USHAIRI Soma shairi kisha ujibu maswali yanayofuata: KIBARUWA: Abdilatif Abdalla Kwenye shamba hilo kubwa asilani hakunyi mvuwa! Ni kwa mitilizi ya jasho langu ndiyo hunweshezewa Kwenye shamba hilo kubwa sasa...

      

USHAIRI
Soma shairi kisha ujibu maswali yanayofuata:
KIBARUWA: Abdilatif Abdalla

Kwenye shamba hilo kubwa asilani hakunyi mvuwa!
Ni kwa mitilizi ya jasho langu ndiyo hunweshezewa
Kwenye shamba hilo kubwa sasa imeshaiva kahawa
Na bunize ni matone ya damu yangu niliyotowa
Ndipo mte ukatipuza!

Buni hiyo itakaangwa buni hiyo itapondwapondwa
Buni hiyo itasagwa na buni hiyo itafyondwafyondwa
Bali itabaki nyeusi kama ngozi yangu Kibaruwa
Waulize ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao
Iulize na mito kwa furaha maji itiririkao
Uulize na upepo mkali kwa ghadhabu uvumao-.

Viulize: Ni nani araukaye na mapema kuzitema mbuga na kuzilaza?
Viulize: Ni nani akweaye minazi tangu kuchapo hadi lingiapo giza?
Viulize: Ni nani abebeshwaye mizigo hadi maungo yakageuka shaza?
Halfuye hana faida moja apatay wala malipo yanayotosheleza-
Isipokuwa kusundugwa na kutupiwa matambara na vyakula viliyooza?
Viulize: Ni nani huyo ni nani!

Viulize: Ni nani aliyemaye mashamba na kuyapoliliya?
Na mimea kochokocho ikajaa kwa uzito ikajinamiya?
Hatimaye nani atajirikaye mali yakammiminikiya
Akatoa na kitambi kama mja mzito wa miezi tisiya
Na akaongeza magari na wanawake kutoka na kuingiya?
Viulize: Ni nani huyo nani

Na hao ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao
Nayo hiyo mito kwa furaha maji itirikao
Na huo upepo mkali wenye ghadhabu uvumao
Vyote hivyo vitatu vitakujibu kawa umoja wao
“Ni Kibaruwa Manamba ndiye mtendaji hayo!”

a) Eleza dhamira ya shairi hili.
b) Kwa kutoa mifano, eleza aina mbili za idhini ya kishairi alizotumia mshairi
c) kwa kurejelea ubeti wa tatu taja na ueleze tamathali ya usemi na mbinu ya kimuundo mshairi aliyoitumia

  

Answers


Kavungya
(a) Maisha ya wafanyakazi na vibarua shambani ni duni na ilhali wanaofaidika
ni wengine

(b)(i) Tabdila- mvuwa, kibarua, tisiya
(ii) Lahaja – mte, kutipuza, mtilizi
(iii) Mazida- tisiya
(iv) Inkisari – ikijinamiya, lingiapo
(v) Kuboronga sarufi – uuliza na upepo

(c)(i) Tamathali za usemi
(ii) Tahishishi/ uhuishi – ndege watambuizao, upepo uvumao kwa ghadhabu, mito
itiririkayo kwa furaha
(iii) Taswira – maji itiririkao, upepo mkali wa ghadhabu uvumao
(iv) Takriri/ uradidi- waulize, iulize, uulize
Kavungya answered the question on June 29, 2019 at 07:10


Next: RIWAYA S.A MOHAMED: UTENGANO “ Katu asingajitia kibuibui na kutanga na njia. Lo, kachoshwa na shimiri za baruti anazoshindiliwa moyoni mwake.” a) eleza muktadha wa dondoo hili. b) taja na...
Previous: A riddle question

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • ISIMU JAMII Eleza majukumu matano matano ya Kiswahili kama lugha ya Kitaifa na Kimataifa.(Solved)

    ISIMU JAMII
    Eleza majukumu matano matano ya Kiswahili kama lugha ya Kitaifa na Kimataifa.

    Date posted: June 29, 2019.  Answers (1)

  • andika maneno yafuatayo katika kauli zilizoonyeshwa katika mabano Neno Kauli ...(Solved)

    andika maneno yafuatayo katika kauli zilizoonyeshwa katika mabano
    Neno Kauli Jibu
    i) Imba (tendesha) ……………………………………
    ii) choka (tendea) …………………………………………

    Date posted: June 29, 2019.  Answers (1)

  • Andika kinyume cha:Furaha amehamia mjini.(Solved)

    Andika kinyume cha:
    Furaha amehamia mjini.

    Date posted: June 29, 2019.  Answers (1)

  • Kanusha sentensi ifuatayo. Hapo napo ndipo nitakapo.(Solved)

    Kanusha sentensi ifuatayo.
    Hapo napo ndipo nitakapo.

    Date posted: June 29, 2019.  Answers (1)

  • Huku ukitoa mifano mwafaka onyesha matumizi mawili ya kinyota(*) katika sarufi ya Kiswahili.(Solved)

    Huku ukitoa mifano mwafaka onyesha matumizi mawili ya kinyota(*)
    katika sarufi ya Kiswahili.

    Date posted: June 29, 2019.  Answers (1)

  • Andika kw msemo halisi: Baba alipotuuliza kama tungependa kwenda Mombasa wakati wa likizo tulimjibu kwamba tulitaka kwenda Kisumu kwa kuwa tulikuwa hatujaliona Ziwa Victoria.(Solved)

    Andika kw msemo halisi: Baba alipotuuliza kama tungependa kwenda
    Mombasa wakati wa likizo tulimjibu kwamba tulitaka kwenda Kisumu
    kwa kuwa tulikuwa hatujaliona Ziwa Victoria.k

    Date posted: June 29, 2019.  Answers (1)

  • Iandike tena sentensi ifuatayo bila kutumia vitenzi visaidizi Wachezaji huenda wakawa wanaweza kushinda mchezo wa leo.(Solved)

    Iandike tena sentensi ifuatayo bila kutumia vitenzi visaidizi
    Wachezaji huenda wakawa wanaweza kushinda mchezo wa leo.

    Date posted: June 29, 2019.  Answers (1)

  • Andika ukubwa wa sentensi: Ndovu wa Kiafrika ameharibu kichaka(Solved)

    Andika ukubwa wa sentensi:
    Ndovu wa Kiafrika ameharibu kichaka

    Date posted: June 29, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha sentensi sahili zilizo katika sentensi mseto ifuatayo: Hamali ambaye ameugua alisema kuwa angekwenda hospitali jana(Solved)

    Bainisha sentensi sahili zilizo katika sentensi mseto ifuatayo:
    Hamali ambaye ameugua alisema kuwa angekwenda hospitali jana

    Date posted: June 29, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi ukitumia kielezi cha jinsi cha nomino ifuatayo: Uganda(Solved)

    Tunga sentensi ukitumia kielezi cha jinsi cha nomino ifuatayo:
    Uganda

    Date posted: June 29, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana mbili za sentensi: Kiharusi chake kimewaitia hofu.(Solved)

    Eleza maana mbili za sentensi:
    Kiharusi chake kimewaitia hofu.

    Date posted: June 29, 2019.  Answers (1)

  • Onyesha shadda katika maneno mawili yafuatayo: i) Malaika ii) Nge(Solved)

    Onyesha shadda katika maneno mawili yafuatayo:
    i) Malaika
    ii) Nge

    Date posted: June 29, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi sahihi ukitumia –fa- katika hali ya mazoa.(Solved)

    Tunga sentensi sahihi ukitumia –fa- katika hali ya mazoa.

    Date posted: June 29, 2019.  Answers (1)

  • Tambua sauti ambazo si za ufizi katika sauti hizi. M, t, n, z, gh.(Solved)

    Tambua sauti ambazo si za ufizi katika sauti hizi.
    M, t, n, z, gh.

    Date posted: June 29, 2019.  Answers (1)

  • Chora vielelezo matawi vya sentensi ifuatayo: Bakari, Roda na Hirsi wamefurahi kupita mtihani.(Solved)

    Chora vielelezo matawi vya sentensi ifuatayo:
    Bakari, Roda na Hirsi wamefurahi kupita mtihani.

    Date posted: June 29, 2019.  Answers (1)

  • Tumia visawe vya maneno yaliyopigwa mstari kuandika tena sentensi ifuatayo: Ukuta umemweumiza mvulana alipokuwa akiuparaga(Solved)

    Tumia visawe vya maneno yaliyopigwa mstari kuandika tena sentensi ifuatayo:
    Ukuta umemweumiza mvulana alipokuwa akiuparaga

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi mbili zifuatazo kama sentensi moja kwa kutumia kiwakilishi kirejeshi. i) duka la Bahati lina bidhaa nyingi ii) Juma anafanya kazi katika duka la Bahati.(Solved)

    Andika sentensi mbili zifuatazo kama sentensi moja kwa kutumia
    kiwakilishi kirejeshi.
    i) duka la Bahati lina bidhaa nyingi
    ii) Juma anafanya kazi katika duka la Bahati.

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • MUHTASARI Utaifa ni mshikamano wa hisia zinazowafungamanisha watu wanaoishi katika taifa moja. Taif huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na ambao wanajitambua kisiasa kama watu wenye mwelekeo,...(Solved)

    MUHTASARI
    Utaifa ni mshikamano wa hisia zinazowafungamanisha watu wanaoishi katika
    taifa moja. Taif huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na ambao wanajitambua
    kisiasa kama watu wenye mwelekeo, mwono na hatima sawa. Utaifa umejengwa kwenye
    hisia za mapenzi kwenye hisisia za mapenzi kwa nchi na utambuzi wa kwamba rangi,
    cheo, hadhi, eneo, kabila au tofauti nyinginezo baina ya watu wanaoishi katika nchi moja
    si sbabu ya kuwatenganisha.

    Nchi moja huweza kuwa na watu wa makabila tofauti, wenye matabaka ya kila nui na
    mawazo ainat. Watu hao wanapotambua kuwa kuna sherisi nyinyine inayowaunganisha
    kama fahari ya kuwa watu waochi hiyo, falsafa na imani sawa ambayo ishara yake kuu ni
    winbo wa taifa na kuwa tofauti kati yao muhimu huwa wamefikia kuunda taifa.

    Mhili mkuu wa utaifa ni uzalendo. Uzaleno ni mapenzi makubwa aliyo nayo mtu kwa
    nchi yake. Malezi haya ndiyo yanyoongoza matendo yake, matamanio yake, mawazo
    yake, itikadi yake mwonoulimwengu wake na muhimu zaidi mkabala wake kuihusu nchi
    yake na hatima ya nchi yenywe. Uzalendo ni nguzo muhimu sana ya taifa. Mzalendo
    hawezi kuyatenda mambo yanayoweza kuletea mkama nchi yake.

    Matendo ya mzalendo huangazwa na mwenge wa mema anayoitakia nchi au taifa lake.
    Hawezi kushiriki kwenye harakati na amali ambazo zinahujumu au kufumua
    mshikamano wa taifa zima au kutawaliwa na kitiba cha kutaka kujinufaisha yeye
    mwenyewe au jamii yake finyu. Matendo ya mzalendo wa kitaifa yanaongozwa na
    mwelekeo wa kuiboresha nchi yake. Swali linalomwongoza mtu huyo ni: nimeifanyia
    nini nchi yangu au taifa lahgu? Alhasili mtu anayeipenda nchi yake hawezi kuongozwa
    na umero wa kibinafsi tu wa kujilimbikia mali, ujiri au pesa. Yuko radhi kuhasirika
    kama mtu binafsi ili taifa au nchi yake inufaike.

    Utaifa ni mche aali ambao unapaliliwa kwa uzalendo, kuepuka hawaa za nafsi, kusinywa
    na taasubi za kikabila na kuach tama ya kujinufaiha. Hali hiyo inapofikiwa, hatima ya
    wanajamii wa taifa linahusika huwa nzuri na mustakabali wao na wa vizazi vyao huwa
    wa matumaini makubwa.

    a) Dondoa sifa kuu za utaifa. (maneno 40- 50)
    b) kwa kutumia maneno kati ya 60-70, onyesho misingi ya kumtathmini mzalendo.

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • UFAHAMU Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Wanasaikolojia wanabainisha kati ya sehemu mbili kuu katika akili ya binadamu: Ung’amuzi na ung’amuzibwete. Ung’amuzi ni sehemu ya ubongo ambayo kimsingi hupanua...(Solved)

    UFAHAMU
    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
    Wanasaikolojia wanabainisha kati ya sehemu mbili kuu katika akili ya binadamu:
    Ung’amuzi na ung’amuzibwete. Ung’amuzi ni sehemu ya ubongo ambayo kimsingi
    hupanua na kudadavua yanayotendeka hususan mchana. Ung’amuzibwete ni
    kibinimethali chake; hufanya kazi wakati binadamu anapolemazwa na usingizi. Baadhi
    ya mambo anayoshuhudia binadamu mchana yanaingia kwenye ung’amuzibwete wake na
    kutokeza katika ndoto zake usiku.

    Kwa mujibu wa mawazo ya Sigmund freud, mwanasaikolojia wa jadi anayechukuliwa
    nawengi kama mwasisi wa taaluma ya saikolojia, mambo yanayopatikana katika
    unga’amuzibwete mambo yana sifa hasi. Freud alidahili kuwa binadamu huyaficha na
    kuyabania kwenye ung’amuzibwete mambo ambayo hawezi juyasema kadamnasi.
    Alieleza kuwa matamanio yasiyokubalika, makatazo ya jamii, fikra na kauli
    zilizoharamishwa na miko ya kijamii hubanwa katika ung’amuzibwete. Shehena hiyo
    ndiyo inayochipuza kwa njia ya ishara za ndoto, mitelezo ya kauli, yaani maneno au kauli
    zinazotukoka bila wenye kukusudia, ishara na lugha ya kitamathali katika uandishi wa
    kibunifu na kadhalika.

    Ung’amuzibwete un uwezo mkubwa wa kuathiri matendo ya binadamu. Huu ndio
    msingi unaowafanya wanasaikolojia wengi, akiwepo freud, kusema kuwa tajiriba ya
    motto inaweza kufichwa kwenye sehemu hiyo na hatimaye kuishia kutokeza katika utu
    uzima wake. Kwa kuwa tunapoingiliana na binadamu wenzetu kila siku
    tunayang’amuzibwete unapotawala binadamu wenzetu watashindwa kutuelewa. Hii
    ndiyo hali anayokuwa nayo mwendawazimu. Ung’amuzibwete wake hutawala. Sisi
    tunaotawaliwa na ung’amuzi tunashindwa kumwelewa; naye bila shaka anashindwa
    kutuelewa.

    Carl Gustav Jung, aliyewahi kuwa mwanafunzi wa Freud, aliupinga mwelekeo wa Freud
    wa kuungalia ung’amuzibwete kama jaa la mawazo mabaya, matamanio, nia, fikira tuli
    na dhana ambazo ni hasi. Jung alizuka na dhana mbili muhimu: Ung’amuzibwete wa
    kibinafsi na un’gabuzibwete jumuishi. Alisema mambo, fikra na uzoefu wowote mbaya
    unaomuhusu mtu binafsi . Dhana ya ung’a muzibwete jumuishi aliitumia kuelezea
    sehemu ya akili ya binadamu ambayo inamfanya ayatende matendo Fulani kama
    binadamu wenzake licha ya tofauti zao kiwakati na kijiografia. Kwa mfano, binadamu
    wengi wana sherehe za kuzaliwa motto, kuoza, ibada au mviga unaohusiana na kifo licha
    ya tofauti zao. Jung alisema kuwa kinachochochea hali hii ni urithi Fulani wa kila
    mwanadamu. Urithi huo unapatikana katika ung’amuzibwete jumuishi.

    Upo mwafikiano kati ya wataalamu hawa wawili kuwa ung’auzibwete una uwezo wa
    kuathiri ung’amuzi matendo ya binadamu ya king’amuzi. Wanasaikolojia wanashikilia kuwa binadamu hawezi kukamilika bila kuzihusisha sehemu zote mbile kwa sababu
    zinaathiriana.

    a) Kwan in ung’amuzibwete unaelezwa kama kinyme cha ung’amuzi?
    b) Eleza mtazamo wa Freud kuhusu ung’amuzibwete.
    c) Kwa mujibu wa Freud yaliyomo kwenye ung’amuzibwete hudhihirika vipi?
    d) Eleza tofauti ya mawazo kati ya Sigmund Freud na Carl Gustav Jung.
    e) taja hoja inayowafungamanisha Jung na Freud.

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)

  • ISIMU JAMII Soma kifungu kifuatacho ujibu maswali yanayofuata. Kwa mujibu wa sheria kifungu nambari 3 sehemu ya A ya sheri za nchi, umepatikana na hatia ya kutatiza utulivu...(Solved)

    ISIMU JAMII
    Soma kifungu kifuatacho ujibu maswali yanayofuata.
    Kwa mujibu wa sheria kifungu nambari 3 sehemu ya A ya sheri za nchi, umepatikana na
    hatia ya kutatiza utulivu wa raia wapenda amani kwa kuwatusi na kutisha kuwapiga.
    Kiongozi wa mashtaka amethibitisha haya wa kuwaleta mashahidi ambao wametoa
    ushahidi usiotetereka kuhusu vitendo vyako katika tukio hilo. Korti hii imeonelea una
    hatia na imeamuru ufungwe jela kwa muda wa miaka miwili bila faini ili liwe funzo
    kwako na kwa wenzako wenye tabia kama zako. Una majuma mawili kukata rufani.

    a) Lugha iliyo katika kifungu hiki hutumika katika muktadha upi?
    b) Toa ushaidi wa jibu lako
    c) Zaidi ya sifa zilizo katika kifungu hiki, eleza sifa zingine sita za matumizi ya
    ligha katika muktadha huu.

    Date posted: June 28, 2019.  Answers (1)