Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Ni mambo gani yanayochangia kuanguka kwa mwanafunzi katika swali la ushairi?

Katika kila kiwango, wanafunzi huonekana kama wana shida kubwa sana katika kuyachambua mashairi. Hali hii ni matokeo ya mambo mengi. Yaweza kuwa mashairi waliyokutana nayo mara ya kwanza yalikuwa magumu, au yalikuwa yamechanganya Kiswahili sanifu na lahaja zingine ambazo wasomi hawangezielewa moja kwa moja.

Jambo hili huwakatisha wanagenzi tamaa hasa wanapokosa kulipata katika kamusi msamiati uliotumika. Wanapotamauka, wao huwa hawataki kujishughulisha na mashairi. Huu ndio mwanzo wa kuanguka kwao katika mtihani kwa vile wengi wao hulazimika kukutana na mashairi kwa mara ya kwanza katika chumba cha mtihani. Hiki ni kinyume cha jinsi mambo yanavyostahili kuwa. Ukweli ni kuwa mashairi yanastahili kuwaburudisha wasomi pindi wakutanapo nayo.


Madai kuwa mashairi ya Kiswahili ni magumu kufahamika isipokuwa kwa watu maalum wenye vipawa maalum hayafai. Mwanafunzi ambaye anataka kufanya vizuri katika swali la mashairi ni lazima aanze kuyapenda mapema iwezekanavyo. Ni muhimu aazimie kuyapenda hasa ajuapo kuwa atatahiniwa katika sehemu hii. Kwa vile hana njia ya kuyaepuka,azingatie msemoi wa wazungu usemao kuwa kama hupati upendacho, anza kupenda kile ukipatacho. Ili kuchochea upendo ndani yake, asijishughulishe nayale mashairi ambayo anayaona kama ni magumu. Ajaribu kuyaelewa yale ambayo anayaelewa na kuudondoa ule ujumbe ambao yameubeba na vile vile ajaribu kuufurahia utamu wa maneno yaliyotumika. Atalipata hili kwa kuyasoma kwa sauti. Kila mara, akumbuke kwamba kadiri atakavyokutana na mashairi mengi ndivyo atakavyofurahia na kuyaelewa.


Pili, akikutana na shairi, asishtushwe na msamiati au lahaja iliyotumika. Hata kama haelewi msamiati uliotumika, ajaribu kuelewa ujumbe uliomo katika shairi. Hata hivyo, lazima ajihami na msamiati mwingi iwezakanavyo. Isitoshe, ni muhimu katika mazoezi yake kujaribu kuandika mashairi yake mwenyewe ili aelewe ni kwa nini waandishi huyaandika mashairi jinsi wanavyoandika;Atagundua kwa nini waandishi huyarefusha, huyafupisha au huyabadilisha maana ya maneno mbalimbali.


Ni mambo gani yanayochangia kuanguka kwa mwanafunzi katika swali la ushairi?

Answers


Maurice
(i) Kuogopa mashairi baada ya kulikuta shairi gumu


(ii) Itikadi kuwa mashairi ni magumu

(iii) Kutofanya mazoezi na kukutana na mashairi kwa mara ya kwanza katika chumba cha mtihani.


(iv) Kupata msamiati usiopatikana katika kamusi.
maurice.mutuku answered the question on August 5, 2019 at 06:21

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions