Ukosefu wa ajira hususan miongoni mwa vijana ni tatizo ambalo usugu wake umefikia kima kisichostahimilika tena.

      

Soma taarifa inavofuata kisha uyajibu maswali
Ukosefu wa ajira hususan miongoni mwa vijana ni tatizo ambalo usugu wake umefikia kima kisichostahimilika tena. Ingawa limejitokeza kama tatizo la ulimwengu mzima lakini katika mataifa ya ulimwengu wa tatu, hasa barani Afrika, limekolea zaidi. Ni kweli kwamba tatizo hili si geni ulimwenguni kwani lilikuwepo miaka michache baada ya uhuru wa nchi nyingi za Kiafrika lakini wakati huo mhusika mkuu aliyelaumiwa kwa ukosefu wa ajira ulikuwa ukosefu wa elimu.Katika ulimwengu wa sasa mambo yamebaidika kabisa kama mbingu na ardhi kwani ukosefu wa elimu sio sababu ya ukosefu wa ajira. Ukweli ni kwamba kuwa na elimu ndiyo sababu ya kukosa ajira.Serikali za mataifa mengi zimechukua hatua mbali mbali ili kukabiliana na tatizo hili, si hoja kama baadhi ni za kutapatapa mithili ya mfa maji ambaye hushika maji. Miongoni mwa hatua hizi ni pamoja na kuboreshamazingira ya uwekezaji ili vitega uchumi viongezeke na hivyo kubuni nafasi za ajira. Kupanua fursa za^lNMMR. ngazi zote na kuhimiza mafunzo ya ujasiriamali na ufundi ni hatua nyingine. Vile vile serikali zingine zimebuni mipango inayolenga kuwawezesha vijana kujiajiri wenyewe.Waama, serikali zingine zimechukua hatua za kijasiri kwa kulegeza masharti ya uwekezaji kwa wawekezaji wa kigeni ili kuwavutia waanzishe miradi katika nchi zao kwa tamaa kwamba watabuni nafasi za ajira katika nchi husika. Changamoto moja ambayo imetokea ni kwamba baadhi ya wawekezeji hawa wanatengea wananchi wa nchi walizotoka kazi za kitaalamu na zenye malipo bora huku wenyeji wakiachiwa zile zinazoitwa 'kazi za mikono' tu. Wanawapuuza wataalamu na wasomi walio katika mataifa hayo. Tusisahau pia kuwa baadhi ya wawekezaji hupelekwa katika mataifa wanayowekeza tabia na mienendo inayokinzana na maadili ya nchi pokezi.Tabia kama ubasha au usenge na ndoa za jinsia moja zimenasibishwa na tamaduni ngeni miongoni mwa Waafrika. Katika mkumbo huu ni tatizo la matumizi ya mihadarati ambalo sasa limefuzu kujiunga na majanga mengine ya kimataifa kama ukimwi. Ukweli mchungu ni kwamba maovu haya yametokana na ukarimu wa mataifa yenye tamaa ya kutaka wawekezaji wa kigeni ambao pamoja na kuwekeza, wao huja na 'yao'. Na kwa sababu mkata hana lake, mataifa pokezi yamehiari kuwapokea wawekezaji wa kigeni wakibeza athari mbaya zinazoletwa na watakuja kutahamaki baadaye kwamba mgeni kumpokea kumbe ni kujitongea.Suluhisho lingine, ambalo huenda ni bora zaidi, ni kuwawezesha vijana kujiajiri. Jambo hili linawezekana, mathalani endapo serikali itatenga hazina maalum katika bajeti yake ili kuwapa vijana mikopo yenye masharti nafuu ili waanzishie miradi yao. Itajuzu misaada hii itolewe kwa makundi ya vijana yaliyoandikishwa kama tahadhari moja ya kukabiliana na ufujaji wa pesa unaoweza kutokea misaada ikitolewa kwa watu binafsi. Vile vile kutolewa kwa mafunzo kuhusu usimamizi kwa vijana kabla ya kukabidhiwa pesa hizi itakuwa hatua nyingine ya kuepukana na ubadhirifu.Isitoshe, ustawishaji wa kilimo unaweza kutoa suluhisho lingine kwa tatizo la ukosefu wa ajira. Sharti vijana wahamasishwe ili washiriki katika kilimo ambapo watazalisha maii na kubuni nafasi za ajira katika nchi zao. Hii itarahisishwa kwa kufundisha somo la zaraa katika shule kama somo la lazima.Hakuna shaka kwamba juhudi hizi, na zingine ambazo hazijashughulikiwa katika makala haya, zikizingatiwa, usugu wa ukosefu wa ajira utageuzwa na kuwa tatizo tu!.

Maswali
a) Kwa nini mwandishi amerejea ukosefu wa ajira kama tatizo sugu.
b) Taja hatua nne ambazo zimechukuliwa na mataifa mbalimbali ili kulitatua tatizo la ukosefu wa ajira.
c) Majilio ya wawekezaji wa kigeni yanaweza kuchukuliwa kama hali ya 'kula sumu ili kupata kuishi'. Thibitisha jinsi 'sumu' inavyoahihirika kwa kurejelea mifano miwili katika makala haya
d) Eleza maana ya msamiati ufuatao katika muktadha wa makala haya.
a) Kutahamaki
b) Itajuzu
c) Zaraa

  

Answers


sharon
(a) Limekolea ulimwenguni kote na zaidi barani Afrika.
(b) Yamejitenga kama mbingu na ardhi / yako mbali kama mbingu na ardhi.
(c) i) Kuboresha mazingira ya uwekezaji ili vitega uchumi viongezekena kubuni nafasi za ajira
- Kupewa fursa za kielimu katika ngazi zote na kuhimiza mafunzo ya ujasiriamali na ufundi
- Kubuni mipango ya kuwawezesha vijana kujiajiri.
- Kulegeza masharti ya uwekezaji wa kigeni ili kuwavutia waanzishe miradi ya kubuni nafasi za ajira
- Ustawishaji wa kilimo ili kuzalisha mali na kubuni ajira zozote.
a) i) Wawekezaji wa kigeni huja na tabia kama ubasha / usenga na ndoa za jinsia moja zinazokinzana na maadili.
ii) Huleta tatizo la matumizi ya mihadarati ambalo limefuzu kuwa janga kama ukimwi zozote.
b) kushukia / kutaharuki
- itapasa / itafaa / italazimu / itahusu
- kilimo / ukulima
2. a) Watoto wa maskini hushinda njaa shuleni
- Walimu wao hawana ari ya kufunza na vifaa vya kutosha
- Shule za kibinafsi zina mazingira na vifaa vya kutosha
- Asilimia kubwa ya wanafunzi wanaojiunga na shule za upili hutoka katika shule za kibinafsi
- Juhudi za wizara ya elimu hazijafua dafu
- Nafasi zote katika shule za upili na kitaifa na vyuo huchukuliwa na watoto wa matajiri
- Nafasi ya mtoto maskini inazidi kudidimia zozote, utiririko.
b) Mikakati ya kimaksudi inahitajika kabla ya balaa kuzuka
- Shule za umma ziwe na mpango wa lishe bora
- Utu unahitajika katika utanzi wa wanafunzi katika nzazi mbalimbali
- Shule za umma zinahitajika walimu na vifaa vya kutosha
- Shule za malazi ziwe za viwango sawa ili kila mtoto awe na msingi bora wa elimu
- Ujenzi wa shule vielezo unahitajika katika kila wilaya
sharon kalunda answered the question on September 21, 2019 at 11:08


Next: Nchi za Afrika Mashariki ziliunda kamati ya lugha ili kusanifisha na kukuza Kiswahili. Eleza malengo manne makuu na mafanikio yake katika juhudi za usanifishaji.
Previous: If (5x + 6y): (2x + 10y) = 22: 10 find x: y.

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions


  • Nchi za Afrika Mashariki ziliunda kamati ya lugha ili kusanifisha na kukuza Kiswahili. Eleza malengo manne makuu na mafanikio yake katika juhudi za usanifishaji.(Solved)

    Nchi za Afrika Mashariki ziliunda kamati ya lugha ili kusanifisha na kukuza Kiswahili. Eleza malengo
    manne makuu na mafanikio yake katika juhudi za usanifishaji.

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Tunga sentensi ukitumia 'na' kama; (i) Kuunganisha (ii) Kihusishi(Solved)

    Tunga sentensi ukitumia 'na' kama;
    (i) Kuunganisha
    (ii) Kihusishi

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Andika katika ukubwa wingi. Njia hii inafaa zaidi kuliko ile.(Solved)

    Andika katika ukubwa wingi.
    Njia hii inafaa zaidi kuliko ile.

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizobanwa. Fundika (kitendua) nata (kutendesha)(Solved)

    Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizobanwa.
    Fundika (kitendua)
    nata (kutendesha)

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Andika methali inayotumiwa kutuhimiza kuthamini vitu viliyo karibu kwani ndivyo vitufaavyo wakatiwa janga.(Solved)

    Andika methali inayotumiwa kutuhimiza kuthamini vitu viliyo karibu kwani ndivyo vitufaavyo wakati wa janga.

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha aina za vishazi vilivyotumika katika sentensi hii; Kule alikoenda alilakiwa vizuri.(Solved)

    Bainisha aina za vishazi vilivyotumika katika sentensi hii;
    Kule alikoenda alilakiwa vizuri.

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Unda kitenzi kutokana na nomino; abiria(Solved)

    Unda kitenzi kutokana na nomino;
    abiria

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Kanusha katika wakati ujao hali timilifu. Bwana arusi alivaa suti ya kupendeza.(Solved)

    Kanusha katika wakati ujao hali timilifu.
    Bwana arusi alivaa suti ya kupendeza.

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Andika kitenzi kifuatacho katika hali ya kuamrisha kwa wingi. (-la).(Solved)

    Andika kitenzi kifuatacho katika hali ya kuamrisha kwa wingi.
    (-la).

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Andika kulingana na maagizo. Sherehe ilikuwa na walakini kwa kukosa mpambe. (Tumia neno lingine badala ya walakini)(Solved)

    Andika kulingana na maagizo.
    Sherehe ilikuwa na walakini kwa kukosa mpambe.
    (Tumia neno lingine badala ya walakini)

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Andika katika umoja. Ile ya kujengea haijaletwa.(Solved)

    Andika katika umoja.
    Ile ya kujengea haijaletwa.

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha aina za nomino zilizotumika katika sentensi ifuatayo. Wema alimpa mtoto yule maji ya baraka.(Solved)

    Bainisha aina za nomino zilizotumika katika sentensi ifuatayo.
    Wema alimpa mtoto yule maji ya baraka.

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Ainisha uamilifu wa viambishi katika neno lifuatalo. Alimlilia.(Solved)

    Ainisha uamilifu wa viambishi katika neno lifuatalo.
    Alimlilia.

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Eleza maana ya buda.(Solved)

    Eleza maana ya buda.

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Tofautisha kwa kueleza maneno ya istilahi zifuatazo. (i) Silabi funge (ii) Silabi mwambatano(Solved)

    Tofautisha kwa kueleza maneno ya istilahi zifuatazo.
    (i) Silabi funge
    (ii) Silabi mwambatano

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Bainisha silabi katika neno lifuatalo. Nyweshwa.(Solved)

    Bainisha silabi katika neno lifuatalo.
    Nyweshwa.

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Andika sifa mbilimbili bainifu za sauti. /gh/ /a/(Solved)

    Andika sifa mbilimbili bainifu za sauti.
    /gh/
    /a/

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Je, mtazamo hasi ni nini? Huwa na athari gani kwa binadamu? Mtazamo hasi ni kukata tamaa, kutamauka kuhusu hali, mtu au jambo fulani.(Solved)

    Soma makala haya kisha ujibu maswali yanayofuata.
    Je, mtazamo hasi ni nini? Huwa na athari gani kwa binadamu? Mtazamo hasi ni kukata tamaa, kutamauka kuhusu hali, mtu au jambo fulani. Ni hisia ya kutotaka kushiriki wala kuhusishwa na jambo au hali fulani. Mtazamo huu ndio huwafanya wanafunzi wengi kuchukia au hata kudunisha baadhi ya masomo na walimu wanaoyafundisha. Licha ya wengi kuwa na mtazamo huu, kwa kweli huwa hawatambui. Asilimia kubwa ya wanaotambua hutatizika kujikwamua kutoka katika hali hii.
    Inakadiriwa kwamba mtu wa wastani huwa na takribani mawazo elfu sitini ya kibinafsi kwa kila saa 24. Asilimia 95 ya fikra hizi huwa sawa na siku iliyotangulia, na asilimia 80 ya fikra hizi zilizorudiwa huwa hasi. Isitoshe, fikra hizi nyingi hutokea bila mtu mwenyewe kutambua na huwa ni mazoea. Hii ina maana kwamba watu wengi hawana ufahamu wa athari za fikra hizi maishani mwao.
    Mitazamo hasi ina vyanzo na pia suluhu. Mwanzo kabisa ni imani potovu. Hiki ndicho chanzo cha mitazamo hasi. Kushikilia imani potovu kuhusu maisha pamoja na matukio fulani maishani hujenga mtazamo hasi. Unayaona maisha kwa macho ya imani zako na iwapo imani hizo ni potovu, basi hutayathamini maisha yako ili kukabiliana na hali hii, sharti kwanza ubadili imani yako. Uamini kwamba mabadiliko yanaweza kutokea na uchukue hatua ya kuanzisha mabadiliko hayo maishani mwako. Unahitaji kuepuka fikra hasi zinazoambatana na maisha yako ya awali na kulithamini kila tukio maishani kama tukio huru; Lisilo na uhusiano na yaliyowahi kukutamausha.
    Kujikwamua kutoka katika imani duni unahitaji kuibuka na idadi kubwa ya imani chanya kuliko zilizo hasi kuhusu hali mahsusi. Baada ya hilo, zikabili imani zako potovu moja baada ya nyingine huku ukijiuliza endapo imani hizo ni kweli na endapo zina mashiko. Tumia dakika tano hivi kila siku kushadidiafikra chanya inayokinzana na ile inayokudidimiza. Ukifanya hivi kwa takriban siku thelathini imani yako itaanza kuchukua mkondo unaofaa. Familia yako na rafiki unaoandamana nao huathiri pakubwa hisia zako. Wakiwa na mtazamo hasi huweza kukushawishi ukaanza kuhisi wanavyohisi na kuyaona mambo kwa mtazamo wao. Kukabiliana na hali wapaswa kudhibiti hisia zako.
    Tawala namna unavyohisi na kukabiliana na hali mbalimbali bila kuathiriwa na wandani hawa. Epuka wandani wa aina hii kadri inavyowezekana, ikiwezekana, jitenge nao ili ujifunze kuwa na uhuru wa kufanya maamuzi yako binafsi bila kuathiriwa nao. Unapaswa kupunguza ushirika hata na jamaa zako wanaokuingiza katika hali ya kutamauka. Punguza muda wa kukaa nao hasa wanapogeukia mkondo huu wa kukutatiza tamaa.
    Mazingira hasi ni kizingiti kingine. Pengine huoni ukuruba baina ya maisha yako na mazingira unamokulia au unamokaa. Ukweli ni kwamba, huenda umedumu katika mazingira hayo na kuyazoea hata ukafikiri huwezi kuyabadilisha. Kadri unavyohisi huna uwezo wa kuyabadilisha ndivyo unajizamisha zaidi mtazamo hasi. Ili kukabiliana na hali hii, unahitaji kuelewa kwamba fikra zako au za watangulizi wako ndizo silikuingiza katika mazingira haya. Kwa hivyo, unapaswa kubadili mkondo wa fikra zako na kuanza kujaribu mazoezi ambayo umekuwa ukiyaona kama usiyoyaweza. Hatua kwa hatua utagundua panapo jitihada na uelekezi unaofaa kwamba mazoezi hayo yamekuwa mepesi na hivyo kukubakikishia kuyabadilisha mazingira yako.
    unapojikuta ukilalamika jinsi ulivyokerwa na hali fulani, hii ndiyo sababu hasa ya kuwa na mtazamo hasi kuhusu hali hizo. Inaweza kukuwia vigumu kulikubali hili lakini kadiri utakavyolikubali mapema ndivyo utayaboresha maisha yako mapema. Kulalamika tu kutakudumisha katika hali zisizokuridhisha. Kwa hivyo, ili uyabadilishe maisha yako sharti ukome kulalamika tu kutakudumisha katika hali zisizokuridhisha. Kwa hivyo, ili uyabadilishe maisha yako sharti ukome kulalamika na kuanza kujikwamua toka kwenye hali hizo. Katika kufanikisha jambo lolote jema sharti viwepo vizingiti njiani. Mtendaji wa jambo lolote jema liwalo ana jukumu la kuibuka na mikakati mwafaka ya kuvikabili vizingiti hivi ili afanikishe ndoto yake. Hii ndiyo sababu unapaswa kuchukua hatua kutokea sasa ili kupanga na kutekeleza mikakati itakayoupindua mtazamo wako hasi uwe chanya. Kwa jinsi hii utayabadilisha maisha yako yawe ya kuridhisha zaidi na kuwa kielelezo kwa wengi waliotamaushwa na mitazamo hasi.
    Maswali.

    (a) Fupisha aya ya kwanza. (maneno 45-50)
    (b) Eleza namna ya kukabiliana na mitazamo hasi. (maneno 70 - 80)

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Imefika wakati ambapo kila mmoja lazima ajiulize swali kuhusu tuelekeapo kama jamii, mustakabali wa kizazi cha sasa ni upi?(Solved)

    Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yafuatayo.
    Imefika wakati ambapo kila mmoja lazima ajiulize swali kuhusu tuelekeapo kama jamii, mustakabali wa kizazi cha sasa ni upi?
    Nauliza swali kuhusiana na misururu ya visa ambayo kwa kweli imeibua hofu na wasiwasi kuhusu msingi wa kimaadili miongoni mwa vijana wetu. Kuna hatari ijapo; mbaya sana. Ni hali ambayo huenda ikatusahaulisha msingi wa tulikotoka na tuelekeapo.
    Kwanza, ni kisa cha Alhamisi usiku ambapo zaidi ya vijana 300 walinaswa katika nyumba moja katika mtaa wa Phenom, Nairobi katika kile kiliaminika kuwa ―hafla ya ukosefu wa maadili‖. Kisa hicho kilikujia siku chache baada ya serikali kupiga marufuku hafla moja ya burudani na ukosefu wa maadili maarufu ―Project X‖ ambapo vijana walikuwa wakitarajiwa kuhudhuria.
    Kulingana na taarifa za ‗kanuni‘ za tamasha hiyo, vijana walitakiwa kuvaa mavazi mafupi ambayo yanaonyesha sehemu zao za mwili kwa wazi. Taarifa zilisema kuwa washiriki pia wangeruhusiwa kucheza densi wakiwa uchi kama mojawapo ya kanuni za burudani. Isitoshe, kisa hicho kinakujia baada ya vingine vingi, ambapo vijana wamenaswa na maafisa wa polisi wakijiburudisha kwa vileo katika klabu nyakati za usiku. Vile vile wanafunzi wengi wamenaswa wakishiriki katika vitendo vya ukosefu wa maadili. Baadhi ya wanafunzi hao huwa chini ya miaka 18! Jijini Nairobi visa hivyo vimekuwa kama ―hali za kawaida‖.
    Yasikitisha kuwa nyakati za wikendi hutakosa kuona kila aina ya vioja na viroja, hasa katika maeneo ya mijini. Ni nyakati hizi ambapo mabinti huenda katika vituo vya burudani wakiwa wamevaa kila aina ya mavazi. La kushangaza ni kuwa, mabinti hao hushindana kuhusu mbinu za ―kuonyesha‖ uchi wao kwa njia mbalimbali. Kwa haya yote, kile kinadhihirika ni kuwa jamii yetu inaelekea kubaya tu katika safari ya kifo. Safari hii huenda ikatufikisha Jehanamu ambayo kuna uwezekano wa kutojikomboa. Kilicho wazi ni kwamba msingi wetu wa kimaadili umeterereka kiasi cha kutorekebika kabisa. Nchi imegeuka jaa la mwigo wa tamaduni zote za kimagharibi. Kwa mfano, tamasha ya Project X ni mwigo wa filamu maarufu ya wanafunzi wa shule za upili iliyorekodiwa nchini Amerika kwenye filamu hivyo, wanafunzi hao wanajihusisha katika kila aina ya uovu wa kimaadili, ufasiri wake mkuu ukiwa ni ‗burudani‘ kwa msingi wa tamaduni za kimagharibi.Kikweli, huu si msimamo wa tamaduni za Kiafrika. Huu si msingi wetu wa kimadili hata kidogo!.Huu ni mwigo wa kishetani ambao lengo lake ni kuizamisha jamii yetu katika lindi la mgogoro wa kitamaduni na kimaadili.
    Mawali.
    a. Maadili ya vijana yamezorota. Kwa mujibu wa taarifa hii thibitisha kauli hii.
    b. Ni nini asili ya projct X‘?
    c. Nyakati za wikendi hutakosa kuona kila aina ya vioja na viroja. Fafanua.
    d. Mwandishi ana maana gani anaposema visa hivyo vimekuwa kama hali za kawaida‘.
    e. Mwandishi ana msimamo upi kuhusu tamaduni za kimagharibi.
    f. Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika kwenye kifungu.
    (i) Kupiga marufuku
    (ii) Mustakabali
    (iii) Umetetereka
    (iv) Filamu

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)

  • Huku ukitoa mifano, bainisha mbinu mbili zinazotumiwa kuunda istilahi mpya katika jamii ya leo.(Solved)

    Huku ukitoa mifano, bainisha mbinu mbili zinazotumiwa kuunda istilahi mpya katika jamii ya leo.

    Date posted: September 21, 2019.  Answers (1)