Tangu miaka ya uhuru, serikali za Afrika zimekuwa zikikariri kwa dhati na hata kula viapo vya kulinda na kutetea haki za raia wao kama zilivyoainishwa...

      

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.
Tangu miaka ya uhuru, serikali za Afrika zimekuwa zikikariri kwa dhati na hata kula viapo vya kulinda na kutetea haki za raia wao kama zilivyoainishwa kwenye katiba. Kadiri miaka inavyozidi na ulevi wa mamlaka kuchukua nafasi katika nafsi za viongozi hao, kiapo chao huishia kuapuliwa katika muda wa kupepesa macho. Ikasalia hali ya maskini pita chini miye mwenye nazo nipite juu. Katika hali kama hii, wanaoishia kuumia aghalabu ni watoto.
Kwa miaka mingi, mtoto wa Afrika amekuwa akiteseka na kusalitika katika dunia hii ya mwenye nguvu mpishe, hasa akiwa anatoka katika familia maskini na jamii isiyothamini utu. Si ajabu kupata mtoto wa Afrika akiishi katika mabanda yaliyo kando ya machimbo katika migodi akitumikishwa katika machimbo hayo. Katika hali kama hizi, siku nenda rudi, utawapata watoto wamevalia matambara, miguu imeparara na midomo kuwakauka huku vichwani wakiwa wamebeba karai za madini kutoka
machimboni. Na mchakato wote wa kutafuta madini hayo unawashirikisha watoto, isipokuwa kupokea pesa, ambao hufanywa na mabwanyenye wanaoishia kuwapa (au hata kuwanyima) watoto wale malipo duni au badala yake wakawalipa wazazi wa watoto hao.
Hali huwa sawa na hiyo katika maeneo ambayo shughuli za uvuvi hutekelezwa. Watoto wengihuingizwa katika ‗biashara‘ ya samaki kwa kisingizio cha kuwapa namna ya kujitegemea katika siku za usoni. Ajabu ni kwamba, mwisho wao huwa papo hapo uvuvini.
Kinachosikitisha sana ni udhalimu ambao umekuwa ukitekelezwa na kundi la watu ambao wanafaa- kwa msingi wa kazi zao- kuwalinda watoto hao na kuwaelekeza katika masuala ya maisha. Je, ni kwa nini mtu mwenye akili zake timamu, ambaye tayari alikwishamaliza masomo na hata kupata kazi, amtunge mimba mwanafunzi na kumzimia ndoto yake maishani? Kwa nini mtoto kama huyo abebeshwe mzigo wa uzazi badala ya kumsaidia na kumtua (au kuwatua wazazi wake) mzigo wa elimu kwa kumpa vifaa vya elimu au kumlipia karo? Pigo kuu huwa pale mtoto kama huyo ni yatima na ndiye anayetegemewa na mhisani wake kuja kuwaauni ndugu zake, kama anao. Jamani, ubinadamu umeenda wapi?
Sikitiko jingine ni pale watoto wanatekwa nyara na kutumikishwa vitani kupigana na mibabe wa kivita. Hii, bila shaka, ni dhuluma ya hali ya juu kwa watoto na ukiukaji mkubwa wa haki zao. Hebu niambie, mtoto mwenye uzani wa chini ya kilo arubaini kuvalishwa sare nzito za kijeshi na kubebeshwa bunduki au hata makombora ambayo yamewazidi uzani. Unyama ulioje huu?
Pamoja na hayo, licha ya serikali za Afrika kuahidi mara kwa mara kwa vinywa vipana kuwa watalinda haki za kimsingi za kila mtoto katika himaya zao ambayo ni kuhakikisha wanapata lishe bora, wanaishi katika mazingira safi, wanapata elimu bora ya msingi na kupata tiba mwafaka - mamilioni ya watoto barani Afrika bado hawaendi shule kwa sababu ya changamoto mbalimbali. Aidha, wengine lukuki huaga kila mwaka kutokana na utapiamlo na ukosefu wa chakula. Dhana kuwa maradhi sugu yameangamizwa ni ya kupotosha kwani kila mwaka, maelfu ya watoto huaga kutokana na maradhi ya kuambukiza au yale yanayoweza kuzuiliwa au kutibiwa, kama malaria. Mamilioni ya wengine wangali
wanaishi katika mitaa ya mabanda na hata kukosa huduma za kimsingi kama maji safi ya matumizi.
Kwa kuwa changamoto hukabiliwa na changamoto, hakuna siku ambapo viongozi wataweza kumaliza utepetevu huu kimiujiza. Muhimu ni kwa kila kiongozi kuitazama jamii yake kwa jicho la ndani na kuweka mikakati ya namna bora ya kuikomboa kutoka katika rima la umaskini, magonjwa na ujinga.
Hili litawezekana tu kwa kuwaona watu wote kuwa na umuhimu katika kuibadilisha jamii wala si kubagua kundi au jamii fulani na kuipendelea nyingine.
a) Fafanua changamoto zinazomkabili mtoto wa Afrika kwa maneno 80.
b) Bainisha mielekeo ambayo viongozi wa Afrika hukazania kuzingatia (maneno 65)

  

Answers


sharon
a)
i) Mtoto anaishi katika mabanda.
ii) Anatumikishwa katika machimbo/vichwani wanabeba karai za madini.
iii) Anavalia matambara.
iv) Miguu inaparara na midomo kukauka.
v) Kupewa au kunyimwa malipo duni.
vi) Mtoto huingizwa katika biashara ya samaki.
vii) Anatungwa mimba na kuzimiwa ndoto maishani /kubebeshwa mzigo wa uzazi
viii) Anatekwa nyara.
ix) Kutumikishwa vitani kupigana na mibabe ya vita kuvalishwa sare nzito na kubebeshwa bunduki au makombora
yaliyowazidi uzani.
x) Haendi shule
xi) Huaga kwa utapiamlo, ukosefu wa chakula na maradhi.
xii) Kukosa huduma za kimsingi kama maji.
b)
i) Kukariri na kula viapo vya kulinda na kutetea haki za raia zilivyoainishwa kwenye katiba .
ii) Hali ya maskini pita chini na mwenye nazo nipite juu/mwenye nguvu mpishe.
iii) Kusaliti mtoto/kuwalipa watoto malipo duni
iv) Kusingizia kuwapa watoto namna ya kujitegemea siku za usoni.
v) Kuwalinda watoto na kuwaelekeza katika masuala ya maisha.
vi) Kuahidi kuwa watalinda haki za kimsingi za kila mtoto.
vii) Maradhi sugu yameangamizwa.
viii) Kumaliza utepetevu.
ix) Kuweka mikakati bora ya kuikomboa jamii.
sharon kalunda answered the question on September 21, 2019 at 07:05


Next: KUKITHIRI kwa visa vya utoaji wa hongo kwa wapiga kura walioshiriki chaguzi ndogo zilizofanyika Jumatatu katika eneobunge la Malindi na Kaunti ya Kericho ni ithibati...
Previous: Use logarithms to evaluate:

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • KUKITHIRI kwa visa vya utoaji wa hongo kwa wapiga kura walioshiriki chaguzi ndogo zilizofanyika Jumatatu katika eneobunge la Malindi na Kaunti ya Kericho ni ithibati...(Solved)

    Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.
    KUKITHIRI kwa visa vya utoaji wa hongo kwa wapiga kura walioshiriki chaguzi ndogo zilizofanyika Jumatatu katika eneobunge la Malindi na Kaunti ya Kericho ni ithibati tosha kuwa ufisadi ume-kita mizizi nchini.
    Kadhalika, visa hivyo vilidhihirisha kuwa demokrasia imedidimia na taasisi za kupambana na visa vya ufisadi zimefifia.
    Mwezi uliopita, Wakenya kupitia mitandao ya kijamii walishtumu Rais wa Uganda Yoweri Museveni kutokana na kile walichotaja kuwa matumizi ya ‗mabavu‘ kuhifadhi kiti chake baada ya kuwatishia wapinzani wake.
    Watumiaji wa mitandao ya kijamii pia walimkosoa Rais Uhuru Kenyatta kwa kumpongeza mwenzake wa Uganda huku wakisema aliunga mkono ukandamizaji wa demokrasia.
    Lakini, visa vya uhongaji wa wapiga kura vilivyoshuhudiwa katika maeneo ya Malindi na Kericho vikitekelezwa na viongozi wa kisiasa hata wengine wakiwa wa muungano tawala wa Jubilee, ni dhihirisho tosha kuwa Wakenya hawakuwa na sababu ya kushutumu Rais Museveni.
    Utumiaji wa mabavu au kununua wapiga kura ili kushinda uchaguzi ni hujuma kwa demokrasia. Baadhi ya wanasiasa pia wameripotiwa kuwa wanatumia fedha zao kusafirisha watu kutoka eneo moja hadi jingine ili wajiandikishe kuwa wapiga kura na wawachague katika uchaguzi ujao. Huu pia ni ukiukaji wa misingi ya demokrasia.
    Ununuaji wa wapiga kura unamaanisha mabwanyenye ambao wamehusishwa na sakata mbalimbali za ufisadi ndio wataendelea kushikilia nyadhifa mbalimbali za uongozi kwa kuwa wao ndio wana mabunda ya fedha za kuhonga wapiga kura.
    Viongozi wanaochaguliwa baada ya kuwahonga wapiga kura hawatafanya maendeleo yoyote na badala yake, watakuwa wakihusika na wizi wa rasilimali za umma ili kupata fedha za kuwahonga watu katika uchaguzi unaofuatia. Mabwanyenye hawa wanafanya kila wawezalo kuhakikisha wapiga kura wanaendelea kuzama katika lindi la umaskini ili waweze kununuliwa kwa urahisi. Sawa na Esau tuliyeelezwa katika Biblia kwamba aliuza urithi wake wa kuzaliwa kwa Yakobo kwa kubadilishana na chakula, maskini pia wako tayari kuuza haki yao ya kuchagua kiongozi bora kwa shilingi mia moja.
    Viongozi wanaotoa hongo kwa wapiga kura kwa lengo la kushinda uchaguzi ni ishara kwamba hawana maono wala sera za mandeleo. Badala yake wanang‘ang‘ania mamlaka ili kujilimbikizia utajiri wala si kusaidia mpiga kura kujiinua kimaisha.
    Maswali
    a) Kwa kurejelea kifungu, visa vya kutoa rushwa kwa wapiga kura vinadhihirisha nini?
    b) Bainisha jinsi nne ambazo viongozi wa kisiasa wanatumia kuendeleza ukiukaji wa misingi ya demokrasia
    c) Fafanua athari za uozo unaorejelewa katika taarifa kwa
    (i) Viongozi
    (ii) Raia
    d) Thibitisha kuwa nyani haoni ngokoye katika muktadha wa makala haya.
    e) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika taarifa.
    (i) Mitandao ya kijamii
    (ii) Mabwanyenye

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Eleza jinsi uwililugha unaweza kuleta athari katika lugha na mawasiliano miongoni mwa wanajamii.(Solved)

    Eleza jinsi uwililugha unaweza kuleta athari katika lugha na mawasiliano miongoni mwa wanajamii.

    Date posted: September 19, 2019.  Answers (1)

  • Eleza juhudi zozote tano zinazotumiwa kukiendeleza Kiswahili sanifu nchini Kenya.(Solved)

    Eleza juhudi zozote tano zinazotumiwa kukiendeleza Kiswahili sanifu nchini Kenya.

    Date posted: September 19, 2019.  Answers (1)

  • Tambua kishazi huru na kishazi tegemezi. Tumeanzisha shirika ili tunyanyue hali yetu.(Solved)

    Tambua kishazi huru na kishazi tegemezi.
    Tumeanzisha shirika ili tunyanyue hali yetu.

    Date posted: September 19, 2019.  Answers (1)

  • Kanusha sentensi hii Ugonjwa huu ungalidhibitiwa mapema kifo kingaliepukwa(Solved)

    Kanusha sentensi hii
    Ugonjwa huu ungalidhibitiwa mapema kifo kingaliepukwa

    Date posted: September 19, 2019.  Answers (1)

  • Badilisha katika kauli ya kutendua. Tundika picha hiyo ukutani na uyabandike maandishi kitabuni.(Solved)

    Badilisha katika kauli ya kutendua.
    Tundika picha hiyo ukutani na uyabandike maandishi kitabuni.

    Date posted: September 19, 2019.  Answers (1)

  • Tambua shamirisho kipozi, kitondo na shamirisho ala katika sentensi ifuatayo. Baba amemnunulia mtoto fulana nzuri iliyoshonwa kwa uzi mwekundu.(Solved)

    Tambua shamirisho kipozi, kitondo na shamirisho ala katika sentensi ifuatayo.
    Baba amemnunulia mtoto fulana nzuri iliyoshonwa kwa uzi mwekundu.

    Date posted: September 19, 2019.  Answers (1)

  • Andika katika msemo wa taarifa; "Tusipofanya kazi yetu kwa bidii na kujitegemea,tutabaki kuwa watumwa katika nchi yetu" Rais alisema.(Solved)

    Andika katika msemo wa taarifa;
    "Tusipofanya kazi yetu kwa bidii na kujitegemea,tutabaki kuwa watumwa katika nchi yetu" Rais alisema.

    Date posted: September 19, 2019.  Answers (1)

  • Kwa kutungia sentensi, tofautisha vitate hivi. i) Ghali ii) Gari(Solved)

    Kwa kutungia sentensi, tofautisha vitate hivi.
    i) Ghali
    ii) Gari

    Date posted: September 19, 2019.  Answers (1)

  • Tumia =O‘ rejeshi. i) Msichana ambaye huja ni mwanasheria ii) Maovu ambayo aliyatenda hayasahauliki(Solved)

    Tumia ‗O‘ rejeshi.
    i) Msichana ambaye huja ni mwanasheria
    ii) Maovu ambayo aliyatenda hayasahauliki

    Date posted: September 19, 2019.  Answers (1)

  • Tambua aina ya vitenzi kwa kutaja majina yake. Babu angali anasoma gazeti(Solved)

    Tambua aina ya vitenzi kwa kutaja majina yake.
    Babu angali anasoma gazeti.

    Date posted: September 19, 2019.  Answers (1)

  • Andika katika hali ya udogo Mbwa mwenye ukali alimfukuza mtoto(Solved)

    Andika katika hali ya udogo
    Mbwa mwenye ukali alimfukuza mtoto

    Date posted: September 19, 2019.  Answers (1)

  • Tambua na ueleze aina za vielezi katika sentinsi hizi. i) Mama alimwamrisha mtoto wake kijeshi ii) Askari hutembea makundi makundi(Solved)

    Tambua na ueleze aina za vielezi katika sentinsi hizi.
    i) Mama alimwamrisha mtoto wake kijeshi
    ii) Askari hutembea makundi makundi

    Date posted: September 19, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi kwa kutumia nomino katika ngeli ya pa- ku- mu.(Solved)

    Tunga sentensi kwa kutumia nomino katika ngeli ya pa- ku- mu.

    Date posted: September 19, 2019.  Answers (1)

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya jedwali. Msichana mtukutu alifukuzwa shule leo asubuhi(Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya jedwali.
    Msichana mtukutu alifukuzwa shule leo asubuhi

    Date posted: September 19, 2019.  Answers (1)

  • Ainisha matumizi ya 'na' katika sentensi i) Marafiki hawa hutembeleleana sana. ii) Amina ni tofauti na kakake(Solved)

    Ainisha matumizi ya 'na' katika sentensi
    i) Marafiki hawa hutembeleleana sana.
    ii) Amina ni tofauti na kakake

    Date posted: September 19, 2019.  Answers (1)

  • Eleze maana mbili za sentensi hii; Jane alifagia chakula chote.(Solved)

    Eleze maana mbili za sentensi hii;
    Jane alifagia chakula chote.

    Date posted: September 19, 2019.  Answers (1)

  • Toa mfano mmoja kwa kila mojawapo. i) Kipasuo ii) Kitambaza(Solved)

    Toa mfano mmoja kwa kila mojawapo.
    i) Kipasuo
    ii) Kitambaza

    Date posted: September 19, 2019.  Answers (1)

  • Taja irabu mbili za nyuma kisha ueleze kwa nini huitwa hivyo.(Solved)

    Taja irabu mbili za nyuma kisha ueleze kwa nini huitwa hivyo.

    Date posted: September 19, 2019.  Answers (1)

  • Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali Dhuluma kwa wanawake sio matokeo ya siasa baada ya uhuru, bali ni matokeo ya hali iliyokuwepo tangu enzi za mababu...(Solved)

    Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali

    Dhuluma kwa wanawake sio matokeo ya siasa baada ya uhuru, bali ni matokeo ya hali iliyokuwepo tangu enzi za mababu zetu, kabla ya ukoloni. Kubaguliwa na kudhulumiwa kwa wanawake kisiasa kunaoana na kunyonywa kwake kijamii kunakoshuhudiwa siku nenda miaka rudi.
    Elimu ya jadi ilimwandaa mwanamke kuwa chombo kitiifu cha mwanaume. Mwanamke aliandaliwa katika unyago na katika mfumo mzima wa malezi kuwa chombo cha kumtumikia mwanamume, kumstarehesha, kumfariji, kumlisha na kumzalia watoto. Mwanamke tangu jadi hakuruhusiwa kushiriki katika shunghuli za kisiasa na utawala wala hakuna mtu aliyeamini kwamba mwanamke angeweza kushikilia wadhifa wowote wa uongozi.
    Demokrasia ya jadi nai husudu sana, ambapo wazee walikaa chini ya mbuyu na kuamua mambo ya jumuiya. Mahakama ya jiji ilikuwa aghalabu ni ya wazee na wanaume peke yao. Hakukuwa na mwanamke aliyeshirikishwa hata kama alikuwa ajuza. Sifa waliyokuwa nayo wanawake ni ile ya ushiri na uganga. Mwanamke yeyote aliyezeeka alidhaniwa kuwa bingwa wa uchawi, ulozi na ushirikina. Kwa hivyo, wanawake ndio waliokuwa washirikina wakubwa, maana fursa ya kupata elimu pana zaidi hawakuwa nayo. Si ajabu kuwa mwanamke alipojitokeza na kusema jambo la busara, alipuuzwa
    napengine kutukanwa hadharani.
    Kwa bahati zuri kumezuka mwamko uliotuingiza katika enzi mpya. Vita vya wanawake vya kujihami na kujiendeleza katika ulimwengu unaotawaliwa na wanaume vimetapakaa kote katika kila sehemu ya dunia
    Wanawake wengi wemakiuka misingi na mizizi ya utamanduni na kung‘oa asasi za kijamii na itikadi ambazo daima zimeendelea kumyanyasa na kumuumbua utu mwanamke tangu jadi. Watetezi wa haki za wanawake zamani walilaumu suala la serikali za mataifa kutochukua hatua za utekelezaji wa maazimio yaliyoendelea kupitishwa na umoja wa mataifa mwaka hadi mwaka. Huku masuala ya wanawake ya kijamii, utu na utamaduni yakishangiliwa kupitishwa, watetezi wameeleza wasiwasi wao ikiwa kupitishwa kwa maazimio kutasaidia kuleta maendeleo ya haraka kwa wanawake kimataifa au katika nchi moja. Fauka ya hayo, baadhi ya wachunguzi wanaonelea kuwa maazimio mengi hayadokezi hatua za kufikiwa haki za wanawake.
    Maazimio mengi yanazungumzia juu ya kuondolewa kwa ubaguzi dhidi ya wanawake, kushiriki kwao katika uendelezaji wa amani ya kimataifa na ushirikiano wa kimataifa, majukumu yao katika jamii, mfuko wa umoja wa mataifa wa wanawake (unifem) na kuimarisha hadhi ya wanawake katika sekretariati ya umoja wa mataifa miongoni mwa shughuli nyingine katika mkabala huu. Wanawake wamejikakamua na kudhihirisha kuwa wao pia wana jukumu muhimu la kutekeleza ili kuyaongoza maisha yao na ya watu wengine. Wadumishaji wa dhuluma za kijinsia hawana budi kusalimu amri na kuukubali ukweli huu, wapende wasipende.
    Mtazamo juu ya haki sawa unatokana na kukubaliwa na kuondolewa kwa aina zote za ubaya dhidi ya wanawake. Kwa bahati mbaya, itikadi na mila za kiasili bado hazitupi nafasi ya kuwashangilia wanawake wanaojitolea mhanga kutetea hadhi yao pamoja naya wanyonge wengine. Wao huonekana kama waasi, wapinga mila na watovu wa utii.Maswali
    (a) Eleza chanzo cha dhuluma kwa wanawake.
    (b) Huku ukitoa mafano, fafanua hali ya dhuluma kwa wanawake kama inavyodhihirika katika makala.
    (c) Eleza hatua ambazo mwanamke amechukua kujikomboa
    (d) Je, jamii imechangia vipi katika kumdunisha mwanamke
    (e) Fafanua maana ya misemo ifuatayo;
    i) Wamekiuka misingi
    ii) Kupitishwa kwa maazimio
    iii) Wanaojitolea mhanga

    Date posted: September 19, 2019.  Answers (1)