Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Imefika wakati ambapo kila mmoja lazima ajiulize swali kuhusu tuelekeapo kama jamii, mustakabali wa kizazi cha sasa ni upi?

      

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yafuatayo.
Imefika wakati ambapo kila mmoja lazima ajiulize swali kuhusu tuelekeapo kama jamii, mustakabali wa kizazi cha sasa ni upi?
Nauliza swali kuhusiana na misururu ya visa ambayo kwa kweli imeibua hofu na wasiwasi kuhusu msingi wa kimaadili miongoni mwa vijana wetu. Kuna hatari ijapo; mbaya sana. Ni hali ambayo huenda ikatusahaulisha msingi wa tulikotoka na tuelekeapo.
Kwanza, ni kisa cha Alhamisi usiku ambapo zaidi ya vijana 300 walinaswa katika nyumba moja katika mtaa wa Phenom, Nairobi katika kile kiliaminika kuwa ―hafla ya ukosefu wa maadili‖. Kisa hicho kilikujia siku chache baada ya serikali kupiga marufuku hafla moja ya burudani na ukosefu wa maadili maarufu ―Project X‖ ambapo vijana walikuwa wakitarajiwa kuhudhuria.
Kulingana na taarifa za ‗kanuni‘ za tamasha hiyo, vijana walitakiwa kuvaa mavazi mafupi ambayo yanaonyesha sehemu zao za mwili kwa wazi. Taarifa zilisema kuwa washiriki pia wangeruhusiwa kucheza densi wakiwa uchi kama mojawapo ya kanuni za burudani. Isitoshe, kisa hicho kinakujia baada ya vingine vingi, ambapo vijana wamenaswa na maafisa wa polisi wakijiburudisha kwa vileo katika klabu nyakati za usiku. Vile vile wanafunzi wengi wamenaswa wakishiriki katika vitendo vya ukosefu wa maadili. Baadhi ya wanafunzi hao huwa chini ya miaka 18! Jijini Nairobi visa hivyo vimekuwa kama ―hali za kawaida‖.
Yasikitisha kuwa nyakati za wikendi hutakosa kuona kila aina ya vioja na viroja, hasa katika maeneo ya mijini. Ni nyakati hizi ambapo mabinti huenda katika vituo vya burudani wakiwa wamevaa kila aina ya mavazi. La kushangaza ni kuwa, mabinti hao hushindana kuhusu mbinu za ―kuonyesha‖ uchi wao kwa njia mbalimbali. Kwa haya yote, kile kinadhihirika ni kuwa jamii yetu inaelekea kubaya tu katika safari ya kifo. Safari hii huenda ikatufikisha Jehanamu ambayo kuna uwezekano wa kutojikomboa. Kilicho wazi ni kwamba msingi wetu wa kimaadili umeterereka kiasi cha kutorekebika kabisa. Nchi imegeuka jaa la mwigo wa tamaduni zote za kimagharibi. Kwa mfano, tamasha ya Project X ni mwigo wa filamu maarufu ya wanafunzi wa shule za upili iliyorekodiwa nchini Amerika kwenye filamu hivyo, wanafunzi hao wanajihusisha katika kila aina ya uovu wa kimaadili, ufasiri wake mkuu ukiwa ni ‗burudani‘ kwa msingi wa tamaduni za kimagharibi.Kikweli, huu si msimamo wa tamaduni za Kiafrika. Huu si msingi wetu wa kimadili hata kidogo!.Huu ni mwigo wa kishetani ambao lengo lake ni kuizamisha jamii yetu katika lindi la mgogoro wa kitamaduni na kimaadili.
Mawali.
a. Maadili ya vijana yamezorota. Kwa mujibu wa taarifa hii thibitisha kauli hii.
b. Ni nini asili ya projct X‘?
c. Nyakati za wikendi hutakosa kuona kila aina ya vioja na viroja. Fafanua.
d. Mwandishi ana maana gani anaposema visa hivyo vimekuwa kama hali za kawaida‘.
e. Mwandishi ana msimamo upi kuhusu tamaduni za kimagharibi.
f. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika kwenye kifungu.
(i) Kupiga marufuku
(ii) Mustakabali
(iii) Umetetereka
(iv) Filamu

  

Answers


sharon
(a) (i) Vijana walitarajiwa kuhudhuria hafla moja ya burudani na ukosefu wa maadili maarufu 'Project X‘ iliyopigwa marufuku na serikali.
(ii) Vijana walitakiwa kuvaa mavazi mafupi yaliyoonyesha sehemu zao za mwili kwa wazi.
(iii) Washiriki wangeruhusiwa kucheza densi wakiwa uchi kama mojawapo ya kanuni za burudani.
(iv) Visa vya vijana kunaswa na maafisa wa polisi wakijiburudisha kwa vileo katika klabu nyakati za usiku.
(b) Filamu maarufu ya wanafunzi wa shule za upili iliyorekodiwa nchini Amerika, ambapo wanajihusisha katika kila aina ya uovu? wa kimaadili
(c) Ni nyakati hizi ambapo mabinti huenda katika vituo vya burudani wakiwa wamevaa kila aina ya mavazi. Mabinti hushindana =kuonyesha‘ uchi wao kwa njia mbalimbali.
(d) mazoea, desturi
(e) tamaduni za kimagharibi zinazua mgogoro wa kimaadili.Ni kinyume na msimamo wa tamaduni za Kiafrika.
(f) Kukatazwa kuzuiliwa
Maisha ya baadaye
Umeharibika
Sinema, picha
sharon kalunda answered the question on September 21, 2019 at 09:26


Next: Two bags A and B contain red and blue balls.Bag A contains 2 blue balls and 3 red balls while bag B contains 3 blue...
Previous: Je, mtazamo hasi ni nini? Huwa na athari gani kwa binadamu? Mtazamo hasi ni kukata tamaa, kutamauka kuhusu hali, mtu au jambo fulani.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions