Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Jadili ufaafu wa anwani: Tumbo lisiloshiba kwenye hadithi hii

      

Jadili ufaafu wa anwani: Tumbo lisiloshiba kwenye hadithi hii

  

Answers


Maurice
Anwani hii imetumika kijazanda kuashiria ile hali ya kutotesheka na alichonacho binadamu

(i) Bwana tumbo anaingia mkahawa wa mzee mago. Anaitisha na kula chakula chote.

(ii) Jiji lina tumbo ambalo halishibi. Jiji limepambwa vyema limejaa mikahawa, departmental stores, casinos lakini linataka kupanua tumbo lake hadi katika mtaa wa madongoporomoka

(iii) Jitu anataka kuchukua mashamba ya wanamadongoporomoka.
Mabuldoza yanabomoa mashamba yao asubuhi na mapema.


(iv) Jiji limejaa hiki na kile, hili na lile,limejaa hadi pomoni.
Halijaacha hata nafasi ya mtu kuvuta pumzi. Huuu ni ubinafsi na huashiria mfano wa jiji kuwa na Tumbo lisiloshiba.

(v) Majengo makubwa yaliyoko jijini yananuia kuwanyanyasa wanamadongoporomoka na kumeza vipande vyao vya ardhi. Vipande hivi vya ardhi vinanuiwa kutumika ili kuwahi kujenga majengo bora zaidi ya starehe ya wakubwa.



(vi) Tumbo la viongozi halishibi katika unyakuzi wa ardhi za watu.


(vii) Wateja wanaokuja kwa Mzee Mago mkahawani ni wengi , hili linatokana na matumbo yao kutoshiba.

(viii) Kupitia sharia zilizoko tunaona hali ya kutotosheka ama kutoshiba kwa viongozi kisheria. Wanabadilisha sharia kwa manufaa yao binafsi, sheria hizi zinamkandamiza mwananchi.


(ix) Wakazi wa Madongoporomoka wanaonekana kushiba hali ya sahau, tumbo la akili la Mago halishibi kamwe. Badala ya kusahau anaendelea kukumbuka mengi kuhusu jinsi ya kupigania haki.
maurice.mutuku answered the question on August 3, 2019 at 11:27


Next: Eleza madhila kumi yaliyompata Kabwela
Previous: Linganisha bahari za shairi A na B

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions