mawazo kati ya Sigmund Freud na Carl Gustav Jung.
e) taja hoja inayowafungamanisha Jung na Freud.

  

Answers


Kavungya
(a) Ung’amuzibwete hufanya kazi mtu akiwa amelala/ usiku kinyume na
ung’amuzi hufanya kazi mtu akiwa macho/ mchana.

(b) (i) Mambo yanayopatikana katika ung’amuzimbwete yana hasi hubana
(ii) Huficha mambo ambayo mwanadamu hawezi kuyasema/ peupe/
kadamnazi
(iii) Hubaa matamanio yasiyo kubalika na jami/ makala
(iv) Hubania kauli zuluzoharamishwa na miko ya kijamii.
Huficha na kubana mambo ambayo binadamu hawezi kuyasema

(c) (i) Kwa ishara za ndoto
(ii) Kwa mitelezo ya kauli
(iii) Kwa ishara
(iv) Kwa matumizi ya lugha ya kitamathali katika uandushi

(d) Fred anawaza kuwa ung’amuzibwete ni jaa la mambo hazi ilhali Jung ana
dhana mbili kuhusu un’amuzibwete – ile ya kibinafsi na jumuishi. Fred
ana mtazamo wa dhana hasi katika ung’amuzibwete tofauti na jung
ambaye anawaza dhana ya jumuishi.

(e) Ung’amuzibwete una uwezo wa kuathiri ungamuzi na matendo ya
binadamu ya king’amuzi.
Kavungya answered the question on June 28, 2019 at 10:03


Next: ISIMU JAMII Soma kifungu kifuatacho ujibu maswali yanayofuata. Kwa mujibu wa sheria kifungu nambari 3 sehemu ya A ya sheri za nchi, umepatikana na hatia ya kutatiza utulivu...
Previous: MUHTASARI Utaifa ni mshikamano wa hisia zinazowafungamanisha watu wanaoishi katika taifa moja. Taif huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na ambao wanajitambua kisiasa kama watu wenye mwelekeo,...

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions