Assumpta Matei: Chozi la Heri Alijiona kama mfa maji ambaye anakabiliwa na mtutumo wa mawimbi ya misiba, mmoja baada ya mwingine. (a) Bainisha muktadha wa dondoo hili....

      

Assumpta Matei: Chozi la Heri

Alijiona kama mfa maji ambaye anakabiliwa na mtutumo wa mawimbi ya misiba, mmoja baada ya mwingine.

(a) Bainisha muktadha wa dondoo hili.

(b) Eleza sifa tatu za anayerejelewa katika dondoo hili.

(c) Eleza tamathali ya usemi iliyotumika katika dondoo hili.

(d) Fafanua masaibu yaliyomkumba mrejelewa.

(e) Huku ukitolea mifano riwayani, jadili matatizo yanayowakumba wanajamii katika ndoa.

  

Answers


Martin
(a) Bainisha muktadha wa dondoo hili.

1. Ni maneno ya mwandishi/msimulizi.
2. Anamrejelea Lunga Kiriri Kangata
3. Ni baada ya kutolewa katika Msitu wa Mamba.
4. Moyo wa Lunga ulikuwa umekataa kuyakubali mazingira mapya katika Mlima wa Simba.

(b) Eleza sifa tatu za anayerejelewa.

1. Msomi – alikuwa anasomea kilimo ambapo baadaye aliajiriwa kama Afisa wa Kilimo nyanjani.
2. Mhifadhi mazingira/mwajibikaji – aliasisi Chama cha Watunza Mazingira wasio na Mipaka akiwa shuleni. Anawahutubia kuhusu uhifadhi wa mazingira.
3. Mwenye bidii – baada ya kustaafishwa anafanya kazi ya ukulima kwa bidii hadi anaitwa jina la msimbo ‘ mkulima namba wani’.
4. Mwenye msimamo thabiti – licha ya rai za wakubwa anapinga tendo la kuwapa raia mahindi yaliyoharibika.
5. Mtetezi wa haki – anahiari kupoteza riziki ili kuyaokoa maisha ya wanyonge wasio na hatia.
6. Mwenye tamaa- anapoona uzuri wa zao la mahindi katika shamba la babake, anapatwa na uchu unaolemaza uadilifu wake.
7. Mwenye mapenzi ya dhati – anajisabilia kwa hali na mali kumridhia na kumpendeza mkewe.

(c) Eleza tamathali ya usemi katika dondoo.
Tashbihi – alijiona kama mfa maji

d)Fafanua masaibu yaliyomkumba mrejelewa

1. Kuachishwa kazi kwa kupinga uagizaji wa mahindi mabaya.
2. Kufukuzwa katika Msitu wa Mamba hivyo kupoteza mali yake yote.
3. Anakosa pesa za kuwapeleka wanawe hata katika shule za watu wa kima wastani kwa sababu alilipwa fidia isiyotosha.
4. Anawapoteza ndugu na marafiki zake.
5. Kuachwa na mkewe Naomi.
6. Kufurushwa kutoka kwa Kiriri wakati wa wa zahama baada ya kutawazwa

(e) Huku ukitoa mifano riwayani, jadili matatizo yanayowakumba wanajamii katika ndoa.

i. Wanaume kushtakiwa kwa kubaka wake zao. Tete anasema kuwa sheria hiyo inamnyima mwanaume haki ya kuhusiana kimapenzi na mkewe.
ii. Upweke katika ndoa unaosababisha majonzi na hata kifo - Kiriri anaaga dunia kutokana na kihoro cha kufilisika na ukiwa alioachiwa na mkewe, Annete.
iii. Umaskini unasambaratisha ndoa. Ndoa ya Lunga na Naomi inavunjika kutokana na hali ya umaskini.
iv. Kuna uzinifu katika ndoa - Bwana Tenge alizini na wanawake wengi mkewe Bi. Kimai alipoenda mashambani.
v. Wakwe kuingilia ndoa - Ndoa kati ya Subira na Kaizari inavunjika kwa kuwa Subira alihisi kuwa anaonewa hasa na mama mkwe; vivyo hivyo na ile ya Selume.
vi. Kutofautiana kimsimamo/ kisiasa - Selume analaumiwa kwa kumuunga mkono Mwekevu ambaye alikuwa mpinzani mkuu wa muwaania kiti waliyemuunga mkono wakweze. (uk. 30)
vii. Ukabila - Selume anaachwa na mkewe na kumwoa mke mwingine kutoka kabila lake.
viii. Kukosa kupata watoto katika ndoa - Neema anakosa kujaliwa kupata watoto
marto answered the question on September 24, 2019 at 07:59


Next: The figure below shows the graph of Log P against Log Q. Given that P = aQn , find the value of a and n
Previous: Solve the following equation for 00 = x = 3600 Sin4 x – Cos4x = 0

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Exams With Marking Schemes

Related Questions