Maovu yametamalaki katika jamii ya Riwaya ya Chozi la Heri, tetea kauli hii kwa kutolea hoja kumi.

      

Maovu yametamalaki katika jamii ya Riwaya ya Chozi la Heri, tetea kauli hii kwa kutolea hoja kumi.

  

Answers


Maurice
(i) Biashara haramu kama ile ya uuzaji wa dawa za kulevya- Dick alipotekwa nyara alilazimika kuuza dawa za kulevya kwa muda wa miaka kumi.


(ii) Kuna ukabila-unajitokeza kikamilifu wakati kulizuka vita vya baada ya kutawazwa.
Majirani waliwageuka wenzao ambao walikuwa wametoka katika kabila au ukoo tofauti.

(iii) Mauaji- watu wengi waliwapoteza wapendwa wao kutokano na migogoro iliyozuka baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya.

(iv) Matumizi ya pombe haramu-vijana wa vyuo vikuu wanabugia pombe hii ya sumu inayowafanya wengine kuiaga dunia.


(v) Ukeketaji wa watoto wa kike- wasichana wa Shule ya msingi wanapitishwa tohara.
Wasichana wengine wanayapoteza maisha yao huku wengine wakiponea chupuchupu na kuwa hospitalini kwa mfano Tuama.

(vi) Ndoa za mapema- wasichana wachanga wanalazimishwa kuolewa na vizee na kuacha masomo yao.


(vii) Uporaji wa mali ya wengine- wakati vita vya baada ya kutawazwa kuzuka, watu walionekano kupora maduka ya Kihindi, Kiarabu na hata ya Waafrika wenzao.


(viii) Wanawake huavya mimba- Sauna alipachikwa mimba na babake mlezi.
Mamake mzazi alimsaidia kuavya kisha akamwonya dhidi ya kumwambia yeyote kuhusu unyama wa babake.


(ix) Wazazi wanahusiana kimapenzi na watoto wao- Sauna alipachikwa mimba na babake mlezi.
Mamake mzazi alimsaidia kuavya kisha akamwonya dhidi ya kumwambia yeyote kuhusu unyama wa babake.


(x) Kutupwa kwa watoto wadogo
maurice.mutuku answered the question on August 3, 2019 at 09:42


Next: Ni mambo gani yaliyowakumba wale ambao kitovu chao si hicho?
Previous: Eleza mbinu kumi anazotumia Majoka kuendeleza uongozi wake Sagamoyo.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions