(j) (ch) (ny) (sh) (y)
sharon kalunda answered the question on September 24, 2019 at 10:12
- Bwana Spika, ninaomba kufahamishwa kwa nini Waziri wa Biashara ameshindwa kuchukua hatua kukomesha uuzaji wa vileo hatari kwa watoto wa shule.
(a) Fafanua sifa zozote tano...(Solved)
Bwana Spika, ninaomba kufahamishwa kwa nini Waziri wa Biashara ameshindwa kuchukua hatua kukomesha uuzaji wa vileo hatari kwa watoto wa shule.
(a) Fafanua sifa zozote tano za sajili inayorejelewa na maneno haya
b)Eleza mambo yaliyochangia msambao wa Lugha ya Kiswahili kabla ya kuondoka kwa wakoloni barani
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)
- Jaza nafasi zifuatazo.
Mkwezi hupanda miti............. hufanya kazi maktabani, mpanzi ........, ...... huendesha gari la moshi na mpagazi ......(Solved)
Jaza nafasi zifuatazo.
Mkwezi hupanda miti............. hufanya kazi maktabani, mpanzi ........, ...... huendesha gari la moshi na mpagazi ......
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)
- Tofautisha matumizi ya ‘Ngali’ katika tungo hizi.
Mama angali mlimani
Otiende angalisoma kwa bidi angaliishi maisha mema.(Solved)
Tofautisha matumizi ya ‘Ngali’ katika tungo hizi.
Mama angali mlimani
Otiende angalisoma kwa bidi angaliishi maisha mema.
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)
- Onyesha na ueleze matumizi ya viwakifishi vifuatavyo.
Kibainishi
Mkwaju(Solved)
Onyesha na ueleze matumizi ya viwakifishi vifuatavyo.
Kibainishi
Mkwaju
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)
- Pambanua kwa michoro ya matawi sentensi inayofuata.
Ikiwa atawasili mapema, atafungua mkutano(Solved)
Pambanua kwa michoro ya matawi sentensi inayofuata.
Ikiwa atawasili mapema, atafungua mkutano
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)
- Bainisha matumizi ya ‘ KI’ katika sentensi hii.
Seremala akiwasili leo atakuwa akitengeneza kiti cha kitoto chake(Solved)
Bainisha matumizi ya ‘ KI’ katika sentensi hii.
Seremala akiwasili leo atakuwa akitengeneza kiti cha kitoto chake
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)
- Tumia O rejeshi tamati. Mwanafunzi ambaye hufanikiwa ni yule ambaye hudurusu kwa makini.(Solved)
Tumia O rejeshi tamati. Mwanafunzi ambaye hufanikiwa ni yule ambaye hudurusu kwa makini.
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)
- Tumia kivumishi cha a- unganifu katika sentensi ili kuleta dhana ya sifa.(Solved)
Tumia kivumishi cha a- unganifu katika sentensi ili kuleta dhana ya sifa.
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)
- Andika umoja wa sentensi inayofuata katika hali yakinifu.
Kina mama wasingefika mapema fuoni, wasingewahi mashua.(Solved)
Andika umoja wa sentensi inayofuata katika hali yakinifu.
Kina mama wasingefika mapema fuoni, wasingewahi mashua.
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)
- Tambua kiima, aina za shamirisho na chagizo katika sentensi hii.
Kimemletea taabu sana.
Kiima:
Shamirisho:
Chagizo:(Solved)
Tambua kiima, aina za shamirisho na chagizo katika sentensi hii.
Kimemletea taabu sana.
Kiima:
Shamirisho:
Chagizo:
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)
- Ainisha vishazi katika sentensi, Endapo atanialika, nitamtembelea.(Solved)
Ainisha vishazi katika sentensi, Endapo atanialika, nitamtembelea.
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)
- Andika sentensi inayofuata katika usemi halisi ukianza na kihisishi cha dharau.
Mzee Anandwa alishangaa na kusema kuwa kijana huyo alikuwa amekuwa kaida kama Kirongwe.(Solved)
Andika sentensi inayofuata katika usemi halisi ukianza na kihisishi cha dharau.
Mzee Anandwa alishangaa na kusema kuwa kijana huyo alikuwa amekuwa kaida kama Kirongwe.
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)
- Sentensi zinazofuata ni za aina gani?
(i) Nyamari aliadhibiwa madhali alifika darasani akiwa amechelewa sana
(ii) Mimi sijaelewa kamwe somo hili
(iii) Watoto ambao walipotea juzi wamepatikana...(Solved)
Sentensi zinazofuata ni za aina gani?
(i) Nyamari aliadhibiwa madhali alifika darasani akiwa amechelewa sana
(ii) Mimi sijaelewa kamwe somo hili
(iii) Watoto ambao walipotea juzi wamepatikana leo asubuhi
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)
- Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii.
Wanakujua huku(Solved)
Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii.
Wanakujua huku
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)
- Tungia sentensi moja ziara na maziara ili kubainisha maana zao.(Solved)
Tungia sentensi moja ziara na maziara ili kubainisha maana zao.
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)
- Andika sentensi katika wakati usiodhihirika ukitumia nomino moja ya jamii.(Solved)
Andika sentensi katika wakati usiodhihirika ukitumia nomino moja ya jamii.
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)
- Tumia kitenzi kishirikishi kipungufu bila kupoteza maana ya sentensi hii.
Mwanafunzi mmoja angali analala bwenini(Solved)
Tumia kitenzi kishirikishi kipungufu bila kupoteza maana ya sentensi hii.
Mwanafunzi mmoja angali analala bwenini
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)
- Andika neno lenye vipengele vinavyofuata vya kisarufi – kikanushi, ngeli, wakati,kitendwa, mzizi na kiishio.(Solved)
Andika neno lenye vipengele vinavyofuata vya kisarufi – kikanushi, ngeli, wakati,kitendwa, mzizi na kiishio.
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)
- Linganua kwa namna mbili sauti /e/ na /a/(Solved)
Linganua kwa namna mbili sauti /e/ na /a/
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)
- Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali.Mwana wa Adamu ni kiumbe cha ajabu! Ni kiumbe kilichopewa uwezo wa kuhodhi na kumiliki kila kitu; kiumbe kilichopewa akili(Solved)
Soma Makala yafuatayo kisha ujibu maswali.
Mwana wa Adamu ni kiumbe cha ajabu! Ni kiumbe kilichopewa uwezo wa kuhodhi na kumiliki kila kitu; kiumbe kilichopewa akili
Mwana wa Adamu ni kiumbe cha ajabu! Ni kiumbe kilichopewa uwezo wa kuhodhi na kumiliki kila kitu; kiumbe kilichopewa akili na maarifa fuvu tele ili kuratibu shughuli na mambo; kiumbe kilichopewa uwezo wa kuwasiliana na kutumia sauti nasibu ili kuwa na urari na muwala; kiumbe kilichopewa uwezo wa kufaidi viumbe wengine kwa njia mbalimbali na jumla jamala; hichi ndicho kiumbe kilichopewa idhini maalum ya kuzaana na kujaza dunia. Huyu ndiye mwana wa mama Hawa ambaye sasa amegeuka ndovu kumla mwanawe.
Kwa sababu ya bongo alizonazo, binadamu ana uwezo wa kutumia teknolojia kwa manufaa yake na ithibati zipo tele. Binadamu ametumia nyambizi kuzuru chini ya bahari; amefika mwezini; amevumbua mangala; amevumbua uyoka; amevumbua tarakilishi na sasa shughuli zake ni za kutandaridhi. Mwenyewe yuasema kuwa dunia yake imekuwa kitongoji katika muumano huu.
Chambacho wavyele , akili nyingi huondoa maarifa. Binadamu amekuwa dubwana linalojenga kushoto na kubomoa kulia na tuna sababu ya kulisoza dubwana hili kidole.
Rabana ndiye msanii asiye mfanowe kwani aliisawiri dunia kwa kila lililo jema kwa siku sita mtawalia na kumpa binadamu mazingira murua. Rabuka akaona yote yalikuwa mema na mazuri ; akamwambia binadamu, ‘’Haya, twende kazi !’’
Viwanda vya binadamu vinatiririsha maji-taka ovyo hadi mitoni, maziwani na baharini na matokeo yamekuwa ni vifo vya viumbe vya majini kama samaki ambavyo ni urithi aliyopewa na muumba. Hakuna kiumbe kinachoweza kustahimili Maisha bila maji safi. Maji yote sasa yametiwa sum na binadamu kwa sababu ya ‘maendeleo’ yake. Joshi kutoka katika viwanda vivyo hivyo nalo limehasiri ukanda wa ozoni ambao sasa umeruhusu jua kutuhasiri kwa joto kali mno. Siku hizi inasemekana kuwa kuna mvua ya asidi inayonyesha katika baadhi ya sehemu za dunia na kuleta mdhara makubwa. Labda hata mabahari yamekasirika kwa sababu hivi majuzi katika kile kilichoitwa ‘tsunami’ bahari lilihamia nchi kavu na kusomba maelfu ya binadamu na kuwameza wazima wazima. Vimbunga navyo vimetokea
kwa wingi. Wataalamu wanasema kuwa viwango vya miyeyuko vitazidi kwa sababu ya joto na kiwango cha maji kitazidi pia. Binadamu atatorokea wapi?
Idadi ya binadamu imezidi hadi kiasi asichoweza kukishughulikia kwa sababu anaijaza kwa sababu anadai kuwa aliruhusiwa kuijaza. Hii ni Imani potovu. Anasahau kuwa alipewa ubongo wa kuwaza na kuwazua kabla ya kufanya chochote. Dhiki, maradhi na ufukara zimehamia kwa binadamu na kumtia kiwewe.
Binadamu amefyeka misitu kwa kutaka makao, mashamba, mbao, makaa, ujenzi wa nyumba na barabara na mahitaji mengine mengi. Wanyama wamefurushwa na wengi kuangamia kwa sababu ya ukosefu wa chakula na wengine kushindwa kuhimili mabadiliko katika mazingira. Chemchemi za maji zimekauka nalo jangwa limeanza kutuzuru kwa kasi inayotisha. kazi ya binadamu imekuwa ya kusukia Kamba motoni. Itambidi aanze kujenga kwa matofali ya barafu.
MASWALI
(a) Jadili jinsi binadamu anaweza kutumia uwezo wake vizuri.
Matayarisho
Jibu
(b) Ukirejelea kifungu kizima, onyesha jinsi binadamu ametumia nafasi yake vibaya.
matayarisho
Jibu
Date posted: September 24, 2019. Answers (1)