Trusted since 2008
Study resources on Kenyaplex

Get ready-made curriculum aligned revision materials

Exam papers, notes, holiday assignments and topical questions – all aligned to the Kenyan curriculum.

Andika neno lenye vipengele vinavyofuata vya kisarufi – kikanushi, ngeli, wakati,kitendwa, mzizi na kiishio.

Andika neno lenye vipengele vinavyofuata vya kisarufi – kikanushi, ngeli, wakati,kitendwa, mzizi na kiishio.

Answers


Martin
Hakikutusaidia/ halikumfuata/ hawakuyachukua
marto answered the question on September 24, 2019 at 08:45

Answer Attachments

Exams With Marking Schemes

Related Questions

  • Linganua kwa namna mbili sauti /e/ na /a/ (Solved)

    Linganua kwa namna mbili sauti /e/ na /a/

    Date posted: September 24, 2019 .    Answers (1)

  • Unda nomino kutokana na kivumishi kifuatacho: Tepetevu (Solved)

    Unda nomino kutokana na kivumishi kifuatacho:
    Tepetevu

    Date posted: September 23, 2019 .    Answers (1)

  • Andika upya sentensi kwa kutumia "O" rejeshi tamati. Gari lililoanguka si lile unalolizungumzia. (Solved)

    Andika upya sentensi kwa kutumia "O" rejeshi tamati.
    Gari lililoanguka si lile unalolizungumzia.

    Date posted: September 23, 2019 .    Answers (1)

  • Tunga sentensi sahihi ukitumia vitenzi vifuatavyo katika hali ya kufanyiza. i) - La ii) - Nywa iii) -Fa (Solved)

    Tunga sentensi sahihi ukitumia vitenzi vifuatavyo katika hali ya kufanyiza.
    i) - La
    ii) - Nywa
    iii) -Fa

    Date posted: September 23, 2019 .    Answers (1)

  • Toa maana mbili ya sentensi ifuatayo: Leteni! (Solved)

    Toa maana mbili ya sentensi ifuatayo:
    Leteni!

    Date posted: September 23, 2019 .    Answers (1)

  • Yakinisha sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali timilifu wingi. Msomi hakutuzwa siku hiyo. (Solved)

    Yakinisha sentensi ifuatayo katika wakati ujao hali timilifu wingi.
    Msomi hakutuzwa siku hiyo.

    Date posted: September 23, 2019 .    Answers (1)

  • Kanusha sentensi ifuatayo :- Kuliko na vita kwahitaji amani. (Solved)

    Kanusha sentensi ifuatayo :-
    Kuliko na vita kwahitaji amani.

    Date posted: September 23, 2019 .    Answers (1)

  • Bainisha shamirisho kipozi na kitondo katika sentensi hii. Nyanya ametengezewa kitanda kizuri na mjukuu wake. (Solved)

    Bainisha shamirisho kipozi na kitondo katika sentensi hii.
    Nyanya ametengezewa kitanda kizuri na mjukuu wake.

    Date posted: September 23, 2019 .    Answers (1)

  • Bainisha mofimu - LI- katika tungo hii. Alivyolikimbilia (Solved)

    Bainisha mofimu - LI- katika tungo hii.
    Alivyolikimbilia

    Date posted: September 23, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza sifa bainifu za sauti /j/. (Solved)

    Eleza sifa bainifu za sauti /j/.

    Date posted: September 23, 2019 .    Answers (1)

  • Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia vishale Alimwona mamba majini alipopiga mbizi. (Solved)

    Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia vishale
    Alimwona mamba majini alipopiga mbizi.

    Date posted: September 23, 2019 .    Answers (1)

  • Kutokana na kigezo cha jinsi hewa inavyozuliwa,taja aina mbili za konsonanti na utolee mifano kila moja. (Solved)

    Kutokana na kigezo cha jinsi hewa inavyozuliwa,taja aina mbili za konsonanti na utolee mifano kila moja.

    Date posted: September 23, 2019 .    Answers (1)

  • Eleza vikwazo mbali mbali vinavyotatiza ukuaji wa Fasihi Simulizi. (Solved)

    Eleza vikwazo mbali mbali vinavyotatiza ukuaji wa Fasihi Simulizi.

    Date posted: September 23, 2019 .    Answers (1)

  • Fafanua mbinu nne ambazo hutumika kuzua misimu. (Solved)

    Fafanua mbinu nne ambazo hutumika kuzua misimu.

    Date posted: September 23, 2019 .    Answers (1)

  • Ukosefu wa ajira hususan miongoni mwa vijana ni tatizo ambalo usugu wake umefikia kima kisichostahimilika tena. (Solved)

    Soma taarifa inavofuata kisha uyajibu maswali
    Ukosefu wa ajira hususan miongoni mwa vijana ni tatizo ambalo usugu wake umefikia kima kisichostahimilika tena. Ingawa limejitokeza kama tatizo la ulimwengu mzima lakini katika mataifa ya ulimwengu wa tatu, hasa barani Afrika, limekolea zaidi. Ni kweli kwamba tatizo hili si geni ulimwenguni kwani lilikuwepo miaka michache baada ya uhuru wa nchi nyingi za Kiafrika lakini wakati huo mhusika mkuu aliyelaumiwa kwa ukosefu wa ajira ulikuwa ukosefu wa elimu.Katika ulimwengu wa sasa mambo yamebaidika kabisa kama mbingu na ardhi kwani ukosefu wa elimu sio sababu ya ukosefu wa ajira. Ukweli ni kwamba kuwa na elimu ndiyo sababu ya kukosa ajira.Serikali za mataifa mengi zimechukua hatua mbali mbali ili kukabiliana na tatizo hili, si hoja kama baadhi ni za kutapatapa mithili ya mfa maji ambaye hushika maji. Miongoni mwa hatua hizi ni pamoja na kuboreshamazingira ya uwekezaji ili vitega uchumi viongezeke na hivyo kubuni nafasi za ajira. Kupanua fursa za^lNMMR. ngazi zote na kuhimiza mafunzo ya ujasiriamali na ufundi ni hatua nyingine. Vile vile serikali zingine zimebuni mipango inayolenga kuwawezesha vijana kujiajiri wenyewe.Waama, serikali zingine zimechukua hatua za kijasiri kwa kulegeza masharti ya uwekezaji kwa wawekezaji wa kigeni ili kuwavutia waanzishe miradi katika nchi zao kwa tamaa kwamba watabuni nafasi za ajira katika nchi husika. Changamoto moja ambayo imetokea ni kwamba baadhi ya wawekezeji hawa wanatengea wananchi wa nchi walizotoka kazi za kitaalamu na zenye malipo bora huku wenyeji wakiachiwa zile zinazoitwa 'kazi za mikono' tu. Wanawapuuza wataalamu na wasomi walio katika mataifa hayo. Tusisahau pia kuwa baadhi ya wawekezaji hupelekwa katika mataifa wanayowekeza tabia na mienendo inayokinzana na maadili ya nchi pokezi.Tabia kama ubasha au usenge na ndoa za jinsia moja zimenasibishwa na tamaduni ngeni miongoni mwa Waafrika. Katika mkumbo huu ni tatizo la matumizi ya mihadarati ambalo sasa limefuzu kujiunga na majanga mengine ya kimataifa kama ukimwi. Ukweli mchungu ni kwamba maovu haya yametokana na ukarimu wa mataifa yenye tamaa ya kutaka wawekezaji wa kigeni ambao pamoja na kuwekeza, wao huja na 'yao'. Na kwa sababu mkata hana lake, mataifa pokezi yamehiari kuwapokea wawekezaji wa kigeni wakibeza athari mbaya zinazoletwa na watakuja kutahamaki baadaye kwamba mgeni kumpokea kumbe ni kujitongea.Suluhisho lingine, ambalo huenda ni bora zaidi, ni kuwawezesha vijana kujiajiri. Jambo hili linawezekana, mathalani endapo serikali itatenga hazina maalum katika bajeti yake ili kuwapa vijana mikopo yenye masharti nafuu ili waanzishie miradi yao. Itajuzu misaada hii itolewe kwa makundi ya vijana yaliyoandikishwa kama tahadhari moja ya kukabiliana na ufujaji wa pesa unaoweza kutokea misaada ikitolewa kwa watu binafsi. Vile vile kutolewa kwa mafunzo kuhusu usimamizi kwa vijana kabla ya kukabidhiwa pesa hizi itakuwa hatua nyingine ya kuepukana na ubadhirifu.Isitoshe, ustawishaji wa kilimo unaweza kutoa suluhisho lingine kwa tatizo la ukosefu wa ajira. Sharti vijana wahamasishwe ili washiriki katika kilimo ambapo watazalisha maii na kubuni nafasi za ajira katika nchi zao. Hii itarahisishwa kwa kufundisha somo la zaraa katika shule kama somo la lazima.Hakuna shaka kwamba juhudi hizi, na zingine ambazo hazijashughulikiwa katika makala haya, zikizingatiwa, usugu wa ukosefu wa ajira utageuzwa na kuwa tatizo tu!.

    Maswali
    a) Kwa nini mwandishi amerejea ukosefu wa ajira kama tatizo sugu.
    b) Taja hatua nne ambazo zimechukuliwa na mataifa mbalimbali ili kulitatua tatizo la ukosefu wa ajira.
    c) Majilio ya wawekezaji wa kigeni yanaweza kuchukuliwa kama hali ya 'kula sumu ili kupata kuishi'. Thibitisha jinsi 'sumu' inavyoahihirika kwa kurejelea mifano miwili katika makala haya
    d) Eleza maana ya msamiati ufuatao katika muktadha wa makala haya.
    a) Kutahamaki
    b) Itajuzu
    c) Zaraa

    Date posted: September 21, 2019 .    Answers (1)

  • Nchi za Afrika Mashariki ziliunda kamati ya lugha ili kusanifisha na kukuza Kiswahili. Eleza malengo manne makuu na mafanikio yake katika juhudi za usanifishaji. (Solved)

    Nchi za Afrika Mashariki ziliunda kamati ya lugha ili kusanifisha na kukuza Kiswahili. Eleza malengo
    manne makuu na mafanikio yake katika juhudi za usanifishaji.

    Date posted: September 21, 2019 .    Answers (1)

  • Tunga sentensi ukitumia 'na' kama; (i) Kuunganisha (ii) Kihusishi (Solved)

    Tunga sentensi ukitumia 'na' kama;
    (i) Kuunganisha
    (ii) Kihusishi

    Date posted: September 21, 2019 .    Answers (1)

  • Andika katika ukubwa wingi. Njia hii inafaa zaidi kuliko ile. (Solved)

    Andika katika ukubwa wingi.
    Njia hii inafaa zaidi kuliko ile.

    Date posted: September 21, 2019 .    Answers (1)

  • Andika methali inayotumiwa kutuhimiza kuthamini vitu viliyo karibu kwani ndivyo vitufaavyo wakatiwa janga. (Solved)

    Andika methali inayotumiwa kutuhimiza kuthamini vitu viliyo karibu kwani ndivyo vitufaavyo wakati wa janga.

    Date posted: September 21, 2019 .    Answers (1)

  • Unda kitenzi kutokana na nomino; abiria (Solved)

    Unda kitenzi kutokana na nomino;
    abiria

    Date posted: September 21, 2019 .    Answers (1)