Bainisha dhamira ya mtunzi wa shairi hili

      

1.Kijana tuza makini, nikwambie usikile
Chakula mahotelini, si kizuri usikile
Ufikapo mlangoni, kizingiti usikile

2. Nenda kaseme nyumbani, kesho asubuhi siji
Nitakwenda makondeni, kawashunge shunge siji
Na hata hapo jioni, kama nitakuja siji

3. Na kama wenda mjini, upatapo nyumba panga
Upahame mizimuni, palozingirwa na panga
Hapana tena amani, kutwa mwapigana panga

4. Na kesho kija shambani, uonapo mti panda
Kwea hadi kileleni, ujifiche kwenye panda
Kaziyo ulinde chini, mimea tuliyopanda

5. Kishuka ola shinani, njugu merundika chungu
Njugu peleka nyumbani, zisije zikawa chungu
Kaanga sufuriani, au pia kwenye chungu

6. Kileta maji jioni, ndoo jitwike na kata
Kata njema ya majani, laini wezayo kata
Kumbuka ya kisimani, huteki ela kwa kata

7. Ninawahi kibandani, nikaliezeke paa
Nipate lindia nyuni, na wanyama kama paa
Kwani kiola angani, naona jua lapaa

8.Kisha takwea mtini, nimeona bivu tunda
Sina usono moyoni, ela tunda kisha tunda
Nimpe wangu mwendeni, jioni nishike tunda

9.Meanza wao uneni, hapo nami ndipo kamba
Leo wenda hawaoni, kama wa bahari kamba
Wajijaza kimiani, wakijitatia kamba

10. Mtoto wachoma yakini, japo liwe moja kaa
Ukikupata takoni, ni shida huwezi kaa
Ela hufaa mekoni, kutoka nswi na kaa



Bainisha dhamira ya mtunzi wa shairi hili

  

Answers


Maurice
Kufunza maana mbalimbali za maneno
maurice.mutuku answered the question on August 6, 2019 at 05:57


Next: Gome Engineering Ltd. Employees job order cost system. The company use predetermined overheads rates in rime manufacturing overheads to jobs.
Previous: The figure below shows a ray of light incident on a plane mirror.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions