Get premium membership and access questions with answers, video lessons as well as revision papers.

Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali.Mwana wa Adamu ni kiumbe cha ajabu! Ni kiumbe kilichopewa uwezo wa kuhodhi na kumiliki kila kitu; kiumbe kilichopewa akili

      

Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali.

Mwana wa Adamu ni kiumbe cha ajabu! Ni kiumbe kilichopewa uwezo wa kuhodhi na kumiliki kila kitu; kiumbe kilichopewa akili

Mwana wa Adamu ni kiumbe cha ajabu! Ni kiumbe kilichopewa uwezo wa kuhodhi na kumiliki kila kitu; kiumbe kilichopewa akili na maarifa fuvu tele ili kuratibu shughuli na mambo; kiumbe kilichopewa uwezo wa kuwasiliana na kutumia sauti nasibu ili kuwa na urari na muwala; kiumbe kilichopewa uwezo wa kufaidi viumbe wengine kwa njia mbalimbali na jumla jamala; hichi ndicho kiumbe kilichopewa idhini maalum ya kuzaana na kujaza dunia. Huyu ndiye mwana wa mama Hawa ambaye sasa amegeuka ndovu kumla mwanawe.
Kwa sababu ya bongo alizonazo, binadamu ana uwezo wa kutumia teknolojia kwa manufaa yake na ithibati zipo tele. Binadamu ametumia nyambizi kuzuru chini ya bahari; amefika mwezini; amevumbua mangala; amevumbua uyoka; amevumbua tarakilishi na sasa shughuli zake ni za kutandaridhi. Mwenyewe yuasema kuwa dunia yake imekuwa kitongoji katika muumano huu.
Chambacho wavyele , akili nyingi huondoa maarifa. Binadamu amekuwa dubwana linalojenga kushoto na kubomoa kulia na tuna sababu ya kulisoza dubwana hili kidole.
Rabana ndiye msanii asiye mfanowe kwani aliisawiri dunia kwa kila lililo jema kwa siku sita mtawalia na kumpa binadamu mazingira murua. Rabuka akaona yote yalikuwa mema na mazuri ; akamwambia binadamu, ‘’Haya, twende kazi !’’
Viwanda vya binadamu vinatiririsha maji-taka ovyo hadi mitoni, maziwani na baharini na matokeo yamekuwa ni vifo vya viumbe vya majini kama samaki ambavyo ni urithi aliyopewa na muumba. Hakuna kiumbe kinachoweza kustahimili Maisha bila maji safi. Maji yote sasa yametiwa sum na binadamu kwa sababu ya ‘maendeleo’ yake. Joshi kutoka katika viwanda vivyo hivyo nalo limehasiri ukanda wa ozoni ambao sasa umeruhusu jua kutuhasiri kwa joto kali mno. Siku hizi inasemekana kuwa kuna mvua ya asidi inayonyesha katika baadhi ya sehemu za dunia na kuleta mdhara makubwa. Labda hata mabahari yamekasirika kwa sababu hivi majuzi katika kile kilichoitwa ‘tsunami’ bahari lilihamia nchi kavu na kusomba maelfu ya binadamu na kuwameza wazima wazima. Vimbunga navyo vimetokea

kwa wingi. Wataalamu wanasema kuwa viwango vya miyeyuko vitazidi kwa sababu ya joto na kiwango cha maji kitazidi pia. Binadamu atatorokea wapi?
Idadi ya binadamu imezidi hadi kiasi asichoweza kukishughulikia kwa sababu anaijaza kwa sababu anadai kuwa aliruhusiwa kuijaza. Hii ni Imani potovu. Anasahau kuwa alipewa ubongo wa kuwaza na kuwazua kabla ya kufanya chochote. Dhiki, maradhi na ufukara zimehamia kwa binadamu na kumtia kiwewe.
Binadamu amefyeka misitu kwa kutaka makao, mashamba, mbao, makaa, ujenzi wa nyumba na barabara na mahitaji mengine mengi. Wanyama wamefurushwa na wengi kuangamia kwa sababu ya ukosefu wa chakula na wengine kushindwa kuhimili mabadiliko katika mazingira. Chemchemi za maji zimekauka nalo jangwa limeanza kutuzuru kwa kasi inayotisha. kazi ya binadamu imekuwa ya kusukia Kamba motoni. Itambidi aanze kujenga kwa matofali ya barafu.

MASWALI

(a) Jadili jinsi binadamu anaweza kutumia uwezo wake vizuri.

Matayarisho



Jibu

(b) Ukirejelea kifungu kizima, onyesha jinsi binadamu ametumia nafasi yake vibaya.

matayarisho

Jibu

  

Answers


Martin
a)Jadili jinsi binadamu anaweza kutumia uwezo wake vizuri
- Binadamu ana akili na maarifa fuvu tele wa kuratibu shughuli na mambo
- Anaweza kuwasiliana na kutumia sauti nasibu kuleta urari
- Kufaidi viumbe wengine
- Kutumia teknolojia kwa manufaa yake
- Ametumia nyambizi kuzuru chini ya bahari na kufika mwezini
- Kutekeleza uvumbuzi

b)Ukirejelea kifungu kizima,kizima , onyesha jinsi binadamu ametumia nafasi yake vibaya.

Jibu

- Amegeuka ndovu kumla mwanawe
- Amekuwa dubwana linalotengeneza na kuharibu /linalojenga kushoto na kubomoa kulia
- Viwanda vyake vinachafua maji na hivyo kuua viumbe vya majini.
- Joshi kutoka viwanda linahasiri ozoni na kusababisha joto kali
- Amesababisha mvua ya asidi inayoleta madhara makubwa
- Ameongeza idadi hadi kiwango asichoweza kukishughulikia
- Amefyeka misitu ili kupata makao
- Kwa kutowaza, amejisababishia dhiki, maradhi na ufukara.


marto answered the question on September 24, 2019 at 08:42


Next: Under a transformation represented by a matrix a triangle of area 10 cm2 is mapped on to a triangle whose area is 110 cm2....
Previous: Linganua kwa namna mbili sauti /e/ na /a/

View More Kiswahili Questions and Answers | Return to Questions Index


Learn High School English on YouTube

Related Questions