Huku ukitoa mifano mwafaka ,eleza miundo tano ya methali.

      

Huku ukitoa mifano mwafaka ,eleza miundo tano ya methali.

  

Answers


Maurice
(i) Sitiari-ahadi ni deni.

(ii) Tashbihi-usilolijua ni kama usiku wa giza

(iii) Tashhisi-paka akiondoka panya hutawala.

(iv) Takriri- chovya chovya humaliza buyu la asali.

(v) Swali balagha- mla ni mla leo mla jana kalani?

(vi) Taswira-mpanda farasi wawili hupasuka msamba.

(vii) Chuku- mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi.

(viii) Tanakali za sauti- chururu si ndondondo!

(ix) Kinaya- kwenye miti hakuna wajenzi.

(x) Kejeli-ucha mungu si kilemba cheupe

(xi) Jazanda-kupanda mchongoma kushuka ndio kazi.

(xii) Kweli kinzani-wagombanao ndio wapatanao.

(xiii) Taashira- kuku mgeni hakosi Kamba mguuni.
maurice.mutuku answered the question on August 3, 2019 at 09:01


Next: Define Service
Previous: Eleza tofauti nne kati ya methali na vitendawili.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions