Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Je, mtazamo hasi ni nini? Huwa na athari gani kwa binadamu? Mtazamo hasi ni kukata tamaa, kutamauka kuhusu hali, mtu au jambo fulani.

      

Soma makala haya kisha ujibu maswali yanayofuata.
Je, mtazamo hasi ni nini? Huwa na athari gani kwa binadamu? Mtazamo hasi ni kukata tamaa, kutamauka kuhusu hali, mtu au jambo fulani. Ni hisia ya kutotaka kushiriki wala kuhusishwa na jambo au hali fulani. Mtazamo huu ndio huwafanya wanafunzi wengi kuchukia au hata kudunisha baadhi ya masomo na walimu wanaoyafundisha. Licha ya wengi kuwa na mtazamo huu, kwa kweli huwa hawatambui. Asilimia kubwa ya wanaotambua hutatizika kujikwamua kutoka katika hali hii.
Inakadiriwa kwamba mtu wa wastani huwa na takribani mawazo elfu sitini ya kibinafsi kwa kila saa 24. Asilimia 95 ya fikra hizi huwa sawa na siku iliyotangulia, na asilimia 80 ya fikra hizi zilizorudiwa huwa hasi. Isitoshe, fikra hizi nyingi hutokea bila mtu mwenyewe kutambua na huwa ni mazoea. Hii ina maana kwamba watu wengi hawana ufahamu wa athari za fikra hizi maishani mwao.
Mitazamo hasi ina vyanzo na pia suluhu. Mwanzo kabisa ni imani potovu. Hiki ndicho chanzo cha mitazamo hasi. Kushikilia imani potovu kuhusu maisha pamoja na matukio fulani maishani hujenga mtazamo hasi. Unayaona maisha kwa macho ya imani zako na iwapo imani hizo ni potovu, basi hutayathamini maisha yako ili kukabiliana na hali hii, sharti kwanza ubadili imani yako. Uamini kwamba mabadiliko yanaweza kutokea na uchukue hatua ya kuanzisha mabadiliko hayo maishani mwako. Unahitaji kuepuka fikra hasi zinazoambatana na maisha yako ya awali na kulithamini kila tukio maishani kama tukio huru; Lisilo na uhusiano na yaliyowahi kukutamausha.
Kujikwamua kutoka katika imani duni unahitaji kuibuka na idadi kubwa ya imani chanya kuliko zilizo hasi kuhusu hali mahsusi. Baada ya hilo, zikabili imani zako potovu moja baada ya nyingine huku ukijiuliza endapo imani hizo ni kweli na endapo zina mashiko. Tumia dakika tano hivi kila siku kushadidiafikra chanya inayokinzana na ile inayokudidimiza. Ukifanya hivi kwa takriban siku thelathini imani yako itaanza kuchukua mkondo unaofaa. Familia yako na rafiki unaoandamana nao huathiri pakubwa hisia zako. Wakiwa na mtazamo hasi huweza kukushawishi ukaanza kuhisi wanavyohisi na kuyaona mambo kwa mtazamo wao. Kukabiliana na hali wapaswa kudhibiti hisia zako.
Tawala namna unavyohisi na kukabiliana na hali mbalimbali bila kuathiriwa na wandani hawa. Epuka wandani wa aina hii kadri inavyowezekana, ikiwezekana, jitenge nao ili ujifunze kuwa na uhuru wa kufanya maamuzi yako binafsi bila kuathiriwa nao. Unapaswa kupunguza ushirika hata na jamaa zako wanaokuingiza katika hali ya kutamauka. Punguza muda wa kukaa nao hasa wanapogeukia mkondo huu wa kukutatiza tamaa.
Mazingira hasi ni kizingiti kingine. Pengine huoni ukuruba baina ya maisha yako na mazingira unamokulia au unamokaa. Ukweli ni kwamba, huenda umedumu katika mazingira hayo na kuyazoea hata ukafikiri huwezi kuyabadilisha. Kadri unavyohisi huna uwezo wa kuyabadilisha ndivyo unajizamisha zaidi mtazamo hasi. Ili kukabiliana na hali hii, unahitaji kuelewa kwamba fikra zako au za watangulizi wako ndizo silikuingiza katika mazingira haya. Kwa hivyo, unapaswa kubadili mkondo wa fikra zako na kuanza kujaribu mazoezi ambayo umekuwa ukiyaona kama usiyoyaweza. Hatua kwa hatua utagundua panapo jitihada na uelekezi unaofaa kwamba mazoezi hayo yamekuwa mepesi na hivyo kukubakikishia kuyabadilisha mazingira yako.
unapojikuta ukilalamika jinsi ulivyokerwa na hali fulani, hii ndiyo sababu hasa ya kuwa na mtazamo hasi kuhusu hali hizo. Inaweza kukuwia vigumu kulikubali hili lakini kadiri utakavyolikubali mapema ndivyo utayaboresha maisha yako mapema. Kulalamika tu kutakudumisha katika hali zisizokuridhisha. Kwa hivyo, ili uyabadilishe maisha yako sharti ukome kulalamika tu kutakudumisha katika hali zisizokuridhisha. Kwa hivyo, ili uyabadilishe maisha yako sharti ukome kulalamika na kuanza kujikwamua toka kwenye hali hizo. Katika kufanikisha jambo lolote jema sharti viwepo vizingiti njiani. Mtendaji wa jambo lolote jema liwalo ana jukumu la kuibuka na mikakati mwafaka ya kuvikabili vizingiti hivi ili afanikishe ndoto yake. Hii ndiyo sababu unapaswa kuchukua hatua kutokea sasa ili kupanga na kutekeleza mikakati itakayoupindua mtazamo wako hasi uwe chanya. Kwa jinsi hii utayabadilisha maisha yako yawe ya kuridhisha zaidi na kuwa kielelezo kwa wengi waliotamaushwa na mitazamo hasi.
Maswali.

(a) Fupisha aya ya kwanza. (maneno 45-50)
(b) Eleza namna ya kukabiliana na mitazamo hasi. (maneno 70 - 80)

  

Answers


sharon
(a) (a) Mtazamo hasi ni kutamauka kuhusu hali, mtu au jambo fulani.
(b) Ni hisia ya kutotaka kushiriki wala kuhusishwa na jambo au hali fulani.
(c) Mtazamo huu huwafanya wanafunzi kuchukiana.
(d) Kudunisha baadhi ya masomo na wanaoyafundisha.
(e) Walio na mtazamo huu hawatambui.
(f) Wanaotambua hutatizika kujikwamua kutoka hali hii.
(b) (a) Kuibuka na idadi kubwa ya imani changa kuliko hasi.
(b) Kukabili imani potovu moja baada ya nyingine.
(c) Tumia dakika tano kila siku kushadidia fikra chanya.
(d) Inayokinzana na inayokudidimiza.
(e) Kudhibiti hisia zako unapokabiliana na familia yenye mtazamo hasi.
(f) Tawala namna unavyohisi na kukabiliana na hali mbalimbali bila kuathiriwa na wandani.
(g) Kupunguza ushiriki na jamaa wanaokuingizakatika hali ya kutamauka.
(h) Kubadili mkondo wa fikra zako na kuanza kujaribu.
(i) Mazoezi ambayo umekuwa ukiyaona kama usiyoyaweza.
(j) Kukoma kulalamika na kuanza kujikwamua toka kwenye hali zisizokuridhisha.
sharon kalunda answered the question on September 21, 2019 at 09:32


Next: Imefika wakati ambapo kila mmoja lazima ajiulize swali kuhusu tuelekeapo kama jamii, mustakabali wa kizazi cha sasa ni upi?
Previous: Complete the table below for y = 2cos x and y = sin(x+30)

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions