Ni hatua gani ambazo serikali imechukua katika kuimarisha afya ya umma?

      

Ni hatua gani ambazo serikali imechukua katika kuimarisha afya ya umma?

  

Answers


Maurice
(i) Serikali, imeongeza vituo vya kufunzia madaktari na wauguzi.

(ii) Serikali imeendeleza wizara ya afya inayoimarisha afya chini ya uongozi wa waziri wa
afya.

(iii) Serikali, kupitia kwa uwiano wa wafanyikazi (C.B.A.) wameongezea madaktari na
wauguzi mshahara na marupurupu.

(iv) Serikali inawachunguza wageni wanaoingia nchini ili wasilete magonjwa sugu kama
Ebola.

(v) Serikali imeimarisha mazingira ili kuzuia magonjwa sugu kama Malaria.

(vi) Serikali inachunguza hospitali za kibinafsi ili wasiwape wagonjwa huduma duni.

(vii) Kulipia wanafunzi wote bima ya N.H.I.F


(viii) Kulipia kina mama wanapojifungua – Linda mama.

(ix) Kuongezea majumba ya kujifungulia.

(x) Kufungua zahanati mbalimbali huko vijijini na kuhakikisha kuwa wanapata dawa bila
malipo.

(xi) Wamenunua vifaa mbalimbali vya kuchunguza magonjwa.

(xii) Serikali inatuma dawa katika hospitali za umma.

(xiii) Serikali imehamasisha raia kuhusu umuhimu wa kuwa na bima.

(xiv) Serikali imeongeza ambulensi za kusafirisha wagonjwa mahututi.

(xv) Serikali imeongeza vyumba na vifaa vya kufanyia upasuaji.

(xvi) Serikali imeanzisha vituo vya kushughulikia na kuhamasisha wagonjwa wenye
magonjwa sugu kama kansa.
maurice.mutuku answered the question on August 2, 2019 at 05:27


Next: Discuss the various types of organizational resources and capabilities
Previous: Toa anwani mwafaka kwa taarifa hii.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions