Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

RIWAYA S.A MOHAMED: UTENGANO “ Katu asingajitia kibuibui na kutanga na njia. Lo, kachoshwa na shimiri za baruti anazoshindiliwa moyoni mwake.” a) eleza muktadha wa dondoo hili. b) taja na...

      

RIWAYA
S.A MOHAMED: UTENGANO

“ Katu asingajitia kibuibui na kutanga na njia. Lo, kachoshwa na shimiri za baruti
anazoshindiliwa moyoni mwake.”
a) eleza muktadha wa dondoo hili.
b) taja na ufafunue tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili
c) Eleza umuhimu wa kisa kinachorejelewa na dondoo.
d) kwa kurejelea matukio mengine katika riwaya ya Utengano, fafanua maudhui
mawili yayoashiriwa na dondoo hili.

  

Answers


Kavungya
a) (i) Haya ni maelezo ya mwandishi kuhusu mawazo ya selume katika ndoa.
(ii) Anahisi hana mume kwani shoka amepuuza wajibu wake/ mzohali
(iii) Amemwachia jukumu la malezi na kutafuta riziki, kazi ya Shoka ni
kudoea alichotafuta selume.
(iv) Kama si wanawe Selume hangejisumbua kutafuta chakula

(b)(i) Sitiara/ jazanda
Mfano: Shimiri za baruti
Maalezo: Matatizo ya ndoa
(ii) Msemo/ Nahau: kutanga na njia – kuhangaika, kutafuta
(iii) Nida/ siyahi: Lo- kuonyesha hisia za kuchukizwa na mkondo wa ndoa
yake.

(c)(i) Kudhulumiwa kwa mwanamke katika ndoa kama. Selume na shoka
(ii) Kutowajibika kwa wanaume. Kama Shoka
(iii) Wanawake kuendelea kubaki katika ndoa zenye matatizo kwa sababu ya
watoto wao na kujitolea katika yaliyopuuzwa na waume wao.

d) 1 Asasi ya ndoa/ unyumba – ndoa ya maksuudi na tamima na ya maksuudi na mwanasururu
(i) Matatizo kati ya mume n mke
(ii) Dhiki zinazowakumba wanawake katika ndoa
(iii) Tamima analazimika kutawa kwa amri ya mumewe Bw. Maksuudi
(iv) Hana ruhusa ya kutoka wala kumwalika mtu nyumbani.
(v) Analazimika kujifungua nyumbani licha ya ushauri wa madaktari
kutokana na kufukuzwa nyumbani.
(vi) Ananyimwa uhuru wa kuwa na mwanawe mdogo anayeishia kufariki
(vii) Tabia ya Bw. Maksuudi inaishia kuivunja jamaa yao.
(viii) Bw. Maksuudi anamwacha mkewe na kuwafuata wanawake wengine
huko nje
(ix) Mwanamke ananyimwa uhuru wa kuishi kama kiumbe anaweza kujiamlia
(x) Mwanamke hana uhuru wa kiuchumi. Km Mwanasururu ananyimwa
urithi wake.
2 Utengamano wa kijinsia/ taasubi ya kiume/ utengano kati ya wanawake na wanaume/ mgogoro wa kijinsia
(i) Wanawake wanatumiwa kama vyombo vya starehe km. kazija na
maksuudi, shoka na mainmuna.
(ii) Uhusiano kati ya mwanamke na mwanaume unatawaliwa na chuki na
kisasa – Biti. Kocho/ Farashuu na maksuudi, kazija na maksudi.
(iii) Tamina anateswa na maksuudi hataki kumsamehe na kumrudia
anapomtaka kufanya hivyo.
(iv) Uhusiano wa Maimuna na Bw. Maksuudi babake unaonyesha chuki
inayotokana na matendo ya maksuudi mwenyewe.
(v) Kazija anapanga njama ya kumfumanisha maksuudi na mwanawe Musa.
3 Ukatili
(i) Maksuudi anavyomtenda Bi. Tamina
(ii) Maksuudi anavyomtenda mwanasururu
(iii) Maksuudi kumpiga na kumfukuza/ taliki Bi. Tamina ilhali ana tumbo bichi
4 Dhiki/ kudhulumiwa kwa wanawake
(i) Maksuudi kutawisha Bi. Tamina na Maimuna
(ii) Maksuudi kumwendea kinyume Bi. Tamina ( Jicho la nje)
(iii) Maksuudi kumpora Mwanasururu mali yake
(iv) Wanawake kuachwa nyuma kielimu na kikazi
5 Nafasi ya mwanamke katika jamii
(i) Wanawake kujihusisha na ukahaba ili kujikimu
(ii) Wahusika wengine waliishi maisha katika makazi duni km. Farashuu,
Maimuna, Mwanasururu.
6 Umaskini
(i) Wanawake kujihusisha na ukahaba ili kujikimu
(ii) Wahusika wengine waliishi maisha katika makazi duni km Farashuu,
Maimuna, Mwanasururu.
Kavungya answered the question on June 29, 2019 at 07:02


Next: ISIMU JAMII Eleza majukumu matano matano ya Kiswahili kama lugha ya Kitaifa na Kimataifa.
Previous: USHAIRI Soma shairi kisha ujibu maswali yanayofuata: KIBARUWA: Abdilatif Abdalla Kwenye shamba hilo kubwa asilani hakunyi mvuwa! Ni kwa mitilizi ya jasho langu ndiyo hunweshezewa Kwenye shamba hilo kubwa sasa...

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions