Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

“ulitaka wahamie wapi siku kama hizi?....Fafanua sifa za msemaji wa dondoo hii.

TAMTHLIA: KIGOGO

“ulitaka wahamie wapi siku kama hizi? Wamekuja kuuguza majeraha yao ya kufungiwa soko?”

Fafanua sifa za msemaji wa dondoo hii.

Answers

Maurice
Ngurumo

(i) Katili –anamvunja Tunu mguu

(ii) Kibarakala/ kikaragosi - anatumiwa na utawala wa Majoka kukandamiza upinzani

(iii) Mpenda raha - ashiriki ulevi mangweni

(iv) Msherati - ana uhusiano wa kimapenzi na Asiya mkewe Boza

(v) Binafsi - hajali hali ya wanaotegemea soko anapokataa kushirikiza kufunguliwa kwake.

(vi) Fisadi - anasema hupokea hongo kutoka watu wa Kigogo

(vii) Msaliti - Anajivunia kuvunja sheria badala ya kuzifuata kama raia mzalendo

(viii) Mwenye taasubi ya kiume - asema afadhali ampe paka wa majoka kura lakini si mwananmke

(ix) Mwenye maringo - anaringia ukatili wake uliomletea sifa kwa wengi.
maurice.mutuku answered the question on August 5, 2019 at 08:06

Next: Kando na kufungiwa soko, wanasagamoyo wanauguza majeraha yepi mengine yanayosababishwa na utawala wa Majoka.
Previous: List the Concepts of Cost accounting

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index

Learn High School English on YouTube

Related Questions

  • Kando na kufungiwa soko, wanasagamoyo wanauguza majeraha yepi mengine yanayosababishwa na utawala wa Majoka.(Solved)

    TAMTHLIA: KIGOGO

    Kando na kufungiwa soko, wanasagamoyo wanauguza majeraha yepi mengine yanayosababishwa na utawala wa Majoka?

    Date posted: August 5, 2019.  Answers (1)

  • Tambua mbinu mbili za lugha katika dondoo hili.(Solved)

    “ulitaka wahamie wapi siku kama hizi? Wamekuja kuuguza majeraha yao ya kufungiwa soko?”

    Tambua mbinu mbili za lugha katika dondoo hili.

    Date posted: August 5, 2019.  Answers (1)

  • Weka maneno haya katika muktadha wake(Solved)

    “ulitaka wahamie wapi siku kama hizi? Wamekuja kuuguza majeraha yao ya kufungiwa soko?”

    Weka maneno haya katika muktadha wake

    Date posted: August 5, 2019.  Answers (1)

  • Kwa kurejelea tamthlia ya KIGOGO, Thibitisha ukweli wa dondoo hili.(Solved)

    “Kitabu si jalada, fungua ndani usome mambo. Kitanda usichokilalia kunguni mwake huwajui.”

    Kwa kurejelea tamthlia ya KIGOGO, Thibitisha ukweli wa dondoo hili.

    Date posted: August 5, 2019.  Answers (1)

  • Eleza muktadha wa dondoo hili(Solved)

    TAMTHLIA: KIGOGO

    “Kitabu si jalada, fungua ndani usome mambo. Kitanda usichokilalia kunguni mwake huwajui.”

    Eleza muktadha wa dondoo hili

    Date posted: August 5, 2019.  Answers (1)

  • Kwa kurejelea riwaya nzima eleza changamoto zinazoikumba jinsia ya “mwanagenzi”(Solved)

    RIWAYA: CHOZI LA HERI

    Kwa kurejelea riwaya nzima eleza changamoto zinazoikumba jinsia ya “mwanagenzi”

    Date posted: August 5, 2019.  Answers (1)

  • Taja na ueleze mbinu mbili za lugha zinazijitokekeza katika dondoo hili.(Solved)

    Riwaya-Chozi la Heri

    Taja na ueleze mbinu mbili za lugha zinazijitokekeza katika dondoo hili.

    Date posted: August 5, 2019.  Answers (1)

  • Weka dondoo hili katika muktadha wake.(Solved)

    RIWAYA: CHOZI LA HERI

    “……kama mataifa hayakushinda majabali miaka kumi iliyopita itakuwa huyu mwanagenzi ambaye hata mgwisho sisi ndio tulimfunza.”

    Weka dondoo hili katika muktadha wake.

    Date posted: August 5, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha shamirisho kipozi na shamisisho kitondo katika sentensi ifuatayo: Onyango alimnunulia simu mpenzi wake.(Solved)

    Bainisha shamirisho kipozi na shamisisho kitondo katika sentensi ifuatayo:
    Onyango alimnunulia simu mpenzi wake.

    Date posted: August 5, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi zifuatazo kulingana na maagizo uliyopewa. Ngome ya wanajeshi ilifanyiwa ukarabati. (Andika katika hali ya mazoea).(Solved)

    Andika sentensi zifuatazo kulingana na maagizo uliyopewa.
    Ngome ya wanajeshi ilifanyiwa ukarabati. (Andika katika hali ya mazoea).

    Date posted: August 5, 2019.  Answers (1)

  • Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa “Nitaleta mzazi kesho na nitamwimbia wimbo huu hapa.” Bushonga alisema.(Solved)

    Andika sentensi ifuatayo katika usemi wa taarifa
    “Nitaleta mzazi kesho na nitamwimbia wimbo huu hapa.” Bushonga alisema.

    Date posted: August 5, 2019.  Answers (1)

  • Kiimbo ni nini? Huku ukibainisha matumizi ya kiimbo tunga sentensi mbili.(Solved)

    Kiimbo ni nini?

    Huku ukibainisha matumizi ya kiimbo tunga sentensi mbili.

    Date posted: August 5, 2019.  Answers (1)

  • Andika ngeli za maneno haya: (i) Kawa (ii) Baridi(Solved)

    Andika ngeli za maneno haya:

    (i) Kawa

    (ii) Baridi

    Date posted: August 5, 2019.  Answers (1)

  • Akifisha sentensi ifuatayo: lo daudi ameshindwa(Solved)

    Akifisha sentensi ifuatayo:
    lo daudi ameshindwa

    Date posted: August 5, 2019.  Answers (1)

  • changanua sentensi ifuatayo kwa mfumo wa mstari. Ng’ombe waliovamia shamba letu wamesababisha uharibifu mkubwa.(Solved)

    changanua sentensi ifuatayo kwa mfumo wa mstari.
    Ng’ombe waliovamia shamba letu wamesababisha uharibifu mkubwa.

    Date posted: August 5, 2019.  Answers (1)

  • Majina mengi katika ngeli ya U-ZI huchukua kiambishi U katika umoja lakini viambishi tofauti katika wingi. Andika majina mawili ukionyesha viambishi hivyo tofauti katika umoja...(Solved)

    Majina mengi katika ngeli ya U-ZI huchukua kiambishi U katika umoja lakini viambishi tofauti katika wingi. Andika majina mawili ukionyesha viambishi hivyo tofauti katika umoja na wingi.

    Date posted: August 5, 2019.  Answers (1)

  • Eleza sifa za konsonanti zifuatazo: (i) /h/ (ii) /r/(Solved)

    Eleza sifa za konsonanti zifuatazo:

    (i) /h/

    (ii) /r/

    Date posted: August 5, 2019.  Answers (1)

  • Mwandishi amependekeza hatua gani kuchukuliwa ili mwanafunzi afaulu katika maswali ya mashairi?(Solved)

    Katika kila kiwango, wanafunzi huonekana kama wana shida kubwa sana katika kuyachambua mashairi. Hali hii ni matokeo ya mambo mengi. Yaweza kuwa mashairi waliyokutana nayo mara ya kwanza yalikuwa magumu, au yalikuwa yamechanganya Kiswahili sanifu na lahaja zingine ambazo wasomi hawangezielewa moja kwa moja.

    Jambo hili huwakatisha wanagenzi tamaa hasa wanapokosa kulipata katika kamusi msamiati uliotumika. Wanapotamauka, wao huwa hawataki kujishughulisha na mashairi. Huu ndio mwanzo wa kuanguka kwao katika mtihani kwa vile wengi wao hulazimika kukutana na mashairi kwa mara ya kwanza katika chumba cha mtihani. Hiki ni kinyume cha jinsi mambo yanavyostahili kuwa. Ukweli ni kuwa mashairi yanastahili kuwaburudisha wasomi pindi wakutanapo nayo.

    Madai kuwa mashairi ya Kiswahili ni magumu kufahamika isipokuwa kwa watu maalum wenye vipawa maalum hayafai. Mwanafunzi ambaye anataka kufanya vizuri katika swali la mashairi ni lazima aanze kuyapenda mapema iwezekanavyo. Ni muhimu aazimie kuyapenda hasa ajuapo kuwa atatahiniwa katika sehemu hii. Kwa vile hana njia ya kuyaepuka,azingatie msemoi wa wazungu usemao kuwa kama hupati upendacho, anza kupenda kile ukipatacho. Ili kuchochea upendo ndani yake, asijishughulishe nayale mashairi ambayo anayaona kama ni magumu. Ajaribu kuyaelewa yale ambayo anayaelewa na kuudondoa ule ujumbe ambao yameubeba na vile vile ajaribu kuufurahia utamu wa maneno yaliyotumika. Atalipata hili kwa kuyasoma kwa sauti. Kila mara, akumbuke kwamba kadiri atakavyokutana na mashairi mengi ndivyo atakavyofurahia na kuyaelewa.

    Pili, akikutana na shairi, asishtushwe na msamiati au lahaja iliyotumika. Hata kama haelewi msamiati uliotumika, ajaribu kuelewa ujumbe uliomo katika shairi. Hata hivyo, lazima ajihami na msamiati mwingi iwezakanavyo. Isitoshe, ni muhimu katika mazoezi yake kujaribu kuandika mashairi yake mwenyewe ili aelewe ni kwa nini waandishi huyaandika mashairi jinsi wanavyoandika;Atagundua kwa nini waandishi huyarefusha, huyafupisha au huyabadilisha maana ya maneno mbalimbali.

    Mwandishi amependekeza hatua gani kuchukuliwa ili mwanafunzi afaulu katika maswali ya mashairi?

    Date posted: August 5, 2019.  Answers (1)

  • Ni mambo gani yanayochangia kuanguka kwa mwanafunzi katika swali la ushairi?(Solved)

    Ni mambo gani yanayochangia kuanguka kwa mwanafunzi katika swali la ushairi?

    Date posted: August 5, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika mashairi. (i) Ja (ii) Sharuti (iii) Utukufu (iv) Baidi(Solved)

    SHAIRI A: HOFU YA BIN-ADAMU

    Hofu za wanyonge, ni nguvu za matajiri,

    Ambazo zinawaponda, wanapotaka usawa.

    Hofu ya watawala, ni kupoteza uhuru,

    Wa kutawala kwa mbavu, pamoja na utukutu.

    Hofu za mwanamke ,mwanamke wa sasa,

    Ni kutumiwa ja rungu, daima kuwekwa nyuma.

    Hofu za mmcha-mungu, ni maisha ya baadaye,

    Maana hana hakika, ndio aogopa kifo.

    Hofu za wasomi, ni kwamba wako baidi,

    Na wale wateteao, ambao ni sawa nao.

    SHAIRI B: AMANI

    Uhuru pia Amani
    Usifikirie ni zawadi
    Ambayo inapeanwa
    Pasipo mikwaruzano

    Kama wataka hakiyo
    Shariti uwe tayari Kupokeza roho yako
    Pamoja na ya mwingine

    Uhuru ja ini la fani
    Ambalo kulifikia
    Sharti uwe jasiri
    Jasiri aso kifani

    Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika mashairi.

    (i) Ja

    (ii) Sharuti

    (iii) Utukufu

    (iv) Baidi

    Date posted: August 3, 2019.  Answers (1)