Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Eleza matumizi ya mbinu zifuatazo katika tamthilia hii:(i) Jazanda(ii) Sadfa(iii) Mbinu rejeshi (iv) Wimbo

      

TAMTHILIA KIGOGO

Eleza matumizi ya mbinu zifuatazo katika tamthilia hii:

(i) Jazanda

(ii) Sadfa

(iii) Mbinu rejeshi

(iv) Wimbo

  

Answers


Maurice
(a) Jazanda

(i) Kinyago cha shujaaa anachochonga Sudi kwamba shujaa huyo ni mkubwa kuliko jina lake na urembo wa shujaa huyo ni bora zaidi.Shujaa anayerejelewa hapa ni Tunu,yale ambayo anatendea Sagamoyo ni makuu kuliko jina lake,kutetea haki za wanyonge.

(ii) Husda anamwambia Ashua kuwa hawezi kumtoa bonge kinywani hivi hivi.
Bonge na Majoka bwanake Husda kuwa Ashua hawezi kumnyang'anya bwana.

(iii) Husda kumwita Majoka pwagu,pwagu ni mwizi na Majoka amewaibia wanasagamoyo;ananyakua ardhi,anaiba kodi na kuwalaghai wanasagamoyo.


(iv) Husda anamwambia Ashua kuwa ameshindwa kufuga kuku na kanga hatamweza.Kuku ni mumewe Sudi,na Kanga ni Majoka, kwamba Ashua ameshindwa kumtunza Sudi na Majoka hampati.

(v) Tunu kuwekewa vidhibiti mwendo ni kukomeshwa au kuwekewa vikwazo ili afe moyo kutetea haki za wanasagamoyo.

(vi) Majoka anasema kuwa hatatumia bomu kuulia mbu.
Anamrejelea Tunu kuwa mbu kumaanisha hatatumia nguvu nyingi kumwangamiza.

(vii) Majoka anasema ili kuongoza Sagamoyo ni lazima uwe na ngozi ngumu, kumaanisha ni lazima uwe mkali na mwenye nguvu.

(viii) Jukwaa kupakwa rangi kwa ajili ya sherehe ya uhuru ni kufunika uozo ulio Sagamoyo.

(ix) Majoka anaposema salamu zinamngoja Sudi kwake,salamu ni Ashua mkewe aliye ndani ya jela.


(x) Majoka anamshauri Sudi anawe mikono iwapo anataka kula na watu wazima.


(xi) Kunawa mikono ni kukubali kuchonga kinyago ndiposa Ashua mkewe aachiliwe.


(xii) Chopi anamwambia Sudi iwapo shamba limemshinda kulima aseme.
Shamba anayorejelea Ashua kuwa iwapo Ashua amemshinda kutunza, aseme atunziwe na Majoka.

(xiii) Siafu huwa wengi na si rahisi kuwamaliza.
Siafu ni wanasagamoyo ambao ni wengi kuliko Majoka na si rahisi kuwashinda.
Hatimaye raia wanamshinda Majoka.

(xiv) Tunu anasema kuwa moto umewaka na utateketea wasipouzima.
Moto ni harakati za mapinduzi Sagamoyo.
Kuteketea ni kumng`oa Majoka mamlakani.




(b) Sadfa

(i) Majoka akiwa ofisini mwake,Ashua anaingia bila kutarajiwa.

(ii) Ashua akiwa na Majoka ofisini,Husda anaingia bila kutarajiwa,Ashua anamaka nakubakia kinywa wazi.

(iii) Majoka anaposoma gazeti anaona maoni kuwa Tunu awanie uongozi Sagamoyo, hakutarajia kuyaona maoni hayo gazetini.

(iv) Chopi wanapozungumza na Majoka Mwango anafika na habari kuwa Majoka ana wageni,Tunu na Sudi ambao hakutarajia.

(v) Majoka anapongojea Husda katika hoteli ya kifahari Sagamoyo ,Kenga anafika na habari kuwa mipango haikwenda walivyopanga, kuwa Tunu bado yupo, hakuvunjwa miguu,Majoka hatarajii Tunu kuwa mzima.


(vi) Ni sadfa kuwa kifo cha Ngao Junior kutokea sawia na kifo cha Ngurumo.


(vii) Inasadifu kuwa siku ya sherehe ndio waandamanaji wanakuwa na mkutano katika soko la chapa kazi wakati ambapo wanatarajiwa kuhudhuria sherehe.




(c) Mbinu rejeshi

(i) Majoka anakumbuka hadithi kuwa binadamu siku zote humwauni kuku na kumhini kunguru.


(ii) Majoka anarejelea siku Ashua alipokataa pete yake ya uchumba kuwa hiyo ndiyo siku aliyojikosea heshima na sasa hangekuwa ombaomba.


(iii) Majoka anarejelea kisa cha kifo cha Jabali na wafuasi wake,jinsi walivyopanga njama na kumwangamiza.


(iv) Ashua anakumbuka mengi Sudi aliyomwahidi siku zao za kwanza za mapenzi.


(v) Tukio la Mzee Marara kumfukuza Tunu ndotoni ni la zamani,la utotoni.

(vi) Hashima anakumbuka jinsi alivyoathirika na marehemu mume wake.
Mararana watu wake waliwatendea ukatili.

(vii) Sudi akiwa kwa mama pima anakumbuka mashujaa waliofungwa wakati wa ukoloni.
Mashujaa hao waliangaisha wakoloni na hata wengine wakaenda jongomeo.



(d) Wimbo

(i) Wimbo wa uzalenzo.

Wimbo huu unaimbwa katika kituo cha habari cha wazalendo,ni wimbo unaosifu Sagamoyo na kiongozi wake.


(ii) Wimbo wa hashima

Anaimba wimbo huu akiwa nyumbani kwake.
Wimbo huu unaashiria kuwa mambo hubadilika,kila siku wasema heri yalipita jana.


(iii)Wimbo wa mama pima

Ni wimbo wa kishairi unaorejelea Sudi na Tunu.
Mama pima anawashauri wajipe raha kwa kujiunga nao katika ulevi.


(iv) Wimbo wa ngurumo

Ngurumo anaimba wimbo kwa mama pima akimrejelea Tunu.
Ni wimbo wa kumsuta Tunu kwa kuwa yeye ni mwanamke anapaswa kuolewa.



(v) Wimbo wa umati

Umati unaimba wimbo katika lango la soko la chapa kazi.
Watu wanaimba kuwa yote yanawezekana bila Majoka.
Wimbo huu unasifia juhudi za Tunu kuikomboa Sagamoyo na kuleta uhuru halisi.


(vi) Wimbo wa Ashua.

Ashua anaimba kuwa soko lafunguliwa bila chopi kumaanishwa vikaragosi hawana nguvu dhidi ya wanamapinduzi.
maurice.mutuku answered the question on August 3, 2019 at 10:22


Next: Eleza mbinu kumi anazotumia Majoka kuendeleza uongozi wake Sagamoyo.
Previous: Eleza muktadha wa dondoo hili

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions