Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Pauline Kea: Kigogo 'Hivi vishahada vyao wanavyovipata siku hizi vinawavimbisha vichwa!' (a) Eleza muktadha wa dondoo hili. (b) Taja tamathali zozote mbili zinazojitokeza katika dondoo hili. (c)...

      

Pauline Kea: Kigogo

'Hivi vishahada vyao wanavyovipata siku hizi vinawavimbisha vichwa!'

(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.

(b) Taja tamathali zozote mbili zinazojitokeza katika dondoo hili.

(c) Eleza changamoto zilizomkabili mrejelewa na wenzake.

  

Answers


Martin
(a) Muktadha wa dondoo

i. Haya ni maneno ya Majoka
ii. Anamzungumzia Kenga
iii. Wamo Ofisini mwa Mzee Majoka
iv. Ni baada ya Majoka kusoma kwenye gazeti kwamba Tunu aliongoza maandamano na hata kuwahutubia wanahabari.

(b) Tamathali zozote mbili zinazojitokeza katika dondoo hili.

i. Nahau - vinawavimbisha vichwa kuwafanya wenye kiburi.
ii. Keli/ dhihaka – hivi vishahada vyao kudhalilisha shahada.
iii. Nidaa – vinawavimbisha vichwa! Hisia/ hasira ya Majoka.
iv. Jazanda – vimbisha vichwa – kuwa na kiburi

(c) Changamoto zilizomkabili mrejelewa na wenzake.

i. Kujerehiwa – Tunu anapigwa na kujeruhiwa na vijana wahuni.
ii. Usingiziaji – Tunu anasingiziwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Sudi.
iii. Kuenezwa kwa propaganda – Tunu anaambiwa kuwa Sudi anawinda roho yake.
iv. Serikali kufunga vyombo vya habari – Runinga ya Mzalendo
v. Mauaji ya waandamanaji – waandamanaji watano wanauawa.
vi. Wafuasi wake kutaka kukata tama – Sudi alitaka kuacha harakati za kupigania haki awashughulikie watoto.
vii. Kudhalilishwa – Ngurumo anamwambia kuwa hana wasifu wowote katika Sagamoyo.
viii. Kukabiliana na watu waliojaa taasubi za kiume – Ngurumo anamwambia kuwa hawezi kumpigia mwanamke kura pengine paka wake.
ix. Kukabiliana na masimango ya walevi – walevi wanamwimbia Tunu wimbo wa kumsimanga kuwa alistahili kuwa ameolewa.
x. Kupokea vitisho kutoka kwa viongozi - Majoka anamwambia kuwa mcheza na tope haachi kurukiwa
xi. Changamoto ya kukabiliana na vishawishi – Majoka anajaribu kumshawishi Tunu kukubali kuolewa na mwanawe (Ngao Junior)
xii. Kuzuiliwa kwa wafuasi wake – mkewe Sudi (Ashua) anazuiliwa
xiii. Changamoto ya kuwashawishi walevi kuhudhuria mikutano yao. Ngurumo anasema kuwa hawawezi kuhudhuria mkutano wa Tunu bali watenda kwa kigogo wao kwa dhifa.
xiv. Ubaguzi wa kijinsia – Majoka anakashifu maasi ya Tunu kuwa yanaongozwa na mwanamke.

marto answered the question on September 24, 2019 at 08:06


Next: Solve the following equation for 00 = x = 3600 Sin4 x – Cos4x = 0
Previous: Given Log m = x and log n = y, find x and y if Log m2 n = 4 and Log mn3 = 7

View More Kiswahili Fasihi Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions