Mzizi wa neno ni neno la msingi kabisa ambalo haungezewa vipengele vingine ili kuunda mawasiliano.
ghanadavid answered the question on July 11, 2019 at 16:40
- State the contributions of parastatals to the economic development of Kenya.(Solved)
State the contributions of parastatals to the economic development of Kenya.
Date posted: July 2, 2019. Answers (1)
- USHAIRI
Soma shairi kisha ujibu maswali yanayofuata:
KIBARUWA: Abdilatif Abdalla
Kwenye shamba hilo kubwa asilani hakunyi mvuwa!
Ni kwa mitilizi ya jasho langu ndiyo hunweshezewa
Kwenye shamba hilo kubwa sasa...(Solved)
USHAIRI
Soma shairi kisha ujibu maswali yanayofuata:
KIBARUWA: Abdilatif Abdalla
Kwenye shamba hilo kubwa asilani hakunyi mvuwa!
Ni kwa mitilizi ya jasho langu ndiyo hunweshezewa
Kwenye shamba hilo kubwa sasa imeshaiva kahawa
Na bunize ni matone ya damu yangu niliyotowa
Ndipo mte ukatipuza!
Buni hiyo itakaangwa buni hiyo itapondwapondwa
Buni hiyo itasagwa na buni hiyo itafyondwafyondwa
Bali itabaki nyeusi kama ngozi yangu Kibaruwa
Waulize ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao
Iulize na mito kwa furaha maji itiririkao
Uulize na upepo mkali kwa ghadhabu uvumao-.
Viulize: Ni nani araukaye na mapema kuzitema mbuga na kuzilaza?
Viulize: Ni nani akweaye minazi tangu kuchapo hadi lingiapo giza?
Viulize: Ni nani abebeshwaye mizigo hadi maungo yakageuka shaza?
Halfuye hana faida moja apatay wala malipo yanayotosheleza-
Isipokuwa kusundugwa na kutupiwa matambara na vyakula viliyooza?
Viulize: Ni nani huyo ni nani!
Viulize: Ni nani aliyemaye mashamba na kuyapoliliya?
Na mimea kochokocho ikajaa kwa uzito ikajinamiya?
Hatimaye nani atajirikaye mali yakammiminikiya
Akatoa na kitambi kama mja mzito wa miezi tisiya
Na akaongeza magari na wanawake kutoka na kuingiya?
Viulize: Ni nani huyo nani
Na hao ndege kwa nyimbo nyanana watutumbuizao
Nayo hiyo mito kwa furaha maji itirikao
Na huo upepo mkali wenye ghadhabu uvumao
Vyote hivyo vitatu vitakujibu kawa umoja wao
“Ni Kibaruwa Manamba ndiye mtendaji hayo!”
a) Eleza dhamira ya shairi hili.
b) Kwa kutoa mifano, eleza aina mbili za idhini ya kishairi alizotumia mshairi
c) kwa kurejelea ubeti wa tatu taja na ueleze tamathali ya usemi na mbinu ya kimuundo mshairi aliyoitumia
Date posted: June 29, 2019. Answers (1)
- ISIMU JAMII
Eleza majukumu matano matano ya Kiswahili kama lugha ya Kitaifa na Kimataifa.(Solved)
ISIMU JAMII
Eleza majukumu matano matano ya Kiswahili kama lugha ya Kitaifa na Kimataifa.
Date posted: June 29, 2019. Answers (1)
- andika maneno yafuatayo katika kauli zilizoonyeshwa katika mabano
Neno Kauli ...(Solved)
andika maneno yafuatayo katika kauli zilizoonyeshwa katika mabano
Neno Kauli Jibu
i) Imba (tendesha) ……………………………………
ii) choka (tendea) …………………………………………
Date posted: June 29, 2019. Answers (1)
- Andika kinyume cha:Furaha amehamia mjini.(Solved)
Andika kinyume cha:
Furaha amehamia mjini.
Date posted: June 29, 2019. Answers (1)
- Kanusha sentensi ifuatayo.
Hapo napo ndipo nitakapo.(Solved)
Kanusha sentensi ifuatayo.
Hapo napo ndipo nitakapo.
Date posted: June 29, 2019. Answers (1)
- Huku ukitoa mifano mwafaka onyesha matumizi mawili ya kinyota(*)
katika sarufi ya Kiswahili.(Solved)
Huku ukitoa mifano mwafaka onyesha matumizi mawili ya kinyota(*)
katika sarufi ya Kiswahili.
Date posted: June 29, 2019. Answers (1)
- Andika kw msemo halisi: Baba alipotuuliza kama tungependa kwenda
Mombasa wakati wa likizo tulimjibu kwamba tulitaka kwenda Kisumu
kwa kuwa tulikuwa hatujaliona Ziwa Victoria.(Solved)
Andika kw msemo halisi: Baba alipotuuliza kama tungependa kwenda
Mombasa wakati wa likizo tulimjibu kwamba tulitaka kwenda Kisumu
kwa kuwa tulikuwa hatujaliona Ziwa Victoria.k
Date posted: June 29, 2019. Answers (1)
- Iandike tena sentensi ifuatayo bila kutumia vitenzi visaidizi
Wachezaji huenda wakawa wanaweza kushinda mchezo wa leo.(Solved)
Iandike tena sentensi ifuatayo bila kutumia vitenzi visaidizi
Wachezaji huenda wakawa wanaweza kushinda mchezo wa leo.
Date posted: June 29, 2019. Answers (1)
- Andika ukubwa wa sentensi:
Ndovu wa Kiafrika ameharibu kichaka(Solved)
Andika ukubwa wa sentensi:
Ndovu wa Kiafrika ameharibu kichaka
Date posted: June 29, 2019. Answers (1)
- Bainisha sentensi sahili zilizo katika sentensi mseto ifuatayo:
Hamali ambaye ameugua alisema kuwa angekwenda hospitali jana(Solved)
Bainisha sentensi sahili zilizo katika sentensi mseto ifuatayo:
Hamali ambaye ameugua alisema kuwa angekwenda hospitali jana
Date posted: June 29, 2019. Answers (1)
- Tunga sentensi ukitumia kielezi cha jinsi cha nomino ifuatayo:
Uganda(Solved)
Tunga sentensi ukitumia kielezi cha jinsi cha nomino ifuatayo:
Uganda
Date posted: June 29, 2019. Answers (1)
- Eleza maana mbili za sentensi:
Kiharusi chake kimewaitia hofu.(Solved)
Eleza maana mbili za sentensi:
Kiharusi chake kimewaitia hofu.
Date posted: June 29, 2019. Answers (1)
- Onyesha shadda katika maneno mawili yafuatayo:
i) Malaika
ii) Nge(Solved)
Onyesha shadda katika maneno mawili yafuatayo:
i) Malaika
ii) Nge
Date posted: June 29, 2019. Answers (1)
- Tunga sentensi sahihi ukitumia –fa- katika hali ya mazoa.(Solved)
Tunga sentensi sahihi ukitumia –fa- katika hali ya mazoa.
Date posted: June 29, 2019. Answers (1)
- Tambua sauti ambazo si za ufizi katika sauti hizi.
M, t, n, z, gh.(Solved)
Tambua sauti ambazo si za ufizi katika sauti hizi.
M, t, n, z, gh.
Date posted: June 29, 2019. Answers (1)
- Chora vielelezo matawi vya sentensi ifuatayo:
Bakari, Roda na Hirsi wamefurahi kupita mtihani.(Solved)
Chora vielelezo matawi vya sentensi ifuatayo:
Bakari, Roda na Hirsi wamefurahi kupita mtihani.
Date posted: June 29, 2019. Answers (1)
- Tumia visawe vya maneno yaliyopigwa mstari kuandika tena sentensi ifuatayo:
Ukuta umemweumiza mvulana alipokuwa akiuparaga(Solved)
Tumia visawe vya maneno yaliyopigwa mstari kuandika tena sentensi ifuatayo:
Ukuta umemweumiza mvulana alipokuwa akiuparaga
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- Andika sentensi mbili zifuatazo kama sentensi moja kwa kutumia
kiwakilishi kirejeshi.
i) duka la Bahati lina bidhaa nyingi
ii) Juma anafanya kazi katika duka la Bahati.(Solved)
Andika sentensi mbili zifuatazo kama sentensi moja kwa kutumia
kiwakilishi kirejeshi.
i) duka la Bahati lina bidhaa nyingi
ii) Juma anafanya kazi katika duka la Bahati.
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)
- MUHTASARI
Utaifa ni mshikamano wa hisia zinazowafungamanisha watu wanaoishi katika
taifa moja. Taif huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na ambao wanajitambua
kisiasa kama watu wenye mwelekeo,...(Solved)
MUHTASARI
Utaifa ni mshikamano wa hisia zinazowafungamanisha watu wanaoishi katika
taifa moja. Taif huundwa na watu wanaoishi katika nchi moja na ambao wanajitambua
kisiasa kama watu wenye mwelekeo, mwono na hatima sawa. Utaifa umejengwa kwenye
hisia za mapenzi kwenye hisisia za mapenzi kwa nchi na utambuzi wa kwamba rangi,
cheo, hadhi, eneo, kabila au tofauti nyinginezo baina ya watu wanaoishi katika nchi moja
si sbabu ya kuwatenganisha.
Nchi moja huweza kuwa na watu wa makabila tofauti, wenye matabaka ya kila nui na
mawazo ainat. Watu hao wanapotambua kuwa kuna sherisi nyinyine inayowaunganisha
kama fahari ya kuwa watu waochi hiyo, falsafa na imani sawa ambayo ishara yake kuu ni
winbo wa taifa na kuwa tofauti kati yao muhimu huwa wamefikia kuunda taifa.
Mhili mkuu wa utaifa ni uzalendo. Uzaleno ni mapenzi makubwa aliyo nayo mtu kwa
nchi yake. Malezi haya ndiyo yanyoongoza matendo yake, matamanio yake, mawazo
yake, itikadi yake mwonoulimwengu wake na muhimu zaidi mkabala wake kuihusu nchi
yake na hatima ya nchi yenywe. Uzalendo ni nguzo muhimu sana ya taifa. Mzalendo
hawezi kuyatenda mambo yanayoweza kuletea mkama nchi yake.
Matendo ya mzalendo huangazwa na mwenge wa mema anayoitakia nchi au taifa lake.
Hawezi kushiriki kwenye harakati na amali ambazo zinahujumu au kufumua
mshikamano wa taifa zima au kutawaliwa na kitiba cha kutaka kujinufaisha yeye
mwenyewe au jamii yake finyu. Matendo ya mzalendo wa kitaifa yanaongozwa na
mwelekeo wa kuiboresha nchi yake. Swali linalomwongoza mtu huyo ni: nimeifanyia
nini nchi yangu au taifa lahgu? Alhasili mtu anayeipenda nchi yake hawezi kuongozwa
na umero wa kibinafsi tu wa kujilimbikia mali, ujiri au pesa. Yuko radhi kuhasirika
kama mtu binafsi ili taifa au nchi yake inufaike.
Utaifa ni mche aali ambao unapaliliwa kwa uzalendo, kuepuka hawaa za nafsi, kusinywa
na taasubi za kikabila na kuach tama ya kujinufaiha. Hali hiyo inapofikiwa, hatima ya
wanajamii wa taifa linahusika huwa nzuri na mustakabali wao na wa vizazi vyao huwa
wa matumaini makubwa.
a) Dondoa sifa kuu za utaifa. (maneno 40- 50)
b) kwa kutumia maneno kati ya 60-70, onyesho misingi ya kumtathmini mzalendo.
Date posted: June 28, 2019. Answers (1)