Eleza tofauti nne kati ya methali na vitendawili.

      

Eleza tofauti nne kati ya methali na vitendawili.

  

Answers


Maurice
(i) Vitendawili huwa na fomula maalum ya uwasilishaji ilhali methali hazina.

(ii) Fumbo la vitendawali lazima lifumbuliwe papo hapo ilihali la methali halifumbuliwi papo hapo.

(iii) Vitendawili ni maarufu miongoni mwa watoto na vijana ilhali methali ni kwa watu wazima au wazee ili kuonyesha hekima.


(iv) Vitendawili hutolewa katika vikao maalum ilhali methali si lazima zitengewe vikao.

(v) Hadhira ya vitendawili huwa tendi ilhali ya methali huwa tuli.
maurice.mutuku answered the question on August 3, 2019 at 09:03


Next: Huku ukitoa mifano mwafaka ,eleza miundo tano ya methali.
Previous: Eleza umuhimu wa semi katika jamii.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions