Eleza mbinu kumi anazotumia Majoka kuendeleza uongozi wake Sagamoyo.

      

TAMTHILIA KIGOGO

Eleza mbinu kumi anazotumia Majoka kuendeleza uongozi wake Sagamoyo.

  

Answers


Maurice
(i) Uvumi-Watu wa Majoka wanaeneza uvumi kuwa Sudi na Ashua ndio wanawinda roho ya Tunu.

(ii) Ahadi za uongo-Madai ya Majoka kuwa atatoa chakula kwa wasiojiweza si ya kweli.


(iii) Vitisho-Wanasagamoyo wanatishwa kwa kurushiwa vijikaratasi wahame.
Majoka anatumia polisi kuwatisha wanasagamoyo.


(iv) Mapendeleo.Ashua baada ya kufuzu kutoka chuo kikuu alipewa kazi katika Majoka and Majoka academy akakataa,sasa angekuwa mwalimu mkuu katika mojawapo ya shule za kifahari,viongozi hupendelea wengine kutumia njia zisizo halali.
Majoka alimpa Tunu kazi kiwandani akakataa.

(v) Jela-Viongozi hufungia wanaowapinga jela.
Ashua anatiwa ndani,kuna washukiwa wengi ndani.

(vi) Polisi-Majoka anatumia polisi kutawanya waandamanaji wanaodai haki zao.

(vii) Ulaghai- Majoka anapanga kuongeza mishahara ya walimu na wauguzi kwa aslimia kidogo kisha apandishe kodi.

(viii) Kudhibiti vyombo vya dola.
Majoka anapanga kufunga vituo vya runinga sagamoyo ili abaki na vichache anavyotaka vya kutangaza habari anazotaka.

(ix) Wavamizi-Majoka anatumia wavamizi,Tunua na anaumizwa mfupa wa muundi,Siti ana majeraha kutokana na uvamizi.


(x) Ulinzi mkali-Majoka na watu wake wana ulinzi mkali.
Kenga anawalinzi,Majoka analindwa na maafisa wa polisi.

(xi) Kufuta kazi wasiomuunga-Majoka anamfuta kazi kingi kwa kutomtii kupiga watu risasi sokoni Chapakazi.
maurice.mutuku answered the question on August 3, 2019 at 09:52


Next: Maovu yametamalaki katika jamii ya Riwaya ya Chozi la Heri, tetea kauli hii kwa kutolea hoja kumi.
Previous: Eleza matumizi ya mbinu zifuatazo katika tamthilia hii:(i) Jazanda(ii) Sadfa(iii) Mbinu rejeshi (iv) Wimbo

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions