Toa anwani mwafaka kwa taarifa hii.

      

HABARI zisizoridhisha kuhusu shambulizi la kigaidi katika kituo cha biashara cha Westgate, Kaunti ya
Nairobi ambapo watu wapatao 67 waliaga dunia na wengine zaidi ya 175 wakaachwa na majeraha,
zinaendelea kufichuka. Magazeti yaliangazia habari kwamba mawaziri wanne pamoja na maafisa wakuu
wa usalama nchini walipashwa habari za kijasusi kuhusu mipango ya magaidi wa Al-Shabaab kutekeleza
shambulizi hilo. Inadaiwa kwamba viongozi hao hawakuchukua hatua za kuzuia shambulizi hilo.


Habari zaidi zilieleza kwamba kituo hicho kilikuwa kinafanyiwa uchunguzi na idara ya Kitaifa ya Ujasusi
(NIS) kabla ya kushambuliwa na magaidi. Imeripotiwa kwamba wachunguzaji wa ujasusi walikuwa
katika kituo hicho masaa machache kabla ya magaidi hao kufika na kuanza kuwafyatulia risasi walinda
usalama, wateja na wafanyabiashara. Inadaiwa wachunguzaji hao 'waliwasiliana' na maafisa wa polisi
wanaoshika doria mara kwa mara katika kituo hicho ambacho kimetajwa kuwa miongoni mwa maeneo
muhimu sana jijini Nairobi.

Habari hizi zote zinawapa Wakenya ujumbe mmoja; kwamba baadhi ya maafisa wakuu na idara za
serikali zilizembea katika majukumu yao ya kuwahakikishia Wakenya na wageni wote wanaozuru Kenya,
usalama. Ingawa hatupingi kwamba maafisa hao wanapaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa
kuzembea kazini, jambo muhimu ambalo Wakenya wanataka sasa si lawama bali hakikisho kwamba
maisha yao hayapo hatarini wanapoendelea na shughuli zao za kila siku za kuijenga nchi.

Vitisho vilivyotolewa na magaidi hao ambao wamesema wanapanga kutekeleza mashambulizi mengine
ndivyo vinavyowakosesha Wakenya Usingizi. Wahenga walisema tusahau yaliyopita na tugange yajayo.
Serikali inapaswa kutumia shambulizi la Westgate kama funzo litakalozifanya idara zake za usalama
kuamka usingizini na kuhakikisha kwamba Wakenya wasio na hatia hawapotezi tena maisha yao katika
mashambulizi kama haya.

Lakini mbona Wakenya nao wasianze kuuthamini usalama wao wenyewe? Hali ya usalama nchini
itaimarika maradufu kama Wakenya wote watachakua jukumu la kuwajua vyema majirani wao na
kuripoti jambo lolote lisilo la kawaida kwa maafisa wa usalama.


Shambulizi hili lingezuiwa kama Wakenya wangekuwa na mazoea ya kutaka kuwafahamu vyema watu
wanaoishi karibu nao kwani inadaiwa kwamba magaidi hawa waliwasili nchini kitambo na kukodisha
nyumba ambako waliendeleza mipanga yao. Badala ya kuwalimbikizia lawama polisi, mbona tusishikane
nao ili kuhakikisha kwamba watu wenye nia mbaya mitaani mwetu wanakamatwa na kuchukuliwa hatua
za kisheria?



Toa anwani mwafaka kwa taarifa hii.

  

Answers


Maurice
Shambulizi la kigaidi Ugaidi Shambulizi la Westgate Mkasa wa Westgate
maurice.mutuku answered the question on August 2, 2019 at 05:41


Next: Ni hatua gani ambazo serikali imechukua katika kuimarisha afya ya umma?
Previous: Taja maafa yaliyosababishwa na tukio linalorejelewa.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions