Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.
i) Athari ya mazingira /wenzao.
ii) Kujinasibisha na kundi Fulani
iii) Kuhifadhi siri/ukweli Fulani ili kutenga wengine.
iv) Kuiga mitindo mipya ya matumizi ya lugha katika muziki wa kisasa na vyombo vya habari /athari ya vyombo vya habari na muziki wa kisasa.
v) Kukwepa masharti (kanuni/ kaida za matumizi ya lugha rasmi/sarufu inayotatiza wengi.
vi) Uraibu wa vijana /kuonyesha wamechanuka kimawazo.
vii) Kurithishwa na wazazi.
viii) Ukosefu wa ufasaha wa lugha.
ix) Kufahamu lugha zaidi ya moja
sharon kalunda answered the question on September 21, 2019 at 08:53
- Andika methali inayoafiki maelezo:
Hakuna chema kisichokuwa na madhara.(Solved)
Andika methali inayoafiki maelezo:
Hakuna chema kisichokuwa na madhara.
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Andika sentensi ifuatayo upya kwa kufuata maagizo.
Mama anapika kutwa kwa sababu ya wageni (Tilia mkazo kwa kinyume)(Solved)
Andika sentensi ifuatayo upya kwa kufuata maagizo.
Mama anapika kutwa kwa sababu ya wageni (Tilia mkazo kwa kinyume)
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Unganisha sentensi zifuatazo kwa kugeuza moja kuwa kishazi tegemezi
i) Majisifu aliingia ukumbini
ii) Sote tulisimama(Solved)
Unganisha sentensi zifuatazo kwa kugeuza moja kuwa kishazi tegemezi
i) Majisifu aliingia ukumbini
ii) Sote tulisimama
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Kanusha sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea.
Amekuja hapa.(Solved)
Kanusha sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea.
Amekuja hapa.
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Geuza sentensi ifuatayo katika kauli ya kutendata:
Miyaa maridadi ilisukwa na msusi stadi.(Solved)
Geuza sentensi ifuatayo katika kauli ya kutendata:
Miyaa maridadi ilisukwa na msusi stadi.
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Eleza maana mbili za sentensi:
Mali atawaalika wengine.(Solved)
Eleza maana mbili za sentensi:
Mali atawaalika wengine.
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Andika sentensi ifuatayo upya ukitumia neno badala ya 'ki' ya masharti.
Ukifika mapema utampata.(Solved)
Andika sentensi ifuatayo upya ukitumia neno badala ya 'ki' ya masharti.
Ukifika mapema utampata.
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Nomino zifuatazo zimo katika ngeli gani?
(i)Siwa
(ii)Kipunye(Solved)
Nomino zifuatazo zimo katika ngeli gani?
(i)Siwa
(ii)Kipunye
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Changanua vipashio vya kisarufi katika kiarifa cha sentensi ifuatayo.
Hawa ndio waliopigana.(Solved)
Changanua vipashio vya kisarufi katika kiarifa cha sentensi ifuatayo.
Hawa ndio waliopigana.
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Akifisha sentensi ifuatayo kuonyesha usemi halisi:
Mosi atakuja kesho.(Solved)
Akifisha sentensi ifuatayo kuonyesha usemi halisi:
Mosi atakuja kesho.
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Tunga sentensi mbili tofauti kudhihirisha kuwa neno "bunda" ni kitawe.(Solved)
Tunga sentensi mbili tofauti kudhihirisha kuwa neno "bunda" ni kitawe.
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Andika visawe viwili vya nahau:
Fanya inda.(Solved)
Andika visawe viwili vya nahau:
Fanya inda.
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha jedwali:
Ule mkongojo ulioletewa babu utauzwa na fundi maarufu.(Solved)
Changanua sentensi ifuatayo kwa kielelezo cha jedwali:
Ule mkongojo ulioletewa babu utauzwa na fundi maarufu.
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Ainisha virai katika sentensi ifuatayo.
Amenijibu kwa hasira.(Solved)
Ainisha virai katika sentensi ifuatayo.
Amenijibu kwa hasira.
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Sahihisha sentensi hii.
Wasichana mabinti mapacha waliozeshwa mume mmoja.(Solved)
Sahihisha sentensi hii.
Wasichana mabinti mapacha waliozeshwa mume mmoja.
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Tumia mzizi- enye katika sentensi kama kihusishi.(Solved)
Tumia mzizi- enye katika sentensi kama kihusishi.
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Ainisha maneno katika sentensi ifuatayo:-
Shehena ya dawa ilikuwa bandarini(Solved)
Ainisha maneno katika sentensi ifuatayo:-
Shehena ya dawa ilikuwa bandarini
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Onyesha muundo wa silabi katika neno wachanjwao(Solved)
Onyesha muundo wa silabi katika neno wachanjwao
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Andika neno lenye mfumo ufuatao wa vitamkwa. Nazali ya ufizi + kipasuo cha kaakaa gumu + irabu ya juu nyuma + kizuiwa ghuna cha kaakaa...(Solved)
Andika neno lenye mfumo ufuatao wa vitamkwa. Nazali ya ufizi + kipasuo cha kaakaa gumu + irabu ya juu nyuma + kizuiwa ghuna cha kaakaa laini + irabu ya chini wastani.
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Tangu miaka ya uhuru, serikali za Afrika zimekuwa zikikariri kwa dhati na hata kula viapo vya kulinda na kutetea haki za raia wao kama zilivyoainishwa...(Solved)
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali.
Tangu miaka ya uhuru, serikali za Afrika zimekuwa zikikariri kwa dhati na hata kula viapo vya kulinda na kutetea haki za raia wao kama zilivyoainishwa kwenye katiba. Kadiri miaka inavyozidi na ulevi wa mamlaka kuchukua nafasi katika nafsi za viongozi hao, kiapo chao huishia kuapuliwa katika muda wa kupepesa macho. Ikasalia hali ya maskini pita chini miye mwenye nazo nipite juu. Katika hali kama hii, wanaoishia kuumia aghalabu ni watoto.
Kwa miaka mingi, mtoto wa Afrika amekuwa akiteseka na kusalitika katika dunia hii ya mwenye nguvu mpishe, hasa akiwa anatoka katika familia maskini na jamii isiyothamini utu. Si ajabu kupata mtoto wa Afrika akiishi katika mabanda yaliyo kando ya machimbo katika migodi akitumikishwa katika machimbo hayo. Katika hali kama hizi, siku nenda rudi, utawapata watoto wamevalia matambara, miguu imeparara na midomo kuwakauka huku vichwani wakiwa wamebeba karai za madini kutoka
machimboni. Na mchakato wote wa kutafuta madini hayo unawashirikisha watoto, isipokuwa kupokea pesa, ambao hufanywa na mabwanyenye wanaoishia kuwapa (au hata kuwanyima) watoto wale malipo duni au badala yake wakawalipa wazazi wa watoto hao.
Hali huwa sawa na hiyo katika maeneo ambayo shughuli za uvuvi hutekelezwa. Watoto wengihuingizwa katika ‗biashara‘ ya samaki kwa kisingizio cha kuwapa namna ya kujitegemea katika siku za usoni. Ajabu ni kwamba, mwisho wao huwa papo hapo uvuvini.
Kinachosikitisha sana ni udhalimu ambao umekuwa ukitekelezwa na kundi la watu ambao wanafaa- kwa msingi wa kazi zao- kuwalinda watoto hao na kuwaelekeza katika masuala ya maisha. Je, ni kwa nini mtu mwenye akili zake timamu, ambaye tayari alikwishamaliza masomo na hata kupata kazi, amtunge mimba mwanafunzi na kumzimia ndoto yake maishani? Kwa nini mtoto kama huyo abebeshwe mzigo wa uzazi badala ya kumsaidia na kumtua (au kuwatua wazazi wake) mzigo wa elimu kwa kumpa vifaa vya elimu au kumlipia karo? Pigo kuu huwa pale mtoto kama huyo ni yatima na ndiye anayetegemewa na mhisani wake kuja kuwaauni ndugu zake, kama anao. Jamani, ubinadamu umeenda wapi?
Sikitiko jingine ni pale watoto wanatekwa nyara na kutumikishwa vitani kupigana na mibabe wa kivita. Hii, bila shaka, ni dhuluma ya hali ya juu kwa watoto na ukiukaji mkubwa wa haki zao. Hebu niambie, mtoto mwenye uzani wa chini ya kilo arubaini kuvalishwa sare nzito za kijeshi na kubebeshwa bunduki au hata makombora ambayo yamewazidi uzani. Unyama ulioje huu?
Pamoja na hayo, licha ya serikali za Afrika kuahidi mara kwa mara kwa vinywa vipana kuwa watalinda haki za kimsingi za kila mtoto katika himaya zao ambayo ni kuhakikisha wanapata lishe bora, wanaishi katika mazingira safi, wanapata elimu bora ya msingi na kupata tiba mwafaka - mamilioni ya watoto barani Afrika bado hawaendi shule kwa sababu ya changamoto mbalimbali. Aidha, wengine lukuki huaga kila mwaka kutokana na utapiamlo na ukosefu wa chakula. Dhana kuwa maradhi sugu yameangamizwa ni ya kupotosha kwani kila mwaka, maelfu ya watoto huaga kutokana na maradhi ya kuambukiza au yale yanayoweza kuzuiliwa au kutibiwa, kama malaria. Mamilioni ya wengine wangali
wanaishi katika mitaa ya mabanda na hata kukosa huduma za kimsingi kama maji safi ya matumizi.
Kwa kuwa changamoto hukabiliwa na changamoto, hakuna siku ambapo viongozi wataweza kumaliza utepetevu huu kimiujiza. Muhimu ni kwa kila kiongozi kuitazama jamii yake kwa jicho la ndani na kuweka mikakati ya namna bora ya kuikomboa kutoka katika rima la umaskini, magonjwa na ujinga.
Hili litawezekana tu kwa kuwaona watu wote kuwa na umuhimu katika kuibadilisha jamii wala si kubagua kundi au jamii fulani na kuipendelea nyingine.
a) Fafanua changamoto zinazomkabili mtoto wa Afrika kwa maneno 80.
b) Bainisha mielekeo ambayo viongozi wa Afrika hukazania kuzingatia (maneno 65)
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)