MUHTASARI Utaifa ni mshikamano wa hisia zinazowafungamanisha watu wanaoishi katika taifa moja. Taif huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na ambao wanajitambua kisiasa kama watu wenye mwelekeo,...

      

MUHTASARI
Utaifa ni mshikamano wa hisia zinazowafungamanisha watu wanaoishi katika
taifa moja. Taif huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na ambao wanajitambua
kisiasa kama watu wenye mwelekeo, mwono na hatima sawa. Utaifa umejengwa kwenye
hisia za mapenzi kwenye hisisia za mapenzi kwa nchi na utambuzi wa kwamba rangi,
cheo, hadhi, eneo, kabila au tofauti nyinginezo baina ya watu wanaoishi katika nchi moja
si sbabu ya kuwatenganisha.

Nchi moja huweza kuwa na watu wa makabila tofauti, wenye matabaka ya kila nui na
mawazo ainat. Watu hao wanapotambua kuwa kuna sherisi nyinyine inayowaunganisha
kama fahari ya kuwa watu waochi hiyo, falsafa na imani sawa ambayo ishara yake kuu ni
winbo wa taifa na kuwa tofauti kati yao muhimu huwa wamefikia kuunda taifa.

Mhili mkuu wa utaifa ni uzalendo. Uzaleno ni mapenzi makubwa aliyo nayo mtu kwa
nchi yake. Malezi haya ndiyo yanyoongoza matendo yake, matamanio yake, mawazo
yake, itikadi yake mwonoulimwengu wake na muhimu zaidi mkabala wake kuihusu nchi
yake na hatima ya nchi yenywe. Uzalendo ni nguzo muhimu sana ya taifa. Mzalendo
hawezi kuyatenda mambo yanayoweza kuletea mkama nchi yake.

Matendo ya mzalendo huangazwa na mwenge wa mema anayoitakia nchi au taifa lake.
Hawezi kushiriki kwenye harakati na amali ambazo zinahujumu au kufumua
mshikamano wa taifa zima au kutawaliwa na kitiba cha kutaka kujinufaisha yeye
mwenyewe au jamii yake finyu. Matendo ya mzalendo wa kitaifa yanaongozwa na
mwelekeo wa kuiboresha nchi yake. Swali linalomwongoza mtu huyo ni: nimeifanyia
nini nchi yangu au taifa lahgu? Alhasili mtu anayeipenda nchi yake hawezi kuongozwa
na umero wa kibinafsi tu wa kujilimbikia mali, ujiri au pesa. Yuko radhi kuhasirika
kama mtu binafsi ili taifa au nchi yake inufaike.

Utaifa ni mche aali ambao unapaliliwa kwa uzalendo, kuepuka hawaa za nafsi, kusinywa
na taasubi za kikabila na kuach tama ya kujinufaiha. Hali hiyo inapofikiwa, hatima ya
wanajamii wa taifa linahusika huwa nzuri na mustakabali wao na wa vizazi vyao huwa
wa matumaini makubwa.

a) Dondoa sifa kuu za utaifa. (maneno 40- 50)
b) kwa kutumia maneno kati ya 60-70, onyesho misingi ya kumtathmini mzalendo.

  

Answers


Kavungya
(a) (i) Mshikamano wa hisia
(ii) Mwelekeo mmoja
(iii) Mwono na/ hatima sawa
(iv) Hisia za mapenzi kwa nchi/ uzalendo
(v) Hauna ubanguzi
(vi) Falsafa na/ imani sawa/ itikadisaw

(b) (i) Mzalendo anaipenda nchi yake
(ii) Hawezi kuyatenda mambo yanayoweza kuiletea nakama nchi yake
huanzazwa na mwanga wa mema anayoitakia nchi yake.
(iii) Hawezi kutawaliwa na ubinafsi na umero wa kujilimbikia mali.
(iv) Matendo yake houngozwa na mwelekeo wa kuiberesha nchi yake.
(v) Yuko radhi kuhasirika kama mtu binafsi taifa lake linufaike
(vi) Hana taasubi za kikabila
Kavungya answered the question on June 28, 2019 at 10:06


Next: UFAHAMU Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Wanasaikolojia wanabainisha kati ya sehemu mbili kuu katika akili ya binadamu: Ung’amuzi na ung’amuzibwete. Ung’amuzi ni sehemu ya ubongo ambayo kimsingi hupanua...
Previous: Andika sentensi mbili zifuatazo kama sentensi moja kwa kutumia kiwakilishi kirejeshi. i) duka la Bahati lina bidhaa nyingi ii) Juma anafanya kazi katika duka la Bahati.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions