Wasomi watakuwa wametuzwa siku hizo.
sharon kalunda answered the question on September 23, 2019 at 13:39
- Kanusha sentensi ifuatayo :-
Kuliko na vita kwahitaji amani.(Solved)
Kanusha sentensi ifuatayo :-
Kuliko na vita kwahitaji amani.
Date posted: September 23, 2019. Answers (1)
- Bainisha shamirisho kipozi na kitondo katika sentensi hii.
Nyanya ametengezewa kitanda kizuri na mjukuu wake.(Solved)
Bainisha shamirisho kipozi na kitondo katika sentensi hii.
Nyanya ametengezewa kitanda kizuri na mjukuu wake.
Date posted: September 23, 2019. Answers (1)
- Bainisha mofimu - LI- katika tungo hii.
Alivyolikimbilia(Solved)
Bainisha mofimu - LI- katika tungo hii.
Alivyolikimbilia
Date posted: September 23, 2019. Answers (1)
- Eleza sifa bainifu za sauti /j/.(Solved)
Eleza sifa bainifu za sauti /j/.
Date posted: September 23, 2019. Answers (1)
- Andika misemo inayoafiki hali zifuatazo
(i) Kubahatika
(ii) Ubahaili(Solved)
Andika misemo inayoafiki hali zifuatazo
(i) Kubahatika
(ii) Ubahaili
Date posted: September 23, 2019. Answers (1)
- Akifisha sentensi ifuatayo.
Juma Maria ulimwona Farida Maria la hakuwepo jana.(Solved)
Akifisha sentensi ifuatayo.
Juma Maria ulimwona Farida Maria la hakuwepo jana.
Date posted: September 23, 2019. Answers (1)
- Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia vishale Alimwona mamba majini alipopiga mbizi.(Solved)
Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia vishale
Alimwona mamba majini alipopiga mbizi.
Date posted: September 23, 2019. Answers (1)
- Tambua aina ya kivumishi na kihusishi katika sentensi ifuatayo.
Kijana mgeni amekaribishwa na mgeni.(Solved)
Tambua aina ya kivumishi na kihusishi katika sentensi ifuatayo.
Kijana mgeni amekaribishwa na mgeni.
Date posted: September 23, 2019. Answers (1)
- Bainisha matumizi ya kiambishi "ku" katika sentensi hii.
Naomi atakupikia chai alafu aende kule uwanjani.(Solved)
Bainisha matumizi ya kiambishi "ku" katika sentensi hii.
Naomi atakupikia chai alafu aende kule uwanjani.
Date posted: September 23, 2019. Answers (1)
- Bainisha shamirisho katika tungo lifuatalo.
Mwanafunzi alipewa dawati na mwalimu jana jioni(Solved)
Bainisha shamirisho katika tungo lifuatalo.
Mwanafunzi alipewa dawati na mwalimu jana jioni.
Date posted: September 23, 2019. Answers (1)
- Onyesha kiarifu katika sentensi ifuatayo
Mtoto aliyezungumza na nyanyake ameingia darasa lililochafuliwa na watundu.(Solved)
Onyesha kiarifu katika sentensi ifuatayo
Mtoto aliyezungumza na nyanyake ameingia darasa lililochafuliwa na watundu.
Date posted: September 23, 2019. Answers (1)
- Kutokana na kigezo cha jinsi hewa inavyozuliwa,taja aina mbili za konsonanti na utolee mifano kila moja.(Solved)
Kutokana na kigezo cha jinsi hewa inavyozuliwa,taja aina mbili za konsonanti na utolee mifano kila moja.
Date posted: September 23, 2019. Answers (1)
- Idara ya polisi nchini imelaumiwa kwa muda mrefu kutokana na visa vya mauaji ya kiholela, utepetevu na ufisadi miongoni mwao.(Solved)
Idara ya polisi nchini imelaumiwa kwa muda mrefu kutokana na visa vya mauaji ya kiholela, utepetevu na ufisadi miongoni mwao.Ni kutokana na kilio cha mwananchi pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali ambapo serikali imejitolea sabili kubadili hali katika idara hiyo huku tume mbali mbali zilizobuniwa zikitoa mapendekezo muhimu ya kurekebisha idara hiyo. Matokeo ya hivi punde kutoka kwa shirika la Transparency International liliorodhesha idara ya polisi kama idara fisadi zaidi nchini,maoni ambayo yalisisitiziwa na shirika la kutetea haki za kibinadamu .Ufisadi bado umekita mizizi katika idara ya polisi tangu mabadiliko yaanze upande wa trafiki na hata ndani ya polisi,.Serikali imejitolea kupambana na ufisadi unaonekana kuwa kidonda ndugu katika idara ya polisi. Wananchi wanasema kuwa polisi ni mafisadi na kusahau kuwa ufisadi unashirikisha watu wawili na wote wanapaswa kufunguliwa mashtaka,lazima raia na polisi wazingatie hili.Na ili kuleta mabadiliko muhimu katika idara ya polisi,mapendekezo yote pamoja na ya tume zingine za hapo awali lazima yatekelezwa na kwa mujibu wa katiba mpya.Lazima mabadiliko yaanze kuanzia juu kwani maafisa wadogo hulazimiswa kuchukua hongo ili wapelekee wakubwa wao,ni lazima shughuli ya kuwachagua maafisa waliobora ifanyike kisheria ili mabadiliko yaanze kutoka kwa wakuu wa maafisa wa polisi.
Polisi kidogo wameweza kubadili ile lugha yao ya matusi na ukali kwa rai.Raia nao hawajabadilika,bado wana uwoga dhidi ya polisi na itachukua muda kwani wanadhania kuwa kikosi ni kile kile cha kitambo.Kwa upande wa polisi, hakuna mageuzi yamefanyika.Unaposafiri kuja mjini polisi wangali wana chukua hongo kutoka kwa wenye matatu na kuwaruhusu kubeba kupita kiasi, pia usalama umedorora sana kwani kumekuwa na visa vingi vya mauaji hapa mjini.ukiangalia maafisa wa polisi hakuna mageuzi makubwa yameshuhudiwa haswa kwa upande wa maafisa wa trafiki bado ni wale wale na ufisadi ungali upo.
Mabadiliko ambayo tunataka ni ile polisi wasikae mahali kwa muda hadi wanajuana na mafisadi na majambazi.Maafisa wa polisi wanafaa kuhudumu katika kituo kimoja kwa muda usiozidi miaka mitatu.Kwa kufuata njia hiyo mabadiliko yatapatikana.Juhudi nyingi zikielekezwa katika kubadili kikosi cha polisi wananchi wanapaswa kuhamasishwa ili nao wawezakubadilikahaswa kuhusuiana na mtazamo wao kwa maafisa wa polisi .Na huku tukijaribu kubadili maafisa wa polisi wananchi pia wanapaswa kuelimishwa ili waweze kubadili mtazamo wao kuhusu maafisa hao.Ni bayana kuwa ili kuweza kuleta mabadiliko ya kutamanika katika kikosi cha polisi na haswa katika kupambana na ufisadi uliokita mizizi wananchi sawia na maafisa wa polisi wanajukumu la pamoja kuleta mabadiliko hayo yatakayopelekea kuwepo kwa mlahaka mzuri kati ya maafisa wa polisi na raia.Hatimaye kuwepo kwa huduma bora itakayochangia pakubwa kuboresha uchumi wa taifa na kuafikiwa kwa ruwaza ya mwaka 2030.
Maswali
a) Kipe kifungu hiki kichwa mwafaka.
b) Thibitisha kwamba ufisadi ni kidonda ndugu ukirejelea makala haya..
c) Ni vipi ufisadi katika idara ya polisi unaweza kuzikwa katika kaburi la sahau?
d) "Wananchi ndio wanapaswa kulaumiwa kwa ufisadi."Thibitisha.
(e) "Serikali imepiga hatua katika kuleta mabadiliko katika idara ya polisi.Onyesha kinayacha usemi huu.
(f) Taja manufaa yoyote mawili yanayotokana na mabadiliko katika idara ya polisi
(g) Eleza maana ya:
(i) Mlahaka
(ii) Utepetevu
(iii) Kujitolea sabili
Date posted: September 23, 2019. Answers (1)
- Eleza vikwazo mbali mbali vinavyotatiza ukuaji wa Fasihi Simulizi.(Solved)
Eleza vikwazo mbali mbali vinavyotatiza ukuaji wa Fasihi Simulizi.
Date posted: September 23, 2019. Answers (1)
- Fafanua mbinu nne ambazo hutumika kuzua misimu.(Solved)
Fafanua mbinu nne ambazo hutumika kuzua misimu.
Date posted: September 23, 2019. Answers (1)
- Ukosefu wa ajira hususan miongoni mwa vijana ni tatizo ambalo usugu wake umefikia kima kisichostahimilika tena.(Solved)
Soma taarifa inavofuata kisha uyajibu maswali
Ukosefu wa ajira hususan miongoni mwa vijana ni tatizo ambalo usugu wake umefikia kima kisichostahimilika tena. Ingawa limejitokeza kama tatizo la ulimwengu mzima lakini katika mataifa ya ulimwengu wa tatu, hasa barani Afrika, limekolea zaidi. Ni kweli kwamba tatizo hili si geni ulimwenguni kwani lilikuwepo miaka michache baada ya uhuru wa nchi nyingi za Kiafrika lakini wakati huo mhusika mkuu aliyelaumiwa kwa ukosefu wa ajira ulikuwa ukosefu wa elimu.Katika ulimwengu wa sasa mambo yamebaidika kabisa kama mbingu na ardhi kwani ukosefu wa elimu sio sababu ya ukosefu wa ajira. Ukweli ni kwamba kuwa na elimu ndiyo sababu ya kukosa ajira.Serikali za mataifa mengi zimechukua hatua mbali mbali ili kukabiliana na tatizo hili, si hoja kama baadhi ni za kutapatapa mithili ya mfa maji ambaye hushika maji. Miongoni mwa hatua hizi ni pamoja na kuboreshamazingira ya uwekezaji ili vitega uchumi viongezeke na hivyo kubuni nafasi za ajira. Kupanua fursa za^lNMMR. ngazi zote na kuhimiza mafunzo ya ujasiriamali na ufundi ni hatua nyingine. Vile vile serikali zingine zimebuni mipango inayolenga kuwawezesha vijana kujiajiri wenyewe.Waama, serikali zingine zimechukua hatua za kijasiri kwa kulegeza masharti ya uwekezaji kwa wawekezaji wa kigeni ili kuwavutia waanzishe miradi katika nchi zao kwa tamaa kwamba watabuni nafasi za ajira katika nchi husika. Changamoto moja ambayo imetokea ni kwamba baadhi ya wawekezeji hawa wanatengea wananchi wa nchi walizotoka kazi za kitaalamu na zenye malipo bora huku wenyeji wakiachiwa zile zinazoitwa 'kazi za mikono' tu. Wanawapuuza wataalamu na wasomi walio katika mataifa hayo. Tusisahau pia kuwa baadhi ya wawekezaji hupelekwa katika mataifa wanayowekeza tabia na mienendo inayokinzana na maadili ya nchi pokezi.Tabia kama ubasha au usenge na ndoa za jinsia moja zimenasibishwa na tamaduni ngeni miongoni mwa Waafrika. Katika mkumbo huu ni tatizo la matumizi ya mihadarati ambalo sasa limefuzu kujiunga na majanga mengine ya kimataifa kama ukimwi. Ukweli mchungu ni kwamba maovu haya yametokana na ukarimu wa mataifa yenye tamaa ya kutaka wawekezaji wa kigeni ambao pamoja na kuwekeza, wao huja na 'yao'. Na kwa sababu mkata hana lake, mataifa pokezi yamehiari kuwapokea wawekezaji wa kigeni wakibeza athari mbaya zinazoletwa na watakuja kutahamaki baadaye kwamba mgeni kumpokea kumbe ni kujitongea.Suluhisho lingine, ambalo huenda ni bora zaidi, ni kuwawezesha vijana kujiajiri. Jambo hili linawezekana, mathalani endapo serikali itatenga hazina maalum katika bajeti yake ili kuwapa vijana mikopo yenye masharti nafuu ili waanzishie miradi yao. Itajuzu misaada hii itolewe kwa makundi ya vijana yaliyoandikishwa kama tahadhari moja ya kukabiliana na ufujaji wa pesa unaoweza kutokea misaada ikitolewa kwa watu binafsi. Vile vile kutolewa kwa mafunzo kuhusu usimamizi kwa vijana kabla ya kukabidhiwa pesa hizi itakuwa hatua nyingine ya kuepukana na ubadhirifu.Isitoshe, ustawishaji wa kilimo unaweza kutoa suluhisho lingine kwa tatizo la ukosefu wa ajira. Sharti vijana wahamasishwe ili washiriki katika kilimo ambapo watazalisha maii na kubuni nafasi za ajira katika nchi zao. Hii itarahisishwa kwa kufundisha somo la zaraa katika shule kama somo la lazima.Hakuna shaka kwamba juhudi hizi, na zingine ambazo hazijashughulikiwa katika makala haya, zikizingatiwa, usugu wa ukosefu wa ajira utageuzwa na kuwa tatizo tu!.
Maswali
a) Kwa nini mwandishi amerejea ukosefu wa ajira kama tatizo sugu.
b) Taja hatua nne ambazo zimechukuliwa na mataifa mbalimbali ili kulitatua tatizo la ukosefu wa ajira.
c) Majilio ya wawekezaji wa kigeni yanaweza kuchukuliwa kama hali ya 'kula sumu ili kupata kuishi'. Thibitisha jinsi 'sumu' inavyoahihirika kwa kurejelea mifano miwili katika makala haya
d) Eleza maana ya msamiati ufuatao katika muktadha wa makala haya.
a) Kutahamaki
b) Itajuzu
c) Zaraa
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Nchi za Afrika Mashariki ziliunda kamati ya lugha ili kusanifisha na kukuza Kiswahili. Eleza malengo
manne makuu na mafanikio yake katika juhudi za usanifishaji.(Solved)
Nchi za Afrika Mashariki ziliunda kamati ya lugha ili kusanifisha na kukuza Kiswahili. Eleza malengo
manne makuu na mafanikio yake katika juhudi za usanifishaji.
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Tunga sentensi ukitumia 'na' kama;
(i) Kuunganisha
(ii) Kihusishi(Solved)
Tunga sentensi ukitumia 'na' kama;
(i) Kuunganisha
(ii) Kihusishi
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Andika katika ukubwa wingi.
Njia hii inafaa zaidi kuliko ile.(Solved)
Andika katika ukubwa wingi.
Njia hii inafaa zaidi kuliko ile.
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)
- Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizobanwa.
Fundika (kitendua)
nata (kutendesha)(Solved)
Nyambua vitenzi vifuatavyo katika kauli zilizobanwa.
Fundika (kitendua)
nata (kutendesha)
Date posted: September 21, 2019. Answers (1)