Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Taja na utoe mifano miwili ya tamathali za usemi zilizotumika katika mashairi yote mawili.

      

SHAIRI A: HOFU YA BIN-ADAMU

Hofu za wanyonge, ni nguvu za matajiri,

Ambazo zinawaponda, wanapotaka usawa.


Hofu ya watawala, ni kupoteza uhuru,

Wa kutawala kwa mbavu, pamoja na utukutu.



Hofu za mwanamke ,mwanamke wa sasa,

Ni kutumiwa ja rungu, daima kuwekwa nyuma.


Hofu za mmcha-mungu, ni maisha ya baadaye,

Maana hana hakika, ndio aogopa kifo.


Hofu za wasomi, ni kwamba wako baidi,

Na wale wateteao, ambao ni sawa nao.




SHAIRI B: AMANI

Uhuru pia Amani
Usifikirie ni zawadi
Ambayo inapeanwa
Pasipo mikwaruzano



Kama wataka hakiyo
Shariti uwe tayari Kupokeza roho yako
Pamoja na ya mwingine



Uhuru ja ini la fani
Ambalo kulifikia
Sharti uwe jasiri
Jasiri aso kifani


Taja na utoe mifano miwili ya tamathali za usemi zilizotumika katika mashairi yote mawili.

  

Answers


Maurice
(i) Takriri-neno hofu,mwanamke.

(ii) Tashihishi/uhuishi-zinazowapanda.

(iii)Tashbihi-kutumiwa ja rungu/uhuru ja ini la faru.
maurice.mutuku answered the question on August 3, 2019 at 11:42


Next: Andika ubeti wa pili wa shairi B kati lugha nathari.
Previous: Taja na utoe mifano miwili idhini ya mtunzi uliotumika katika mashairi yote mawili.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions